Faida 12 za karafuu mwilini na jinsi ya kutumia
Karafuu ni moja ya mimea ambayo hutumiwa zaidi kama kiungo cha chakula vilevile hutumiwa kama dawa ya kuhifadhia vyakula vingine visiharibike.
Mbali na kutumiwa kama kiungo, karafuu hutumiwa zaidi kutengenezea manukato na sabuni kutokana na harufu yake nzuri.
Mmea huu asili yake ni visiwa vya Molucca (Indonesia).
Lakini kwa sasa wazalishaji wakuu wa mmea huu duniani ni Tanzania (Zanzibar) na
Madagascar.
Mmea huu huota kwa kupandikizwa mbegu na huwa tayari kuvunwa miaka 4 baada ya kuoteshwa. Baada ya kukomaa huvunwa mara 2 kwa mwaka.
Maua
ambayo bado hayajachanua huvunwa na kukaushwa na jua, tayari kwa matumizi.
Tafiti mbalimbali za kisayansi zimethibitisha uwezo wa karafuu wa kutibu na kuzuia magonjwa mbalimbali ya binadamu.
Baadhi ya magonjwa hayo ni pamoja na kutapika, maumivu, bakteria mbalimbali na maradhi ya meno.
Viambata hai ndani ya karafuu na faida zake.
Kuna kemikali mbalimbali ambazo hupatikana ndani ya mmea huu wa karafuu ambazo zimeonyesha uwezo mkubwa wa kupambana na magonjwa ya binadamu.
Baadhi ya kemikali hizo ni kama ifuatavyo;
- Kemikali za phenolic: Hili ni kundi la kemikali ambalo hupatikana katika karafuu. Kemikali hizi zina kazi nyingi mwilini, lakini kubwa ni uwezo wa kuangamiza bakteria, fangasi, minyoo na kutuliza maumivu. Moja ya kemikali muhimu katika kundi hili la phenolic ni eugenol, acetyl eugenol, methyl salicylate, pinene, vanillin hidroxibenzoic acids na hydoxiphenyl propens.
- Kemikali za flavonoids: Kemikali hizi huondoa sumu mwilini, kuangamiza virusi na bakteria. Baadhi ya kemikali hizi za quercetin na kaempferol.
- Pia kuna kemikali za biflorin, oleanolic acid, orsellinic acid, myricetin, ellagic acid na rhamnocitrin ambazo huangamiza vimelea vinavyoshambulia meno.
Faida za karafuu mwilini.
Yafuatayo ni magonjwa ambayo huweza kutibiwa kwa kutumia
karafuu.
01: Magonjwa ya meno.
Kemikali ya Eugenol ambayo hupatikana kwa zaidi ya 85%
katika mafuta ya karafuu ina uwezo wa kuua na kuzuia maambukizi katika meno.
Vilevile kemikali hii na nyinginezo katika karafuu zina
uwezo mkubwa wa kutuliza maumivu na hivyo kutumiwa kama tiba ya meno yanayouma.
02: Kutibu magonjwa ya minyoo na amoeba.
Eugenol pamoja na kemikali nyinginezo katika karafuu zina
uwezo wa kuangamiza vimelea mbalimbali ambavyo husababisha magonjwa ya minyoo
na amoeba.
Kutibu maradhi yaliyotengeneza usugu wa dawa.
Kwa baadhi ya magonjwa hasa ya fangasi na bakteria ambayo
hayaitikii tena tiba za kawaida za dawa za kisasa.
Matumizi ya karafuu (mafuta) ni msaada mkubwa kutokana na
uwepo wa kundi la kemikali mbalimbali zinazofanya kazi kwa ushirikiano wa hali
ya juu.
03: Hutumika kama kinga ya maradhi mbalimbali.
Mafuta ya karafuu ambayo yana kiwango kikubwa cha kemikali za Eugenol na flavonoids huweza kutumika ka kinga ya magonjwa mbalimbali.
Mfano
magonjwa ya meno, magonjwa ya aleji, chunusi na maumivu.
04: Kutibu maradhi ya sukari na damu kuganda.
Kemikali za tannis, ellagic acid, gallic acid na flavonoids
zimeonyesha uwezo mkubwa wa kusaidia damu kuganda hasa watu wenye tatizo la anemia.
Vilevile kemikali hizi zimeonyesha uwezo wa kusaidia mwili
katika mchakato wa kuweka mlinganyo wa sukari mwilini.
05: Kutibu magonjwa ya fangasi.
Karafuu inawea kutumika kwa kunywa au kwa kupaka mafuta yake ili kutibu maradhi ya fangasi.
Fangasi za mdomoni, ngozi na fangasi ya damu aina zote hizi za fangasi huweza kutibiwa na karafuu. Eugenol ndio kinara wa mapambano haya katika karafuu.
06: Hutumika kutibu majipu na chunusi.
Karafuu ikichanganywa na mafuta ya rosemary hutumika kutibu
na kuangamiza bakteria wa S. aureus ambaye husababisha majipu.
Vilevile bakteria wa P. vulgaris ambaye husababisha chunusi na
bakteria wa S. epidermidis ambaye husababisha chunusi, mapunye na vibarango.
07: Kutibu na kuzuia ukuaji wa virusi.
Kemikali ya Eugeniin ndani ya karafuu imeonyesha uwezo
mkubwa wa kuzuia na kuthibiti ukuaji wa virusi mwilini.
Baadhi ya virusi ambao huweza kuthibitiwa na kemikali hii ni
Virusi wa mkanda wa jeshi, virusi wa mafua, virusi wa herpes wanaoshambulia
midomo na virusi wa homa ya ini type C.
08: Kuondoa sumu mwilini.
Viantioksideshaji vya flavonoids katika karafuu vina uwezo
wa kupunguza kiwango cha chaji huru mwilini na baadhi ya madini huru mwilini
kama zebaki ambayo ni hatari kwa uhai wa seli za mwili.
09: Kutuliza maumivu.
Eugenol katika karafuu ina uwezo wa kutuliza maumivu
mbalimbali ya mwili kama vile, maumifu ya misuli, maumivu ya neva hasa kwa
wenye kisukari. Vilevile maumivu ya mgongo, maumivu ya maungio na maumivu ya
kichwa.
10: Kutibu saratani.
Kemikali za Eugenol na dihydrodieugenol zimeonyesha uwezo wa kuua seli zinazokua bila uthibiti mwilini.
Pia uwezo wake wa kuingilia hatua mbalimbali
za utengenezwaji wa protini katika seli hizi za saratani.
11: Kutibu na kulinda ini dhidi ya magonjwa.
Kemikali za sanguinarine na benzo phenanthridine ndani ya
karafuu zimethibitishwa kitaalamu kutibu na kutoa ulinzi katika ini dhidi ya
maradhi mbalimbali.
12: Kutibu maradhi ya mzunguko wa damu.
Eugenol na kemikali nyinginezo zimeonyesha uwezo mkubwa wa
kutibu maradhi ya mzunguko wa damu kutokana na uwezo wake wa kupunguza
shinikizo la damu.
Hii inasaidia kuimarisha usafirishwaji wa damu na huweza
kutumiwa na watu wenye matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume.
13: Kuzuia kuharisha na kutapika.
Matatizo mablimbali ya mfumo wa chakula yanaweza kutibiwa na
karafuu mfano, kutapika, kuharisha, kujamba na tumbo kujaa gesi.
Faida nyinginezo.
Hutumika kama dawa ya kufukuza wadudu, kuiarisha kumbukumbu,
kutibu vidonda na kutuliza homa.
Sehemu ipi ya mmea hutumika kama tiba
Majani, maua na fundo la maua ambalo bado halijachanua ndio
hutumiwa kama tiba. Na sehemu hizi huweza kutumiwa kama juisi, mafuta au
matone.
Jinsi ya kutumia Karafuu kama dawa
Maandalizi.
Jinsi ya kutengeneza juisi: vuna fundo amablo bado
halijachanua maua au maua kisha loweka katika maji kwa siku 5 au loweka katika
pombe kali (70%) kwa siku 3, uwiano ni vipande 2 vya karafuu katika mililita 50
za maji. Chuja juisi yako na tayari kwa matumizi.
Jinsi ya kutengeneza mafuta ya karafuu: mafuta ya karafuu
huvunwa kutoka katika majani na matawi laini yaliyo karibu na majani. Loweka
majani ya karafuu katika pombe kali kwa muda wa siku 7 hadi 15.
Matumizi.
Tumia juisi ya karafuu mililita 130, nusu glasi kila baada
ya masaa 8. Kwa ajili ya kutibu kuharisha, kutapika, kichefuchefu, vidonda vya
tumbo na maradhi mengineyo ya ndani kama yalivyoolodheshwa hapo juu.
Tumia kwa kudondoshea matone 3 hadi 5 mdomoni kwa maradhi ya
kinywa na meno kisha acha walau dakika 3 bila kumeza wala kutema.
Tumia mafuta ya karafuu kwa kudondoshea matone 2 kwa maradhi
ya mdomo na kinywa, matone 2 katika nusu glasi kwa kunywa na tumia kiwango stahiki kwa
kupaka kwa watu wenye matatizo ya ngozi.
Hitimisho
Mbali na kutumiwa kama kiungo cha chakula, karafuu ni miongoni mwa mitishamba yenye uwezo wa kutibu matatizo mengi ya afya.
Matumizi ya mara kwa mara ya karafuu si tu yatakusaidia kutibu maradhi mbalimbali ya mwili, lakini pia itakusaidia kukupa kinga dhidi ya maradhi haya.