Fangasi za ukeni, chanzo, dalili na tiba
Fangasi za ukeni ni aina ya fangasi ambayo hushambulia maeneo ya uke na husababishwa na kundi la vimelea vya fangasi lijulikanalo kama Candida.
Candida albicans ni aina mojawapo ya fangasi kutoka katika kundi hili ambaye huchangia kwa kiasi kikubwa tatizo hili la fangasi za ukeni.
Candida albicans ndio aina ya fangasi anayeongoza kwa kusababisha tatizo hili ambapo husababisha zaidi ya asilimia 90% ya matatizo yote ya fangasi za ukeni kwa wanawake.
Baadhi ya vimelea hivi hushirikiana na mifumo mbalimbali ya mwili kwa faida. Moja ya vimelea ambavyo huishi mwilini kwa faida ni fangasi jamii ya Candida albicans.
Katika mwili wa mwanamke fangasi hawa hupatikana kwa wingi maeneo ya uke. Wakiwa ukeni fangasi hawa husaidia kutoa ulinzi dhidi ya vimelea wengineo ambao ni hatari kwa mwili, vilevile husaidia kuleta mlinganyo wa chaji ukeni.
Ikiwa kutatokea mvurugiko wa mazingira yanayowaweka fangasi hawa katika mlinganyo na kuwasababisha kuzaliana kwa wingi kupita kiasi.
Moja bakteria muhimu mwili anayeathiriwa na matumizi ya dawa za antibiotiki ni Lactobacillus ambaye hupatikana maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo ukeni.
Akiwa ukeni husaidia kuleta mlinganyo wa chaji katika kiwango cha PH 3-4. kiwango hiki husaidia uthibiti wa ukuaji wa fangasi ukeni.
Mfano wa dawa hizi za antibiotiki ni Amoxycillin, Tetracycline na Doxycyline.
Jasho inayojificha katika mikunjo ya nyama za unene mwilini ni moja ya mazingira yanayochagiza ukuaji wa fangasi hawa.
Pili ni mabadiliko ya homoni ambayo ni moja ya chanzo kikubwa cha maradhi ya fangasi.
Dozi yake huwa ni kati ya siku 3 hadi 7 kulingana na maelekezo ya daktari au mfamasia..
Vilevile dawa hizi huweza kutumika katika mseto ambapo mgonjwa anatumia dawa zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Mara nyingi dawa mseto za fangasi hutumiwa kwa namna ya vidonge vya kunywa.
Ikiwa fangasi ni sugu kiasi cha kushindwa kuitikia dawa basi dawa aina ya Boric acid hutumika kama mbadala. Dawa hii hutumiwa kwa kupachika ukeni na si kunywa.
Baadhi ya njia hizo ni pamoja na;
Jambo bora na la pekee ni kufika kituo cha afya kwa ajili ya ushauri nasaha na kupima ili kupata uhakika wa chanzo cha dalili hizi ikiwa zinatokana na fangasi au matatizo mengine.
Ili kuepukana na matatizo ya fangasi ukeni ni vizuri kwa mwanamke kufuata miongozo na ushauri sahihi wa kitaalamu.
Matumizi ya antibiotiki na ujauzito ni sababu zisizoepukika kwa mwanamke, kwa hivyo ni vyema kufuata miongozo sahihi ya matumizi ya dawa hatarishi za antibiotiki.
Vilevile kufuata ushauri nasaha juu ya utunzaji bora wa mimba na namna ya kupambana na mgonjwa andamizi kipindi cha ujauzito.
Candida albicans ni aina mojawapo ya fangasi kutoka katika kundi hili ambaye huchangia kwa kiasi kikubwa tatizo hili la fangasi za ukeni.
Candida albicans ndio aina ya fangasi anayeongoza kwa kusababisha tatizo hili ambapo husababisha zaidi ya asilimia 90% ya matatizo yote ya fangasi za ukeni kwa wanawake.
Fangasi ukeni hutokeaji?
Baadhi ya mifumo na maeneo mbalimbali ya miili yetu hufanya kazi kwa msaada wa vimelea mbalimbali vya bakteria, fangasi na minyoo.Baadhi ya vimelea hivi hushirikiana na mifumo mbalimbali ya mwili kwa faida. Moja ya vimelea ambavyo huishi mwilini kwa faida ni fangasi jamii ya Candida albicans.
Katika mwili wa mwanamke fangasi hawa hupatikana kwa wingi maeneo ya uke. Wakiwa ukeni fangasi hawa husaidia kutoa ulinzi dhidi ya vimelea wengineo ambao ni hatari kwa mwili, vilevile husaidia kuleta mlinganyo wa chaji ukeni.
Ikiwa kutatokea mvurugiko wa mazingira yanayowaweka fangasi hawa katika mlinganyo na kuwasababisha kuzaliana kwa wingi kupita kiasi.
Fangasi huyu hugeuka na kuwa hatari iwapo kiwango chake cha idadi kitabadilika kuliko kawaida inayotakiwa, hali hii inapotokea hupelekea tatizo la fangasi kuonekana.
Yapo mambo kadhaa ambayo yanaweza kupelekea kuvurugika kwa kiwango cha fangasi hawa ukeni kiasi cha kusababisha maradhi ya fangasi. Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na mimba na kisukari.
Katika hatua za awali tatizo hili si hatari sana kwa afya ya mwili na mara nyingi iwapo kinga ya mwili iko imara tatizo linaweza kuisha lenyewe.
Ikiwa tatizo litahitaji tiba basi ni vyema kufanya matibabu haraka iwezekanavyo kwa kuwa kushindwa kudhibiti tatizo la fangasi ukeni kwa wakati kunaweza kusababisha kutengenezwa kwa fangasi sugu.
Fangasi sugu ukeni huweza kusababisha kusambaa kwa fangasi hawa maeneo mengine ya mwili hususa kupitia damu na kuathiri maeneo mengineyo mwili.
Baadhi ya mambo yanayoweza kusababisha kuzaliana kwa fangasi wa C. albicans na kusababisha matatizo ukeni ni;
Yapo mambo kadhaa ambayo yanaweza kupelekea kuvurugika kwa kiwango cha fangasi hawa ukeni kiasi cha kusababisha maradhi ya fangasi. Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na mimba na kisukari.
Katika hatua za awali tatizo hili si hatari sana kwa afya ya mwili na mara nyingi iwapo kinga ya mwili iko imara tatizo linaweza kuisha lenyewe.
Ikiwa tatizo litahitaji tiba basi ni vyema kufanya matibabu haraka iwezekanavyo kwa kuwa kushindwa kudhibiti tatizo la fangasi ukeni kwa wakati kunaweza kusababisha kutengenezwa kwa fangasi sugu.
Fangasi sugu ukeni huweza kusababisha kusambaa kwa fangasi hawa maeneo mengine ya mwili hususa kupitia damu na kuathiri maeneo mengineyo mwili.
Sababu za kupata fangasi ukeni
Tatizo la fangasi ukeni husababishwa na kuzaliana kwa wingi kwa fangasi aina ya C. albicans. Yapo mambo kadhaa ambayo huweza kusababisha kuzaliana kwa fangasi hawa kupita kawaida hasa maeneo ya uke.Baadhi ya mambo yanayoweza kusababisha kuzaliana kwa fangasi wa C. albicans na kusababisha matatizo ukeni ni;
#1: Ujauzito
Kipindi cha ujauzito kuna mabadiliko mengi hutokea, mojawapo ni ongezeko la homoni ya oestrojeni ambayo husaidia ukuaji wa C. albicans na bakteria wengineo.#2: Matumizi ya dawa za kupanga uzazi
Asilimia kubwa ya dawa za kupanga uzazi ni homoni. Dawa hizi huathiri mfumo wa homoni wa mwili kwa kiasi kikubwa.Moja ya athari ni kuongezeka kwa homoni ya oestrojeni mbayo husaidia vimelea wengi wa magonjwa kukua ikiwemo C. albicans.
#3: Maradhi ya kisukari
Kisukari husababisha fangasi za ukeni kwa aina kuu mbili, moja ni kutokana na kupungua kwa kinga za mwili, na pili ni uzalishwaji wa mkojo wenye sukari nyingi. Sukari hii katika mkojo inapofika ukeni hutumiwa na fangasi hawa kama chakula hivyo kuwafanya kunawili na kuzaliana kwa wingi.#4: Matumizi ya dawa za antibiotiki.
Dawa hizi ni mahususi kwa ajili ya kutibu maradhi ya bakteria. Matumizi ya dawa hizi huangamiza bakteria mbalimbali mwilini hata wale wa faida ambao husaidia kuleta mlinganyo wa C. albicans mwilini.Moja bakteria muhimu mwili anayeathiriwa na matumizi ya dawa za antibiotiki ni Lactobacillus ambaye hupatikana maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo ukeni.
Akiwa ukeni husaidia kuleta mlinganyo wa chaji katika kiwango cha PH 3-4. kiwango hiki husaidia uthibiti wa ukuaji wa fangasi ukeni.
Mfano wa dawa hizi za antibiotiki ni Amoxycillin, Tetracycline na Doxycyline.
#5: Matumizi ya dawa kundi la corticosteroidi.
Hizi ni dawa ambazo hutibu maradhi mbalimbali yakiwemo pumu, mzio na uvimbe. Matumizi ya muda mrefu ya dawa hizi husababisha kupunguwa kwa kinga za mwili.#6: Unene na kitambi.
Wanawake wanene wako katika hatari ya kupata fangasi kutokana na sababu kuu mbili ambazo ni mabadiliko ya homoni na jasho.Jasho inayojificha katika mikunjo ya nyama za unene mwilini ni moja ya mazingira yanayochagiza ukuaji wa fangasi hawa.
Pili ni mabadiliko ya homoni ambayo ni moja ya chanzo kikubwa cha maradhi ya fangasi.
#7: Upungufu wa kinga mwilini.
Kupungua kwa kinga mwilini ni chanzo cha matatizo mengi ya afya ya mwili mojawapo ni tatizo la fangasi. Watu wenye UKIMWI huathiriwa zaidi na tatizo hili la fangasi kwa kuwa kinga zao za mwili ziko chini.#8: Matumizi ya nguo zenye unyevu na kubana.
Fangasi huzaliana zaidi katika hali ya unyevu na kiwango kidogo cha hewa ya oksijeni. Nguo za kupana huzuia sehemu ya mwili kufikiwa na hewa ya oksijeni, hewa hii pekee inaweza kuwa tiba bora ya fangasi.Dalili za fangasi ukeni
Zifuatazo ni dalili kuu ambazo huashiria kuathiriwa na fangasi ukeni;- Miwasho maeneo ya uke
- Michubuko na kuhisi uke kuwaka moto
- Maumivu wakati wa kujamiana au kukojoa
- Kunaweza kutengenezwa vidonda
- Ute mweupe ambao unaweza kuwa mzito au mwepesi
- Kupasuka kwa maeneo ya uke hasa mashavu ya uke
- Uvimbe katika mashavu ya uke wenye rangi ya wekundu
- Ngozi kubanduka hasa wakati wa kujikuna
Jinsi ya kutibu fangasi za ukeni.
Bila kujali ni kwa kiwango gani fangasi zimekuathiri ukeni, kuna njia nyingi na dawa ambazo unaweza kuzitumia kupambana na tatizo hili. Njia hizo zinaweza kuwa za kisasa au kienyeji.Njia za kisasa za kutibu fangasi ukeni
Njia hizi hutegemea na hatua ya maambukizi, ikiwa ni ya kawaida au ni fangasi sugu. Matibabu hutofautiana kulingana na aina ya fangasi.Fangasi za kawaida
Dawa zinazotumika zaidi ni fluconazole, miconazole, itraconazole na terconazole. Ambapo dawa hizi huweza kupatikana katika muundo wa vidonge vya kunywa, sindano , kupaka na vidonge vya kupachika ukeni.Dozi yake huwa ni kati ya siku 3 hadi 7 kulingana na maelekezo ya daktari au mfamasia..
Fangasi sugu za ukeni.
Dawa zinazotumika kutibu fangasi ya kawaida hutumika pia kutibu fangasi sugu lakini muda hutofautiana. Kwa fangasi sugu matibabu huweza kuchukua kati ya wiki 2 hadi miezi sita.Vilevile dawa hizi huweza kutumika katika mseto ambapo mgonjwa anatumia dawa zaidi ya moja kwa wakati mmoja. Mara nyingi dawa mseto za fangasi hutumiwa kwa namna ya vidonge vya kunywa.
Ikiwa fangasi ni sugu kiasi cha kushindwa kuitikia dawa basi dawa aina ya Boric acid hutumika kama mbadala. Dawa hii hutumiwa kwa kupachika ukeni na si kunywa.
Njia za kienyeji za kutibu fangasi.
Kuna njia kadhaa za kienyeji ambazo zimethibitishwa kutibu ama kupunguza fangasi wa ukeni. Baadhi ya njia hizo ni pamoja na;- Kitunguu saumu, kwa kupala au kupachika.
- Mwarobaini kupaka au kunywa.
- Aloe vera kupaka.
- Tangawizi na bizali kunywa au kupaka.
- Mdalasini kupaka.
Jinsi ya kujikinga na tatizo la fangasi ukeni.
Kuna njia na mambo kadhaa ambayo ukiyazingatia utapunguza uwezekano wa kupatwa na tatizo hili la fangasi ukeni.Baadhi ya njia hizo ni pamoja na;
- Kuepuka nguo za kubana na zenye unyevu
- Epuka matumizi ya vipodozi vya harufu ukeni
- Zingatia usafi binafsi hasa kipindi cha hedhi
- Epuka matumizi ya mara kwa mara ya Pad, tampoon na douches
- Tumia dawa za antibiotiki na corticosteroidi pale inapotakiwa tu
- Zingatia ushauri wa jinsi ya kupunguza tatizo wakati wa ujauzito
Hitimisho
Dalili zilizotajwa hapo juu hazitokani na maradhi ya fangasi pekee. Yapo maradhi kadhaa ambayo huweza kusababisha dalili hizi.Jambo bora na la pekee ni kufika kituo cha afya kwa ajili ya ushauri nasaha na kupima ili kupata uhakika wa chanzo cha dalili hizi ikiwa zinatokana na fangasi au matatizo mengine.