Dalili za bawasiri, aina zake na tiba.
Bawasili (kikundu) ni uvimbe unaotokea katika sehemu ya mfumo wa haja kubwa, uvimbe huu unatokana na kutuna kwa mishipa ya damu na huweza kutokea sehemu ya ndani ya mfereji wa haja kubwa au sehemu ya nje kuzunguka tundu la haja kubwa.
Tatizo la bawasili hujitokeza ikiwa ni matokeo ya kuharibiwa kwa tishu mbalimbali zilizopo katika mfereji wa haja kubwa.
Tatizo la bawasili hujitokeza ikiwa ni matokeo ya kuharibiwa kwa tishu mbalimbali zilizopo katika mfereji wa haja kubwa.
Tishu zinazoweza kuharibiwa ni pamoja na tishu za mishipa ya damu, tishu za neva, tishu za misuli na tishu zinazounda ukuta wa mfereji wa haja kubwa.
Kuharibiwa kwa tishu hizi kunapelekea kutengenezwa kwa uvimbe katika eneo hili la haja kubwa.
Bawasiri inasababishwa na nini?
Hakuna jibu la uhakikika ni kwa namna gani bawasiri hutokea lakini wataalamu wa afya wanakubaliana na nadharia ya kwamba kuharibiwa na kulegea kwa misuli hasa ile ya treitz ndio sababu kuu inayoweza kupelekea mtu kupata bawasiri.
Misuli hii ya Treitz ndio hushikilia tishu na seli mbalimbali katika maeneo haya ya haja kubwa zikiwamo zile za damu.
Kulegea kwa misuli hii kunafanya mishipa ya damu kupoteza uimara wake, hali hii inasababisha mishipa hiyo kujikunja na kufanya damu kupata ugumu wa kusafiri kiurahisi.
Kulegea kwa misuli hii kunafanya mishipa ya damu kupoteza uimara wake, hali hii inasababisha mishipa hiyo kujikunja na kufanya damu kupata ugumu wa kusafiri kiurahisi.
Jambo hili husababisha damu kutuama na kujaa maeneo ya haja kubwa kisha hutengeneza uvimbe.
Aina za bawasiri.
Bawasiri imegawanywa katika aina kuu mbili ambazo ni- Bawasiri ya ndani na
- Aina ya pili ni Bawasiri ya nje.
Takwimu zinaonyesha kuwa 80% ya wagonjwa hushambuliwa na bawasiri ya ndani, 5% hushambuliwa na bawasiri ya nje huku 15% ya wagonjwa hushambuliwa na bawasiri mchanganyiko, yaani zote za aina mbili kwa wakati mmoja.
Bawasiri ya ndani.
Aina hii ya bawasili hutokea wakati uvimbe unaotokana na mlundikano wa damu katika mishipa ya damu ya vena hutokea ndani ya mfereji wa puru/haja kubwa.Aina hii ni ngumu kuitambua kwa vile sehemu ya ndani ya mfereji wa haja kubwa haijafikiwa na seli za neva kwa kiasi kikubwa kama ilivyo sehemu za nje za puru.
Jambo hili kuwapo kwa kiwango kidogo cha neva ndani ya mfereji wa haja kubwa linafanya kuwe na ugumu wa kuhisi uvimbe, na pia ndio sababu kuu ya kwanini aina hii ya bawasiri haiambatani na maumivu.
Njia kuu ya kutambua aina hii ya bawasili ni kuwepo kwa damu katika kinyesi, damu ambayo hutokana na majeraha yanayotokea kutokana na mkandamizo mkubwa wa kinyesi wakati wa kujisaidia, au msuguano wa uvimbe na kuta za mfereji wa haja kubwa ambao husababishwa na baadhi ya shughuli za kila siku.
Mara chache sana mgonjwa huweza kupata maumivu ikiwa tu kumetokea jeraha kubwa ndani ya eneo la uvimbe au maeneo jirani na uvimbe. Na hii inaweza kusaidia kutambua tatizo kwa haraka zaidi.
Aina hii ya bawasiri imegawanywa katika makundi kulingana na ni kwa namna gani tatizo ni kubwa ama ni hatua ipi tatizo limefikia.
Njia kuu ya kutambua aina hii ya bawasili ni kuwepo kwa damu katika kinyesi, damu ambayo hutokana na majeraha yanayotokea kutokana na mkandamizo mkubwa wa kinyesi wakati wa kujisaidia, au msuguano wa uvimbe na kuta za mfereji wa haja kubwa ambao husababishwa na baadhi ya shughuli za kila siku.
Mara chache sana mgonjwa huweza kupata maumivu ikiwa tu kumetokea jeraha kubwa ndani ya eneo la uvimbe au maeneo jirani na uvimbe. Na hii inaweza kusaidia kutambua tatizo kwa haraka zaidi.
Aina hii ya bawasiri imegawanywa katika makundi kulingana na ni kwa namna gani tatizo ni kubwa ama ni hatua ipi tatizo limefikia.
Mgawanyiko huu ni kama ifuatavyo;
- Bawasiri ya ndani aina ya kwanza: Hii ni hatua ya awali ambapo uvimbe unakuwa ndani muda wote, haujitokezi kwa nje hata kama kumetokea msukumo mkubwa ndani ya mfereji wa haja kubwa, mfano wakati wa kutoa haja kubwa. Hatua hii Inaweza kuambatana na damu au isiambatane, unaweza kuitambua damu hiyo kupitia kitambaa safi.
- Bawasiri ya ndani hatua ya pili: Hii ni hatua ambapo uvimbe unakuwa ndani lakini unajitokeza nje ikiwa kuna msukumo/mgandamizo ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na uvimbe huu hujirudi wenyewe baada ya mgandamizo kuisha ama baada ya kumaliza kutoa haja kubwa. Hatua hii huambatana na damu kila mara uvimbe unapotoka nje.
- Bawasiri ya ndani hatua ya tatu: Hii ni hatua ambayo uvimbe unakuwa ndani lakini unajitokeza nje ikiwa kuna msukumo/mgandamizo ndani ya mfereji wa haja kubwa au uvimbe unaweza kujitokeza katika hali ya kawaida bila hata kuwapo kwa mgandamizo au msukumo. Uvimbe huu haujirudi wenyewe mpaka kwa msaada ama wa kidole au kifaa chochote kitumike kuusukuma ndani. Hatua hii huambatana na damu nyingi kila mara uvimbe unapotoka nje.
- Bawasili ya ndani hatua ya nne: Hatua hii tatizo huwa ni kubwa zaidi ambapo uvimbe unakuwa umejitokeza muda wote na hauwezi kurudi ndani hata kwa ukisukumwa kurudi ndani. Hatua hii huambatana na damu nyingi kiasi cha kusababisha nguo za ndani kulowa damu.
Bawasiri ya nje.
Aina hii ya bawasili hutokea wakati uvimbe unaotokana na mlundikano wa damu katika mishipa ya vena unatokea sehemu ya nje ya puru, yaani kuzunguka ncha ya mlango wa haja kubwa.Aina hii ni rahisi kuitambua kwa sababu uvimbe hujitokeza na kwa vile sehemu hii ya ncha ya puru imezungukwa na kiwango kikubwa cha seli za neva, uvimbe katika eneo hili huambatana na muwasho na maumivu makali.
Bawasiri ya nje pia imegawanywa katika hali kuu tatu kulingana na ukubwa wa uvimbe.
Bawasiri ya nje pia imegawanywa katika hali kuu tatu kulingana na ukubwa wa uvimbe.
Mgawanyiko huu ni kama ifuatavyo;
- Bawasili ya nje isiyokuwa na uvimbe unaoonekana: Katika aina hii ya bawasiri ya nje mgonjwa hupata muwasho na maumivu ya kawaida eneo la ncha za tundu la haja kubwa.
- Bawasiri ya nje iliyo na uvimbe: Katika aina hii ya bawasiri ya nje uvimbe unakuwa ni wa kawaida na umechukua eneo ambalo ni chini ya nusu ya mduara wa tundu la haja kubwa.
- Bawasili ya nje iliyo na uvimbe: Katika aina hii ya bawasiri ya nje uvimbe unakuwa ni mkubwa na umechukua eneo lote la mduara wa tundu la haja kubwa.
Dalili za bawasiri.
Katika hatua za awali si rahisi kugundua kwamba una tatizo la bawasili hasa ikiwa ni bawasili ya ndani.Lakini kuna ishara na viashiria vya awali kabisa ambavyo vinaweza kukusaidia kugundua tatizo hili.
Baadhi ya dalili muhimu za bawasiri ni pamoja na;
#1: Kutokwa na damu.
Hii ni dalili ya mwanzo kabisa ya bawasiri, damu inaweza kutoka kabla au baada ya kutoa haja kubwa.Damu kabla ya kutoa haja kubwa mara nyingi husababishwa na mazoezi au kazi ngumu na mara nyingi inapaswa kuwa nyekundu iliyokolea na kuelekea kuwa nyeusi ingawa si lazima.
Wakati mwingine damu huweza kuwa nyepesi na nyekundu iliyoiva, hii inaweza kuwa ni ishara ya uwepo wa tatizo linguine kama vile saratani ya utumbo mpana au uvimbe kwenye utumbo.
Wakati mwingine damu huweza kuwa nyepesi na nyekundu iliyoiva, hii inaweza kuwa ni ishara ya uwepo wa tatizo linguine kama vile saratani ya utumbo mpana au uvimbe kwenye utumbo.
Ikiwa kiwango cha damu ni kikubwa kiasi cha kuogofya basi ni vyema kuwahi kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi.
#2: Uwepo wa uvimbe.
Hii ni dalili ya muhimu zaidi, na ni kigezo kikubwa cha kutambua ni hatua gani tatizo limefikia.Kwa bawasiri ya ndani ni vigumu kutambua uvimbe huu ingawa unaweza kujitokeza wakati wa kutoa haja kubwa.
Lakini pia ikiwa unatokwa na damu au unahisi kuwashwa unaweza kujichunguza mwenyewe kujua ikiwa kuna uvimbe wowote katika mfereji wa haja kubwa kwa kutumia kidole.
Kwa bawasiri ya nje maumivu ni kigezo kiikubwa na unaweza kuyapata hata katika hatua za mwanzo kabisa za tatizo.
#3: Maumivu sehemu ya puru.
Si rahisi kupata maumivu hasa ikiwa ni bawasiri ya ndani ingawa inawezekana hasa ikiwa kuna majeraha au michbuko ndani ya mfereji wa haja kubwa.Kwa bawasiri ya nje maumivu ni kigezo kiikubwa na unaweza kuyapata hata katika hatua za mwanzo kabisa za tatizo.
#5: Muwasho hasa maeneo ya nje ya puru.
Kuwepo kwa uvimbe kunapelekea uzalishwaji wa ute. Ute huu huchochea muwasho katika maeneo ya puru.Muwasho katika maeneo haya unaweza kusababishwa pia na magonjwa mengine kama vile mzio, fangasi, saratani au kisukari.
#6: Kutokwa na uchafu.
Majimaji ya uchafu yaliyochanganyikana na ute au damu yanaweza kuonekana hasa katika hatua mbaya za tatizo.Uchafu huo huambatana na harufu mbaya. Kutokwa na uchafu huu inaweza kuwa ni ishara ya uwepo wa tatizo linguine kama vile fistula, uvimbe katika utumbo na ugonjwa ujulikanao kama Crohn.
#7: Haja kubwa mara kwa mara.
Kubanwa na haja kubwa mara kwa mara kunaweza kutokea hasa katika bawasiri ya ndani iliyofikia katika hatua mbaya.Ikiwa unabanwa na haja zaidi ya mara 4 kwa siku hili si jambo la la kawaida kwa mgonjwa wa bawasiri na inapaswa kuhudhuria kituo cha afya kwa uchunguzi zaidi.
Hizi ni sababu na dalili kuu za ugonjwa wa bawasiri, kufahamu jinsi ya kutibu tatizo hili soma makala hii:
Dawa ya bawasiri