Tatizo la miguu kuwaka moto, Chanzo, Dalili na Tiba
Miguu kuwaka moto ni tatizo ambalo linaweza kutokea kutokana na sababu mbalimbali za kiafya, lakini kubwa ni kudhoofika au kuharibika kwa seli za neva pembeni ya miguu.
Kwa sehemu kubwa matatizo ya neva kudhoofu au kuharibika husababishwa zaidi na kisukari na matumizi ya pombe kwa muda mrefu.
Seli za neva zilizoharibika au kudhoofika husababisha utumaji wa taarifa katika ubongo kuathiriwa, ambapo mara nyingi seli hizi zikipata hitilafu hutuma taarifa katika ubongo ambazo ubongo huzitafsiri kama maumivu.
Kwa sehemu kubwa matatizo ya neva kudhoofu au kuharibika husababishwa zaidi na kisukari na matumizi ya pombe kwa muda mrefu.
Seli za neva zilizoharibika au kudhoofika husababisha utumaji wa taarifa katika ubongo kuathiriwa, ambapo mara nyingi seli hizi zikipata hitilafu hutuma taarifa katika ubongo ambazo ubongo huzitafsiri kama maumivu.
Nini husababisha miguu kuwaka moto?
Mbali na kisukari na ulevi wa pombe, zipo sababu nyinginezo nyingi ambazo husababisha kudhoofu na kuharibika kwa seli hizi za neve mwilini, sababu hizo ni pamoja na;- Maradhi ya Kisukari
- Matumizi ya pombe ya muda mrefu
- Uchovu
- Matumizi ya kupita kiasi ya virutubisho vya vitamini B (mojawapo ni folic acid)
- Matumizi ya muda mrefu ya dawa za shinikizo la damu, Kisukari na Kifua kikuu.
- Matatizo ya mzio/aleji
- Uzito mkubwa
- Magonjwa ya ngozi, mfano fangasi
- Maradhi ya mfumo wa mzunguko wa damu kama vile kiharusi na kuganda kwa damu kwenye mishipa ya damu ya miguuni
- Kuwepo kwa sumu na kemikali sumu mwilini mfano Madini ya zebaki na shaba nyekundu.
- Upungufu wa vitamini B
- Maambukizi ya VVU na UKIMWI
- Sababu binafsi za kibaolojia za mwili
Dalili za ugonjwa wa miguu kuwaka moto
Ugonjwa huu una dalili nyingi zikiwemo:- Miguu kupata ganzi
- Kuhisi kuchomwa na kitu chenye ncha kali miguuni
- Kuhisi miguu kuwa na majimaji kwa ndani
- Joto kali maeneo ya miguuni
- Kuhisi kama unaungua miguuni
- Kushindwa kutembea au kusimama
- Maumivu makali ya miguu.
Jinsi ya kutibu tatizo la miguu kuwaka moto
Ili kutibu au kuleta nafuu ya tatizo la miguu kuwaka moto, unapaswa kufahamu chanzo cha tatizo.
Zipo sababu mbalimbali zinazosababisha tatizo hili, vivyo hivyo tiba zake pia hutofautiana.
Mgonjwa anapaswa kuzingatia mambo yafuatayo;
Vilevile unaweza kutumia vidonge maalumu vya virutubisho hivi vya vitamini B hasa vitamini B12, Vitamini B9 (folic acid) na Vitamini B6.
Zipo sababu mbalimbali zinazosababisha tatizo hili, vivyo hivyo tiba zake pia hutofautiana.
Tiba ya miguu kuwaka moto kwa watu wenye Kisukari
Kwa wanaosumbuliwa na tatizo hili kwa sababu ya kisukari, njia pekee ni kuhakikisha kiwango cha sukari kinakuwa katika mlinganyo sahihi.Mgonjwa anapaswa kuzingatia mambo yafuatayo;
- Zingatia lishe bora ambayo ni rafiki kwa wagonjwa wa kisukari.
- Hakikisha unatumia dawa kama inavyoelekezwa, inaweza kuwa ni vidonge au sindano za insulini.
Tiba ya miguu kuwaka moto inayotokana na upungufu wa vitamin B
Ikiwa tatizo linatokana na upungufu wa vitamini B mwilini basi unashauriwa kutumia vyakula vyenye kiwango kikubwa cha virutubisho hivi.Vilevile unaweza kutumia vidonge maalumu vya virutubisho hivi vya vitamini B hasa vitamini B12, Vitamini B9 (folic acid) na Vitamini B6.
Tiba ya miguu kuwaka moto inayotokana na Ulevi
Kuacha unywaji pombe kupita kiasi kunasaidia kuzuia uharibifu wa neva unaoendelea na inaruhusu neva hizi kupona.Tiba ya miguu kuwaka moto kwa wenye maradhi ya figo
Punguza matumizi ya kemikali katika vyakula au vinywaji, punguza sumu za mwili kwa kutumia vyakula kama matunda, na pia kunywa maji ya kutosha mara kwa maraTiba nyinginezo bila kujali chanzo
- Fanya mazoezi ya mwili kama kukimbia na Kutembea, vilevile fanya massage ya miguu mara kwa mara
- Punguza uzito uliopitiliza
- Tumia dawa za kisasa ikiwa tatizo lako ni kubwa
- Weka miguu yako katika maji ya vuguvugu yenye chumvi
- Tumia dawa za kutuliza maumivu haza zile za kuchua
- Tumia dawa au vyakula vinavyosaidia damu kusafiri kwa urahisi, mfano Asali mbichi, shubiri/aloe vera gel na limao vyote hivi huweza kutumika kwa kupaka.
Hitimisho
Matumizi ya dawa za kisasa kutibu tatizo la miguu kuwaka moto ni nyingi na hatari endapo zitatumika kiholela.Hakikisha unawasiliana na Mfamasia au daktari kwa ushauri zaidi wa aina gani ya dawa utumie na kwa kiwango gani.