Madhara ya kiungulia, sababu na tiba asili
Kiungulia ni tatizo katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula ambalo husababishwa na kucheuliwa kwa mchanganyiko wa tindikali na chakula kutoka tumboni kuelekea katika koo la chakula.
Tindikali hii ni salama ikiwa katika tumbo pekee kwa vile sehemu nyingine za mfumo wa mmen'enyo wa chakula hazina ukuta unaoweza stahimili tindikali hii.
Mchanganyiko huu wenye tindikali husababisha kuungua kwa koo la chakula jambo linalopelekea maumivu makali katika koo la chakula.
Koo la chakula na kiungulia.
Nyongo huzalisha tindikali iitwayo Hydrogen Chloride(HCl), tindikali hii ni kali kiasi cha kuyeyusha chuma.Tindikali hii huzalishwa na kusafirishwa tumboni ambako hutumika kusaidia kumeng'enywa kwa chakula, vilevile husaidia kuangamiza vimelea ambao wako katika chakula.
Tumbo limeundwa na ukuta au kiwambo madhubuti ambacho kina uwezo wa kuzuia tindikali hii isizifikie sehemu za ndani za tumbo na kuziharibu.
Tumbo limeundwa na ukuta au kiwambo madhubuti ambacho kina uwezo wa kuzuia tindikali hii isizifikie sehemu za ndani za tumbo na kuziharibu.
Iwapo tindikali hii haitadhibitiwa inaweza kuleta athari kubwa katika mfumo wa chakula. Vidonda vya tumbo ni moja ya athari kubwa za tindikali hii iwapo ulinzi unaotolewa na ukuta wa tumbo utateteleka.
Tindikali hii ni salama ikiwa katika tumbo pekee kwa vile sehemu nyingine za mfumo wa mmen'enyo wa chakula hazina ukuta unaoweza stahimili tindikali hii.
Moja ya sehemu ya mfumo ambao hushambuliwa zaidi na tindikali hii ni koo la chakula ambalo halijaundwa na ukuta stahimilivu dhidi ya tindikali.
Ikiwa tindikali hii itafika katika koo la chakula husababisha kuunguzwa kwa eneo hili na kupelekea maumivu makali mithili ya moto.
Kati ya tumbo na koo la chakula kuna mlango ambao unadhibiti upitaji wa vyakula kati ya tumbo na koo la chakula.
Kati ya tumbo na koo la chakula kuna mlango ambao unadhibiti upitaji wa vyakula kati ya tumbo na koo la chakula.
Kuathiriwa kwa mlango huu ndio hasa sababu kubwa ya kutokea kwa tatizo la kiungulia.
Yapo mambo mengi yanayoweza kuathiri utendaji kazi wa mlango huu, moja ya mambo hayo ni msukumo mkubwa wa chakula kutoka tumboni au kusinyaa na kutanuka kwa misuli inayothibiti ufungukaji wa mlango huo.
Kiungulia husababishwa na nini?
Tatizo la kiungulia huwapata watu aina zote bila kujali jinsia, rangi wala umri. Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kiungulia lakini kubwa ni kutumia vitu au vyakula ambavyo hupelekea kutengenezwa kwa tindikali nyingi zaidi tumboni.Baadhi ya mambo yanayosababisha tatizo la kiungulia ni:
- Vyakula ambavyo husababishwa kutengenezwa kwa tindikali nyigi kupita kiwango, mfano maharage, viazi na mihogo.
- Matumizi ya chumvi nyingi katika vyakula
- Ukosefu wa vyakula vyenye nyuzinyuzi kama vile mbogamboga na matunda.
- Matumizi ya pombe na kafeini, Kafeini hupatikana zaidi katika vinywaji vya kuongeza nguvu.
- Kitambi
- Kutojihusisha na mazoezi.
- Matumizi ya baadhi ya madawa kama vile dawa za pumu na usingizi.
Dalili kuu za kiungulia
- Maumivu wakati wa kumeza chakula.
- Kutapika na kichefuchefu mara kwa mara
- Maumivu ya kifua na tumbo
- Muwasho katika koo la chakula
- Harufu mbaya ya kinywa.
- Kupatwa na matatizo ya homa ya mapafu (nimonia).
Tiba ya kiungulia
Kiungulia kinaweza kutibiwa lakini pia unaweza kujikinga na hatari ya kupata kiungulia kwa kufanya mambo yafuatayo;Tiba za kisasa
Matumizi ya dawa za kisasa, hii ni kwa watu tayari wanaosumbuliwa na kiungulia, kuna dawa za aina tofauti za kutibu kiungulia ambazo hutofautiana kulingana na aina ya mgonjwa.Mfano wa dawa hizo ni omeprazole, rabeprazole, aluminum na Magnesium.
Tiba asili ya kiungulia
- Epuka vyakula ambavyo husababisha kiungulia kama chocolate, soda na juice zenye tindikali
- Usile chakula kingi kupita kiasi.
- Epuka kuvaa vitu vinavyobana tumbo baada ya kula mfano mshipi(mkanda wa suruali au sketi)
- Usilale kwa muda wa masaa 2-3 mara tu baada ya kula.
- Tumia tangawizi, juisi ya tofaa na papai.
- Tumia majivu ya mkaa.
Madhara ya kiungulia
Kutokutibu kiungulia ambacho hukushambulia mara kwa mara ni hatari kwa afya yako kwa vile huweza kusababisha matatizo yafuatayo;- Uvimbejoto sehemu za koo la chakula:ambao unaweza kusababisha vidonda na koo kupoteza uwezo wa kufanya kazi.
- Kutengenezwa kwa kovu katika koo la chakula ambako kunapelekea koo la chakula kupoteza uwezo wa kufanya kazi.
- Kubadilika kwa seli za koo la chakula kunakopelekea koo la chakula kupoteza asili yake. Tatizo hili kitaalamu huitwa Barrett's esophagus.
Hitimisho
Kiungulia ni moja ya matatizo ya kawaida sana kwa watu wa aina zote. Mara nyingi tatizo hili hujitokeza na kuisha lenyewe baada ya muda mfupi.
Ikiwa tatizo hili hukutokea mara kwa mara ni vizuri kufika kituo cha afya ili kuonana na mtaalamu wa afya kwa ajili ya ushauri zaidi.
Kuchelewa kutibu tatizo hili la kiungulia ni hatari kwa sababu tatizo hili huweza kupelekea ugonjwa hatari wa saratani ya koo.