Faida za vitamini C mwilini, madhara na vyakula vyenye vitamin C kwa wingi
Mwili wako unahitaji vitamini C katika kufanikisha kazi zaidi ya 300 mwilini mwako. Baadhi ya faida za Vitamini C mwilini ni kutengeneza collagen.
Collagen ni kiunganishi chenye nguvu ambacho hushikilia mifupa yako pamoja, huunganisha misuli yako kwenye mifupa, kuimarisha mishipa ya damu na huweka viungo vya mwili na ngozi yako katika hali nzuri.
Mwili wako hauwezi kutengenezwa collagen ikiwa hakuna vitamini C ya kutosha mwilini.
Collagen husaidia kurekebisha uharibifu wa aina mbalimbali katika mwili wako, ikiwemo kuponya majeraha ya kila aina kama vile,
Vilevile mwili wako hauwezi kutumia vitamini nyingine kama vile vitamini B bila bila kuwepo kwa Vitamini C.
Mfumo wako wa kinga unahitaji vitamini C nyingi ili kufanya kazi katika viwango vya juu.

- Mifupa iliyovunjika,
- Viungo vilivyoteguka,
- Vidonda
- Mipasuko ya ngozi
Vilevile mwili wako hauwezi kutumia vitamini nyingine kama vile vitamini B bila bila kuwepo kwa Vitamini C.
Mfumo wako wa kinga unahitaji vitamini C nyingi ili kufanya kazi katika viwango vya juu.
Ikiwa haupati vitamini C vya kutosha, uko uwezekano wa kuugua mara kwa mara na kuchelewa kupona ikiwa utapatwa na magonjwa.
Vilevile vitamini C inakusaidia kutibu ama kuleta nafuu katika magonjwa kadhaa ikiwemo
Mambo haya yote mawili yanamaanisha kwamba unahitaji vitamini C kila siku kupitia vyakula na virutubisho.
Unahitaji kiasi kisichopungua miligramu 10 za vitamini C kila siku ili kuepukana na tatizo la kutoka damu kwenye fizi ambalo ndio ishara kubwa ya upungufu wa vitamini C.
Ingawa unaweza kutumia kiasi cha hadi miligramu 500 kwa siku hasa ukiwa unasumbuliwa na maradhi mbalimbali ya mwili kama vile pumu.
Matumizi ya zaidi ya miligramu 500 za vitamini C kwa siku ni bora zaidi katika kutibu pumu kuliko kutumia dawa za pumu.
Jedwali linaloonesha viwango vya vitamini C kwa kila siku katika makundi mbalimbali ya watu
Viwango hivi ni kwa watu wasiovuta sigara, uvutaji huathiri kiwango cha vitamini C kwa asilimia zaidi ya 40 ya viwango vinavyohitajika mwilini kila siku.
Sigara huasababisha Vitamini C kuvunjwa na kutolewa kama takamwili kwa haraka zaidi kuliko kawaida
Ikiwa unavuta sigara, tumia kiasi kisichopungua miligramu 1,000 kila siku. Kiasi hiki pia kinaweza kusaidia kukukinga dhidi ya aina mbili za saratani ambazo huwaathiri zaidi wavuta sigara ambazo ni:
Kiseyeye ni ugonjwa ambao unasababishwa na upungufu wa vitamini C na kupelekea fizi kuvimba na kutoka damu.
Kuna vitamini C katika kila matunda na mboga za kijani.
Kikombe kimoja cha juisi ya matunda mabichi ya kakadu kina miligramu zaidi ya 2700 za Vitamini C, ikilinganishwa na miligramu 80 ambazo unaweza kuzipata kwenye chungwa la ukubwa wa kati.
Bila kujali umri, matumizi ya kila siku ya vitamini C yanaweza kuwa msaada katika kukupa ulinzi dhabiti juu ya matatizo mbalimbali ya kiafya.
Vilevile vitamini C inakusaidia kutibu ama kuleta nafuu katika magonjwa kadhaa ikiwemo
- Matatizo ya kisukari
- Mafua na kikohozi
- Kuimarisha afya ya uzazi kwa wanaume.
Kwanini Vitamini C ni muhimu mwilini?
Mwili wa binadamu hauwezi kutengeneza Vitamini C, vilevile Vitamini C ni mumunyifu katika maji, kwa hivyo haiwezi kuhifadhi kwenye mwili wako kwa muda mrefu.Mambo haya yote mawili yanamaanisha kwamba unahitaji vitamini C kila siku kupitia vyakula na virutubisho.
Unahitaji kiasi kisichopungua miligramu 10 za vitamini C kila siku ili kuepukana na tatizo la kutoka damu kwenye fizi ambalo ndio ishara kubwa ya upungufu wa vitamini C.
Ingawa unaweza kutumia kiasi cha hadi miligramu 500 kwa siku hasa ukiwa unasumbuliwa na maradhi mbalimbali ya mwili kama vile pumu.
Matumizi ya zaidi ya miligramu 500 za vitamini C kwa siku ni bora zaidi katika kutibu pumu kuliko kutumia dawa za pumu.
Jedwali linaloonesha viwango vya vitamini C kwa kila siku katika makundi mbalimbali ya watu
|
Kiwango kinachotakiwa cha vitamini C
mwili kwa makundi ya watu |
|
|
Miaka |
Dozi ya vitamini C katika miligramu |
|
0–0.5 |
30 |
|
0.5–1 |
35 |
|
1-3 |
40 |
|
4-6 |
45 |
|
7-10 |
50 |
|
11-14 |
50 |
|
Wanaume 15+ |
60 |
|
Wanawake 15+ |
60 |
|
Wajawazito |
70 |
|
Wanaonyonyesha |
95 |
Viwango hivi ni kwa watu wasiovuta sigara, uvutaji huathiri kiwango cha vitamini C kwa asilimia zaidi ya 40 ya viwango vinavyohitajika mwilini kila siku.
Sigara huasababisha Vitamini C kuvunjwa na kutolewa kama takamwili kwa haraka zaidi kuliko kawaida
Ikiwa unavuta sigara, tumia kiasi kisichopungua miligramu 1,000 kila siku. Kiasi hiki pia kinaweza kusaidia kukukinga dhidi ya aina mbili za saratani ambazo huwaathiri zaidi wavuta sigara ambazo ni:
- Saratani ya koromeo na
- Saratani ya koo la chakula.
Mahitaji ya vitamini C kwa makundi mbalimbali ya watu
- Wavutaji sigara: Kama ilivyoelezwa hapo awali, moshi wa sigara husababisha kupotea kwa vitamini C kwa haraka mwilini. Kwa hivyo unahitaji Vitamini C ya ziada ili kupambana na uharibifu unaofanywa na moshi katika seli. Kwa wavutaji unaweza kutumia zaidi ya miligramu 1000 ya vitamini C kila siku.
- Watu wenye kisukari: Vitamini C haiingii kwenye seli zako vizuri ikiwa una kisukari, kwa hivyo unahitaji kiwango kikubwa cha vitamini C kwa siku ili kufidia. Unashauriwa kutumia si chini ya miligramu 500 za vitamini C kwa siku.
- Una mzio au pumu: Ili Kupambana na athari za mzio na mashambulizi ya pumu, mwili hutumia kiwango kikubwa cha Vitamini C kwa hivyo unahitaji vitamini C ya ziada.
- Mgonjwa wa mafua: Mfumo wako wa kinga unahitaji Vitamini C nyingi hasa wakati unapigana na, ugonjwa. Kwa wagonjwa mbalimbali matumizi ya vitamini C yanapaswa kuwa makubwa.
- Watu waliofanyiwa upasuaji: Vitamini C husaidia kuponya majeraha na kupambana na maambukizi. Unashsuriwa kutumia vitamini C kwa wingi ikiwa umefanyiwa upasuaji.
- Msongo wa mawazo na sonona: Unapokuwa na msongo wa mawazo, Mifumo ya mwili wako hutumia Vitamini C kwa kiwango kikubwa, hivyo unahitaji kiwango kikubwa cha vitamini C kila siku.
- Watu wanaotumia dawa na wazee: Wazee wanahitaji vitamini C zaidi kwa ujumla, hasa ikiwa wanatumia dawa mbalimbali, kwa sababu dawa nyingi huathiri Ufyonzwaji wa Vitamini C mwilini.
- Wajawazito na wanaonyonyesha: Unahitaji vitamini C ya ziada ili kukidhi mahitaji ya mtoto na mama.
Dalili za upungufu wa vitamini C mwilini.
Ikiwa utakosa vitamini C kwa muda mrefu, unaweza kupata ugonjwa wa kiseyeye.Kiseyeye ni ugonjwa ambao unasababishwa na upungufu wa vitamini C na kupelekea fizi kuvimba na kutoka damu.
Dalili za upungufu wa vitamini C ni pamoja na;
- Uchovu
- Fizi kuvimba na kutoka damu
- Meno kulegea na kutoka
- Michubuko na vidonda mdomoni
- Vidonda na majeraha kuchelewa kupona
- Upungufu wa damu mwilini
- Kupoteza hamu ya kula
- Udhaifu wa misuli
- Kutoka damu puani
- Kuugua mara kwa mara
Vyakula vyenye vitamini C kwa wingi
Kwa bahati nzuri, Vitamini C hupatikana katika matunda na mboga nyingi za kawaida ambazo karibu kila mtu anaweza kuzipata kwa gharama nafuu kabisa.Kuna vitamini C katika kila matunda na mboga za kijani.
- Tikiti
- Mapera
- Maembe na
- Mapapai
- Machungwa
- Limao
- Acerola
- Zabibu
- Viazi
- Kakadu
- Nyanya
- Spinachi
- Broccoli
- Pilipili
Kikombe kimoja cha juisi ya matunda mabichi ya kakadu kina miligramu zaidi ya 2700 za Vitamini C, ikilinganishwa na miligramu 80 ambazo unaweza kuzipata kwenye chungwa la ukubwa wa kati.
Faida za vitamini C mwilini
- Kupunguza mafuta ya mwili
- Kuimarisha kinga ya mwili
- Kutibu mafua na homa
- Husaidia kutibu vidonda na Michubuko
- Kutibu vidonda mdomoni
- Huimarisha na kulinda afya ya mbegu za kiume
- Huleta nafuu kwa watu wenye matatizo ya macho
- Inasaidia kuondoa sumu ya shaba nyekundu mwilini hivyo kukukinga na maradhi ya damu
- Huzuia uwezekano wa kuzaa watoto njiti kwa kuwa huimarisha afya ya mfuko uliomuhifadhi mtoto tumboni
- Inasaidia kupambana na matatizo ya ngozi
- Inakuepusha na matatizo ya kutoka damu katika fizi
- Husaidia kukkukinga na matatizo ya mzio na pumu
- Hukulinda dhidi ya maradhi ya saratani
- Husaidia watu wenye ugonjwa wa kisukari
- Kuondoa sumu za mwili: Kazi ya kubwa ya Vitamini C ni kunasa chaji huru (sumu za mwili) na kuzibadilisha kabla hazijafanya uharibifu wa seli zako. Pia husaidia viantioksideshaji vingine vya mwili kufanya kazi kwa ufanisi, ikiwemo vitamini E.
- Kuzuia magonjwa ya moyo: Vitamini C ni muhimu katika kutibu na kuleta nafuu katika matatizo mbali mbali ya moyo na mzunguko wa damu kama shinikizo la damu.
Hitimisho
Vitamini C ni muhimu kwa mfumo wako wa kinga, tishu zinazounganisha mifupa, afya ya moyo na mishipa ya damu. Vilevile ni kirutubisho muhimu ambacho husaidia kupunguza sumu mwilini.Bila kujali umri, matumizi ya kila siku ya vitamini C yanaweza kuwa msaada katika kukupa ulinzi dhabiti juu ya matatizo mbalimbali ya kiafya.