Faida kuu za vitamini D mwilini na vyanzo vyake
Vitamini D ni moja ya virutubisho muhimu zaidi mwilini kutokana na kazi yake ya kusaidia kutengenezwa kwa mifupa, kuimarisha mfumo wa fahamu na kuimarisha kinga ya mwili.
Vilevile virutubisho hivi vya vitamini D vimeonyesha uwezo wa kuzuia na kupambana na maradhi ya saratani hususa ni saratani ya utumbo mpana wa chakula.
Ili madini joto ya kalisiumu yaweze kufyonzwa kutoka katika vyakula mbalimbali na kuingia mwili kwa ajili ya kutumiwa, mwili wako unahitaji vitamini D.
Vitamini D ndio inadhibiti ufyonzwaji wa madini joto ya kalisiumu katika mwili. Ikiwa mwili wako hauna vitamini D ya kutosha, basi kiwango cha madini joto ya kalisiumu pia kitakuwa chini.
Kutokana na umuhimu wa madini joto ya kalisiumu mwilini, upungufu wa madini haya huweza kusababisha matatizo yafuatayo;
Kimsingi tunaweza kuipata vitamini D katika vyakula lakini pia katika miili yetu.
Kuanzia jua la saa 12 asubuhi hadi saa 4 asubuhi na saa 11 jioni hadi saa 1 usiku ni muda mzuri zaidi.
Vitamini D3 inayotengenezwa katika ngozi husafirishwa hadi katika ini na figo ambako inabadilishwa katika muundo wa vitamini D, muundo ambao mwili huweza kuitumia moja kwa moja.
Ikiwa katika ini na figo, vitamini D3 hubadilishwa katika muundo wa vitamini D, huku kiwango kidogo kikibaki katika muundo wa vitamini D3.
Vitamini D ndani ya ini na figo husaidia kufyonza madini joto ya kalisiumu kutoka katika damu, huku kiwango kingine cha vitamini D kikipelekwa katika mfumo wa chakula ili kusaidia kufyonzwa kwa madini joto ya kalisiumu kutoka katika vyakula.
Vilevile baadhi ya vitamini D husafiri moja kwa moja katika mifupa ili kusaidia kutengenezwa kwa mifupa.
Katika vyakula virutubisho hivi huwa katika muundo wa vitamini D2 (ergocalciferol). Mwili wako pia una uwezo wa kufyonza na kubadili aina hii ya vitamini kisha kutumiwa mwilini.
Baadhi ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamini D ni pamoja na;
Kwa wazee kuanzia miaka 51 na kuendelea hali ni tofauti, kwa sababu kadri umri unavoongezeka uwezo wa mwili wako kutengenezwa vitamini D unapungua, hivyo unahitaji kupata vitamini hii kutoka katika vyakula au vidonge maalumu vya virutubisho hivi.
Upungufu wa vitamini D kwa watu wenye umri mkubwa ni moja ya sababu zinazopelekea kupata matatizo ya mifupa.
Ili kupunguza uwezekano wa kupata matatizo ya mifupa na stamina, watu wenye umri wa kuanzia miaka 55 wanashauriwa kutumia si chini ya 700iu za vitamini D sambamba na kiwango kisichopungua 500mg cha kalisiumu.
Zifuatazo ni dalili za upungufu wa vitamini D mwilini;
Makundi hayo ni kama ifuatavyo;
Tofauti na aina nyingine za vitamini, mwili wako ndio chanzo kikubwa cha virutubisho hivi kutokana na kwamba hakuna vyakula vingi vyenye vitamini D ambavyo unaweza kuvipata kirahisi.
Maziwa yaliyosindikwa kiwandani na mafuta ya Samaki ndio vyanzo vikuu vya vitamini D kutoka katika vyakula.
Hakikisha unakaa juani ili kusaidia mwili kutengeneza virutubisho hivi, na ikiwa uko katika kundi ambalo ni rahisi kupata upungufu wa virutubisho hivi kama ilivyoanishwa katika Makala hii, pata ushauri wa kitaalamu kutoka kwa mfamasia au daktari ili kupata msaada.
Vilevile virutubisho hivi vya vitamini D vimeonyesha uwezo wa kuzuia na kupambana na maradhi ya saratani hususa ni saratani ya utumbo mpana wa chakula.
Kwanini unahitaji vitamini D?
Ili mifupa ya mwili wako itengenezwe kwa ufanisi, unahitaji madini joto ya kalisiumu. Madini haya ndio husaidia kutengenezwa kwa mifupa mbalimbali ya mwili wako na meno.Ili madini joto ya kalisiumu yaweze kufyonzwa kutoka katika vyakula mbalimbali na kuingia mwili kwa ajili ya kutumiwa, mwili wako unahitaji vitamini D.
Vitamini D ndio inadhibiti ufyonzwaji wa madini joto ya kalisiumu katika mwili. Ikiwa mwili wako hauna vitamini D ya kutosha, basi kiwango cha madini joto ya kalisiumu pia kitakuwa chini.
Kutokana na umuhimu wa madini joto ya kalisiumu mwilini, upungufu wa madini haya huweza kusababisha matatizo yafuatayo;
- Matatizo ya mifupa
- Matatizo ya mfumo wa fahamu kama vile kupoteza kumbukumbu
- Ujazo mdogo wa mifupa, kwa wanawake tatizo hili huwasababishia ugumba
Chanzo kikuu cha vitamini D
Tofauti na aina nyingine za vitamini, vitamini D sio lazima uipate kwenye chakula pekee, mwili wako pia una uwezo wa kutengenezwa vitamini D kwa msaada wa mwanga wa jua.Kimsingi tunaweza kuipata vitamini D katika vyakula lakini pia katika miili yetu.
Vitamini D kutoka katika mwanga wa jua
Ili mwili wako uweze kutengenezwa vitamini d unahitaji kukaa katika mwanga wa jua kwa muda usiopungua dakika 10.Kuanzia jua la saa 12 asubuhi hadi saa 4 asubuhi na saa 11 jioni hadi saa 1 usiku ni muda mzuri zaidi.
Jinsi gani mwili hutengeneza vitamini D kutokana na jua?
Mwanga wa jua unapoifikia ngozi yako, hubadilisha aina fulani ya mafuta(rehemu) yaliyopo katika ngozi yako kuwa katika muundo wa vitamini D3 (cholecalciferol).Vitamini D3 inayotengenezwa katika ngozi husafirishwa hadi katika ini na figo ambako inabadilishwa katika muundo wa vitamini D, muundo ambao mwili huweza kuitumia moja kwa moja.
Ikiwa katika ini na figo, vitamini D3 hubadilishwa katika muundo wa vitamini D, huku kiwango kidogo kikibaki katika muundo wa vitamini D3.
Vitamini D ndani ya ini na figo husaidia kufyonza madini joto ya kalisiumu kutoka katika damu, huku kiwango kingine cha vitamini D kikipelekwa katika mfumo wa chakula ili kusaidia kufyonzwa kwa madini joto ya kalisiumu kutoka katika vyakula.
Vilevile baadhi ya vitamini D husafiri moja kwa moja katika mifupa ili kusaidia kutengenezwa kwa mifupa.
Vitamini D kutoka katika vyakula
Mbali na mwili kuwa na uwezo wa kutengenezwa vitamini D, tunaweza kuvipata virutubisho hivi katika baadhi ya vyakula.Katika vyakula virutubisho hivi huwa katika muundo wa vitamini D2 (ergocalciferol). Mwili wako pia una uwezo wa kufyonza na kubadili aina hii ya vitamini kisha kutumiwa mwilini.
Baadhi ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamini D ni pamoja na;
- Maziwa
- Samaki
- Mafuta ya samaki
- Maini
- Mayai
- Siagi
Ni kiasi gani cha vitamini D unahitaji kwa siku?
Kwa watu wenye umri kati ya miaka 0 hadi 45 wanahitaji kiasi kisichopungua 200iu, kiasi hiki kinaweza kupatikana kwa kukaa juani kila siku kwa muda usiopungua dakika 10.Kwa wazee kuanzia miaka 51 na kuendelea hali ni tofauti, kwa sababu kadri umri unavoongezeka uwezo wa mwili wako kutengenezwa vitamini D unapungua, hivyo unahitaji kupata vitamini hii kutoka katika vyakula au vidonge maalumu vya virutubisho hivi.
Upungufu wa vitamini D kwa watu wenye umri mkubwa ni moja ya sababu zinazopelekea kupata matatizo ya mifupa.
Ili kupunguza uwezekano wa kupata matatizo ya mifupa na stamina, watu wenye umri wa kuanzia miaka 55 wanashauriwa kutumia si chini ya 700iu za vitamini D sambamba na kiwango kisichopungua 500mg cha kalisiumu.
Upungufu wa vitamini D mwilini
Kulingana na uchache wa vyakula vyenye vitamini D kwa wingi, njia kuu ya kupata virutubisho hivi ni kupitia mwanga wa jua.Zifuatazo ni dalili za upungufu wa vitamini D mwilini;
- Kwa watoto, hupatwa na tatizo la matege.
- Maumivu ya mifupa mara kwa mara
- Ni rahisi kupata ajali za kuvunjika mifupa
Nani yuko katika hatari za kupata upungufu wa vitamini D?
Kuna baadhi ya makundi mbalimbali ya watu ambao wanaweza kupata tatizo la upungufu wa vitamini D kwa urahisi.Makundi hayo ni kama ifuatavyo;
- Wazee kuanzia miaka 55 na kuendelea: sababu kubwa ni kwamba mwili wako unapoteza uwezo wa kutengenezwa vitamini D.
- Watu ambao hapati jua mara kwa mara: jua ndio chanzo kikuu cha vitamini D, ikiwa haupati jua la kutosha kuna uwezekano ukapata upungufu wa vitamini D, hasa wamama wanaonyonyesha na wagonjwa wasiojiweza kutembea.
- Matatizo ya ini au figo: ikiwa ina matatizo katika ini au figo basi mwili wako hauwezi kubadili vitamini D3 katika muundo ambao mwili unaweza kutumia.
- Unatumia dawa za kupunguza mafuta: kama vile cholestyramine au colestipol dawa hizi huzuia ufyonzwaji wa vitamini D na vitamini nyinginezo katika mwili.
- Unatumia dawa za mzio/aleji: mfano cortisone, prednisone, na dexamethasone. Dawa hizi hupunguza kiwango cha vitamini D3 mwilini.
- Ikiwa unatumia dawa za kifafa: mfano phenobarbital, dawa hizi huathiri matumizi ya vitamini D mwilini.
- Ikiwa uko katika mpango lishe maalumu: mfano watu ambao hupunguza uzito na watu ambao hawatumii vyakula kutoka katika wanyama na sio watu wa kukaa juani.
- Walevi: pombe huzuia kufyonzwa kwa vitamini D kutoka katika utumbo na kuingia mwilini.
Faida za vitamini D mwilini
- Kuimarisha kinga ya mwili
- Hutibu na kuzuia maradhi ya saratani, hasa saratani ya utumbo mpana
- Inatibu matatizo ya ngozi kama vile vibarango
- Inaimarisha usikivu
- Inazuia matatizo ya matege kwa watoto
- Inapunguza matatizo ya mifupa
- Inasaidia kuwaka mlinganyo wa ujazo wa mifupa
Hitimisho
Vitamini D ni moja ya virutubisho muhimu na vya lazima mwilini kutokana na kazi yake muhimu ya kusaidia kutengenezwa kwa mifupa.Tofauti na aina nyingine za vitamini, mwili wako ndio chanzo kikubwa cha virutubisho hivi kutokana na kwamba hakuna vyakula vingi vyenye vitamini D ambavyo unaweza kuvipata kirahisi.