Dalili za mimba changa ya wiki moja hadi miezi mitatu
Dalili za mimba ni matokeo ya mabadiliko makubwa ya kiumbo na kibaolojia yanayotokea kwa mama mjamzito ambayo husababishwa na kutengenezwa kwa placenta na kijusi.
Katika kufahamu ni mabadiliko yapi ni ya kawaida na yapi si ya kawaida, vipindi vya ujauzito vimewekwa katika hatua kuu tatu ambapo kila hatua ina aina fulani ya mabadiliko ya kimwili na kibaolojia ambayo ni ya kawaida na mjamzito anapoyaona hapaswi kuwa na wasiwasi.
Wakati mwingine tumbo linaweza kuwa kubwa upande mmoja tu, ikiwa hii hujitokeza ndani ya wiki 8 za mwanzo, basi fahamu ya kwamba hali hii ni kawaida na mabadiliko haya huisha baada ya kuingia kipindi cha pili cha mimba.
Mabadiliko haya huanza siku ya kwanza ya mimba kutungwa na kuendelea kadri mimba inavyokuwa.
Mabadiliko haya huambatana na dalili mbalimbali za mimba, dalili ambazo zinatupatia ishara ya kwamba maendeleo ya mtoto tumboni ni salama.
Kwa mama mjamzito, zipo dalili mbalimbali ambazo ni lazima atazionesha katika hatua mbalimbali za kipindi chake cha ujauzito.
Dalili za mimba zinapaswa kuwa ni za kawaida na ambazo zinatarajiwa. Lakini kuna wakati mjamzito anaweza kuona dalili za mimba zisizo za kawaida, katika hali hii unatakiwa kuhudhuria kituo cha afya haraka iwezekanavyo.
Katika kufahamu ni mabadiliko yapi ni ya kawaida na yapi si ya kawaida, vipindi vya ujauzito vimewekwa katika hatua kuu tatu ambapo kila hatua ina aina fulani ya mabadiliko ya kimwili na kibaolojia ambayo ni ya kawaida na mjamzito anapoyaona hapaswi kuwa na wasiwasi.
Vipindi hivyo ni kama ifuatavyo;
- Kipindi cha kwanza cha ujauzito – hiki hujumuisha miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito.
- Kipindi cha pili cha ujauzito – hii huusisha miezi mitatu ya pili ya ujauzito yaani mwezi wanne wa ujauzito hadi mwezi wa sita.
- Kipindi cha tatu cha ujauzito – hiki hujumuisha miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito kuelekea kujifungua yaani mwezi wa saba hadi wa tisa.
Dalili za mimba changa ya kuanzia wiki1 hadi miezi 3
Zifuatazo ni dalili za mimba changa ya kuanzia siku moja hadi miezi mitatu.
Baada ya mimba kutungwa katika mfumo wa uzazi wa mjamzito, homoni kuu mbili hutawala mfumo huo, ambazo ni progesterone na eostrogen, homoni hizi hupelekea mabadiliko yafuatayo katika mfumo wa uzazi.
Baada ya mimba kutungwa katika mfumo wa uzazi wa mjamzito, homoni kuu mbili hutawala mfumo huo, ambazo ni progesterone na eostrogen, homoni hizi hupelekea mabadiliko yafuatayo katika mfumo wa uzazi.
01: Tumbo kuwa gumu na kiuno kutanuka
Mfuko wa uzazi hutanuka na kuimarika kwa ajili ya kupokea na kutunza kijusi.Baada ya kijusi kufika katika mfuko wa uzazi tumbo hutanuka na kuongezeka ukubwa, hali hii hupelekea kuwa gumu na kuanza kuonekana.
Hii hutokea kati ya wiki ya 6 hadi 8 ya ujauzito.
Wakati mwingine tumbo linaweza kuwa kubwa upande mmoja tu, ikiwa hii hujitokeza ndani ya wiki 8 za mwanzo, basi fahamu ya kwamba hali hii ni kawaida na mabadiliko haya huisha baada ya kuingia kipindi cha pili cha mimba.
02: Kutokwa na damu au ute mzito
Kutokwa na damu au ute mzito ambao unaweza kuwa na rangi ya njano, maziwa, kijani au mweupe, inategemea umechanganyikana na nini.
Hii husababishwa na kuundwa kwa mishiba ya damu kwa wingi zaidi katika mfuko wa uzazi, mlango wa kizazi na uke ambapo mishipa hii huwa na lengo la kusaidia ufikishaji wa chakula na hewa kwa kijusi kinachokua.
Kuna wakati mishipa hii hupasuka na kusababisha damu kutoka, usitishike na neno kupasuka, ni jambo la kawaida na mishipa inayopasuka ni midogo kiasi kwamba damu inayopotea kutokana na mishipa hii kutanuka ni ndogo na haiwezi kuleta tatizo lolote.
03: Kukosa hedhi
Kukosa hedhi, hii hutokana na uwepo wa homoni za progesterone na eostrogen ambapo uwepo wao unazuia upevushwaji wa yai lingine.04: Matiti kujaa na chuchu kuvimba
Matiti kujaa na chuchu kuvimba huku zikitengeneza mfano wa vipele vidogo vyenye rangi nyeusi. Hii huanza kutokea kati ya wiki ya 6 hadi 8 ya ujauzito.05: Uchovu na maumivu ya mwili wakati wa asubuhi
Uchovu na maumivu ya mwili wakati wa asubuhi husababishwa na kuongezeka kwa homoni ya HCG.06:Kukosa hamu ya kula na kupata haja kubwa
Ongezeko la homoni ya progesterone kunapunguza kutanuka na kusinyaa kwa misuli ya tumbo hii hupelekea mmeng’enyo wa chakula kuwa chini, mama kukosa hamu ya kula na kupata haja kubwa ngumu.
06: Kichefuchefu, kiungulia na kutapika
Homoni ya HCG husababisha kulegea kwa mlango kati ya koo la chakula na hewa hivyo vyakula kutoka tumboni hupata urahisi wa kutoka ambayo ni sababu kuu ya kupata kichefuchefu, kiungulia na kutapika.
07: Kukojoa mara kwa mara
Kibofu na mfuko wa uzazi viko karibu, Ukuaji wa mfuko wa uzazi hutanuka kiasi cha kuminya kibofu.Hii inapunguza uwezo wa kawaida wa kibofu kuhimili kiwango cha mkojo na uwepo wa kiwango kidogo tu cha mkojo kunajaza kibofu.
08: Kizunguzungu na maumivu ya kichwa
Mabadiliko ya jumla ya homoni hupelekea kusinyaa kwa misuli inayozunguka mishipa ya damu, hii husababisha msukumo wa damu sehemu mbalimbali za mwili kuwa chini.Msukumo wa damu kuwa chini husababisha maumivu ya mwili, uchovu, maumivu ya kichwa na kujihisi mzito. Msukumo wa damu hutajwa kupungua kwa kati ya 5mmHg hadi 10mmHg.
Lakini hali hii hutoweka kuanzia wiki ya 5 ya ujauzito na kuendelea.
09: Mwili kufa ganzi na uchovu
Katika hatua za awali za mimba kuna ongezeko la utengenezwaji wa kemikali za relaxin, kemikali hizi hupunguza utendaji kazi wa misuli na uwezo wa ujongeaji wa maungio ya mwili.Hii husababisha maumivu katika maungio hususa ni kiunoni hasa wakati wa kulala au wakati mjamzito anapokuwa amekaa.
10: Joto kali na kutokwa jasho
Kutokana na kuongezeka kwa mishipa ya damu ili kukidhi mahitaji ya ukuaji wa mtoto, utendaji kazi wa mwili wa mjamzito huongezeka kwa ujumla ambapo hupelekea joto la mwili kuwa juu.Kutokana na sababu hii ni kawaida kwa mama mjamzito kulalamika joto kali.
11: Miguu kujaa maji na mwili kuvimba
Ongezeko la homoni za estrogen, progesterone, aldosterone, na Vasopressin kunasababisha kupungua kwa kasi ya utoaji maji mwilini, hii inapelekea maji kuwa mengi katika seli na kusababisha mjamzito kuvimba mwili mzima hasa sehemu za miguuni.12: Homoni ya HCG
Homoni nyingi huzalishwa wakati wa ujauzito mojawapo ni hii itwayo Human chorionic gonadotropin(HCG).Homoni hii hufanya kazi ya kulinda ukuaji wa mtoto na kuhakikisha kinga za mwili za mjamzito zinabaki katika kiwango kinachotakiwa. Homoni hii huanza kutengenezwa mara tu mimba inapotungwa kwa wanawake wengi homoni hii huanza kutengenezwa ndani ya siku 14 baada ya mimba kutunga.
Homoni hii ya Human chorionic gonadotropin, ndio hutumiwa kama kigezo kikuu cha kutambua kwamba mimba imetungwa.
Homoni hii ya Human chorionic gonadotropin, ndio hutumiwa kama kigezo kikuu cha kutambua kwamba mimba imetungwa.
Unapokwenda Duka la dawa kununua kipimo cha mimba cha Tshs 500 basi unapima uwepo wa homoni hii mwilini.
Hitimisho
Baada ya mimba mabadiliko mengi hujitokeza kwa wanawake, si kila mwanamke ataonyesha dalili zote zilizotajwa katika makala hii.
Kuna baadhi ya dalili hutokea kwa baadhi ya wanawake, ingawa kwa asilimia kubwa dalili za mimba zilizotajwa katika makala hii huwatokea zaidi ya asilimia 90 ya wanawake wote wanopata mimba.
Endapo umebainika kuwa na mimba, hakikisha unahudhuria kliniki kwa ajili ya huduma za mama na mtoto ili kujikinga na athari mbalimbali za kiafya ambazo zinaweza kujitokeza, ikiwemo kupata chanjo muhimu kwa ajili ya mjamzito na ushauri sahihi wa utunzaji mimba.