Jinsi ya kuzuia na kutibu upungufu wa nguvu za kiume kwa haraka

Tatizo la upungufu wa nguvu za kiume linaweza kupunguzwa au kutibiwa kwa namna tofauti. Tiba yake yaweza kuwa ya kutumia vidonge vya kumeza, mitishamba na vyakula, kutumia dawa za kupaka, dawa za kupachika au upasuaji.

Aina gani ya tiba inafaa inategemea na ukubwa wa tatizo na matakwa ya mgonjwa. Dawa nyingi za kutibu tatizo hili isipokuwa upasuaji hazimalizi tatizo bali huleta nafuu.

Kwa baadhi ya wanaume mkusanyiko wa matibabu maalumu ambayo huweza kuhusisha matumizi ya dawa yanaweza kuwasaidia na kumaliza kabisa tatizo.

Kutibu na kumaliza tatizo hili la upungufu wa nguvu za kiume unawezekana kwa kundi la wanaume ambao wanasumbuliwa na tatizo hili kwa sababu zifuatazo.

  • Tatizo linaambatana na sababu za kisaikolojia.
  • Ikiwa tatizo limesababishwa na maradhi katika mfumo wa tezi.
  • Tatizo limetokana na ajali ya kawaida.

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume

01: Matibabu yanayohusisha Matumizi ya dawa.

Katika kutibu au kuleta nafuu ya tatizo hili muathirika anaweza kutumia dawa za kisasa ama dawa za enzi (mitishamba) katika kukabiliana na tatizo hili.

1.1: Matumizi ya Dawa za kisasa za kuongeza nguvu za kiume.

Kwa sasa kundi linalotumiwa zaidi kutibu tatizo hili ni lile linalozuia ufanyaji kazi wa kemikali ya phosphodiesterase type 5 (PDE5).

Kwa kuzuia utendaji kazi wa kemikali hii kunasaidia kusinyaa kwa misuli ya uume kwa muda mrefu.

Hii husaidia damu kufika katika uume na kubaki huko kwa muda wote ambao kemikali hii ya phosphodiesterase type 5 (PDE5) imezuiwa.

Baada ya dawa kuisha mwilini, kemikali hii huendelea na kazi yake ya kawaida na kusababisha misuli kukaza na damu kuondolewa katika uume. 

Kwa hivyo kundi hili la dawa halitibu tatizo bali huleta nafuu ya muda.

Baadhi ya dawa katika kundi hili ni 

  • Sildenafil (Viagra), 
  • Vardenafil na 
  • Tadalafil (Cialis).

Dawa hizi zinapaswa kutumiwa kwa uangalizi mkubwa kwa watu wenye maradhi ya moyo, shinikizo la damu na kisukari kwa vile zinaweza kusababisha matatizo makubwa.

1.2: Matumizi ya dawa asili za kuongeza nguvu za kiume.

Baadhi ya mitshamba ambayo imethibitishwa kitaalamu kutibu tatizo la upungufu wa nguvu za kiume ni pamoja na;

  • mmea wa Ginseng,
  • saw palmetto 
  • Tangawizi na bizari
  • Eccommia
  • Gingko biloba
  • madini ya zinc.
  • virutubisho vyenye DHEA  ambavyo hupatikana kwa wingi katika magimbi.
  • virutubisho vya L-Arginine na pycnogenol ambavyo hupatikana kwa wingi katika tikiti.

Pia matibabu maalumu yajilikanayo kama acupuncture yana msaada mkubwa kwa wanaume wenye tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

02: Matibabu yanayohusisha mazoezi maalumu.

Mazoezi maalumu kama vile kegel yana msaada mkubwa zaidi katika kukusaidia kuondokana na tatizo hili. 

Zoezi hili huimarisha misuli ya uume na ile ya pelvic plexus ambavyo vina mchango mkubwa katika kusimama kwa uume.

03: Matibabu ya kisaikolojia.

Matibabu ya kisaikolojia mara nyingi hayatumii dawa inga kuna wakati yanaweza yakahusisha dawa.

Namna pekee ya kutibu upungufu wa nguvu za kiume kwa njia hii ni kutambua ni jambo gani ndio sababu kuu ya tatizo kwako.

Mara nyingi ushauri nasaha unatosha kuwa tiba ya tatizo hili ikiwa limesababishwa na saikolojia.

Vilevile aina hii ya matibabu inaweza kutumika sambamba na vifaa maalumu au dawa.

Jinsi ya kutambua kuwa tatizo lako ni la kisaikolojia na linahitaji tiba ya kisaikolojia.

  • Mara nyingi tatizo hujitokeza ghafla bila chanzo cha kueleweka.
  • Ikiwa una umri chini ya miaka 30 na tatizo limetokea ghafla.
  • Tatizo hutokea kwa vipindi tofauti na kuna wakati halionekani.
  • Tatizo linatokea kwa baadhi ya wanawake.

Ikiwa tatizo lako hutokea katika namna zilizotajwa hapo juu basi matibabu ya kisaikolojia yanaweza kukusaidia.

Kumbuka matibabu ya kisaikolojia ni magumu zaidi kutokana na utayari wa muathirika na pengine uelewa wa muathiri juu ya jambo ambalo linamsumbua na kupelekea hali hiyo.

04: Matibabu ya homoni.

Homoni ya testosterone hufanya kazi kubwa katika kusaidia ufanyaji kazi wa mfumo wa uzazi wa mwanaume.

Moja ya kazi kubwa ni kusaidia kuongeza ashki ya kujamiana. Kupungua kwa homoni hii kunasababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Kwa wanaume wanaosumbuliwa na upungufu wa nguvu za kiume kutokana na kupungua kwa homoni hii wanaweza kutibiwa kwa kupewa dawa za homoni hii.

Dawa za homoni hii hupatikana katika namna ya vidonge, kupaka, kupachika na sindano.

Wanaume wenye umri mkubwa, kupungua kwa homoni ya testosterone ni moja ya sababu zinazochangia tatizo hili. 

Hii inatokana na kwamba kadri umri unavyokuwa mkubwa kiwango cha homoni hii hupungua mwilini pia.

05: Matumizi ya alprostadil.

Dawa ya alprostadil ambayo huchomwa moja kwa moja katika tishu za uume ( tishu za cavernosa au mirija ya manii). Dawa hii husaidia misuli kusinyaa na kuruhusu damu kuingia katika uume.

Njia hii huweza kuleta madhara yafuatayo:

  • maumivu, 
  • kuharibika kwa muundo wa uume na 
  • kutokwa damu katika mrija wa manii.

06: Njia ya kutumia kifaa cha vacuum.

Kifaa hiki ni mithiri ya chupa ambamo uume huingizwa na hewa iliyo ndani ya chupa hizo huvutwa kutoka nje.

Wakati hewa inatoka damu huvutwa kuelekea katika uume. Uume ukisha simama mpira maarumu unafungwa katika shina la uume kuzuia uume kusinyaa.

Madhara ya njia hii ni pamoja na:

  • michubuko, 
  • kuharibika kwa mishipa ya damu katika uume na 
  • kushindwa kutoa shahawa kwa uhuru.

07: Kupandikiza tishu ngumu ndani ya uume.

Njia hii hutumiwa kwa wanaume ambao tatizo limefika hatua kubwa zaidi. Tishu maalumu zenye vifuko kwa ndani hupandikizwa katika uume.

Kisha kimiminika maalumu (saline) hujazwa katika vifuko hivyo kila wakati mwanaume anapotaka kujamiana. Vifuko hivi vinapojaa uume huimarika na kuwa mgumu tayari kuingia katika uke.

Moja ya hatari kubwa ya tiba hii ni tishu hizi kuozea ndani ya uume jambo linaloweza kuleta madhara makubwa.

08: Matibabu ya upasuaji.

Hii ni njia bora kwa wanaume ambao tatizo limetokana na ajali au kuzaliwa nalo. 

Ikiwa kuna namna yeyote ya kulisahihisha kwa njia ya upasuaji basi hii ni njia bora zaidi na mara nyingi njia hii hutibu na kumaliza kabisa tatizo.

Mfano upasuaji wa kuziba mishipa ya damu ya ateri katika uume.

Mambo ya kuzingatia ili kumaliza tatizo la nguvu za kiume

  • Thibiti mambo hatarishi yanayosababisha upungufu wa nguvu za kiume: Mambo hayo ni Pamoja na kisukari, shinikizo la damu na kiwango cha mafuta mwilini. Vilevile kuepukana na sonona inakuepusha na tatizo hili.
  • Badili mwenendo wa Maisha usiyo Rafiki: Kuepukana na mkazo, epuka matumizi makubwa ya pombe na sigara, zingatia lishe bora, msongo wa mawazo na mazoezi. Vilevile kupumzika, kuwa mwaminifu, kujiamini, kuzungumza na mwenza wako vinaweza kuwa na msaada mkubwa kwako na kukukinga na tatizo hili.

Hitimisho

Ili kutibu tatizo la nguvu za kiume ni vizuri kufahamu chanzo cha tatizo lako kwa sababu si kila njia inaweza kuwa na ufanisi.

Hata hivyo tatizo hili la nguvu za kiume kwa sehemu kubwa husababishwa na mitindo ya maisha na saikolojia.

Ikiwa tatizo lako limesababishwa na sababu za kisaikolojia au mitindo mibovu ya maisha, vyakula, mazoezi na mitishamba ni njia bora zaidi ya kupambana na tatizo hili.

Next Post Previous Post
No Comment
Andika Swali au Maoni
comment url