Ugonjwa wa PID ni nini? Je, ni nani yuko hatarini kupata PID kiurahisi?
Je, unapenda siku moja kuitwa mama? Bila shaka hii ni doto ya kila mwanamke. Lakini unafahamu ya kwamba kuna adui ambaye anaweza kuharibu ndoto zako kiurahisi bila wewe kujua? Adui huyu ni
Njia kuu ni kwa kufanya ngono isiyo salama na mtu ambaye tayari anameathirika na bakteria hawa.
ugonjwa wa PID.
Ni mkusanyiko wa maradhi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke. Maradhi haya huanzia katika shingo ya kizazi na baadae kuenea maeneo ya ndani ya mfumo wa uzazi kama vile ukuta wa tumbo la uzazi, milija ya falopia na ovari.
Kwa sasa ni moja ya tatizo kubwa linalowaacha wanawake wengi na ugumba. Tatizo hili ni hatari kwa kwa sababu dalili zake huonekana wakati tayari mwanamke ameshapoteza uwezo wake wa kuzaa.
Mbali na kupoteza uwezo wa kuzaa pia tatizo hili husababisha kuharibika ama kutoboka kwa milija ya falopia na kutunga usaha katika ovari.
Tatizo hili la PID huwaathiri wanawake wote lakini huwaathiri zaidi wanawake kati ya miaka 18 hadi 30 na wanawake ambao hutumia vidonge kama njia ya uzazi wa mpango.
Pelvic inflammatory disease (PID) ni mkusanyiko wa maradhi katika mfumo wa uzazi ambayo huanzia katika shingo ya kizazi na kuenea maeneo ya ndani ya mfumo wa uzazi wa mwanamke.
Tatizo hili husababishwa na bakteria mbalimbali lakini zaidi ya asilimia 95 ya tatizo hili husababishwa na bakteria wa aina mbili ambao ni;
Kwa sasa ni moja ya tatizo kubwa linalowaacha wanawake wengi na ugumba. Tatizo hili ni hatari kwa kwa sababu dalili zake huonekana wakati tayari mwanamke ameshapoteza uwezo wake wa kuzaa.
Mbali na kupoteza uwezo wa kuzaa pia tatizo hili husababisha kuharibika ama kutoboka kwa milija ya falopia na kutunga usaha katika ovari.
Tatizo hili la PID huwaathiri wanawake wote lakini huwaathiri zaidi wanawake kati ya miaka 18 hadi 30 na wanawake ambao hutumia vidonge kama njia ya uzazi wa mpango.
Ugonjwa wa PID ni nini?
P.I.D ni kifupi cha neno la kiingereza Pelvic inflammatory disease (PID).
Tatizo hili husababishwa na bakteria mbalimbali lakini zaidi ya asilimia 95 ya tatizo hili husababishwa na bakteria wa aina mbili ambao ni;
- Neisseria gonorrhoeae: Kundi hili la bakteria husababisha ugonjwa maarufu wa zinaa ujulikanao kama Gono. Bakteria hawa huishi vizuri katika maeneo yenye joto na unyevu. N. gonorrhoeae anaweza kuathiri sehemu mbalimbali za mwili kama vile milija ya mkojo, koo la chakula, macho na maeneo ya puru. Kwa wanaume bakteria huyu huweza kuathiri epididimisi, kifuko maalumu cha kuhifadhia mbegu za kiume baada ya kutengenezwa.
- Chlamydia trachomatis: C. trachomatis ni aina ya bakteria ambaye anasababisha ugonjwa maarufu wa zinaa ujulikanao kama Clamydia. Bakteria huyu pia anaweaza kuathiri sehemu zote kama ilivyo kwa bakteria wa gono isipokuwa koo la chakula.
Ugonjwa wa PID huambukizwa kwa njia gani?
PID inaweza kuambukizwa kwa njia yoyote ambayo itapelekea bakteria hawa kuingia katika mfumo wa uzazi wa mwanamke.Njia kuu ni kwa kufanya ngono isiyo salama na mtu ambaye tayari anameathirika na bakteria hawa.
Baadhi ya njia nyinginezo ambazo PID inaweza kusambaa ni kupitia;
- Matumizi ya taulo za kike ambazo zimechanganyikana na bakteria.
- Kutoa mimba kwa kutumia mikasi ambayo yaweza kuwa imechanganyikana na bakteria.
- Kupitia mikono, kujishika maeneo ya uke bila kuosha mikono ikiwa mikono yako ina bakteria hawa.
- Kugusana kwa machozi na uke, ikiwa machozi yanatoka kwa mtu mwenye gono ya machoni.
Ni watu gani wako katika hatari ya kupata tatizo la PID.
Wanawake wote wako katika hatari ya kupata PID ingawa kuna baadhi ya makundi ya wanawake wako katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu wa PID.Makundi hayo ni kama yafuatayo;
Wanawake wanaojihusisha na biashara ya kuuza mwili.
Hili ni kundi ambalo liko katika hatari ya kupata magonjwa ya kila namna ikiwemo gono ambayo ndio chanzo kikuu cha PID.Wanawake hawa walio wengi hufanya ngono isiyosalama kwa vile hutanguliza zaidi maslahi kuliko afya zao.
Walio wengi hujikuta wakishiriki ngono bila kujitambua na kuwafanya kuwa kundi lililo katika hatari ya kupata maradhi ya gono au chlamydia.
Vilevile kiwango kikubwa cha homoni za estrogen kinasababisha kutengenezwa kwa ute mwingi kupita kiasi katika shingo ya kizazi. Ute huu hutoa mazingira mazuri kwa manii na bakteria kupenya kwa urahisi.
Wanawake wanaotumia pombe na madawa ya kulevya.
Kundi hili la wanawake hufanya mambo kwa misukumo ya pombe na madawa. Si rahisi kwa kundi hili kudhibiti usalama wao hasa linapokuja suala la ngono.Walio wengi hujikuta wakishiriki ngono bila kujitambua na kuwafanya kuwa kundi lililo katika hatari ya kupata maradhi ya gono au chlamydia.
Wanawake wenye umri mdogo.
Tafiti zinaonyesha wanawake walio na umri wa kati ya miaka 15 hadi 25 ndio kundi linaloathiriwa zaidi na PID. Kuna sababu kuu mbili za kwanini kundi hili liko katika hatari;Kwanza ni sababu za kibaolojiaa:
- Kiwango kikubwa cha homoni za Estrogen.
Vilevile kiwango kikubwa cha homoni za estrogen kinasababisha kutengenezwa kwa ute mwingi kupita kiasi katika shingo ya kizazi. Ute huu hutoa mazingira mazuri kwa manii na bakteria kupenya kwa urahisi.
Pili ni sababu za kibinafsi na tabia
- Hulka na mihemko ya kujamiana.
Tabia hii huwaweka katika hatari ya kupata magonjwa ya zinaa ikiwamo gono na chlamydia.
Ni jambo zuri lakini tafiti zinaonyesha baadhi ya manukato hayo yana kemikali ambazo huua bakteria na fangasi wa akiba ukeni ambao husaidia ulinzi wa uke.
Kufa kwa bakteria na fangasi hawa ambao ni wa faida ukeni kunapunguza ulinzi wa uke na kuweka uke katika mazingira ya kufikiwa na bakteria wa gono na chlamydia kiurahisi.
Kwa wanawake hawa kiwango cha estrogeni huwa ni kikubwa na kupelekea ute mwingi kuzalishwa eneo la mlango wa kizazi.
Wanawake wanaotumia Douches.
Kuna kundi kubwa la wanawake ambao huosha uke kwa sabuni za kunukia na kupaka manukato ukeni ili kupunguza harufu.Ni jambo zuri lakini tafiti zinaonyesha baadhi ya manukato hayo yana kemikali ambazo huua bakteria na fangasi wa akiba ukeni ambao husaidia ulinzi wa uke.
Kufa kwa bakteria na fangasi hawa ambao ni wa faida ukeni kunapunguza ulinzi wa uke na kuweka uke katika mazingira ya kufikiwa na bakteria wa gono na chlamydia kiurahisi.
Wanawake wanaotumia njia za vidonge za uzazi wa mpango.
Dawa za kisasa za kupanga uzazi hasa za kunywa huleta mabadiliko katika mfumo wa homoni. Moja ya homoni inayoathiriwa ni Progesterone.Kwa wanawake hawa kiwango cha estrogeni huwa ni kikubwa na kupelekea ute mwingi kuzalishwa eneo la mlango wa kizazi.
Ute huu husaidia bakteria hawa kusafiri na kuingia kwa urahisi ndani ya mfumo wa uzazi.
Vilevile wanawake wengi wanotumia njia hizi za uzazi wa mpango hawana elimu ya kutosha kiasi kinachopelekea makosa mengi katika utumiaji.
Moja ya changamoto kubwa ni kutokwa damu kila mara. Kuwepo kwa damu ukeni kwa muda mrefu kunatengeneza uchafu ambao unaweza kuwavutia bakteria hawa. Hasa mwanamke asipokuwa msafi.
Wanawake hawa uwezo wa miili yao kupambana na magonjwa uko chini kiasi kwamba wanakuwa hatarini kushambuliwa na kila aina ya ugonjwa kiurahisi.
Vilevile wanawake wengi wanotumia njia hizi za uzazi wa mpango hawana elimu ya kutosha kiasi kinachopelekea makosa mengi katika utumiaji.
Moja ya changamoto kubwa ni kutokwa damu kila mara. Kuwepo kwa damu ukeni kwa muda mrefu kunatengeneza uchafu ambao unaweza kuwavutia bakteria hawa. Hasa mwanamke asipokuwa msafi.
Wanawake wenye UKIMWI.
Upungufu wa kinga mwilini ambao unaweza kusababishwa na mambo mengi kubwa ikiwa ni virusi vya HIV.Wanawake hawa uwezo wa miili yao kupambana na magonjwa uko chini kiasi kwamba wanakuwa hatarini kushambuliwa na kila aina ya ugonjwa kiurahisi.
Hitimisho
PID ni hatari kwa mwanamke kwa sababu inaweza kukuacha mgumba. Hakikisha unafika kituo cha afya mara kwa mara ikiwa uko katika moja ya kundi ambalo linaweza kuathiriwa kiurahisi ili kupata msaada wa vipimo.
Kuchelewa kutibu PID kunaweza kusababisha matatizo mengi ya afya ikiwemo maradhi ya figo.