Dalili kuu 5 za upungufu wa vitamin A mwilini na tiba.
Vitamini A ni virutubisho muhimu katika ukuaji wa seli, kuimarisha kinga ya mwili, Kuimarisha afya ya macho na kusaidia mfumo wa uzazi. Upungufu wa Vitamini A ni tatizo linaloweza kusababisha hatari nyingi za kiafya kama vile;
Sababu kuu inayopelekea watoto kuwa wahanga wakubwa wa tatizo hili ni lishe duni kwa mama wakati akiwa mjamzito na wakati wa kunyonyesha.
Jambo la msingi la kufahamu ni kwamba, kwa watoto wadogo lishe bora kwao inategemea zaidi ushiriki wa wazazi katika kumpangia mtoto mlo ulio bora na kwa wakati.
Kipindi cha ujauzito na kunyonyesha, mama anapaswa kuhakikisha anapata mlo ulio kamili kwa ajili ya kuimarisha afya yake na ya mtoto.
Ikiwa una tatizo hili la Upungufu wa vitamini A mwilini mambo yafuatayo yanaweza kujitokeza;
Upungufu wa vitamini A unaweza kusababisha ugumu wa kushika au kushikisha mimba yaani ugumba kwa wanaume na wanawake.
Lakini pia kwa wanawake wajawazito upungufu wa vitamini A unaweza kupelekea kuharibika kwa mimba.
Hii ni kwa sababu vitamini A ni miongoni mwa virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini kwa ajili ya kazi mbalimbali za mwili zinazoathiri ukuaji.
Vilevile mtu mwenye upungufu wa vitamini A hupata changamoto ya kupona kwa haraka anapougua au kupata majeraha.
- Kupoteza uwezo wa kuona na upofu.
- Matatizo na ngozi,
- Matatizo ya moyo, mapafu na
- Kudhoofu kwa kinga ya mwili.
Nani anaweza kupata tatizo la upungufu wa Vitamini A kwa urahisi?
Mtu yeyote anaweza kupata tatizo la upungufu wa vitamini A lakini makundi yafuatayo yako katika hatari zaidi:Watoto wadogo
Katika nchi zinazoendelea tatizo hili la upungufu wa vitamini A huathiri zaidi watoto wadogo walio chini ya umri wa miaka 5.Sababu kuu inayopelekea watoto kuwa wahanga wakubwa wa tatizo hili ni lishe duni kwa mama wakati akiwa mjamzito na wakati wa kunyonyesha.
Jambo la msingi la kufahamu ni kwamba, kwa watoto wadogo lishe bora kwao inategemea zaidi ushiriki wa wazazi katika kumpangia mtoto mlo ulio bora na kwa wakati.
Kipindi cha ujauzito na kunyonyesha, mama anapaswa kuhakikisha anapata mlo ulio kamili kwa ajili ya kuimarisha afya yake na ya mtoto.
Wajawazito
Vilevile wajawazito na wanawake wanaonyonyesha ni kundi lingine ambalo hupatwa zaidi na tatizo hili la upungufu wa vitamini A kutokana na kushindwa kupata mahitaji muhimu ya lishe ama kuwa na tabia ya kuchagua vyakula wakati wa ujauzito.Watu wenye matatizo haya ya afya
- Matatizo katika mfumo wa chakula ambayo huathiri ufyonzwaji wa vitamini A.
- Matatizo ya kongosho,
- Mtoto kuzaliwa kabla ya wakati,
- Maambukizi ya surua,
- Watu wanaopata lishe duni.
- Matatizo ya ini na nyongo.
Dalili za upungufu wa Vitamini A.
Upungufu wa vitamini A ni tatizo ambalo hujitokeza wakati mwili wako unakosa kiasi cha vitamini A kinachohitaji ili kufanikisha kazi mbalimbali za mwili.Ikiwa una tatizo hili la Upungufu wa vitamini A mwilini mambo yafuatayo yanaweza kujitokeza;
#1: Ngozi kuwa kavu
- Vitamini A ni muhimu kwa uundaji na ukarabati wa seli za ngozi. Pia husaidia kupambana na uvimbe katika ngozi
- Kutopata vitamini A ya kutosha kunaweza kusababisha matatizo ya
- chunusi
- ukurutu katika ngozi
- ngozi kuwasha
- vipele
- ngozi kuvimba
#2: Matatizo ya macho.
Miongoni mwa madhara yanayojulikana sana ya upungufu wa vitamini A ni matatizo ya macho. Upungufu wa vitamini A unaweza kusababisha matatizo mbalimbali ya macho kama vile;- Macho kuwa makavu,
- Kutoa machozi,
- Kushindwa kuona kwenye mwanga hafifu,
- Kupoteza uwezo wa kuona kabisa.
- Upungufu wa vitamini A ni moja ya sababu kubwa ya matatizo ya macho kwa watoto.
#3: Matatizo ya uzazi.
Kwa wanawake na wanaume, Vitamini A ni miongoni mwa virutubisho muhimu sana katika kuimarisha afya ya uzazi kwa sababu husaidia kutengenezwa kwa seli za uzazi.Upungufu wa vitamini A unaweza kusababisha ugumu wa kushika au kushikisha mimba yaani ugumba kwa wanaume na wanawake.
Lakini pia kwa wanawake wajawazito upungufu wa vitamini A unaweza kupelekea kuharibika kwa mimba.
#4: Kudumaa kwa ukuaji wa mwili kwa watoto
Watoto ambao hawapati vitamini A ya kutosha wanaweza kupata tatizo ukuaji duni na kupelekea kudumaa.Hii ni kwa sababu vitamini A ni miongoni mwa virutubisho muhimu vinavyohitajika mwilini kwa ajili ya kazi mbalimbali za mwili zinazoathiri ukuaji.
#5: Kupata maambukizi kiurahisi.
Mtu aliye na upungufu wa vitamini A anaweza kupata maambukizi ya magonjwa mara kwa mara kwa vile kupungua kwa vitamini A kunapelekea kinga ya mwili kudhoofu na kushindwa kukabiliana na maambukizi ya magonjwa.Vilevile mtu mwenye upungufu wa vitamini A hupata changamoto ya kupona kwa haraka anapougua au kupata majeraha.
Tiba ya upungufu wa vitamini A
Matibabu ya upungufu wa kawaida wa vitamini A ni kula vyakula vyenye vitamini A kwa wingi.Ikiwa tatizo ni kubwa zaidi basi unashauriwa kuonana na daktari au mfamasia na anaweza kupendekeza kula vyakula zaidi vyenye vitamini A pamoja na kutumia virutubisho vya vitamini A.
Watu walio katika hatari ya kupata tatizo hili hasa wajawazito, watoto na wenye matatizo ya afya kama ilivyoanishwa hapo juu wanapaswa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara juu ya kiwango cha vitamini A mwilini.
Ukiona dalili zozote zinazoashiria upungufu wa vitamini A kama vile upofu wa usiku, unapaswa kuwasiliana na daktari mara moja.
Hitimisho
Ikiwa una wasiwasi kuhusu kiwango cha vitamini A mwilini mwako, wasiliana na daktari au mfamasia kufanyiwa uchunguzi wa kawaida wa kubaini kama kuna tatizo.Watu walio katika hatari ya kupata tatizo hili hasa wajawazito, watoto na wenye matatizo ya afya kama ilivyoanishwa hapo juu wanapaswa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara juu ya kiwango cha vitamini A mwilini.
Ukiona dalili zozote zinazoashiria upungufu wa vitamini A kama vile upofu wa usiku, unapaswa kuwasiliana na daktari mara moja.