Vyakula vyenye Vitamini A na faida zake mwilini.
Vitamini A ni miongoni mwa virutubisho muhimu zaidi ambavyo miili yetu huhitaji ili kukamilisha kazi mbalimbali za mwili.
Uhitaji wa vitamin A katika miili yetu ni wa lazima ukilinganisha na aina nyingine za vitamini kama vitamini D, sababu kuu ni kwamba miili yetu haina uwezo wa kutengeneza aina hii ya vitamini (vitamin A).
Kwa asilimia 100 miili yetu inategemea vitamini A kutoka katika vyakula.
Vitamini A ni virutubisho muhimu ambavyo husaidia mwili katika mambo mbalimbali ikiwemo;
Unashauriwa kutumia dakika zisizozidi 5 unapopika vyakula hivi katika moto wa kawaida. Hakikisha rangi ya kijani ya vyakula hivi inakuwepo hata baada ya kupika.
Mbali na hitaji la ukuaji Watoto pia wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya magonjwa hivyo matumizi ya vitamini A ni ya muhimu na lazima.
Kwa mama anayenyonyesha mahitaji ya vitamini A huongezeka na anapaswa kula vyakula vyenye vitamini A ili kukidhi mahitaji yake na ya mtoto.
Baadhi ya matatizo yatokanayo na upungufu wa vitamini A ni pamoja na;
Uhitaji wa vitamin A katika miili yetu ni wa lazima ukilinganisha na aina nyingine za vitamini kama vitamini D, sababu kuu ni kwamba miili yetu haina uwezo wa kutengeneza aina hii ya vitamini (vitamin A).
Kwa asilimia 100 miili yetu inategemea vitamini A kutoka katika vyakula.
Vitamini A ni virutubisho muhimu ambavyo husaidia mwili katika mambo mbalimbali ikiwemo;
- Husaidia kudumisha uadilifu na utendaji kazi wa tishu mbalimbali za mwili kama vile tishu za usoni, ngozi, utando wa njia ya kupumua, utumbo, kibofu na tishu za jicho.
- Kusaidia afya ya macho na kuona.
- Husaidia kuimarisha kinga ya mwili.
Chanzo kikuu cha vitamini A
Vitamini A hupatikana katika vyakula mbalimbali ikiwemo nyama, mbogamboga na matunda. Na inaweza kupatikana katika muundo wa namna kuu mbili ambazo ni:- Vitamini A: Huu ni muundo wa vitamini A ambao uko tayari kutumiwa na mwili mara moja. Ikiwa mwili utapokea vitamin A katika muundo huu basi mmeng’enyo wake na matumizi huanza mara moja. Vitamini katika muundo huu ambayo mwili huanza kuutumia mara tu uingiapo mwilini hupatikana zaidi katika bidhaa za wanyama ikiwa ni pamoja na nyama, kuku, samaki na maziwa.
- Provitamin A: Hii ni aina ya vitamini katika muundo wa awali ambapo baada ya kuingia mwilini hugeuzwa kwanza katika muundo wa vitamini A ndio huanza kutumiwa na mwili. Muundo huu wa vitamini A hupatikana zaidi katika mbogamboga na matunda.
Vyakula vyenye vitamini A kwa wingi.
Bidhaa za Wanyama zenye kiwango kikubwa cha virutubisho vya vitamini A ni Pamoja na;- Nyama ya kuku
- Maziwa
- Samaki
- Nyama ya ng’ombe hasa minofu laini.
- Maini
- Maziwa ya mama
- Mayai
- Jibini na
- Siagi.
- Karoti
- Maembe
- Papai
- Viazi vitamu
- Mafuta ya mimea kama vile nazi, alizeti, mawese na pamba.
- Mahindi
- Mbogamboga za majani
- Nyanya
- Vitunguu
- Bilinganya
- Pilipili hoho
- Matango
Unashauriwa kutumia dakika zisizozidi 5 unapopika vyakula hivi katika moto wa kawaida. Hakikisha rangi ya kijani ya vyakula hivi inakuwepo hata baada ya kupika.
Ni kiasi gani cha vitamini unahitaji?
Kwa Watoto wadogo:
Watoto wnahitaji kukua hivyo wanahitaji aina hii ya vitamini kwa kiwango kikubwa kadri iwezekanavyo.Mbali na hitaji la ukuaji Watoto pia wako katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya magonjwa hivyo matumizi ya vitamini A ni ya muhimu na lazima.
Kwa mama anayenyonyesha mahitaji ya vitamini A huongezeka na anapaswa kula vyakula vyenye vitamini A ili kukidhi mahitaji yake na ya mtoto.
Kwa watu wazima;
Kimsingi pamoja na umuhimu mkubwa wa vitamini A lakini mwili hauhitaji kiasi kikubwa cha virutubisho. Matumizi ya kawaida ya mbogamboga na matunda yanatosha kuupatia mwili kiwango kinachotakiwa mwilini.Athari za upungufu wa vitamini A mwilini.
Upungufu wa vitamini A unaweza kusababisha matatizo na magonjwa kadhaa ambayo yanaweza kupelekea hata vifo.Baadhi ya matatizo yatokanayo na upungufu wa vitamini A ni pamoja na;
- Kupoteza uwezo wa kuona vizuri ama upofu hasa kwa watotot. Takwimu zinaonyesha upungufu wa Vitamini A ndio chanzo kikuu cha tatizo la upofu kwa watoto duniani
- Husababisha matatizo ya kujifungua na vifo vya uzazi kwa wajawazito
- Inapunguza uwezo wa mwili kupambana na magonjwa hivyo kuufanya mwili kuwa dhaifu katika kupambana na magonjwa mbalimbali
- Inasababisha matatizo ya uzazi kwa wanawake na wanaume
- Kuongezeka kwa uwezekano wa kupata maradhi ya upungufu wa damu
- Kusababisha matatizo ya ukuaji na kudumaa kwa Watoto
- Kusababisha matatizo ya ukuaji wa mifupa na kupungua kwa ujazo wa mifupa, hii ni moja ya sababu inayopelekea wanawake kupata matatizo ya uzazi
Hitimisho
Upungufu wa Vitamini A umeenea katika mataifa yanayoendelea ikiwemo Tanzania.
Vitamini A ni virutubisho muhimu mwilini na mwili nahitaji virutubisho hivi kwa kiwango kidogo ambacho ni rahisi kukimudu.
Mbali na athari hizi zilizoorodheshwa hapo juu lakini pia upungufu wa vitamini A unaweza kusababisha matatizo mengine kama vile mwili kuvimba na ugumba.
Watu walio na majeraha na chunusi wanaweza kuwa na viwango vya chini vya vitamini A katika damu ni vyema kufanya uchunguzi juu ya kiwango cha vitamini A mwilini mwao.
Ikiwa unashuku kuwa na upungufu wa vitamini A, zungumza na mtaalamu wa afya ili upate ushauri sahihi wa vyakula na virutubisho, ili kurekebisha tatizo.