Fahamu Sababu kuu 8 za Bawasiri na tiba yake
Bawasiri ni nini?
Bawasiri , pia huitwa kikundu, ni tatizo la uvimbe sehemu ya nje au ya ndani ya haja kubwa linalotokea baada damu kutuama katika mishipa ya damu iliyovimba aukujikunja kwenye njia ya haja kubwa.Mishipa inayoweza kuathiriwa ni ile ya ndani au nje ya sehemu ya haja kubwa.
Njia hizi hutumika kwa wagonjwa ambao husumbuliwa na bawasiri ya ndani amabayo ipo katika hatua ya kwanza au ya pili.
Bawasiri inasababishwa na nini?
Yapo mambo kadhaa ambayo yanaweza kuongeza uwezekano wa mtu kupata tatizo la bawasiri. Badhi ya mambo hayo ni kama yafuatayo;
#1: Kutoa haja kubwa ngumu na kutumia muda mrefu chooni.
Wakati wa kutoa haja kubwa ukuta wa ndani wa mfereji wa haja kubwa huvutika na kutoka nje kama sehemu ya ufanyaji kazi wa kawaida wa utoaji kinyesi.
Kinyesi kigumu kupita kawaida kinapelekea misuli kuvutika kupita uwezo wake wa kawaida, ikiwa jambo hili hujirudia mara kwa mara basi misuli ya mfereji wa haja kubwa hulegea.
Kulegea kwa misuli ya mfereji wa haja kubwa kunafanya mishipa ya damu kudhoofu na kukunjika kwa urahisi.
Kulegea kwa misuli ya mfereji wa haja kubwa kunafanya mishipa ya damu kudhoofu na kukunjika kwa urahisi.
Mishipa ya damu inapokunjika damu hushindwa kusafili na kutuwama, kutuwama kwa damu hii ndio kunazalisha uvimbe.
Vilevile kukaa au kuchuchumaa kwa muda mrefu kunasababisha mgadamizo mkubwa maeneo ya haja kubwa.
Vilevile kukaa au kuchuchumaa kwa muda mrefu kunasababisha mgadamizo mkubwa maeneo ya haja kubwa.
Mgandamizo huu unaopelekea kuvutika kwa misuli ya mfereji wa haja kubwa, na mwishowe misuli hii hushindwa kujirudi.
Misuli iliyolegea husababisha mishipa ya damu katika eneo la haja kubwa kujikunja na kuruhusu damu kutuwama.
Kitaalamu unashauriwa kutumia dakika zisizozidi 3 utapokuwa chooni kutoa haja kubwa.
#2: Upungufu wa vyakula vyenye ufumwele.
Vyakula vyenye vyuzinyuzi husaidia kulainisha haja kubwa. Upungufu wa vyakula hivi unapelekea kupatwa na tatizo la kupata haja kubwa ngumu.Haja kubwa inapokuwa ngumu husababisha misuli kuvutika kupita uwezo ambao inaweza himili hivyo kuaribika kwa misuli iliyopo kwenye mfereji wa haja kubwa.
#3: Kuharisha.
Kuharisha mara kwa mara ni moja ya chanzo cha bawasiri kwa sababu muda mwingi misuli hii iliyopo katika mfereji wa haja kubwa hutanuka na kusinyaa.Kutanuka na kusinyaa kwa misuli hii mfululizo kunapelekea misuli hii kulegea na kupoteza uimara wake. Na mwishowe mishipa ya damu kudhoofu na kuruhusu damu kutuama.
#4: Ujauzito/mimba.
Ujauzito ni chanzo ni mija ya sababu kuu ya cha bawasiri kwa wanawake. Wakati wa ujauzito, mama mjamzito hupenda kukaa akitanguliza tumbo na mikono akiweka nyuma kama egemeo.Ukaaji huu unasababisha mgandamizo mkubwa maeneo ya haja kubwa. Mgandamizo huu hulegeza misuli na kudhoofisha mishipa ya damu katika eneo hilo.
Hii ni sababu kuu ya kwanini wajawazito ni moja kundi linaloshambuliwa sana na bawasili.
Vilevile kadri mtoo anavyokua tumboni ndivyo mfuko wa uzazi pia unatanuka, kutanuka huku kunasababisha kuminywa kwa mishipa ya damu ya vena na kuathiri usafirishwaji wa damu katika mishipa hiyo.
Hii ni sababu kuu ya kwanini wajawazito ni moja kundi linaloshambuliwa sana na bawasili.
Vilevile kadri mtoo anavyokua tumboni ndivyo mfuko wa uzazi pia unatanuka, kutanuka huku kunasababisha kuminywa kwa mishipa ya damu ya vena na kuathiri usafirishwaji wa damu katika mishipa hiyo.
Wakati mwingine mishipa hii huminywa kiasi cha kujikunja na kusababisha damu kutuama.
#5: Mazoezi au kazi ngumu.
Mazoezi ya wastani ni muhimu kwa afya yako. Lakini mazoezi mazito kupita kiwango au shughuli nzito zinaweza kuongeza nafasi ya wewe kupata tatizo la bawasiri.Shughuli kama vile kuendesha baiskeli, kupanda mlima na kunyenyua vitu vizito ni baadhi ya vshughuli vinavyoongeza mgandamizo na msuguano katika mfereji wa haja kubwa.
#6: Kukaa kitako kwa muda mrefu.
Kutulia na kukaa kwa muda mrefu kutumia matako huongeza nafasi ya kupata bawasiri. Hii ni kwa sababu uzito wako unaishia kwenye matako.Hii inaongeza mgandamizo katika mfereji wa haja kubwa. Kuongezeka kwa mgandamizo katika mfereji wa haja kubwa kunalegeza misuli na kusababisha mishipa ya damu kudhoofu na damu kutuama.
#7: Tatizo la kurithi.
Kwa baadhi ya watu kuwepo kwa mgandamizo mkubwa eneo la mfereji wa haja kubwa ni kawaida na linatokana na urithi wa chembe fulani za vinasaba ambavyo husababisha hali hiyo.Mara nyingi watu hawa tatizo huongezeka kutokana na kuwepo kwa sababu za kisaikolojia.
Dawa ya bawasiri.
Bawasiri hutibiwa kwa namna kuu mbili kulingana na lengo la matibabu ambapo,- namna ya kwanza ni ile yenye lengo la kutuliza maumivu na kuleta nafuu,
- na namna ya pili ni ile yenye lengo la kuondoa kabisa uvimbe.
Tiba ya bawasiri kwa lengo la kutuliza maumivu na kuleta nafuu.
Kwa kawaida bawasiri hujitokeza na kuisha yenyewe, lakini inapotokea hali inazidi kuwa mbaya au inachelewa kupona, basi mgonjwa anaweza kutumia njia zifuatazo ili kusaidia kuharakisha kupona na kupunguza maumivu.Njia hizi hutumika kwa wagonjwa ambao husumbuliwa na bawasiri ya ndani amabayo ipo katika hatua ya kwanza au ya pili.
Na pia kwa wagonjwa wenye bawasiri ya nje amabyo ipo katika hatua ya kwanza na ya pili pia. Njia hizi ni kama ifuatavyo;
- Kutumia maji ya vuguvugu yenye joto la kati ya 300C hadi 400C: Mgonjwa anatakiwa kukaa ndani ya maji ya vuguvugu kwa muda wa dakika tatu walau mara 3 kwa siku. Hii husaidia katika kupunguza mgandamizo, kuweka maeneo safi dhidi ya maambukizi na kuimarisha mzunguko wad amu.
- Kutumia dawa: Mfano dawa za kutuliza maumivu, kupunguza uvimbe na kusaidia mzunguko wa damu.
- Vyakula nya nyuzinyuzi: Kurekebisha mlo kwa kutumia vyakula vyenye ufumwele kwa wingi.
- Zingatia muda wa kukaa chooni: Kufuata taratibu stahiki wakati wa kutoa haja kubwa kwa kuzingatia mudan a kujiepusha na shughuli zitakazopelekea kutumia muda mrefu chooni, mfano kusoma gazeti au kitabu na kuchezea simu.
- Matumizi ya kupaka ya mitishamba: Unaweza kutumia baadhi ya mitishamba ili kupambana na tatizo, mfano Gotu kola, Aloe vera, Kitunguu saumu, Bizali nyembembe, majani machanga ya muembe na Tui la nazi ni baadhi ya mitishamba inayoweza kukusaidia na tatizo la bawasiri.
Tiba ya bawasiri yenye lengo la kuondoa kabisa uvimbe.
Hakuna dawa ya kutumia na kuondoa kabisa tatizo la bawasiri kwa mara moja zaidi ya kufanyiwa upasuaji mdogo wa kuondoa uvimbe katika eneo la haja kubwa.
Hata hivyo njia zilizoorodheshwa hapo juu zinaweza kukusaidia na kumaliza tatizo ikiwa zitatumika kikamilifu na kwa muda mrefu.