Dalili za Upungufu wa vitamin B changamano mwilini
Si rahisi kupata tatizo la upungufu wa vitamini B changamano kwa sababu Vitamini B changamano hupatikana katika vyakula vingi vya kawaida ambavyo vinapatikana kwa urahisi.
Lakini pia vitamini B huongezwa katika vyakula vingi vya viwandani unavyotumia kama vile mkate na nafaka.
Upungufu wa vitamin B sio kitu cha kawaida sana ingawa kuna Baadhi ya makundi ya watu wako katika hatari ya kupata tatizo hili la upungufu wa virutubisho vya vitamini B.
Ikiwa mlo wako ni duni au una tatizo la usagaji na umeng’enyaji wa chakula basi unaweza kupata tatizo hili kwa urahisi.
Walevi wana uwezekano mkubwa wa kuwa na upungufu wa vitamini B changamano hususa ni thiamini, riboflauini, pyridoxine, na asidi ya folic.
Pia, wazee wanaoishi peke yao au katika nyumba za kuwatunzia wazee mara nyingi hawali chakula vizuri na hawapati Vitamini B za kutosha kutoka katika vyakula vyao.
Mfano; watu ambao hawali vyakula vya wanyama kama vile maziwa au mayai huenda wasipate vitamini B vya kutosha.
Dozi kubwa ya Niasini huweza kusababisha.
Hii ni moja ya Vitamini B ambayo inaweza kuleta uharibifu mkubwa katika mwili. Ikiwa utatumia zaidi ya miligramu 2,000 kwa siku kwa muda mrefu unaweza kupata ukilema wa kutembea na kushindwa kuhisi.
Iwapo una upungufu wa vitamini B moja, huenda ukawa na upungufu wa vitamini nyingine pia.
Vyakula vyenye vitamini B kwa wingi ni pamoja na nyama, kuku, samaki, maziwa na bidhaa za maziwa, karanga, maharagwe, njegere na mboga za majani zenye rangi ya kijani kibichi.
Lakini pia vitamini B huongezwa katika vyakula vingi vya viwandani unavyotumia kama vile mkate na nafaka.
Upungufu wa vitamin B sio kitu cha kawaida sana ingawa kuna Baadhi ya makundi ya watu wako katika hatari ya kupata tatizo hili la upungufu wa virutubisho vya vitamini B.
Ikiwa mlo wako ni duni au una tatizo la usagaji na umeng’enyaji wa chakula basi unaweza kupata tatizo hili kwa urahisi.
Nani anaweza kupata tatizo la upungufu wa vitamini B?
Watu wengine walio katika hatari ya kupata tatizo la upungufu wa vitamini B ni:Watumiaji pombe kupita kawaida
Pombe huzuia uwezo wa mwili kunyonya vitamini B, vilevile na inaharakisha utolewaji nje wa chakula unachokula kama takamwili.Walevi wana uwezekano mkubwa wa kuwa na upungufu wa vitamini B changamano hususa ni thiamini, riboflauini, pyridoxine, na asidi ya folic.
Wazee
Wazee ni kundi lingine lililo kwenye hatari ya kupata tatizo la upungufu wa vitamini B kwa sababu uwezo wa miili yao kufyonza vyakula hivi unapungua kadri umri unavyosonga.Pia, wazee wanaoishi peke yao au katika nyumba za kuwatunzia wazee mara nyingi hawali chakula vizuri na hawapati Vitamini B za kutosha kutoka katika vyakula vyao.
Wavutaji sigara
Moshi wa tumbaku hupunguza ufyonzwaji wa vitamini B.Watu wenye matatizo sugu ya usagaji chakula
Watu hawa wanakosa kiwango cha kutosha cha vitamini B kutoka katika vyakula wanavyokula kutokana na uwezo wao mdogo wa kufyonza virutubisho hivi kutoka katika tumbo kuingia katika seli za mwili.Watu walio katika mpangao maalumu wa lishe.
Kwa watu ambao wako katika mpango fulani wa chakula wako katika hatari ya kupata tatizo hili kwa sababu ya kuchagua vyakula.Mfano; watu ambao hawali vyakula vya wanyama kama vile maziwa au mayai huenda wasipate vitamini B vya kutosha.
Dalili za Upungufu wa Vitamini B Changamano
Ikiwa una upungufu wa vitamini B changamano, unaweza kupata matatizo mbalimbali ya afya kama vile;- upele wa ngozi
- midomo kupasuka
- magamba kwenye midomo
- kuvimba ulimi
- uchovu
- udhaifu
- upungufu wa damu
- Msongo wa mawazo
- kuwashwa mwili
- kichefuchefu
- maumivu ya tumbo
- kuhara
- kuvimbiwa
- kufa ganzi, kuwashwa au miguu kuwaka moto
Madhara ya vitamini B changamano
Vitamini B zote ni mumunyifu katika maji, hii ina maana kwamba virutubisho hivi ni rahisi kutolewa na mwili na si rahisi kusababisha madhara hata kama ukivitumia kwa kiwango kikubwa.Lakini kuna kizuizi kwa aina hizi mbili za vitamini B changamano ambazo ukizitumia kwa kiwango kikubwa zinaweza kukuletea madhara.
Niasini na Vitamini B6 ni vitamini B ambavyo unapaswa kuwa makini unapovitumia kwa sababu vinaweza kusababisha madhara yafuatayo;
Niasini na Vitamini B6 ni vitamini B ambavyo unapaswa kuwa makini unapovitumia kwa sababu vinaweza kusababisha madhara yafuatayo;
Dozi kubwa ya Niasini huweza kusababisha.
- Uso kuwa mzito na kuwa mwekundu
- Kuhisi joto, miguu kuwaka moto au kuwashwa
Hii ni moja ya Vitamini B ambayo inaweza kuleta uharibifu mkubwa katika mwili. Ikiwa utatumia zaidi ya miligramu 2,000 kwa siku kwa muda mrefu unaweza kupata ukilema wa kutembea na kushindwa kuhisi.
Muhimu
Kundi la vitamini B changamano lina aina 8 za vitamini, aina zote nane hufanya kazi kwa kutegemeana.Iwapo una upungufu wa vitamini B moja, huenda ukawa na upungufu wa vitamini nyingine pia.
Vyakula vyenye vitamini B kwa wingi ni pamoja na nyama, kuku, samaki, maziwa na bidhaa za maziwa, karanga, maharagwe, njegere na mboga za majani zenye rangi ya kijani kibichi.