Vyakula vyenye vitamini B kwa wingi na faida zake mwilini

Vitamini B changamano ni kundi la virutubisho ambalo hujumuisha aina nane ya kundi la vitamini B mumunyifu.

Aina hizo ni pamoja na;
  1. Thiamini (vitamini B-1)
  2. Riboflauini (vitamini B-2)
  3. Niasini (vitamini B-3)
  4. Asidi ya pantothenic (vitamini B-5)
  5. Pyridoxini (Vitamini B6)
  6. Biotini (vitamini B-7)
  7. Folic acid (vitamini B-9)
  8. Cobalamini (Vitamini B-12)
Kwa pamoja kundi hili la virutubisho vya Vitamini B changamano husaidia mwili katika mambo mbalimbali kama vile kuimarisha afya ya ubongo, kutengenezwa damu, kuimarisha mzunguko wa damu na kusaidia utendaji wa mwili katika usawa.

Faida za Vitamini B changamano mwilini.

Vitamini B changamano ni muhimu zaidi mwilini kwa vile miili yetu haina uwezo wa kutengenezwa virutubisho hivi. Kwa asilimia 100 miili inategemea vitamini B kutika katika vyakula.

Baadhi ya kazi muhimu za kila aina ya vitamin katika kundi hili la Vitamini B changamano ni kama ifuatavyo;

Faida za Vitamini B1;

  • Husaidia kutengenezwa kwa protini muhimu za mwili
  • Kusaidia utengenezwaji wa nishati ya mwili
  • Husaidia kudhibiti ukuaji wa neva
  • Husaidia utendaji kazi wa ubongo
  • Kuweka akili katika hali ya msawazo.
  • Kuimarisha kumbukumbu

Faida za Vitamini B2;

  • Husaidia kutengenezwa kwa nishati mwilini
  • Inahitajika kwa ajili ya utengenezwaji wa seli nyekundu za damu
  • Husaidia kutengenezwa kwa homoni
  • Inasaidia ubadilishaji na utengenezwaji wa aina nyingine za vitamin B kama vile niasini, folate na vitamini B6
  • Husaidia umeng’enywaji wa mafuta, dawa na vichocheo vya homoni.
  • Inasaidia ufyonzwaji na utumikaji wa madini joto ya chuma chuma
  • Ni miongoni mwa viantioksideshaji muhimu mwilini

Faida za Vitamini B3;

  • Inahitajika kusaidia upatikanaji wa nishati mwilini
  • Husaidia kutengenezwa kwa Baadhi ya vichocheo vya homoni
  • Huondoa sumu mwilini
  • Husaidia kuwaka kiwango cha rehemu (mafuta) mwilini katika usawa

Faida za Asidi ya Vitamini B5;

  • Inahitajika kusaidia upatikanaji wa nishati mwilini
  • Inahitajika kutengeneza vitamini D, homoni, na seli nyekundu za damu

Faida za Vitamini B6;

  • Inahitajika kutengeneza protini, homoni na vimeng’enya
  • Husaidia kuimarisha afya ya mzunguko wa damu na moyo

Faida za Vitamini B7;

  1. Inahitajika kusaidia upatikanaji wa nishati mwilini
  2. Ni muhimu katika kurekebisha sukari ya mwili
  3. Husaidia mawasiliano ya seli za mwili

Faida za Asidi ya Foliki (Vitamini B9);

  • Ukuaji na mgawanyiko wa seli.
  • Inazuia mtoto kuzaliwa na kasoro za kiafya hususa ni matatizo ya moyo

Faida za Vitamini B12;

  • Inahitajika kwa ajili ya kutengenezwa na kuimarisha seli nyekundu za damu.
  • Husaidia kuzuia magonjwa ya moyo.
Hizi ni faida za aina mbalimbali ya vitamin kutoka katika kundi la vitamini B changamano.

Mbali na vitamini B changamano kuna kundi lingine la virutubisho ambalo si vitamini B changamano lakini hufanya kazi zinazoelekeana na kazi zinazofanywa na virutubisho vya vitamini B changamano.

Virutubisho hivyo ni;
  • Choline: Ubongo wako hutumia choline kusaidia kuhifadhi kumbukumbu. Pia husaidia kutibu msongo wa mawazo na inaweza kuwa muhimu katika kutibu homa ya ini.
  • Inositol: Unahitaji inositol kutengeneza utando wa seli au kiwambo cha seli chenye afya na kemikali za usafirishaji wa taarifa mwilini. Pia husaidia kupunguza uharibifu wa neva kwa wagonjwa wa kisukari.
  • Asidi ya Para-aminobenzoiki (PABA): Virutubisho hivi ni viantioksidehaji (viondoa sumu) vikuu vya mwili na husaidia kulinda ngozi yako dhidi ya uharibifu wa jua. Kemikali hii ni miongoni mwa viambata muhimu katika losheni nyingi za ngozi.
  • Asidi ya lipoic: Kisaidizi cha vitamini B, asidi ya lipoic hufanya kazi kwa ukaribu na vitamini B1, riboflauini, niasini, na asidi ya pantotheni kubadilisha wanga, mafuta na protini.
Kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Afya (NIH), ulaji wa kila siku wa vitamini B unaopendekezwa ni  kama ifuatavyo kwa wanawake:
  • B1: miligramu 1.1 (mg)
  • B2: miligramu 1.1
  • B3: miligramu 14 NE
  • B5: 5 mg
  • B6: miligramu 1.3
  • Biotini: mikrogramu 30 (mcg)
  • Asidi ya Folic: 400 mcg DFE
  • B12: 2.4 mcg
Na Kwa wanaume, inapendekeza ulaji wa kila siku kama ifuatavyo:
  • B1: miligramu 1.2
  • B2: miligramu 1.3
  • B3: miligramu 16 NE
  • B5: 5 mg
  • B6: miligramu 1.3
  • Biotin: 30 mcg
  • Asidi ya Folic: 400 mcg DFE
  • B12: 2.4 mcg

Vyakula vyenye vitamini B changamano kwa wingi.

Kwa kawaida baadhi au vitamini B changamano zote hupatikana katika aina moja ya chakula. Mfano maziwa, nyama, samaki, machungwa, siagi ya karanga, mkate, nafaka za kiamsha kinywa, mayai na mtindi.

Vyakula hivi vyote vinakusaidia kupata aina zote za vitamini B changamano.

Baadhi ya vyanzo vikuu vya vitamini B changamano ni kama ifuatavyo;
  • Thiamini (vitamini B-1): Nyama ya nguruwe, maini, samaki, machungwa, mbaazi, siagi ya karanga, ngano, maharagwe, na nafaka.
  • Riboflauini (vitamini B-2): Maziwa, bidhaa za maziwa, nyama, maharagwe, karanga, mboga za majani na parachichi.
  • Niasini (vitamini B-3): Nyama, kuku, samaki, maharagwe, njegere, siagi ya karanga, maziwa na karanga.
  • Asidi ya pantothenic (vitamini B-5): Maini, nyama, samaki, kuku, nafaka, alizeti na maharagwe.
  • Pyridoxini (Vitamini B6): nyama, samaki, kuku, karanga, maharagwe, mbaazi, ndizi, parachichi na viazi.
  • Biotini (vitamini B-7): Maini, mayai, siagi ya karanga, maziwa na ndizi.
  • Asidi ya Folic (vitamini B-9): Mboga majani, maini, machungwa, maharagwe na parachichi.
  • Cobalamin (Vitamini B-12): Nyama, kuku, samaki, maziwa, mtindi, jibini na mayai.

Hitimisho

Kwa sehemu kubwa vitamini B changamano huweza kupatikana katika chakula cha aina moja pekee. Mfano Nyama pekee ina aina zote za vitamini B changamano.
Next Post Previous Post
No Comment
Andika Swali au Maoni
comment url