Magonjwa hatari yanayoongoza kwa vifo Tanzania.
Kwa muda mrefu sasa shirika la afya duniani kushirikiana na nchi wanachama zimekuwa zikifanya tafiti mbalimbali zinazohusu afya na kuchapisha orodha ya magonjwa hatari na matatizo mbalimbali ya kiafya ambayo yanaongoza kwa kusababisha vifo.
Kama moja ya nchi wanachama wa umoja wa mataifa, Tanzania huchapisha orodha ya magonjwa hatari na matatizo mbalimbali ya afya yanayoongoza kwa vifo nchini.
Takwimu za hivi karibuni zilitolewa mwaka 2019 na wizara ya afya na kutoa orodha ya magonjwa yanayoongoza kwa vifo nchini.
Katika makala hii tutaangazia magonjwa 10 hatari zaidi kutoka katika orodha ya magonjwa yanaosababisha vifo nchini.
Tatizo hili limepanda kutoka nafasi ya 11 mwaka 2009 hadi nafasi ya 10 mwaka 2019.
Uvimbe na makovu katika ini ni matokeo ya muda mrefu ya kuharibiwa kwa seli za ini.
Seli hai katika ini zinapoharibiwa, mwili hutengeneza seli zilizokufa ambazo ni mbadala wa seli hai zilizokufa.
Seli hizi zilizokufa hutengeneza kovu. Kadri ini linavyoathiriwa ndivyo seli zilizokufa hutengenezwa kwa wingi na vivyo hivyo kiwango cha kovu huongezeka.
Ikiwa kovu litakuwa kubwa na kudhoofisha utendaji kazi wa ini, basi ini hushindwa kufanya kazi.
Ini ni ogani muhimu sana katika mwili kutokana na kazi yake muhimu ya kuchuja na kuthibiti sumu mbalimbali zinazoingia mwilini.
Kushindwa kufanya kazi kwa ini kunapelekea ogani mbalimbali za mwili kuathiriwa na sumu na hatimaye kifo.
Zipo sababu mbalimbali ambazo huweza kusababisha majeraha katika ini kiasi cha kupelekea ini kushindwa kufanya kazi yake.
Baadhi ya sababu hizo ni;
Kwa mujibu wa takwimu za 2019, takribani vifo 10,253 sawa na 2.8% ya vifo vyote vinavyorekodiwa nchini husababishwa na matatizo ya kuzaliwa.
Magonjwa ya kuzaliwa huathiri sehemu mbalimbali za mwili kama vile;
Tatizo la kiharusi linaweza kutokea sehemu yoyote ya mwili lakini ubongo na moyo ni sehemu ambazo hushambuliwa zaidi na tatizo hili.
Hakuna dalili zozote za muda mrefu ambazo huambatana na tatizo hili la kiharusi ambazo zinaweza kuonekana na kumsaidia mgonjwa kuchukua tahadhali.
Bali kuna dalili za papo kwa papo ambazo zinaashiria shambulizi la kiharusi.
Malaria ndio ugonjwa unaongoza kwa kusababisha vifo vya watoto katika bara la afrika ambapo kwa wastani katika kila dakika 10 mtoto mmoja hupoteza maisha kutokana na ugonjwa wa malaria.
Takwimu zinaonyesha tatizo hili husababisha takribani vifo 18,834 sawa na 5.18% ya vifo vyote nchini. Hata hivyo idadi vifo vitokanavyo na malaria vimepungua ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Chanzo kikubwa cha ugonjwa huu ni mbu aina ya Anoferesi ambaye huishi zaidi maeneo yenye joto, unyevu, vichaka na giza.
Usafi wa mazingira na matumizi ya chandarua chenye dawa ndio njia kuu za kupambana na tatizo hili la malaria.
Tatizo hili hujitokeza kama ilivyo kiharusi cha ubongo lakini linahusisha moyo ambapo damu hushindwa kufika maeneo mbalimbali ya moyo kupitia mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye moyo.
Uzito mkubwa wa mwili na mafuta mengi katika damu ndio sababu kikuu ya tatizo hili.
Dalili kuu za tatizo la shambulizi la moyo ni;
Kwa mujibu wa takwimu, shambulizi la moyo husababisha zaidi ya vifo 23,728 sawa na 6.53% ya vifo vyote vinavyorekodiwa nchini.
Shambulizi la moyo ndio tatizo linaloongoza kwa vifo duniani kote na huwaathiri zaidi watu kutoka mataifa yaliyoendelea kiuchumi.
Kifua kikuu husambazwa kwa njia ya hewa na kwa kiwango kikubwa huathiri mapafu. Mbali na mapafu, tatizo hili linaweza kuathiri maeneo kadhaa ya mwili kama vile ubongo, mifupa na Ugwe mgongo.
Ingawa mtu yeyote anaweza kupata ugonjwa huu lakini kwa sehemu kubwa watu wenye matatizo ya upungufu wa kinga mwilini wako katika hatari ya kupata tatizo hili kwa urahisi zaidi.
Kutokana na hali hii watu wenye maambukizi ya UKIMWI ni moja ya kundi linalooathiriwa zaidi na tatizo hili.
Takwimu za mwaka 2019 zinaonyesha zaidi ya vifo 27,559 sawa na 7.58% ya vifo vyote vinavyorekodiwa nchini husababishwa na ugonjwa huu.
Jitihada za kupambana na tatizo hili nchini Tanzania bado ziko chini kulingana na kwamba ni tatizo linalofanana na homa za kawaida za mafua na kikohozi hasa katika hatua zake za awali.
Hali hii inawafanya watu wengi kupuuza na kudhani ni homa za kawida ili hali ni kifua kikuu.
Fika kituo cha afya kwa vipimo ikiwa unapatwa na homa za mafua na kikohozi mara kwa mara ili kupata uhakika na kuanza matibabu mara moja.
Kifua kikuu au TB inatibika na kupona kabisa na matibabu yake ni bure.
Tatizo la kuharisha ni ishara ya kuwapo kwa hitilafu au maambukizi katika mfumo wa chakula.
Maambukizi haya yanaweza kuwa ya bakteria, virusi auminyoo. Baadhi ya bakteria hatari katika mfumo wa chakula ni pamoja na;
Zaidi ya vifo 30,859 sawa na 8.49% ya vifo vyote vinavyorekodiwa nchini vinatokana na matatizo ya kuharisha na kutapika.
Pamoja na kwamba tatizo hili linapungua kila mwaka lakini bado UKIMWI ni moja ya visababishi vikuu vya vifo nchini ambapo takribani vifo 33,028 sawa na 9.08% ya vifo vyote nchi vinatokana na UKIMWI.
Kujamiana bado ndio njia kuu ya maambukizi huku ngono zembe ikiwa ndio sababu kuu ya ugonjwa huu wa UKIMWI.
Magonjwa yote haya huathiri mfumo wa upumuaji na kwa pamoja huchangia zaidi ya asilimia 10 ya vifo vyote nchini sawa na vifo 37,053 vinavyorekodiwa kila mwaka.
Orodha ya magonjwa hatari yaliyotajwa hapo juu ndio vinara wa vifo nchini ambapo kwa ujumla huchangia zaidi ya asilimia 60 ya vifo vyote vinavyorekodiwa nchini.
Magonjwa mengineyo ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa idadi ya vifo nchini Tanzania ni;
Kuna uwezekano mkubwa ya kwamba idadi ya vifo vilivyotajwa hapa ni kidogo kulingaisha na uhalisia.
Hata hivyo jambo la msingi ni wewe kufahamu magonjwa haya ili kuchukua tahadhari juu ya afya yako na watu wako wa karibu kwa manufaa ya nchi kwa ujumla.
Kama moja ya nchi wanachama wa umoja wa mataifa, Tanzania huchapisha orodha ya magonjwa hatari na matatizo mbalimbali ya afya yanayoongoza kwa vifo nchini.
Takwimu za hivi karibuni zilitolewa mwaka 2019 na wizara ya afya na kutoa orodha ya magonjwa yanayoongoza kwa vifo nchini.
Katika makala hii tutaangazia magonjwa 10 hatari zaidi kutoka katika orodha ya magonjwa yanaosababisha vifo nchini.
Magonjwa yanayoongoza kwa vifo Tanzania.
#10. Matatizo ya uvimbe na makovu katika ini.
Namba kumi katika orodha ni matatizo ya uvimbe na makovu katika ini.
Kulingana na takwimu za mwaka 2009-2019, matatizo ya uvimbe na makovu husababisha takribani vifo 6137 kila mwaka ambayo ni sawa 1.6% ya vifo vyote vinavyorekodiwa nchini Tanzania.
Kulingana na takwimu za mwaka 2009-2019, matatizo ya uvimbe na makovu husababisha takribani vifo 6137 kila mwaka ambayo ni sawa 1.6% ya vifo vyote vinavyorekodiwa nchini Tanzania.
Tatizo hili limepanda kutoka nafasi ya 11 mwaka 2009 hadi nafasi ya 10 mwaka 2019.
Uvimbe na makovu katika ini ni matokeo ya muda mrefu ya kuharibiwa kwa seli za ini.
Seli hai katika ini zinapoharibiwa, mwili hutengeneza seli zilizokufa ambazo ni mbadala wa seli hai zilizokufa.
Seli hizi zilizokufa hutengeneza kovu. Kadri ini linavyoathiriwa ndivyo seli zilizokufa hutengenezwa kwa wingi na vivyo hivyo kiwango cha kovu huongezeka.
Ikiwa kovu litakuwa kubwa na kudhoofisha utendaji kazi wa ini, basi ini hushindwa kufanya kazi.
Ini ni ogani muhimu sana katika mwili kutokana na kazi yake muhimu ya kuchuja na kuthibiti sumu mbalimbali zinazoingia mwilini.
Kushindwa kufanya kazi kwa ini kunapelekea ogani mbalimbali za mwili kuathiriwa na sumu na hatimaye kifo.
Zipo sababu mbalimbali ambazo huweza kusababisha majeraha katika ini kiasi cha kupelekea ini kushindwa kufanya kazi yake.
Baadhi ya sababu hizo ni;
- Unywaji pombe mara kwa mara
- Maambukizi ya virusi vinavyosababisha homa ya ini
- Uzito mkubwa na kitambi na
- Kiwango kikubwa cha madini joto ya chuma kupita kiasi mwilini
#9. Magonjwa ya kuzaliwa.
Namba tisa katika orodha ni magonjwa ya kuzaliwa. Haya ni magonjwa ambayo mtu huzaliwa nayo.Kwa mujibu wa takwimu za 2019, takribani vifo 10,253 sawa na 2.8% ya vifo vyote vinavyorekodiwa nchini husababishwa na matatizo ya kuzaliwa.
Magonjwa ya kuzaliwa huathiri sehemu mbalimbali za mwili kama vile;
- sehemu za nje za mwili mfano kuzaliwa bila viungo vya mwili ,
- kuathiri sehemu za ndani za mwili mfano tundu katika moyo au
- Hitilafu katika utendaji kazi wa ndani wa mwili mfano damu kushindwa kuganda.
- Kurithi kutoka katika vinasaba vya kizazi
- Mapungufu mbalimbali yakiwemo ya lishe kwa mjamzito katika kipindi cha ujauzito
- Ulevi na uvutaji wakati wa ujauzito
- Matumizi ya dawa na baadhi ya tiba, mfano tiba za mionzi (X-Rays)
- Maradhi kwa mama kipindi cha ujauzito
#8. Kiharusi cha ubongo.
Kiharusi cha ubongo kinashika nafasi ya nane. Hili ni moja ya tatatizo hatari zaidi kwa binadamu kutokana na jinsi tatizo hutokea.Tatizo la kiharusi linaweza kutokea sehemu yoyote ya mwili lakini ubongo na moyo ni sehemu ambazo hushambuliwa zaidi na tatizo hili.
- Kiharusi
Ni hali inayotokea pale ambapo damu ya kutosha inashindwa kufika katika ubongo. Damu kuhindwa kufika katika maeneo haya ya ubongo kunaweza kusababishwa na mambo yafuatayo;
- Mafuta mengi yaliyopo mwilini kuziba mishipa ya damu au
- Mishipa ya damu katika ubongo kupasuka na kusababisha damu kuvujia katika maeneo haya
Kuziba au kupasuka kwa mishipa hii ya damu kunapelekea baadhi ya maeneo ya ubongo kukosa hewa ya kutosha ya oksijeni na kusababisha seli nyingi katika maeneo hayo kufa.
Kufa kwa seli hizi huambatana na madhara makubwa ya kiafya kama vile ukilema wa maisha hasa katika mfumo wa fahamu, lakini kubwa zaidi ni kifo.
Hakuna dalili zozote za muda mrefu ambazo huambatana na tatizo hili la kiharusi ambazo zinaweza kuonekana na kumsaidia mgonjwa kuchukua tahadhali.
Bali kuna dalili za papo kwa papo ambazo zinaashiria shambulizi la kiharusi.
Zifuatazo ni dalili za tatizo la kiharusi;
- Mgonjwa hushindwa kuongea ghafla
- Kushindwa kujongea au kutembea
- Uso, mikono na miguu kukaza na kukakamaa
- Maumivu makali ya kichwa na
- Kushindwa kuongea
- 111
- 112
- 114 au
- 999
Takwimu za mwaka 2019 zinaonyesha kiharusi cha ubongo husababisha takribani vifo 13,114 sawa na 3.61% ya vifo vyote vinavyorekodiwa nchini.
#7. Malaria.
Pamoja na kuwa katika nafasi hii, Malaria bado ni moja ya magonjwa hatari na tishio kwa uhai wa binadamu hasa kusini mwa jangwa la sahara.Malaria ndio ugonjwa unaongoza kwa kusababisha vifo vya watoto katika bara la afrika ambapo kwa wastani katika kila dakika 10 mtoto mmoja hupoteza maisha kutokana na ugonjwa wa malaria.
Takwimu zinaonyesha tatizo hili husababisha takribani vifo 18,834 sawa na 5.18% ya vifo vyote nchini. Hata hivyo idadi vifo vitokanavyo na malaria vimepungua ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Chanzo kikubwa cha ugonjwa huu ni mbu aina ya Anoferesi ambaye huishi zaidi maeneo yenye joto, unyevu, vichaka na giza.
Usafi wa mazingira na matumizi ya chandarua chenye dawa ndio njia kuu za kupambana na tatizo hili la malaria.
#6. Shambulizi la moyo.
Kwa jina lingine unaweza kuita kiharusi cha moyo.Tatizo hili hujitokeza kama ilivyo kiharusi cha ubongo lakini linahusisha moyo ambapo damu hushindwa kufika maeneo mbalimbali ya moyo kupitia mishipa ya damu inayosambaza damu kwenye moyo.
Uzito mkubwa wa mwili na mafuta mengi katika damu ndio sababu kikuu ya tatizo hili.
Dalili kuu za tatizo la shambulizi la moyo ni;
- Kufa ganzi kwa mikono,
- Maumivu ya ghafla ya kifua.
- Kushindwa kuongea.
- Kupatwa na kizunguzungu.
Kwa mujibu wa takwimu, shambulizi la moyo husababisha zaidi ya vifo 23,728 sawa na 6.53% ya vifo vyote vinavyorekodiwa nchini.
Shambulizi la moyo ndio tatizo linaloongoza kwa vifo duniani kote na huwaathiri zaidi watu kutoka mataifa yaliyoendelea kiuchumi.
#5. Kifua kikuu.
Nafasi ya tano ni tatizo la kifua kikuu ambalo husababishwa na bakteria ajulikanae kama Mycobacterium tuberculosis.Kifua kikuu husambazwa kwa njia ya hewa na kwa kiwango kikubwa huathiri mapafu. Mbali na mapafu, tatizo hili linaweza kuathiri maeneo kadhaa ya mwili kama vile ubongo, mifupa na Ugwe mgongo.
Ingawa mtu yeyote anaweza kupata ugonjwa huu lakini kwa sehemu kubwa watu wenye matatizo ya upungufu wa kinga mwilini wako katika hatari ya kupata tatizo hili kwa urahisi zaidi.
Kutokana na hali hii watu wenye maambukizi ya UKIMWI ni moja ya kundi linalooathiriwa zaidi na tatizo hili.
Takwimu za mwaka 2019 zinaonyesha zaidi ya vifo 27,559 sawa na 7.58% ya vifo vyote vinavyorekodiwa nchini husababishwa na ugonjwa huu.
Jitihada za kupambana na tatizo hili nchini Tanzania bado ziko chini kulingana na kwamba ni tatizo linalofanana na homa za kawaida za mafua na kikohozi hasa katika hatua zake za awali.
Hali hii inawafanya watu wengi kupuuza na kudhani ni homa za kawida ili hali ni kifua kikuu.
Fika kituo cha afya kwa vipimo ikiwa unapatwa na homa za mafua na kikohozi mara kwa mara ili kupata uhakika na kuanza matibabu mara moja.
Kifua kikuu au TB inatibika na kupona kabisa na matibabu yake ni bure.
#4. Kuharisha na kutapika.
Kutoka nafasi ya nane mwaka 2009 hadi nafasi ya nne mwaka 2019 bila shaka hili ni janga la taifa.Tatizo la kuharisha ni ishara ya kuwapo kwa hitilafu au maambukizi katika mfumo wa chakula.
Maambukizi haya yanaweza kuwa ya bakteria, virusi auminyoo. Baadhi ya bakteria hatari katika mfumo wa chakula ni pamoja na;
- Escherichia coli ambaye anayesababisha tatizo la ghafla la kuharisha.
- Rotavirus huyu ni kirusi anayesababisha kuharisha na kutapika.
- Cryptosporidium kundi la minyoo linalosababisha kuharisha na kutapika.
- Salmonella typhi anayesababisha ugonjwa wa homa ya matumbo (Typhoid).
- Vibrio cholerae anayesababisha ugonjwa wa kipindupindu.
Zaidi ya vifo 30,859 sawa na 8.49% ya vifo vyote vinavyorekodiwa nchini vinatokana na matatizo ya kuharisha na kutapika.
#3. UKIMWI.
Namba tatu katika orodha ni UKIMWI. Hili ni moja ya magonjwa hatari zaidi duniani kwa muda mrefu.Pamoja na kwamba tatizo hili linapungua kila mwaka lakini bado UKIMWI ni moja ya visababishi vikuu vya vifo nchini ambapo takribani vifo 33,028 sawa na 9.08% ya vifo vyote nchi vinatokana na UKIMWI.
Kujamiana bado ndio njia kuu ya maambukizi huku ngono zembe ikiwa ndio sababu kuu ya ugonjwa huu wa UKIMWI.
#2. Homa ya mapafu na milija ya hewa.
Nambari mbili ni homa ya mapafu, nimonia, mafua, uvimbe katika milija ya hewa, maambukizi katika viriba hewa vya mapafu na kikohozi.Magonjwa yote haya huathiri mfumo wa upumuaji na kwa pamoja huchangia zaidi ya asilimia 10 ya vifo vyote nchini sawa na vifo 37,053 vinavyorekodiwa kila mwaka.
Homa ya mapafu husababishwa na bakteria na virusi. Baadhi ya bakteria na virusi hao ni;
Kwa sehemu kubwa magonjwa haya husababishwa na;
Baadhi ya matatizo haya ni kama ifuatavyo;
Hii inafanya idadi ya jumla kwa vifo vinavyorekodiwa kufikia zaidi ya vifo 40000 kwa mwaka.
- Mycoplasma pneumoniae husababisha nimonia na uvimbe katika mapafu.
- Chlamydia spp husababisha Nimonia ambayo huweza kusambaa kwa kujamiana.
- Legionella husababisha maradhi ya mapafu hupatikana kwenye maji machafu.
#1. Magonjwa ya watoto wachanga.
Kwa nchi nyingi zinazoendelea magonjwa ya watoto wachanga ndio huongoza kwa vifo.Kwa sehemu kubwa magonjwa haya husababishwa na;
- Huduma mbovu za afya kwa mama na mtoto kabla na baada ya mtoto kuzaliwa.
- Elimu duni juu ya utunzaji wa mimba.
- Lishe duni kipindi cha ujauzito.
- Mitindo ya hovyo ya maisha kwa mjamzito mfano kuvuta sigara na ulevi.
- Mimba za utotoni.
- Matumizi ya dawa mbalimbali ambazo zinaweza kumuathiri mtoto kabla na baada ya kuzaliwa.
- Matumizi ya kemikali mbalimbali, mfano kemikali katika urembo.
- Tiba za mionzi.
- Matatizo katika vinasaba.
Baadhi ya matatizo haya ni kama ifuatavyo;
Matatizo kipindi mtoto akiwa tumboni mfano;
- Tundu katika ubavu.
- Tundu katika moyo.
- Mtoto kukosa sehemu ya haja kubwa.
- Mtoto kuzaliwa na kichwa kikubwa.
- Mtindio wa ubongo.
- Maji mengi kuzunguka ubongo.
- Mapungufu katika vinasaba mfano magonjwa ya Klinefelter, Turners na Downs.
- Matatizo kipindi cha kuzaliwa.
- Mama kushindwa kusukuma mtoto.
- Mtoto kubanwa kwa muda mrefu bila kupata hewa ya oksijeni.
- Huduma mbovu za awali na za baada ya mama kujifungua.
- Matatizo kipindi cha malezi.
- Elimu duni ya malezi hasa kwa mtoto mwenye matatizo ya afya.
- Lishe duni.
- Hatari mbalimbali za mazingira kama vile ajali.
Hii inafanya idadi ya jumla kwa vifo vinavyorekodiwa kufikia zaidi ya vifo 40000 kwa mwaka.
Hitimisho.
Yapo magonjwa na matatizo mengi ambayo husababisha vifo nchini Tanzania.Orodha ya magonjwa hatari yaliyotajwa hapo juu ndio vinara wa vifo nchini ambapo kwa ujumla huchangia zaidi ya asilimia 60 ya vifo vyote vinavyorekodiwa nchini.
Magonjwa mengineyo ambayo huchangia kwa kiasi kikubwa idadi ya vifo nchini Tanzania ni;
- Saratani ya tezi dume.
- Ajali za barabarani.
- Saratani ya shingo ya kizazi.
- Kisukari.
- Kupoteza kumbukumbu.
- Utapiamlo.
- Shinikizo la damu na;
- Vifo vya wamama wajawazito.