Sababu na madhara ya kitambi kwa wanawake, wanaume na watoto.
Tatizo la tumbo kubwa ama kitambi ni moja ya kisababishi kikubwa cha zaidi ya magonjwa 3 yanayoongoza kwa vifo Tanzania na duniani kwa ujumla.
Shinikizo la damu, kushindwa kupumua na saratani yote haya ni miongoni mwa magonjwa 10 yanayoongoza kwa vifo duniani huku chanzo kikuu ikiwa ni kitambi.
Yapo mambo mengi yanayoweza kuchangia tatizo la tumbo kubwa (kitambi) lakini kula chakula chenye wanga kupita kawaida ndio sababu kuu ya tatizo hili.
Wanawake ni moja ya kundi kubwa ambalo huathiriwa zaidi na tatizo hili na kuwasababishia matatizo mengi.
Moja ya matatizo yanayosababishwa na tatizo la tumbo kubwa (kitambi) kwa wanawake ni kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi na matatizo mengine ya uzazi.
Katika makala hii tutaangazia sababu mbalimbali na madhara yanayotokana na tatizo la kitambi.
Moja ya kundi muhimu la chakula ni wanga. Kundi hili la chakula hutupatia nishati na uwezo wa kufanya kazi wa miili yetu.
Matumizi ya kundi hili la chakula yanapaswa kuzingatia uhitaji wa mwili kwa vile hili ndio aina pekee ya chakula ambayo ikizidi mwilini huhifadhiwa katika namna ya mafuta.
Matumizi ya vyakula vya wanga kupita kawaida husababisha tatizo hili kwa watu wengi hasa wale wasiojishughulisha na shughuli za hapa na pale.
Baadhi ya vyakula hivyo ni;
Mfano;
Huu ni mfano tu na haukuzuii kula, unaweza kula hata calori 5000 kwa siku lakini jambo la msingi ni kwamba ulaji uendane na mahitaji ya mwili.
Mara nyingi sukari ndani ya vinywaji hivi huwa na kiwango kikubwa cha nishati kiasi cha mwili kushindwa kuitumia yote.
Mfano;
Ni rahisi mtu kunywa chupa 3 za juisi ya kiwandani kuliko nusu kilo ya wali. Wakati calori ndani ya chupa tatu ni karibu mara mbili ya calori ndani ya nusu kilo ya wali.
Ni rahisi kuiga aina ya chakula au desturi ya kutojihusisha na mazoezi ya mwili kutoka kwa marafiki. Ni vyema kuchunguza aina ya marafiki ulionao na wanahusika vipi na tatizo la unene uliopita kiasi ulilonalo ama jaribu kutafakari ikiwa wanaweza kuwa chanzo cha wewe kupata tatizo hili.
Vivyo hivyo kadri unavyokuwa na umri mkubwa ndivyo uwezo wa uchakatwaji wa sukari unapungua, hivyo kusababisha mlundikano wa sukari mwilini katika namna ya mafuta.
Hali hii ni salama kwa afya, lakini baada ya kujifungua wanawake wengi hushindwa kupoteza ongezeko la uzito ambalo walilipata wakati wa ujauzito.
Magonjwa haya yanaweza kuathiri mfumo mzima wa mchakato wa matumizi ya sukari mwilini mfano ugonjwa wa cushing syndrome (hitilafu katika tezi ya adrenali).
Vilevile yanaweza kuathiri na kudhoofu utendaji kazi wa mwili, mfano ugonjwa wa maumivu ya maungio ya mwili ambapo mtu hushindwa kutembea hivyo kutojihusisha na shughuli zinazoweza kupunguza mlundikano wa mafuta mwilini.
Mfano mtu anaweza kurithi desturi ya kula kupita kiasi au kula aina fulani ya chakula pekee.
Vilevile mtu anaweza kurithi tabia za uvivu na hivyo kupelekea tatizo kuendelea kuwepo kizazi na kizazi.
Mbali na kurithi tabia lakini pia watu huweza kurithi vinasaba ambavyo kwa kiasi kikubwa ndio huusika na mambo kama vile kasi ya umeng’enywaji wa mafuta na sehemu zipi mafuta yahifadhiwe kwa wingi.
Mgawanyo wa mafuta mwilini kwa kiasi kikubwa huathiriwa na vinasaba.
Baadhi ya watu mgawanyo wa mafuta miilini mwao huthibitiwa na vinasaba ambapo baadhi huifadhi mafuta katika mapaja, wengine tumboni lakini pia wengine makalioni.
Moja ya athari kuu inayosababishwa na mafuta mengi mwilini ni kudhorota kwa utendaji kazi wa mfumo wa homoni mbalimbali za mwili.
Baadhi ya matatizo ya kiafya ambayo mtu huweza kuyapata kutokana na mafuta mengi mwilini ni pamoja na;
Mafuta mengi mwilini hupunguza uwezo wa ufanyaji kazi wa homoni ya insulini.
Homoni hii ndio hufanya kazi ya kumeng’enya na kubadili sukari ya ziada mwilini na kuipeleka katika muundo wa nishati abayo hutumiwa na mwili.
Kushindwa kufanya kazi kwa homoni hii kunaruhusu mlundikano wa sukari katika damu na kusababisha moja ya magonjwa hatari na yenye gharama kubwa ambao ni kisukari aina ya upili.
Saratani hizi husababishwa katika namna kuu zifuatazo;
Baadhi ya matatizo ya moyo yanayoweza kusababishwa na mafuta mengi mwilini ni pamoja na;
Sababu kuu ni kuwapo kwa chembe za mafuta huru katika damu hasa kwa wenye mafuta mengi mwilini, chembe ambazo huweza kuziba mishipa ya damu.
Shinikizo la damu, kushindwa kupumua na saratani yote haya ni miongoni mwa magonjwa 10 yanayoongoza kwa vifo duniani huku chanzo kikuu ikiwa ni kitambi.
Yapo mambo mengi yanayoweza kuchangia tatizo la tumbo kubwa (kitambi) lakini kula chakula chenye wanga kupita kawaida ndio sababu kuu ya tatizo hili.
Wanawake ni moja ya kundi kubwa ambalo huathiriwa zaidi na tatizo hili na kuwasababishia matatizo mengi.
Moja ya matatizo yanayosababishwa na tatizo la tumbo kubwa (kitambi) kwa wanawake ni kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi na matatizo mengine ya uzazi.
Katika makala hii tutaangazia sababu mbalimbali na madhara yanayotokana na tatizo la kitambi.
Sababu zinazopelekea tatizo la tumbo kubwa (kitambi).
Mpango lishe mbaya.
Mwili unahitaji mlo kamili kutoka katika aina zote kuu za chakula katika uwiano sawa kulingana na mahitaji ya mwili.Moja ya kundi muhimu la chakula ni wanga. Kundi hili la chakula hutupatia nishati na uwezo wa kufanya kazi wa miili yetu.
Matumizi ya kundi hili la chakula yanapaswa kuzingatia uhitaji wa mwili kwa vile hili ndio aina pekee ya chakula ambayo ikizidi mwilini huhifadhiwa katika namna ya mafuta.
Matumizi ya vyakula vya wanga kupita kawaida husababisha tatizo hili kwa watu wengi hasa wale wasiojishughulisha na shughuli za hapa na pale.
Baadhi ya vyakula hivyo ni;
- Ugali.
- Wali.
- Viazi.
- Mkate.
- Tambi.
- Chai ya maziwa hasa yenye sukari.
Mfano;
- Robo ya wali pekee uliopikwa ni takribani calori 550.
- Kinywaji juisi ya matunda au soda moja ni kati ya calori 150 hadi 200.
- Mafuta ya kupikia nusu kikombe ni zaidi ya calori 900.
- Mkate kipande kimoja ni calori 80.
Huu ni mfano tu na haukuzuii kula, unaweza kula hata calori 5000 kwa siku lakini jambo la msingi ni kwamba ulaji uendane na mahitaji ya mwili.
Matumizi ya Vinyaji vya nishati (energy drinks).
Vinywaji vingi vyenye ladha ya utamu vimeundwa na kiwango kikubwa cha wanga (sukari).Mara nyingi sukari ndani ya vinywaji hivi huwa na kiwango kikubwa cha nishati kiasi cha mwili kushindwa kuitumia yote.
Mfano;
- Vinyaji vya nishati (energy drinks),
- Soda.
- Pombe hasa bia.
- Juisi za matunda.
Ni rahisi mtu kunywa chupa 3 za juisi ya kiwandani kuliko nusu kilo ya wali. Wakati calori ndani ya chupa tatu ni karibu mara mbili ya calori ndani ya nusu kilo ya wali.
Uzembe na uvivu.
Kwa asilimia kubwa chakula unachokula kina sukari ambayo inapaswa kuupatia nishati mwili. Mwili hutumia nishati hii kupitia shughuli mbalimbali kama vile;- Kutembea.
- Kukimbia.
- Kupika.
- Kuruka kamba.
- Kucheza.
Msukumo kutoka kwa marafiki na jamaa.
Marafiki, ndugu na jamaa wana ushawishi mkubwa katika maisha yako. Aina ya jamaa zako au marafiki inaweza kuwa chanzo cha wewe kuwa na kitambi.Ni rahisi kuiga aina ya chakula au desturi ya kutojihusisha na mazoezi ya mwili kutoka kwa marafiki. Ni vyema kuchunguza aina ya marafiki ulionao na wanahusika vipi na tatizo la unene uliopita kiasi ulilonalo ama jaribu kutafakari ikiwa wanaweza kuwa chanzo cha wewe kupata tatizo hili.
Umri.
Kadri unavokuwa mwili wako unapoteza uwezo wa kiutendaji ikiwemo uchakatwaji wa vyakula mbalimbali.Vivyo hivyo kadri unavyokuwa na umri mkubwa ndivyo uwezo wa uchakatwaji wa sukari unapungua, hivyo kusababisha mlundikano wa sukari mwilini katika namna ya mafuta.
Kitambi kinachotokana na kujifungua.
Wakati wa ujauzito mwanamke huongezeka uzito kwa kiasi kikubwa.Hali hii ni salama kwa afya, lakini baada ya kujifungua wanawake wengi hushindwa kupoteza ongezeko la uzito ambalo walilipata wakati wa ujauzito.
Magonjwa.
Kuna baadhi ya magonjwa husababisha kuongezeka kwa mlundikano wa sukari mwilini.Magonjwa haya yanaweza kuathiri mfumo mzima wa mchakato wa matumizi ya sukari mwilini mfano ugonjwa wa cushing syndrome (hitilafu katika tezi ya adrenali).
Vilevile yanaweza kuathiri na kudhoofu utendaji kazi wa mwili, mfano ugonjwa wa maumivu ya maungio ya mwili ambapo mtu hushindwa kutembea hivyo kutojihusisha na shughuli zinazoweza kupunguza mlundikano wa mafuta mwilini.
Urithi wa tabia na vinasaba.
Kwa watu wengi tatizo la tumbo kubwa (kitambi) huonekana kama ni la ukoo, hii si kweli. Mara nyingi watu hurithi tabia ambazo kitaalamu ndio huchangia kutokea kwa kitambi.Mfano mtu anaweza kurithi desturi ya kula kupita kiasi au kula aina fulani ya chakula pekee.
Vilevile mtu anaweza kurithi tabia za uvivu na hivyo kupelekea tatizo kuendelea kuwepo kizazi na kizazi.
Mbali na kurithi tabia lakini pia watu huweza kurithi vinasaba ambavyo kwa kiasi kikubwa ndio huusika na mambo kama vile kasi ya umeng’enywaji wa mafuta na sehemu zipi mafuta yahifadhiwe kwa wingi.
Mgawanyo wa mafuta mwilini kwa kiasi kikubwa huathiriwa na vinasaba.
Baadhi ya watu mgawanyo wa mafuta miilini mwao huthibitiwa na vinasaba ambapo baadhi huifadhi mafuta katika mapaja, wengine tumboni lakini pia wengine makalioni.
Sababu za kijamii na kisaikolojia.
Pia kuna sababu mbalimbali za kijamii na kisaikolojia ambazo zinaweza kusababisha ongezeko la uzito na kupelekea kitambi. Baadhi ya sababu hizi ni;- Msongo wa mawazo.
- Upweke.
- Wasiwasi.
- Kukosa usingizi.
- Uvutaji sigara na bangi.
- Kuongeza hamu ya kula. mfano uvutaji bange na kukosa usingizi.
- Kuvurugika kwa utendaji kazi wa homoni. mfano msongo wa mawazo.
Madhara ya kiafya yatokanayo na tatizo la kitambi
Kiwango kikubwa cha mafuta mwilini huathiri utendaji kazi wa mwili kwa namna tofauti.Moja ya athari kuu inayosababishwa na mafuta mengi mwilini ni kudhorota kwa utendaji kazi wa mfumo wa homoni mbalimbali za mwili.
Baadhi ya matatizo ya kiafya ambayo mtu huweza kuyapata kutokana na mafuta mengi mwilini ni pamoja na;
Kisukari aina ya upili.
Tafiti za kutosha zimethibitisha kwamba hatari ya kupata kisukari huongezeka mara dufu kwa watu wenye kiwango kikubwa cha mafuta mwilini.Mafuta mengi mwilini hupunguza uwezo wa ufanyaji kazi wa homoni ya insulini.
Homoni hii ndio hufanya kazi ya kumeng’enya na kubadili sukari ya ziada mwilini na kuipeleka katika muundo wa nishati abayo hutumiwa na mwili.
Kushindwa kufanya kazi kwa homoni hii kunaruhusu mlundikano wa sukari katika damu na kusababisha moja ya magonjwa hatari na yenye gharama kubwa ambao ni kisukari aina ya upili.
Magonjwa ya saratani.
Mafuta mengi mwilini husababisha saratani mbalimbali kama vile Saratani ya matiti, saratani ya mlango wa kizazi, saratani ya mfuko wa uzazi, saratani ya koo, saratani ya utumbo n.k.Saratani hizi husababishwa katika namna kuu zifuatazo;
- Ongezeko la insulini.
Kuzidiwa kazi kwa homoni ya insulini kunasababisha mwili kuzalisha insulini kwa wingi zaidi ili kufidia mahitaji ya mwili. Kuongezeka kwa insulini mwilini kunasababisha uzalishwaji wa homoni za oestrojeni.
Homoni hizi hupatikana zaidi kwa wanawake lakini pia hupatikana kwa wanaume. Kiasi kikubwa cha oestrojeni hupelekea seli kuzalishwa kwa wingi hasa maeneo ya uzazi hivyo kuufanya mfumo wa uzazi hasa wa mwanamke kuwa katika hatari ya kushambuliwa na saratani.

- Kutengenezwa kwa uvimbe.
Mafuta mengi huzuia seli mbalimbali za mwili kufikiwa na hewa ya oksijeni kwa urahisi. Hali hii hupelekea seli kufa na mwili kuitikia kwa kutengeneza uvimbe.
Uvimbe usipothibitiwa unaweza kuchagiza ukuaji wa seli usio na uthibiti na hatimaye saratani kutokea. Vilevile homoni za oestrojeni huweza kutengenezwa moja kwa moja kutoka katika mafuta ya mwili kwa msaada wa kichocheo/kichagizi cha aromatase.

Matatizo ya hedhi kwa wanawake.
Moja ya athari kubwa za mafuta mengi mwilini ni mwanamke kuandamwa na matatizo mbalimbali ya hedhi ikiwemo;- Hedhi isiyo na mpangilio.
- Kukosa hedhi.
- Damu nyingi ya hedhi.
- Maumivu makali wakati wa hedhi.
Maradhi ya moyo.
Yapo maatizo mengi ambayo yanaweza kuathiriwa moyo na mzunguko wa damu kwa ujumla. Mafuta mengi mwilini ni chanzo kikuu cha matatizo haya ya moyo.Baadhi ya matatizo ya moyo yanayoweza kusababishwa na mafuta mengi mwilini ni pamoja na;
- Shinikizo la damu.
Mafuta mengi mwilini husababisha mgandamizo kwenye mishipa ya damu. Mgandamizo huu husababisha kipenyo cha mishipa ya damu kupungua na damu kupita kwa shida.
- Matatizo ya figo.
- Kuziba kwa mishipa ya damu.
Hii ni hali ambayo hutokea pale mishipa ya damu huziba hivyo kusababisha sehemu ya pili ya mshipa kukosa damu na hewa ya oksijeni. Hali hii ni hatari kwa uhai na huambatana na maumivu makali sana.
Sababu kuu ni kuwapo kwa chembe za mafuta huru katika damu hasa kwa wenye mafuta mengi mwilini, chembe ambazo huweza kuziba mishipa ya damu.
Hali hii inaweza kutokea sehemu yoyote ya mwili lakini ubongo na moyo ndio sehemu ambazo huathiriwa zaidi. Ikitokea katika moyo huitwa shambulizi la moyo na ikitokea katika ubongo kiharusi.
Kupungua kwa kipenyo katika milija hii kunaongeza msukumo wa ndani ya kifua hivyo kusababisha shida ya kupumua/kukoroma na mtu kukosa usingizi.
Lakini pia mafuta mengi katika nyongo ni moja ya chanzo kikubwa cha kutengenezwa kwa mawe katika ogani hii muhimu kwa ajili ya mmengenyo wa chakula.
Mojawapo ni maumivu makali ya vifundo vya miguu ambayo hutokana na mwili kushindwa kuhimili uzito mkuwa wa mwili.
Pia tatizo la gout ambalo hutokana n na kiwango kikubwa cha dutu za uriate (taka zinazotokana na kuvunjwa kwa protini aina ya purine).
Kiwango cha dutu hizi kinatokana na kuharibiwa kwa figo ambalo hufanya kazi ya kuchuja na kuondoa takamwili hizi.
Kukosa usingizi.
Kukosa usingizi kwa watu wenye kitambi husababishwa na kupungua kwa kipenyo cha milija ya hewa ambayo kuntokana na mlundikano wa mafuta mwilini.Kupungua kwa kipenyo katika milija hii kunaongeza msukumo wa ndani ya kifua hivyo kusababisha shida ya kupumua/kukoroma na mtu kukosa usingizi.
Maradhi ya ini na nyongo.
Mafuta mengi mwilini (rehemu) huweza kuhifadhiwa sehemu yeyote ya mwili ikiwemo ini. Ikiwa mafuta yatafika katika ini basi utendaji kazi wa ogani hii muhimu ya mwili huathiriwa na kuweza kusababisha madhara mengi ikiwemo ini kujaa maji na kuvimba.Lakini pia mafuta mengi katika nyongo ni moja ya chanzo kikubwa cha kutengenezwa kwa mawe katika ogani hii muhimu kwa ajili ya mmengenyo wa chakula.
Maradhi ya maungio ya mwili.
Maradhi mbalimbali yanayoathiri maungio ya mwili huweza kuathiriwa na uwepo wa mafuta mengi mwilini.Mojawapo ni maumivu makali ya vifundo vya miguu ambayo hutokana na mwili kushindwa kuhimili uzito mkuwa wa mwili.
Pia tatizo la gout ambalo hutokana n na kiwango kikubwa cha dutu za uriate (taka zinazotokana na kuvunjwa kwa protini aina ya purine).
Kiwango cha dutu hizi kinatokana na kuharibiwa kwa figo ambalo hufanya kazi ya kuchuja na kuondoa takamwili hizi.
Matatizo ya uzazi kwa wanawake wajawazito.
Wajawazito ni moja ya kundi ambalo huathiriwa zaidi na ongezeko la uzito. Uzito mkubwa kwa wajawazito unaweza kusababisha matatizo yafuatayo;- Kifafa cha mimba.
- Mimba kuharibika.
- Shinikizo la damu.
- Kisukari cha mimba.
Hitimisho
Kwa bahati mbaya tatizo la kitambi huwa haliandamani na kitu chochote ambacho kinaweza kuwa ishara ikiwa tayari umeanza kupata madhara mwilini.
Mara nyingi madhara yake hutokea ghafla na kwa sehemu kubwa madhara yake husababisha vifo vya ghafla au ksababisha magonjwa sugu kama kisukari.
Ikiwa uko katika hatari ya kupata tatizo hili basi unashauriwa kufika kituo cha afya au kuonana na wataalamu wa afya kwa ajili ya uchunguzi.
Baadhi ya mambo unayopaswa kufanya ni kupima urefu na uzito mara kwa mara kisha kokotoa BMI ili kujua ni kwa kiwango gani uko kwenye hatari hii.