Ugonjwa wa Homa ya mapafu, aina zake, sababu na tiba.
Ugonjwa wa Nimonia ni aina ya homa ya mapafu ambayo huathiri vifuko vya hewa (viriba hewa) ndani ya mapafu ambapo viriba hewa ndani ya mapafu huvimba na kujawa na maji au usaha.
Mbali na viriba hewa, ugonjwa huu pia unaathiri milija ya hewa ya bronki ambayo huingiza hewa katika mapafu.
Tatizo hili linaweza kuathiri sehemu ndogo ya pafu au pafu lote kwa ujumla.
Ugonjwa wa Nimonia unaweza kusababishwa na vimelea mbalimbali wamagonjwa kama ile bakteria, virusi, kuvu (fangasi) na minyoo.
Nimonia ni miongoni mwa magonjwa 3 yanayoyoongoza kwa vifo nchini Tanzania ikishika nafasi ya 2.
Katika makala hii tutakudadafulia kwa kina na kwa lugha rahisi mambo yote muhimu unayopaswa kujua kuhusu tatizo hili la nimonia.
Mfumo wa upumuaji kama moja ya mifumo muhimu zaidi katika mwili una mifumo na namna zake kadhaa za ulinzi mbali na ulinzi wa jumla wa mwili.
Hitilafu yeyote katika mifumo hii ya ulinzi ndani ya mapafu inaweza kusababisha mwili kukumbwa na ugonjwa huu wa nimonia.
Hitilafu hizi katika mfumo wa ulinzi zinaweza kusababishwa na mabadiliko ya kiutendaji ya mwili au sababu za kukwaa kutoka nje ya mwili, mfano magonjwa na tabia hatarishi za kiafya.
Baadhi mambo yanayoweza kusababisha hitilafu katika mifumo ya ulinzi katika mfumo wa upumuaji ni ni pamoja na;
Mbali na viriba hewa, ugonjwa huu pia unaathiri milija ya hewa ya bronki ambayo huingiza hewa katika mapafu.
Tatizo hili linaweza kuathiri sehemu ndogo ya pafu au pafu lote kwa ujumla.
Ugonjwa wa Nimonia unaweza kusababishwa na vimelea mbalimbali wamagonjwa kama ile bakteria, virusi, kuvu (fangasi) na minyoo.
Nimonia ni miongoni mwa magonjwa 3 yanayoyoongoza kwa vifo nchini Tanzania ikishika nafasi ya 2.
Katika makala hii tutakudadafulia kwa kina na kwa lugha rahisi mambo yote muhimu unayopaswa kujua kuhusu tatizo hili la nimonia.
Homa ya mapafu husababishwa na nini?
Mwili umeundwa na mifumo kadhaa ya ulinzi dhidi ya hatari mbalimbali za mwili.Mfumo wa upumuaji kama moja ya mifumo muhimu zaidi katika mwili una mifumo na namna zake kadhaa za ulinzi mbali na ulinzi wa jumla wa mwili.
Hitilafu yeyote katika mifumo hii ya ulinzi ndani ya mapafu inaweza kusababisha mwili kukumbwa na ugonjwa huu wa nimonia.
Hitilafu hizi katika mfumo wa ulinzi zinaweza kusababishwa na mabadiliko ya kiutendaji ya mwili au sababu za kukwaa kutoka nje ya mwili, mfano magonjwa na tabia hatarishi za kiafya.
Baadhi mambo yanayoweza kusababisha hitilafu katika mifumo ya ulinzi katika mfumo wa upumuaji ni ni pamoja na;
01: Upungufu wa kinga mwulini.
Kinga za mwili huweza kupungua kwa sababu nyingi lakini moja ya sababu kubwa ni maradhi haya virusi kama UKIMWI na maradhi ya kuvu (fangasi) sugu.
Nimonia ya aina hii husababishwa na bakteria wa Legionella, Mycoplasma pneumoniae, Chlamydia pneumoniae, na Chlamydia psittaci.
Kutokana na kwamba aina hii ya nimonia kwa kiasi kikubwa husababishwa na Mycoplasma pneumoniae kwa hivyo ni kawaida aina hii ya nimonia kwenda sambamba na matatizo ya sikio.
Baadhi ya dalili za aina hii ya nimonia ni pamoja na:
Nimonia ya aina hii inaweza kuwa nimonia kali au ya kawaida.
Vimelea wengi wanaopatikana maeneo ya hospitalini na vituo vya afya wameonyesha kuwa na usugu wa dawa kwa kiasi kikubwa.
Hivyo nimonia inayoambukizwa maeneo ya vituo vya afya inahitaji uangalizi na uratibu mzuri wa matibabu yake ili kuleta ufanisi kwa kuwa hutumia dawa zaidi ya moja.
Mtu aliyeathiriwa na aina hii ya nimonia sehemu kubwa ya milija yake ya bronki inakuwa na uvimbe na baadhi ya maeneo ya mapafu hasa sehemu ambako milija hii inaingia.
Kwa mtu aliyeathiriwa na aina hii ya nimonia ikiwa hatopatiwa tiba kwa haraka basi nimonia ya mapafu hupitia hatua nne kabla ya mwili wenyewe kupambana na tatizo na kulimaliza.
Hatua hizo ni kama ifuatavyo;
02: Kuharibiwa kwa vinyweleo ndani ya mfumo wa upumuaji.
Vinyweleo hivi husaidia kuchuja vimelea mbalimbali vya magonjwa. Tatizo hili kwa kiasi kikubwa husababishwa na uvutaji wa sigara.
03: Hitilafu katika utengenezwaji wa makohozi.
Makohozi katika mfumo wa upumuaji ambayo hufanya kazi ya kudaka uchafu na vimelea vya magonjwa katika hewa.
04: Kulundikana kwa makohozi na ute ndani ya mfumo wa upumuaji hususa ni katika viriba hewa.
Mara nyingi husababishwa na kukujamana kwa milija kadhaa ya hewa au uvimbe katika milija ya ya hewa.
05: Kuvurugika kwa mlinganyo wa vimelea katika mapafu.
Vimelea wa faida mwilini wako kila mahali , mapafu ikiwa ni sehemu mojawapo. Kuharibiwa kwa mlinganyo wa vimelea hawa kunapelekea jamii moja ya vimelea kutawala kuliko nyingine.
Hali hii ni hatari hupelekea mwili kutafsiri jamii inayozidi kawaida kama adui hivyo kusababisha kutengenezwa kwa uvimbe kama njia ya mwili kujihami.
Hitilafu yeyote kati ya hizi zilizotajwa hapa juu zinapelekea mtu kupata ugonjwa wa nimonia kwa urahisi zaidi.
Baadhi ya vimelea ambavyo husababisha tatizo la nimonia ni kama ifuatavyo.
Kwa watu hawa fangasi wafuatao wanaweza kuingia miilini mwao na kuathiri mapafu.Histoplasma.
Njia kuu ambayo bakteria hawa wanaweza kufika katika mapafu ni kupitia hewa.
Yafuatayo ni mambo ambayo yanaongeza nafasi na uwezekano wa vimelea hawa kufika atika mapafu kwa urahisi zaidi.
Hitilafu yeyote kati ya hizi zilizotajwa hapa juu zinapelekea mtu kupata ugonjwa wa nimonia kwa urahisi zaidi.
Jinsi homa ya mapafu inavyotokea.
Uvimbe katika viriba hewa vya mapafu hutokea ikiwa ni mchakato wa kawaida wa mwili kujihami dhidi ya hatari mbalimbali ndani ya mwili. Mara nyingi uvimbe ndani ya mwili hutengenezwa ikiwa kuna jeraha au vimelea.Baadhi ya vimelea ambavyo husababisha tatizo la nimonia ni kama ifuatavyo.
Vimelea vya bakteria.
Kuna kundi kubwa la bakteria ambao husababisha matatizo katika mapafu. Wafuatao ni bakteria mashuhuri kwa kusababisha ugonjwa wa nimonia,Pneumococcus.- Haemophilus influenzae.
- Moraxella catarrhalis.
- Kundi la bakteria jamii ya Streptococcus.
- Legionella, Mycoplasma, Chlamydia.
Vimelea vya virusi.
Baadhi ya virusi ambao husababisha nimonia ni pamoja na;Influenza virus.- Respiratory syncytial virus.
- Parainfluenza virus.
- Adenoviruses.
- COVID-19.
Vimelea wa kuvu(fangasi).
Fangasi wanaweza kusababisha nimonia kwa watu ambao kinga za miili yao ziko chini kutokana na sababu kadhaa ikiwemo magonjwa, mfano UKIMWI.Kwa watu hawa fangasi wafuatao wanaweza kuingia miilini mwao na kuathiri mapafu.Histoplasma.
- Blastomyces.
- Coccidioides.
Jinsi homa ya mapafu inaweza kusambaa.
Ugonjwa wa nimonia unaweza kusambaa kwa njia yeyote ambayo itasababisha bakteria wanaosababisha vimelea hawa kufika katika mapafu.Njia kuu ambayo bakteria hawa wanaweza kufika katika mapafu ni kupitia hewa.
Yafuatayo ni mambo ambayo yanaongeza nafasi na uwezekano wa vimelea hawa kufika atika mapafu kwa urahisi zaidi.
- Kuvuta hewa iliyochanganyikana au kunywa maji yaliyochanganyikana na vimelea hawa. Mfano bakteria Legionella pneumonia husambaa zaidi kwa njia ya hewa.
- Kukaa maeneo yenye msongamano kama vile sokoni, jela na kuchangia mavazi na malazi kunaongeza uwezekano wa kupata bakteria wa treptococcus pneumonia, Mycobacteria, Mycoplasma, na Chlamydia.
- Kujichanganya na wanyama na ndege. Mfano wa vimelea wanaosababisha nimonia na wanopatikana kwenye wanyama ni Coxiella burnetii na Chlamydia psittaci.
- Matumizi ya vifaa vya kusaidia kupumua mfano mipira ya kusaidia kupumua wakati wa upasuaji hasa maeneo ya hospitalini.
Aina za ugonjwa wa homa ya mapafu.
Aina za ugonjwa wa nimonia zimegawaywa kulingana na kuzingatia vigezo vya aina tofauti. Vigezo vikuu vinavyotumiwa kwa sehemu kubwa ni kama ifuatavyo;- Mgawanyo kwa kuzingatia chanzo cha nimonia.
- Mgawanyo unaozingatia eneo ambalo mgonjwa amepata nimonia,
- Na tatu ni mgawanyo kwa kuzingatia maeneo yaliyoathiriwa na tatizo katika mapafu.
Mgawanyo kwa kuzingatia chanzo cha homa ya mapafu.
Katika mgawanyo huu kuna aina kuu mbili za homa ya mapafu (nimonia);Nimonia ya kawaida.
Hii ni aina ya nimonia ambayo inaambatana na dalili za kawaida kama vile;- homa.
- Mafua.
- koo kuwasha.
- Baridi.
- kikohozi cha mara kwa mara.
- maumivu ya kichwa.
- maumivu ya kifua na
- uchovu na maumivu ya misuli.
Nimonia ya aina hii husababishwa na bakteria wa Legionella, Mycoplasma pneumoniae, Chlamydia pneumoniae, na Chlamydia psittaci.
Kutokana na kwamba aina hii ya nimonia kwa kiasi kikubwa husababishwa na Mycoplasma pneumoniae kwa hivyo ni kawaida aina hii ya nimonia kwenda sambamba na matatizo ya sikio.
Nimonia kali.
Hii ni aina ya nimonia ambayo huambatana na homa kali kiasi cha kupelekea mgonjwa kushindwa kufanya shughuli za kila siku. Mara nyingi mgonjwa mwenye aina hii ya nimonia anahitajika kulazwa.Baadhi ya dalili za aina hii ya nimonia ni pamoja na:
- kikohozi kikali kilichoambatana na damu au makohozi ya rangi.
- Kutetemeka.
- Kutokwa jasho jingi.
- Homa kali.
- Maumivu makali ya kifua.
- Kupumua kwa shida
- kupungua uzito na mwili kukosa nguvu.
- Streptococcus pneumoniae,
- Haemophilus influenzae,
- Staphylococcus aureus, streptococci, na
- Moraxella catarrhalis.
Mgawanyo unaozingatia eneo ambalo mgonjwa amepata homa ya mapafu.
Katika mgawanyo huu kuna aina kuu mbili za nimonia, ambazo ni;- Nimonia inayotokana na maambukizi nje ya hospitali.
- Aina ya pili ni Nimonia inayotokana na maambukizi ndani ya hospitali.
Nimonia inayotokana na maambukizi nje ya hospitali.
Hii ni aina ya Nimonia inayoambukizwa katika maeneo yoyote nje ya hospitalini au kituo cha afya. Ni aina ya nimonia mbayo huwaathiri watu wengi zaidi kuliko aina yeyote ya nimonia.Nimonia ya aina hii inaweza kuwa nimonia kali au ya kawaida.
Bakteria wanaoongoza kwa kusababisha aina hii ya nimonia ni Streptococcus pneumoniae, Klebsiella pneumoniae, na Haemophilus influenzae.
Kuvu (fangasi) wanaosababisha aina hii ya nimonia ni pamoja na Histoplasma, Blastomyces, na Coccidioides
Mtu anaweza kupata nimonia akiwa hospitalini katika njia zifuatazo;
Kuvu (fangasi) wanaosababisha aina hii ya nimonia ni pamoja na Histoplasma, Blastomyces, na Coccidioides
Nimonia inayotokana na maambukizi ndani ya kituo cha afya.
Anina hii ya nimonia humpata mtu ambae yupo katika mazingira ya hospitalini. Hospitalini ni mahali ambapo si salama kuishi ama kukaa bila tahadhari muhimu.Mtu anaweza kupata nimonia akiwa hospitalini katika njia zifuatazo;
- Vimelea huingia katika mapafu kupitia mipira ya kupumulia.
- Mtu anaweza kupata nimonia kwa kuvuta hewa au kutumia vifaa vilivyochanganyikana na vimelea.
- Mtu anaweza kupata vimelea vya nimonia anapopatiwa huduma katika gari ya wagonjwa, kugusana na mgonjwa au mhudumu wa afya.
Vimelea wengi wanaopatikana maeneo ya hospitalini na vituo vya afya wameonyesha kuwa na usugu wa dawa kwa kiasi kikubwa.
Hivyo nimonia inayoambukizwa maeneo ya vituo vya afya inahitaji uangalizi na uratibu mzuri wa matibabu yake ili kuleta ufanisi kwa kuwa hutumia dawa zaidi ya moja.
Mgawanyo kwa kuzingatia maeneo yaliyoathiriwa na tatizo katika mapafu.
Katika mgawanyo huu kuna aina kuu mbili za nimonia, ambazo ni;Nimonia ya milija ya bronki.
Hii huathiri kuanzia maeneo ya milija ya hewa ya bronki. Milija hii ndio inayoingiza hewa katika mapafu.Mtu aliyeathiriwa na aina hii ya nimonia sehemu kubwa ya milija yake ya bronki inakuwa na uvimbe na baadhi ya maeneo ya mapafu hasa sehemu ambako milija hii inaingia.
Nimonia ya mapafu.
Hii huathiri zaidi maeneo ya ndani ya mapafu ambapo viriba hewa katika sehemu ndogo au pafu lote kwa ujumla vinavimba na kujaa maji au usaha.Kwa mtu aliyeathiriwa na aina hii ya nimonia ikiwa hatopatiwa tiba kwa haraka basi nimonia ya mapafu hupitia hatua nne kabla ya mwili wenyewe kupambana na tatizo na kulimaliza.
Hatua hizo ni kama ifuatavyo;
- Kwanza ni kulundikana kwa vimelea, maji na seli za ulinzi katika mapafu.
- Pili ni mapafu kuruhusu kuaza kutengeneza uvimba hivyo mapafu huwa magumu.
- Tatu ni kuharibiwa kwa dutu zote zilizoshiriki kutengenezwa kwa uvimbe ikiwemo seli za damu.
- Na mwisho ni kutolewa kwa uchafu uliotengenezwa kama makohozi