Jinsi ya kutambua aina ya ngozi yako
Kama ilivyo maeneo mengine ya mwili kama vile kinywa, Ngozi yetu inahitaji huduma na matunzo ya kila siku angalau mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni.
Katika kuhakikisha utunzaji bora wa ngozi yako, unahitaji kufahamu aina ya ngozi yako.
Ni muhimu kufahamu ikiwa ngozi yako ni ya kawaida, ya
mafuta, ni nyeti, ni kavu, au ni mchanganyiko ili kuweza kuihudumia kikamilifu.
Vilevile unapaswa kufahamu kwamba si kila sehemu ya ngozi
yako inahitaji matunzo sawa.
Kuna baadhi ya sehemu za ngozi kama vile maeneo ya kuzunguka
macho, shingo, uso na midomo, maeneo haya ngozi yake huwa ni tofauti kidogo na
maeneo mengine na yanahitaji matunzo na huduna maalumu.
Jinsi ya kutambua aina ya ngozi yako.
Muonekano bora wa ngozi yako huathiriwa zaidi na aina ya
ngozi yako na utunzaji. Ni vyema kufahamu ya kwamba kila mtu amezaliwa na aina
maalumu ya ngozi na hakuna kinachoweza kubadilisha hilo.
Katika makala hii utapata dondoo muhimu zitakazokusaidia kutambua
aina ya ngozi yako na kukusaidia kuamua njia bora ya utunzaji wa ngozi yako.
Soma kwa makini sehemu hii kwa sababu matunzo yako ya ngozi
pasipo kujua aina yako ya ngozi ni sawa na kazi bure na pengine hupelekea uharibifu
zaidi wa ngozi yako.
Ili kutambua aina yako ya ngozi kiurahisi, historia ya
mabadiliko ya ngozi yako toka kipindi cha utoto ni nguzo muhimu zaidi katika kutambua aina ya ngozi yako.
Njia rahisi itakayotumika kukusaidia kufahamu aina yako ya ngozi
inahusisha maswali ambayo yatahusu historia yako, ikiwa utakumbuka majibu ya maswali mengi utakayoulizwa basi
itarahisisha zoezi la utambuzi wa aina ya ngozi yako.
Na hata kama hautakumbuka baadhi ya majibu ya maswali
utakayoulizwa bado una nafasi ya kutambua aina yako ya ngozi bila wasiwasi.
Katika makala hii tumekuandalia orodha ya maswali 18 ambayo yatatumika kukusaidia kutambua aina ya ngozi yako kwa urahisi zaidi.
Maswali muhimu ya kukusaidia kujua aina ya ngozi yako
Jibu maswali haya kwa majibu ya “Ndio” au “Hapana”. Ili kurahisisha zoezi hili, hakikisha unatumia kalamu na karatasi kisha andika namba ya kila swali ikifuatiwa na jibu lake.
Maswali haya ni kama ifuatavyo;
- Je, ngozi yako ya ni nyororo na hubonyea kama mpira inapoguswa au kuminywa?
- Je, ngozi inayozunguka macho yako muda wote inaoneka kama imevimba au kulegea?
- Je, ngozi yako invutika? Kufahamu kama ngozi yako inavutika fanya hivi binya ngozi yako kwa sekunde 5, kisha iachie. Ikiwa inachukua zaidi ya sekunde 3 kurudi sura yake ya kawaida basi ngozi yako haina sifa ya kuvutika.
- Je, mwonekano wa ngozi yako unang'aa mithili ya uangavu wa mwanga kutoka ndani ya ngozi?
- Je, ukiachana na kukosa usingizi, chakula duni na uvutaji sigara kuna mambo mengine zaidi ambayo hukusababishia matatizo ya ngozi?
- Je mashina ya vinyweleo vyako yanaonekana kuwa makubwa kiasi cha kuyatambua kwa umbali wa sentimita 20?
- Je, ngozi yako ya uso huwa inaonyesha mwangaza wa mafuta ndani ya masaa manne baada ya kuosha uso wako?
- Je, ngozi yako ni nene na ina mwonekano mgumu?
- Je, ngozi yako inaonekana kuwa na muonekano wa ngozi ya mtoto ili hali una umri mkubwa?
- Je, ngozi yako inaungua kwa urahisi unapokuwa juani?
- Je, ngozi yako ina tabia ya kuonesha wekundu inapopigwa na upepo au wakati wa kuoshwa kwa sabuni na maji?
- Je, una matatizo ya mizio/aleji ambayo hupelekea ngozi kuvimba?
- Je, muda mwingi maeneo ya mashavu ya uso wako huwa makavu ukilinganisha na maeneo mengine ya uso kama vile komwe na ngozi kuzunguka pua.
- Je, ngozi yako ni ya kung’ara au kufifia? Jibu ndio ikiwa ni ya kung'ara, hapana ikiwa ni ya kufifia
- Je, una chunusi zenye vichwa vyeupe vinavyoonekana?
- Je! ngozi yako ina mwonekano usio sawa wa makunyanzi?
- Je, huwa unapata matatizo ya chunusi mara kwa mara?
- Je, ngozi yako hupata Maumivu mara kwa mara?
Mchanganuo wa majibu yako ya “Ndio” au “Hapana”
katika maswali haya 18 yapo kama ifuatavyo;
- Ikiwa majibu yako ya “Ndio” ni kati ya 1–4 katika jumla ya majibu yote 18 uliyoyatoa, basi una aina ya ngozi ya kawaida.
- Ikiwa majibu yako ya “Ndio” ni kati ya 5–8 katika jumla ya majibu yote 18 uliyoyatoa basi una aina ya ngozi ya mafuta.
- Kama majibu yako ya “Ndio” ni kati ya 9–12 katika jumla ya majibu yote 18 uliyoyatoa basi una aina ya ngozi nyeti/ngozi nyepesi kuathiriwa na kila kinachogusa ngozi yako.
- Ikiwa majibu yako ya “Ndio” ni kati ya 13–16 katika jumla ya majibu yote 18 uliyoyatoa basi una aina ya ngozi yenye mchanganyiko wa mafuta na ukavu.
- Na ikiwa majibu yako ya “Ndio” ni kati ya 16+ Una aina ya ngozi ambayo hupata chunusi kwa haraka, au ngozi ya chunusi.