Sababu kuu 9 za Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi na tiba yake
Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi ni moja ya tatizo la hedhi linalowasumbua wanawake wengi. Wanawake walio wengi huwa katika wakati mgumu na kujawa na hofu wanapopatwa na tatizo hili.
Mara nyingi tatizo hili haliathiri mpangilio wa mzunguko wa hedhi na hujitokeza katika siku za kawaida za mzunguko. Lakini huambatana na damu nyingi kupita kawaida.
Zipo sababu nyingi ambazo huweza kusababisha mwanamke kutokwa na damu nyingi kupita kawaida katika mzunguko wake wa kawaida.
Ukuaji wa seli wa namna hii unaweza kutokea sehemu nyinezo za mfumo wa uzazi kama vile ovari, milija ya falopia, kibofu na shingo ya kizazi.
Mbali na tatizo hili kusababisha damu nyingi kutoka vilevile huambatana na maumivu makali, kuharibu mpangilio wa hedhi na wakati mwingine husababisha ugumba.
Kwa wanawake wenye PID damu nyingi wakati wa hedhi huambatana na
Kwa sasa wimbi kubwa la wanawake hutumia njia za kisasa za kupanga uzazi kama vile sindano, vidonge, vijiti na vitanzi.
Mbali na faida za kutumia njia hizi lakini njia hizi pia ni moja ya vyanzo vikuu vya matatizo mbalimbali ya mzunguko wa hedhi.
Njia ya kitanzi ni moja ya sababu kuu za kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi kwa sababu ya mabadiliko makubwa ya homoni yanayotokea.
Hali huwa mbaya zaidi katika hatua za mwanzo za kutumia njia hii na wakati mwingine madhara makubwa huweza kutokea ikiwa kitanzi kimekaa vibaya.
Njia hii huondoa kabisa kizazi cha mwanamke na kupoteza uwezo wake wa kuzaa.
Matumizi ya vyakula maalumu kama ifuatavyo;
Kwa hivyo matumizi ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha madini haya ni moja ya msaada mkubwa kwa wanawake wenye tatizo hili.
Ili kuleta mlinganyo wa homoni vitamini A ni moja ya virutubisho vyenye msaada mkubwa. Baadhi ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamini A ni mbogamboga na matunda.
Flavanoidi ni muhimu kwa sababu huimarisha mzunguko wa damu, hupunguza kiwango kikubwa cha oestrogen. Limao na machunga ni moja ya mimea yenye kiwango kikubwa cha flavonoidi.
Baadhi ya mitishamba yenye kiwango kikubwa cha kemikali hizi ni pamoja na
Hedhi inayozidi siku 7, hedhi nzito inayofanya ubadili pedi moja ndani ya masaa mawili, hnapata hedhi nzito inayolowesha hadi nguo za nje, hnapata hedhi nzito inayokulazimu kuamka usiku kubadiri pedi na hedhi inayotoka na mabonge ya damu
Mara nyingi tatizo hili haliathiri mpangilio wa mzunguko wa hedhi na hujitokeza katika siku za kawaida za mzunguko. Lakini huambatana na damu nyingi kupita kawaida.
Zipo sababu nyingi ambazo huweza kusababisha mwanamke kutokwa na damu nyingi kupita kawaida katika mzunguko wake wa kawaida.
Nyingi ya sababu za tatizo hili ni za kawaida ambazo husababishwa na mabadiliko ya kiutendaji ya mwili.
Lakini kuna wakati tatizo hili husababishwa na magonjwa hatari hasa yanayoathiri mfumo wa uzazi kupelekea tatizo kuwa kubwa kiasi cha kuhatarisha uhai wa mwanamke.
Katika hali hii mwanamke huhitaji msaada wa dharula wa kitabibu pamoja na vipimo vya kina ili kubaini iwapo kuna tatizo ambalo ndio chanzo.
Sawa na vijiko 16 vya chai. Ikiwa damu itatoka nyingi zaidi ya kiwango hiki basi mwanamke huwekwa katika kundi la wanawake wenye tatizo hili.
Mabadiliko haya yanaweza kusababishwa na mkazo (stress), matumizi ya dawa, uzito mkubwa na mazoezi mazito.
Wanawake wengi wenye tatizo hili wameonekana kuwa na kiwango kikubwa cha homoni ya oestrogen ambayo hupelekea kuzalishwa kwa prostaglandins kwa wingi.
Prostaglandins ni kemikali ambazo husababisha mishipa ya damu kutanuka vilevile kupunguza uzito wa damu. Jambo hili hupelekea damu kutoka kwa urahisi na kwa wingi.
Uvimbe huu hutokea katika misuli iliyounda kuta za mfuko huu, na huwaathiri zaidi wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 30.
Uvimbe huu unaweza kuonekana kwa kipimo cha mwangwi wa sauti (ultrasound). Na unaweza kuonyesha dalili au usionyeshe.
Ikiwa utaonyesha dalili basi zifuatao ni dalili muhimu ambazo huashiria uwepo wa uvimbe katika mfuko wa uzazi.
Lakini kuna wakati tatizo hili husababishwa na magonjwa hatari hasa yanayoathiri mfumo wa uzazi kupelekea tatizo kuwa kubwa kiasi cha kuhatarisha uhai wa mwanamke.
Katika hali hii mwanamke huhitaji msaada wa dharula wa kitabibu pamoja na vipimo vya kina ili kubaini iwapo kuna tatizo ambalo ndio chanzo.
Kipi ni kiasi sahihi cha damu ya hedhi?
Kitaalamu hedhi iliyo sawa huchukua kati ya siku 3 hadi 5. Katika siku hizi mwanamke atatokwa na damu mfululizo, jumla ya damu kwa siku zote za hedhi haipaswi kuzidi mililita 80.Sawa na vijiko 16 vya chai. Ikiwa damu itatoka nyingi zaidi ya kiwango hiki basi mwanamke huwekwa katika kundi la wanawake wenye tatizo hili.
Sababu za Kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi
Zifuatazo ni baadhi ya sababu kuu ambazo husababisha tatizo la kutokwa damu nyingi kuliko kawaida wakati wa hedhi.1: Mabadiliko ya homoni.
Kwa baadhi ya wanawake ambao hupata tatizo hili bila kuathirika kwa mpangilio wa mzunguko wao basi hii ni moja ya sababu kubwa.Mabadiliko haya yanaweza kusababishwa na mkazo (stress), matumizi ya dawa, uzito mkubwa na mazoezi mazito.
Wanawake wengi wenye tatizo hili wameonekana kuwa na kiwango kikubwa cha homoni ya oestrogen ambayo hupelekea kuzalishwa kwa prostaglandins kwa wingi.
Prostaglandins ni kemikali ambazo husababisha mishipa ya damu kutanuka vilevile kupunguza uzito wa damu. Jambo hili hupelekea damu kutoka kwa urahisi na kwa wingi.
2: Uvimbe katika mfuko wa uzazi.
Uvimbe wa kawaida ambao sio wa saratani katika mfuko wa uzazi ni moja ya sababu za kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi.Uvimbe huu hutokea katika misuli iliyounda kuta za mfuko huu, na huwaathiri zaidi wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 30.
Uvimbe huu unaweza kuonekana kwa kipimo cha mwangwi wa sauti (ultrasound). Na unaweza kuonyesha dalili au usionyeshe.
Ikiwa utaonyesha dalili basi zifuatao ni dalili muhimu ambazo huashiria uwepo wa uvimbe katika mfuko wa uzazi.
- Kukojoa mara kwa mara.
- Maumivu makali chini ya kitovu.
- Tumbo kujaa mithiri ya mjamzito.
- Kuhisi mkandamizo chini ya kitovu.
- Mimba kuharibika mara kwa mara.
3: Ukuaji wa seli za mfuko wa uzazi usio wa kawaida.
Kuna wakati seli zinazounda ukuta wa mfuko wa uzazi huweza kukua bila uthibiti na kusababisha uvimbe mgumu. Uvimbe huu unaweza ukakua na kugeuka kuwa seli za saratani.4: Ukuaji wa seli za mfuko wa uzazi sehemu isiyo sahihi.
Hii hujitokeza ikiwa seli za kawaida za ukuta wa mfuko wa uzazi zinakuwa mahali ambapo si sahihi.Seli hii huendelea kuthibitiwa na homoni za uzazi na kipindi cha hedhi nazo hutolewa nje kama damu hivyo kiwango cha damu kuongezeka.
Ukuaji wa seli wa namna hii unaweza kutokea sehemu nyinezo za mfumo wa uzazi kama vile ovari, milija ya falopia, kibofu na shingo ya kizazi.
Mbali na tatizo hili kusababisha damu nyingi kutoka vilevile huambatana na maumivu makali, kuharibu mpangilio wa hedhi na wakati mwingine husababisha ugumba.
5: Maradhi ya uvimbe katika via vya uzazi (PID).
Haya ni maradhi ambayo husababishwa na maambukizi ya bakteria ambao husambaa kwa njia ya kujamiana au njia nyinginezo.Kwa wanawake wenye PID damu nyingi wakati wa hedhi huambatana na
- Kutokuwapo kwa mpangilio wa mzunguko wa hedhi.
- Homa kali.
- Mwili kuchoka kupita kawaida.
- Uchafu au ute wenye harufu kali ikiwa PID imesababishwa na gonorrhoea.
6: Matumizi njia za vitanzi katika kupanga uzazi.
Kwa sasa ni wanawake wachache sana ambao hutumia njia za asili za kupanga uzazi. Pengine ni kutokana na woga na wasiwasi wa ufanisi wa njia hizi za asili.Kwa sasa wimbi kubwa la wanawake hutumia njia za kisasa za kupanga uzazi kama vile sindano, vidonge, vijiti na vitanzi.
Mbali na faida za kutumia njia hizi lakini njia hizi pia ni moja ya vyanzo vikuu vya matatizo mbalimbali ya mzunguko wa hedhi.
Njia ya kitanzi ni moja ya sababu kuu za kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi kwa sababu ya mabadiliko makubwa ya homoni yanayotokea.
Hali huwa mbaya zaidi katika hatua za mwanzo za kutumia njia hii na wakati mwingine madhara makubwa huweza kutokea ikiwa kitanzi kimekaa vibaya.
7: Upungufu wa lishe.
Upungufu wa lishe mwilini ni chanzo mojawapo cha kutoka damu nyingi kupita kawaida. Upungufu wa madini joto ya chuma husababisha ugonjwa wa kutokwa damu.Ikiwa mwanamke atakuwa na upungufu wa madini haya basi inaweza kuwa ni hatari zaidi kwa afya yake.
Yote haya ni magonjwa hatari kwa vile husababisha damu kutoka bila kuganda kwa muda mrefu. Vilevile maradhi katika ini yanaweza kuwa chanzo cha kupata hedhi yenye damu nyingi kupita kawaida.
Hii ni kutokana na umuhimu wa ini katika kutengeneza kemikali zinazosaidia damu kuganda. Hivyo kuathirika kwa ini na uzalishaji wa kemikali hizi huathirika pia.
Lengo ni kutambua chanzo hasa ikiwa chanzo ni ugonjwa. Mtaalamu wa afya anaweza kutumia njia mbalimbali kufanikisha uchunguzi wake kama vile;
8: Magonjwa ya damu kushindwa kuganda.
Magonjwa kama anemia (damu kushindwa kuganda), von Willebrand (upungufu wa kemikali ya factor x ambayo husaidia damu kuganda.Yote haya ni magonjwa hatari kwa vile husababisha damu kutoka bila kuganda kwa muda mrefu. Vilevile maradhi katika ini yanaweza kuwa chanzo cha kupata hedhi yenye damu nyingi kupita kawaida.
Hii ni kutokana na umuhimu wa ini katika kutengeneza kemikali zinazosaidia damu kuganda. Hivyo kuathirika kwa ini na uzalishaji wa kemikali hizi huathirika pia.
9: Kuharibika kwa mimba.
Wakati mwingine mwanamke hupata hedhi yenye damu nyingi ikiwa mimba imeharibika ama kwa kukusudia au bila kukusudia.Jinsi gani ya kutambua sababu ya kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi.
Hakuna njia moja ya kutambua ni nini kinasababisha tatizo hili kwa mwanamke bali kuna mkusanyiko wa vipimo na uchunguzi ambavyo vinaweza kutumika.Lengo ni kutambua chanzo hasa ikiwa chanzo ni ugonjwa. Mtaalamu wa afya anaweza kutumia njia mbalimbali kufanikisha uchunguzi wake kama vile;
- Kupima sampuli yad amu.
- Kupima ute kutoka katika mfumo wa uzazi.
- Kutumia vifaa vya mwangwi sauti (ultrasound).
- Kwa kutumia vifaa vya kamera.
Dawa ya kuzuia kutokwa damu nyingi ya hedhi
Njia za kawaida za kuzuia damu nyingi ya hedhi
- Kurekebisha mitindo ya maisha.
- Kufanya mazoezi,
- kula vizuri,
- kupumzisha mwili
- kupunguza msongo wa mawazo.
Njia za kisasa za kuzuia damu nyingi ya hedhi
Ikiwa tatizo linatokana na mabadiliko ya homoni basi mwanamke anaweza kutumia dawa maalumu za homoni ili kuleta msawazo wa homoni mwilini. Baadhi ya dawa hizo ni pamoja na;- Progestogens.
- Prostaglandins inhibitors.
- Progestogen-releasing IUD.
- GnRH agonists
Njia hii huondoa kabisa kizazi cha mwanamke na kupoteza uwezo wake wa kuzaa.
Njia za asili za kuzuia damu nyingi ya hedhi
Kuna vyakula na mitishamba ya aina mbalimbali ambayo huweza kusaidia kuleta ulinganifu wa homoni mwilini vile vile kuzuia damu kutoka kwa wingi.Matumizi ya vyakula maalumu kama ifuatavyo;
01: Madini joto ya chuma.
Utafiti unaonyesha wanawake wengi wanaosumbuliwa na kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi wa upungufu wa madini ya chuma (iron).Kwa hivyo matumizi ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha madini haya ni moja ya msaada mkubwa kwa wanawake wenye tatizo hili.
Baadhi ya vyakula hivyo ni
- figili,
- matembele,
- samaki
- nyama nyekundu.
02: Vitamini A.
Vitamini A husaidia kutengenezwa kwa homoni za oestrogen. Upungufu wa vitamini A unasababisha kupungua kwa homoni ya oestrogen.Ili kuleta mlinganyo wa homoni vitamini A ni moja ya virutubisho vyenye msaada mkubwa. Baadhi ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamini A ni mbogamboga na matunda.
03: Vitamini K.
Virutubisho hivi husaidia damu kuganda. Mboga za majani ni chanzo kikuu cha virutubisho hivi vya vitamini K.04: Kemikali za flavonoidi.
Kundi hili la kemikali lina kazi nyingi sana mwilini, kwa mwanamke mwenye tatizo la kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi.Flavanoidi ni muhimu kwa sababu huimarisha mzunguko wa damu, hupunguza kiwango kikubwa cha oestrogen. Limao na machunga ni moja ya mimea yenye kiwango kikubwa cha flavonoidi.
05: Mitishamba inayopunguza kasi ya damu katika mfuko wa uzazi.
Kemikali za saponins, flavonoids na tannis zimeonyesha msaada mkubwa katika kupunguza kasi ya utokaji damu katika kuta za mfuko wa uzazi.Baadhi ya mitishamba yenye kiwango kikubwa cha kemikali hizi ni pamoja na
- Trillium erectum(bethroot),
- Equisetum arvense(Horsetail),
- Achillea millefolium(yarrow),
- Tienchi ginseng.
- Capsella bursa-pastoris(shepherd purse)
- Hydrastis canadensis(goldenseal),
- Alchemilla vulgaris (lady's mantle),
- Geranium maculatum(wild geranium)
06: Mitishamba inayopunguza maumivu ya hedhi.
Zipo kemikali ambazo hutumika kutibu maumivu yatokanayo na hedhi kwa ufanisi wa hali ya juu. Baadhi ya mitishamba hiyo ni pamoja na- Angelica sinensis(female ginseng),
- Chamaelirium luteum(blazing star),
- Rubus idaeus(red raspberry).
- Caulophyllum thalictroides(blue cohosh),
- Mitchella repens(partridge berry),
- Aletris farinose(colic root),
- Paeonia lactiflora(peony)
- Rehmannia glutinosa(chinese foxglove)
- Withania somnifera(ashwagandha/winter cherry),
- Hypericum perforatum(st john's wort)
Hitimisho
Tatizo la kutokwa damu nyingi ya hedhi ni la kawaida sana kwa wanawake. Mwanamke anapaswa kutilia shaka tatizo hili iwapo atapata dalili zifuatazo;
Hedhi inayozidi siku 7, hedhi nzito inayofanya ubadili pedi moja ndani ya masaa mawili, hnapata hedhi nzito inayolowesha hadi nguo za nje, hnapata hedhi nzito inayokulazimu kuamka usiku kubadiri pedi na hedhi inayotoka na mabonge ya damu
Mbali na tiba zilizoorodheshwa katika makala hii, tatizo hili linaweza kuwa kubwa kiasi cha kupelekea tiba maalumu na za juu zaidi kutumiwa kama vile; upasuaji wa kuondoa uvimbe, Upasuaji wa kuzibua mishipa ya damu katika mji wa uzazi na dawa maalumu za kugandisha damu.