Jinsi ya kutunza ngozi kwa watu wenye miaka 0 hadi 20
Utunzaji wa ngozi una changamoto nyingi. Zipo sababu nyingi ambazo husababisha utunzaji wa ngozi kuwa changamoto.
Baadhi ya changamoto hizi ni ufahamu mdogo kuhusu mahitaji ya ngozi katika vipindi mbalimbali ya ukuaji.
Ni ngozi ambayo inakuwa na kila sifa ya uzuri na uwezo mkubwa wa kujitengeneza kwa ufanisi wa hali ya juu ndani ya muda mfupi pindi ipatapo majeraha madogo na michubuko.
Kawaida mtoto anatakiwa kuogeshwa mara moja kwa siku kwa sabuni safi isiyoweza kuleta madhara katika ngozi ya mtoto.
Mtoto anapofikisha umri wa miaka 3 na kuendelea hali hubadilika kidogo. Hii inatokana na hali na hamasa ya mtoto kutaka kujifunza na kucheza michezo kadhaa ambayo inaweza kumsababishia ajali au maambukizi ya magonjwa ya ngozi.
Mtoto anapofikia hatua hii njia pekee na bora ya kuhakikisha muonekano wa ngozi yake unakuwa imara ni;
Katika hatua hii kuna changamoto kuu mbili zinazoweza kuathiri muonekano na afya ya ngozi. Changamoto hizo ni:
Moja ya mabadiliko haya ni ongezeko la utengenezwaji wa homoni za uzazi. Kutengenezwa kwa homoni hizi kunaathiri tezi za sebamu.
Homoni hizi husababisha kutengenezwa kwa mafuta katika ngozi. Mafuta haya yanaweza kuwa mengi kiasi cha kuathiri utendaji kazi wa ngozi.
Athari za mafuta katika ngozi yatokanayo na ongezeko la homoni kunategemea zaidi na aina ya ngozi ya muhusika.
Kwa watu ambao ngozi zao ni za asili ya mafuta, basi mabadiliko haya huwa na athari hasi zaidi kwao.
Mafuta mengi katika ngozi husababisha mambo yafuatayo ambayo si rafiki kwa afya ya ngozi yako:
Baadhi ya changamoto hizi ni ufahamu mdogo kuhusu mahitaji ya ngozi katika vipindi mbalimbali ya ukuaji.
Katika makala hii tutakuangazia njia mbalimbali za kutunza ngozi kwa makundi mbalimbali, kuanzia watoto wenye miaka 0 hadi vijana wa miaka 20.
Jinsi ya kutunza ngozi kwa watoto wenye miaka 0 hadi 10
Kwa mtoto mwenye afya njema ngozi yake huwa ni bora, imara na yenye muonekano mzuri wa kuvutia.Ni ngozi ambayo inakuwa na kila sifa ya uzuri na uwezo mkubwa wa kujitengeneza kwa ufanisi wa hali ya juu ndani ya muda mfupi pindi ipatapo majeraha madogo na michubuko.
Kawaida mtoto anatakiwa kuogeshwa mara moja kwa siku kwa sabuni safi isiyoweza kuleta madhara katika ngozi ya mtoto.
Mtoto anapofikisha umri wa miaka 3 na kuendelea hali hubadilika kidogo. Hii inatokana na hali na hamasa ya mtoto kutaka kujifunza na kucheza michezo kadhaa ambayo inaweza kumsababishia ajali au maambukizi ya magonjwa ya ngozi.
Mtoto anapofikia hatua hii njia pekee na bora ya kuhakikisha muonekano wa ngozi yake unakuwa imara ni;
- Kumuandalia mazingira safi ya kucheza na kujifunza.
- Kumuweka mbali na mambo yanayoweza kumsababishia ajali.
- Kumtafutia maligahafi sahihi za kuchezea ili kuimarisha na kutunza hali ya kujifunza na ubunifu.
- Kumsaidia usafi kwa ujumla ikiwemo usafi wa mwili na nguo kwa ujumla.
- Hakikisha anapata chakula bora kwa ukuaji wa ngozi na afya ya mwili kwa ujumla.
- Tumia vipodozi vya kumkinga na jua aendapo shuleni ama awapo nyumbani.
- Matunda na mboga za majani ni muhimu zaidi kwa mtoto.
Jinsi ya kutunza ngozi kwa vijana wenye miaka 10 hadi 20.
Mtoto afikishapo miaka 10 hadi 14 ngozi yake huanza kubadilika na afikiapo hatua ya balehe ngozi hubadilika kwa kiasi kikubwa.Katika hatua hii kuna changamoto kuu mbili zinazoweza kuathiri muonekano na afya ya ngozi. Changamoto hizo ni:
- Ongezeko la uzalishwaji wa homoni za uzazi.
- Msukumo wa kutaka kuwa na mvuto kunakosababishwa na balehe, makundi, marafiki na misukumo ya mitandao ya kijamii.
- Ongezeko la uzalishwaji wa homoni za uzazi.
Moja ya mabadiliko haya ni ongezeko la utengenezwaji wa homoni za uzazi. Kutengenezwa kwa homoni hizi kunaathiri tezi za sebamu.
Homoni hizi husababisha kutengenezwa kwa mafuta katika ngozi. Mafuta haya yanaweza kuwa mengi kiasi cha kuathiri utendaji kazi wa ngozi.
Athari za mafuta katika ngozi yatokanayo na ongezeko la homoni kunategemea zaidi na aina ya ngozi ya muhusika.
Kwa watu ambao ngozi zao ni za asili ya mafuta, basi mabadiliko haya huwa na athari hasi zaidi kwao.
Mafuta mengi katika ngozi husababisha mambo yafuatayo ambayo si rafiki kwa afya ya ngozi yako:
- Ngozi kushindwa kupumua vizuri.
- Husababisha ngozi kushika uchafu kwa urahisi.
- Kusababisha jasho kugandamana katika ngozi kwa urahisi.
- Kutoa mazingira rafiki ya vimelea kuzaliana katika ngozi.
Chunusi hizi zinaweza kujitokeza sehemu yoyote ya ngozi ya mwili, lakini usoni na mgongoni ndio huathiriwa zaidi.
Lakini kama ni mtu ambaye unakuwa juani kwa muda mrefu walau dakika 30 kwa siku basi unashauri kutumia vipodozi hivi ili kuongeza ufanisi wa ulinzi katika ngozi.
Kwa kutumia njia sahihi za utunzaji, ngozi nyeusi ni urembo usio kifani na aina yeyote ya urembo wa mwonekano.
Saikolojia ya kwamba ngozi bora ni lazima iwe na rangi nyeupe au kahawia hii ni saikolojia ya kitumwa na ni moja ya mambo yanayowasababishia watu wengi matatizo ya ngozi na saratani kwa kujiingiza kwenye matumizi hatari ya kemikali na vipodozi.
Katika umri huu wa balehe ni jambo la kawaida kwa vijana wengi kutamani ngozi zenye muonekano wa rangi nyeupe au kahawia.
Matamanio haya huwafanya kutumia kemikali na vipodozi kadhaa kwa lengo la kuwa na mionekano ya rangi hizi.
Moja ya vipodozi wanavyotumia ni santans. Santans ni vipodozi ambavyo hubadili rangi ya ngozi kwa muda mfupi.
Kwa sehemu kubwa vipodozi hivi ni salama ikiwa vitatumika kwa kiasi mfano udongo. Lakini matumizi ya mara kwa mara ya vipodozi hivi ni moja ya sababu kubwa zinazoelekea kuwahi kuzeeka kwa ngozi.
Mambo muhimu ya kuzingatia katika kutunza ngozi
Ili kuzuia au kupunguza athari hii yafuatayo ni muhimu kuzingatiwa katika utunzaji wa ngozi yako;- Usipasue chunusi, kwa kufanya hivyo unasambaza bakteria ambao husababisha tatizo hili sehemu nyingine za mwili.
- Zingatia usafi binafsi na wa mazingira yanayokuzunguka.
- Tumia kipodozi mahususi kulingana na aina ya ngozi yako.
- Fanya Scrub walau mara 2 kwa wiki, usizidisha kwa maana scrub pia inaweza kuongeza tatizo ikiwa itafanywa kupita kawaida ya mwili kuhimili.
- Kwa wale ambao ngozi zao ni za mafuta wanaweza kutumia dawa maalumu za kuzuia kuzaliana kwa bakteria, vilevile dawa za kuua bakteria na kukausha vidonda.
- Usitumie vipodozi vinavyobadili rangi ya ngozi yako, mfano suntan (kipodozi kinachokufanya uonekane na rangi ya kahawia). Vipodozi hivi huboresha muonekano lakini ni hatari kutumiwa kwa muda mrefu.
- Usitumie vipodozi mara kwa mara, mara moja au mbili kwa siku inatosha.
- Hakikisha unakwenda kitandani umenawa uso na kuoga vilevile usilale umepaka vipodozi mwilini au usoni.
- Hakikisha unanyoa nywele zako maeneo yote ya mwili.
- Ikiwa ngozi yako imeathika zaidi usisite kuonana na wataalamu wa ngozi.
- Kula vyakula vyenye virutubisho vya vitamini muhimu kwa wingi kama vila matunda, mbegu, samaki na maini.
- Usitumie vyakula vyenye sukari kwa wingi kwa kuwa huchagiza kutengenezwa kwa uvimbe katika mwili wako.fanya mazoezi na shiriki katika michezo.
- Tumia vipodozi vinavyozuia mwanga wa jua.
Lakini kama ni mtu ambaye unakuwa juani kwa muda mrefu walau dakika 30 kwa siku basi unashauri kutumia vipodozi hivi ili kuongeza ufanisi wa ulinzi katika ngozi.
Hitimisho
Rangi nyeusi ndio rangi bora na stahimilivu zaidi dhidi ya hatari mbalimbali za ngozi hasa mionzi ya jua.Kwa kutumia njia sahihi za utunzaji, ngozi nyeusi ni urembo usio kifani na aina yeyote ya urembo wa mwonekano.