Mambo makuu 2 yanayoathiri ubora wa ngozi yako
Urembo wa ngozi ni moja ya vitu muhimu katika kuimarisha muonekano wako. Je, unafahamu ya kuwa unaweza kuwa na ngozi bora na yenye muonekano mzuri bila kujali umri wako.
Ni kweli kwamba kila uongezekapo umri ngozi yako pia hupata mabadiliko na changamoto mpya.
Mfano unapokuwa mtoto ngozi yako huwa ni nzuri na yenye kuvutia kupita kawaida, hali hii hubadilika pale unapofikia umri wa balehe.
Mabadiliko haya husababishwa na ongezeko la utengenezwaji wa homoni za uzazi ambazo kwa sehemu kubwa hubadili muonekano wa ngozi.
Katika hatua hii changamoto kubwa ni ongezeko la homoni.
Kwa kutambua changamoto mbalimbali za ubora wa ngozi zinazojitokeza kwa watu katika hatua mbalimbali za ukuaji, hii itakusaidia kufahamu ni jinsi gani ya kutunza na nini cha kufanya kukabiliana na changamoto husika.
Katika makala hii tutaangazia ni changamoto gani uzitegemee katika hatua mbalimbali za ukuaji ambazo huathiri ubora na mwonekano wa ngozi yako kwa sehemu kubwa.
Ulizaliwa na aina fulani ya mpangilio wa vinasaba katika kuthibiti muonekano na ukuaji wa ngozi yako.
Kila mtu anazaliwa tayari mpangilio wake wa vinasaba umeshatoa muelekeo wa ukuaji wa ngozi yake ambapo;
Si rahisi kupambana na mapungufu yeyote yanayosababishwa na vinasaba kwa maana hivo ndivyo ulivyo na hauwezi kubadilika kiurahisi.
Habari njema ni kwamba kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia baadhi ya mapungufu yatokanayo na vinasaba yanaweza kupatiwa ufumbuzi.
Vilevile tabia na mitindo kadhaa ya maisha binafsi pia magonjwa na hali ya afya ya mwili kwa ujumla.
Baadhi ya mambo ambayo huathiri ubora wa ngozi ni pamoja na;
Ni kweli kwamba kila uongezekapo umri ngozi yako pia hupata mabadiliko na changamoto mpya.
Mfano unapokuwa mtoto ngozi yako huwa ni nzuri na yenye kuvutia kupita kawaida, hali hii hubadilika pale unapofikia umri wa balehe.
Mabadiliko haya husababishwa na ongezeko la utengenezwaji wa homoni za uzazi ambazo kwa sehemu kubwa hubadili muonekano wa ngozi.
Katika hatua hii changamoto kubwa ni ongezeko la homoni.
Kwa kutambua changamoto mbalimbali za ubora wa ngozi zinazojitokeza kwa watu katika hatua mbalimbali za ukuaji, hii itakusaidia kufahamu ni jinsi gani ya kutunza na nini cha kufanya kukabiliana na changamoto husika.
Katika makala hii tutaangazia ni changamoto gani uzitegemee katika hatua mbalimbali za ukuaji ambazo huathiri ubora na mwonekano wa ngozi yako kwa sehemu kubwa.
Mambo yanyoathiri kuzeeka kwa ngozi.
Mabadiliko ya muonekano, umbo na ubora wa ngozi hutokea kwa kutegemea zaidi mambo makuu mawili;- Msukumo wa vinasaba.
- Msukumo wa mazingira ya nje ya mwili na tabia.
Vinasaba na muonekano wa ngozi.
Katika msukumo huu wa mabadiliko ya ngozi hutegemea zaidi na chembe za urithi au vinasaba (DNA).Ulizaliwa na aina fulani ya mpangilio wa vinasaba katika kuthibiti muonekano na ukuaji wa ngozi yako.
Kila mtu anazaliwa tayari mpangilio wake wa vinasaba umeshatoa muelekeo wa ukuaji wa ngozi yake ambapo;
- Baadhi ya watu vinasaba vyao husababisha mikunjo na makunyanzi toka wakiwa wadogo.
- Wengine vinasaba huarakisha uzeekaji wa ngozi.
- Huku baadhi yao viasaba vya viko katika mpangilio wa kuchelewesha uzee.
Si rahisi kupambana na mapungufu yeyote yanayosababishwa na vinasaba kwa maana hivo ndivyo ulivyo na hauwezi kubadilika kiurahisi.
Habari njema ni kwamba kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia baadhi ya mapungufu yatokanayo na vinasaba yanaweza kupatiwa ufumbuzi.
Athari za mazingira na tabia katika muonekano wa ngozi.
Katika muktadha huu mabadiliko ya ngozi huathiriwa zaidi na vitu mbalimbali katika mazingira ambavyo ama huifikia ngozi moja kwa moja kwa kugusana au kutokugusana.Vilevile tabia na mitindo kadhaa ya maisha binafsi pia magonjwa na hali ya afya ya mwili kwa ujumla.
Baadhi ya mambo ambayo huathiri ubora wa ngozi ni pamoja na;
- Mwanga wa jua.
- Matumizi ya vipodozi.
- Magonjwa mbalimbali ya ngozi na mwili kwa ujumla.
- Usafi binafsi wa mwili.
- Ulevi.
- Uvutaji wa sigara.
- Aina ya vyakula unavyotumia.
Hitimisho
Mbali na vinasaba, sababu nyinginezo zote ambazo huathiri ubora wa ngozi zinaweza kudhibitiwa kiurahisi.
Mfano chakula, vipodozi na usafi binafsi, vyote hivi huweza kudhibitiwa kwa urahisi iwapo utapata elimu bora juu ya aina ya ngozi yako na nini ngozi yako inahitaji.