Utunzaji wa ngozi ya mwili, mambo muhimu ya kufahamu
Ngozi ni kiungo tata na ndicho kiungo kikubwa zaidi katika mwili wako. Muonekano wa ngozi yako unaweza kutoa taswira halisi juu ya afya yako kwa ujumla.
Ngozi yako ni utambulisho wako, kwa sababu ndio kitu cha kwanza kuonekana kwa watu, upende usipende watu watakuhukumu kutokana na muonekano wa ngozi yako.
Makovu, mapunye, vibalango, vipele, na matatizo mengine ya ngozi ni viashiria vya kwamba kuna tatizo katika ngozi au matatizo mengineyo ya kiafya.
Kwa hivyo hali ya ngozi yako ni jambo la muhimu na la kutilia maanani.
Kuna vipodozi vya kila aina ambavyo hupatikana katika gharama tofauti, lakini kwa sehemu kubwa ngozi yako inahitaji chakula na si vipodozi kama unavyodhani.
Jambo la msingi ni kufahamu aina ya ngozi yako na nini inahitaji ili kuhakikisha afya na muonekano wa ngozi yako unakuwa bora.
Ngozi yako ni utambulisho wako, kwa sababu ndio kitu cha kwanza kuonekana kwa watu, upende usipende watu watakuhukumu kutokana na muonekano wa ngozi yako.
Makovu, mapunye, vibalango, vipele, na matatizo mengine ya ngozi ni viashiria vya kwamba kuna tatizo katika ngozi au matatizo mengineyo ya kiafya.
Kwa hivyo hali ya ngozi yako ni jambo la muhimu na la kutilia maanani.
Kwanini ni muhimu kutunza ngozi yako?
Ngozi ni utambulisho, utambulisho ambao unaweza kukusaidia katika kufanikisha mambo mbalimbali katika maisha ikiwemo;- Muonekano wa ngozi unaweza kukusaidia kupata au kukosa mchumba au mwenza wa maisha kiurahisi
- Baadhi ya kazi hasa za sanaa zinahitaji muonekano mzuri wa nje hasa ngozi, muonekano wa ngozi unaweza kuathiri upatikanaji wa aina hizi za kazi
- Muonekano wa ngozi yako unaweza kukuamulia aina ya marafiki.
- Vilevile muonekano wa ngozi unaweza kuathiri biashara yako kwa wateja wako hasa biashara za urembo na chakula.
Jinsi ya kutunza ngozi yako.
Katika kuhakikisha muonekano bora wa ngozi yako wenye afya, unapaswa kuzingatia vitu vikubwa 3 ambavyo ni;- Aina za ngozi za mwili.
- Chakula unachokula ndani ya mwili
- Na vitu unavyopaka katika ngozi yako
Kuna gharama gani katika kutunza ngozi yako?
Tofauti na unavyodhani , ya kwamba kuwa na ngozi bora kunahitaji pesa nyingi! Hapana, nadharia hii si sahihi kwa kuwa utunzaji wa ngozi ni kufuata miongozo bora kulingana na aina yako ya ngozi.Kuna vipodozi vya kila aina ambavyo hupatikana katika gharama tofauti, lakini kwa sehemu kubwa ngozi yako inahitaji chakula na si vipodozi kama unavyodhani.
Jambo la msingi ni kufahamu aina ya ngozi yako na nini inahitaji ili kuhakikisha afya na muonekano wa ngozi yako unakuwa bora.
Ngozi bora ina sifa zipi?
Ngozi bora yenye muonekano mzuri na wa kuvutia ina sifa Zifuatazo- Ngozi bora ni angavu yenye rangi inayoeleweka
- Kwa ngozi za kiafrika rangi ya ngozi inaweza kuwa nyeusi, maji ya kunde au kahawia
- Ngozi haitakiwi kuwa kavu sana, iwe na unyevu lakini yenye uangavu
- Ngozi bora huvutika bila kuharibu muonekano wake
- Pia ngozi bora haitakiwi kujimenya wala kutengenezwa magamba
- Ngozi bora haina madoa, vipele, au wekundu
Kuwa mwangalifu usihukumu ngozi yako kulingana na picha za wanamitindo mitandaoni na kwenye matangazo.
Picha hizi zimehaririwa kwa kiwango kikubwa kiasi cha kuficha vinyweleo na mikunjo midogo midogo ambayo ni ya kawaida katika ngozi.
Mabadiliko ya ngozi
Fahamu ya kwamba ngozi bora haiokei kwa siku moja. Ngozi bora inahitaji jitihada kubwa hasa katika kubadili na kujitoa sadaka kwa baadhi ya mitindo ya maisha.
Hata kama utafanikiwa kufuata taratibu za utunzaji bora wa ngozi, fahamu kwamba si kila siku ngozi yako itakuwa na muonekano bora.
Kuna mambo ambayo kwa wakati fulani yanaweza kusababisha muonekano wa ngozi yako kubadilika bila kujali ni kwa kiwango gani unaitunza ngozi yako.
Katika nyakati hizi ni vizuri kujitathmini ni kujua ni nini kimepelekea mabadiliko ya ghafla kuliko kuanza kutumia vipodozi.
Baadhi ya mambo ambayo yanaweza kusababisha mabadiliko ya ghafla ya muonekano wa ngozi yako ni pamoja na;
Imezoeleka kuwa ngozi huwa na muonekano bora na wa kuvutia zaidi kwa watu wenye umri wa kati ya miaka 20 hadi 30.
Lakini ukweli ni kwamba katika umri wowote unaweza kuwa na ngozi bora na ya kuvutia iwapo utafuata miongozo bora ya namna nzuri ya kutunza ngozi yako.
Ngozi ndio ogani kubwa zaidi katika mwili wako kuliko ogani nyingine yoyote.
Katika mwili wako ngozi ina kazi kuu zifuatazo:
Pamoja na kwamba ngozi hupata chakula kupitia damu ambayo hufika katika ngozi kupitia mtandao wa mishipa ya damu, chakula ni moja ya msaada mkubwa ambao ngozi inahitaji kutoka kwako.
Kutokufanya hivyo kunaichosha ngozi kwa haraka na kuisababisha kuzidiwa na kuizeeka mapema.
Keratinocytes, seli hizi husaidia kutengenezwa seli za ngozi zilizoharibiwa,
Melanocytes, seli hizi husaidia kutengenezwa rangi ya ngozi, kwa asili rangi inayotengenezwa na seli hizi ni nyeusi, na muonekano wa rangi nyeusi wa mtu hutegemea na kiwango cha rangi kilichotengenezwa na seli hizi
Langerhans cells, seli hizi husaidia kuimarisha kinga maeneo ya ngozi kwa kutambua hisia na migusu ambayo ianakuja karibu na ngozi.
Tabaka la nje limegawanyika katika matabaka makuu 6 ambayo ni;
Kupukutika au kujimenya kwa seli hizi ni kitendo cha kibaolojia cha kiautomatiki lakini pia kitendo hiki kinaweza kuharakishwa na matumizi ya vipodozi yanayomenya ngozi.
Mfano matumizi ya Scrub huharakisha hatua hii.
Tabaka hili limeundwa na mafuta kwa kiasi kikubwa.
Seli katika tabaka hili imeshonana kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba ikiwa zitapata jeraha basi sehemu kubwa ya seli huathiriwa.
Ni katika tabaka hili ambapo saratani nyingi za ngozi huanzia ikiwa litapata hitilafu.
Seli za keratini na Melanini zote hupatikana katika tabaka hili. Hitilafu katika sehemu hii inaweza kupelekea kupata matatizo ya saratani kwa urahisi.
Tabaka hili limeundwa na vitu vifuatavyo:
Mchanganyiko wa takamwili hizi una hali ya tindikali ambayo inatoa faida ya ulinzi dhidi ya vimelea vinavyoathiri ngozi.
Hata kama utafanikiwa kufuata taratibu za utunzaji bora wa ngozi, fahamu kwamba si kila siku ngozi yako itakuwa na muonekano bora.
Kuna mambo ambayo kwa wakati fulani yanaweza kusababisha muonekano wa ngozi yako kubadilika bila kujali ni kwa kiwango gani unaitunza ngozi yako.
Katika nyakati hizi ni vizuri kujitathmini ni kujua ni nini kimepelekea mabadiliko ya ghafla kuliko kuanza kutumia vipodozi.
Baadhi ya mambo ambayo yanaweza kusababisha mabadiliko ya ghafla ya muonekano wa ngozi yako ni pamoja na;
- Mabadiliko ya homoni, hasa wakati wa hedhi kwa wanawake.
- Msongo wa mawazo
- Kukosa usingizi wa kutosha
- Vilevile unapaswa kufahamu ya kuwa ngozi huzeeka, na kadri inavyozeeka ndivyo inapoteza ubora.
Imezoeleka kuwa ngozi huwa na muonekano bora na wa kuvutia zaidi kwa watu wenye umri wa kati ya miaka 20 hadi 30.
Lakini ukweli ni kwamba katika umri wowote unaweza kuwa na ngozi bora na ya kuvutia iwapo utafuata miongozo bora ya namna nzuri ya kutunza ngozi yako.
Umuhimu wa ngozi mwilini
Ngozi ni ogani iliyofunika maeneo yote ya mwili wako ambayo kwa sehemu kubwa imeundwa na seli zilizokufa.Ngozi ndio ogani kubwa zaidi katika mwili wako kuliko ogani nyingine yoyote.
Katika mwili wako ngozi ina kazi kuu zifuatazo:
- Inalinda sehemu za ndani za mwili kama vile mishipa ya damu, nyama na mifupa.
- Inasaidia kurekebisha jotoridi la mwili.
- Ngozi ni kinga ya awali dhidi ya vimelea vinavyoingia na kuathiri sehemu za ndani za mwili.
- Mwili husaidia utoajitaka mwili kupitia mfumo wa jasho.
- Husaidia kufyonza na kupunguza athari za mwanga wa jua ambao ni hatari kwa afya.
- Ngozi hufanya kazi sambamba na mwanga wa jua wa alfajiri kutengeneza virutubisho vya Vitamini D. ambavyo ni muhimu kwa afya ya meno, ngozi na mifupa.
- Ngozi huzalisha dutu muhimu za rangi za melanini ambao husaidia kulinda ngozi dhidi ya mionzi hatari.
Pamoja na kwamba ngozi hupata chakula kupitia damu ambayo hufika katika ngozi kupitia mtandao wa mishipa ya damu, chakula ni moja ya msaada mkubwa ambao ngozi inahitaji kutoka kwako.
Kutokufanya hivyo kunaichosha ngozi kwa haraka na kuisababisha kuzidiwa na kuizeeka mapema.
Sayansi ya ngozi na Matabaka ya ngozi.
Tabaka la nje.
Hili ni tabaka la nje kabisa la ngozi ambalo linaonekana. Tabaka hili lina upana wa kati ya milimita 0.5 had 1 na limeundwa na seli za aina tatu ambazo niKeratinocytes, seli hizi husaidia kutengenezwa seli za ngozi zilizoharibiwa,
Melanocytes, seli hizi husaidia kutengenezwa rangi ya ngozi, kwa asili rangi inayotengenezwa na seli hizi ni nyeusi, na muonekano wa rangi nyeusi wa mtu hutegemea na kiwango cha rangi kilichotengenezwa na seli hizi
Langerhans cells, seli hizi husaidia kuimarisha kinga maeneo ya ngozi kwa kutambua hisia na migusu ambayo ianakuja karibu na ngozi.
Tabaka la nje limegawanyika katika matabaka makuu 6 ambayo ni;
01: Stratum disjunctum sehemu ya juu kabisa ya tabaka la nje.
Tabaka hili limeundwa na seli zilizokufa, mafuta na protini muhimu ya keratini. Seli hizi mfu hupukutika kila baada ya mwezi mmoja na kupelekea ngozi kutengeneza seli nyingine mpya.Kupukutika au kujimenya kwa seli hizi ni kitendo cha kibaolojia cha kiautomatiki lakini pia kitendo hiki kinaweza kuharakishwa na matumizi ya vipodozi yanayomenya ngozi.
Mfano matumizi ya Scrub huharakisha hatua hii.
02: Sehemu ya pili ya tabaka la nje kwenda chini ni stratum corneum.
Katika tabaka hili ni seli hai ambazo zinaelekea kufa kwa ajili ya kutengeneza tabaka la juu. Katika tabaka hili hakuna maji ingawa maji yanaweza kufika kutoka juu ya ngozi kupitia kuoga au vipodozi.Tabaka hili limeundwa na mafuta kwa kiasi kikubwa.
Seli katika tabaka hili imeshonana kwa kiasi kikubwa kiasi kwamba ikiwa zitapata jeraha basi sehemu kubwa ya seli huathiriwa.
03: Inayofuatia ni sehemu ya tatu ya tabaka la nje ambayo huitwa nistratum lucidum.
Tabaka hili linapatikana katika ngozi za mikono na nyayo za miguu. Katika tabaka hili kuna kiwango kikubwa cha dutu za filamenti ambazo huongeza uimara wa ngozi katika maeneo haya.04: Sehemu ya nne ni stratum granulosum.
Katika tabaka hili kuna kiwango kikubwa cha dutu muhimu inazosaidia ngozi kuwa nyororo na mbichi muda wote.05: Sehemu ya tano ya tabaka la nje ni ni stratum spinosum.
Ni katika tabaka hili ambapo seli za Langerhans zinapatikana kwa wingi. Seli hizi husaidia kutoa ulinzi na kinga mbalimbali za maradhi dhidi ya ngozi.Ni katika tabaka hili ambapo saratani nyingi za ngozi huanzia ikiwa litapata hitilafu.
06: Na sehemu ya sita ya tabaka la nje ni stratum germinativum.
Hili ni tabaka la chini kabisa la tabaka la juu la ngozi ambalo ndiko safari ya utengenezwaji wa seli na dutu zote zinazounda ngozi huanzia.Seli za keratini na Melanini zote hupatikana katika tabaka hili. Hitilafu katika sehemu hii inaweza kupelekea kupata matatizo ya saratani kwa urahisi.
Tabaka la kati la Ngozi .
Hili ni tabaka chini ya tabaka la juu (epidemisi) la ngozi. Tabaka hili ndio hudhibiti na kurekebisha muundo wa ngozi kwa ujumla.Tabaka hili limeundwa na vitu vifuatavyo:
- Tezi za jasho.
- Mishipa ya damu.
- Tezi za ute wa sebamu.
- Mashina ya vinyweleo.
- Mfumo wa limfu (mfumo wa ukusanyaji maji na vimiminika mbalimbali vya mwili).
- Protini za colajeni na elastini ambazo husaidia muundo na muonekano wa ngozi usipoteze asili yake.
Mchanganyiko wa takamwili hizi una hali ya tindikali ambayo inatoa faida ya ulinzi dhidi ya vimelea vinavyoathiri ngozi.
Tabaka la ndani la ngozi.
Hili hupatikana chini kabisa baada ya tabaka la juu na la kati. Tabaka hili limeundwa na;- tishu za mafuta,
- tezi za sebamu,
- protini za kolajeni na
- vitamin C.
Tishu za mafuta
Tishu hizi hufanya kazi ya kurekebisha joto la ngozi na mwili na kufyonza mitikisiko na mitetemo ya ngozi ambayo inaweza kusababisha ngozi kuharibika.
Tishu hizi za mafuta zimeshikiliwa na tishu za misuli iliyofunika mifupa. Hakuna vipodozi vinavyoweza kuathiri tabaka hili kwa urahisi.
Tabaka hili hupoteza uwezo wake kadri umri unavyoongezeka hivyo kuiacha ngozi ikiwa na msaada hafifu wa kujishikiza hivyo kuifanya ngozi kupoteza umbo na mwonekano wake.
Hali hii husababishwa kutokea kwa makunyanzi kadri unavyoongezeka umri.
Urembo wa ngozi ni zaidi ya kile unachopaka moja kwa moja juu ya ngozi. Chakula na jinsi unavyoishi vinaathiri kwa kiasi kikubwa ngozi yako.
Vipodozi vinavyomenya ngozi huweza kukusaidia kutengenezwa kwa seli mpya za ngozi hivyo kuimarisha muonekano wako. Mfano scrub.
Kiwango cha ute kwa sehemu kubwa huathiri ubora wa ngozi kutokana na watu kushindwa kujua ni aina gani ya kipodozi atumie kulingana na kiwango cha ute katika ngozi yake.
Katika kufanikisha hili elimu juu ya aina ya ngozi, vyakula bora kwa ajili ya ngozi, muundo wa ngozi na jinsi ngozi inafanya kazi ni muhimu zaidi katika kukusaidia kuchagua njia sahihi na bora ya kutunza ngozi yako.
Tishu hizi za mafuta zimeshikiliwa na tishu za misuli iliyofunika mifupa. Hakuna vipodozi vinavyoweza kuathiri tabaka hili kwa urahisi.
Tabaka hili hupoteza uwezo wake kadri umri unavyoongezeka hivyo kuiacha ngozi ikiwa na msaada hafifu wa kujishikiza hivyo kuifanya ngozi kupoteza umbo na mwonekano wake.
Hali hii husababishwa kutokea kwa makunyanzi kadri unavyoongezeka umri.
Urembo wa ngozi ni zaidi ya kile unachopaka moja kwa moja juu ya ngozi. Chakula na jinsi unavyoishi vinaathiri kwa kiasi kikubwa ngozi yako.
Vipodozi vinavyomenya ngozi huweza kukusaidia kutengenezwa kwa seli mpya za ngozi hivyo kuimarisha muonekano wako. Mfano scrub.
Tezi za sebamu
Tezi za sebamu huzalisha ute ambao husaidia kulainisha ngozi. Ute huu haupaswi kuzidi au kupungua.Kiwango cha ute kwa sehemu kubwa huathiri ubora wa ngozi kutokana na watu kushindwa kujua ni aina gani ya kipodozi atumie kulingana na kiwango cha ute katika ngozi yake.
Protini za colajeni na elastini
Protini za colajeni na elastini husaidia kuimarisha muonekano na umbao wa ngozi. Kupungua kwa protini hii kwa sehemu kubwa kunasababishwa na umri kuongezeka.Vitamini C
Vitamini C ambayo hupatikana kwa wingi katika ngozi husaidia kutengenezwa kwa protini hii hivyo matumizi vya matunda kwa wingi huchelewesha uzee.Hitimisho.
Ngozi bora na yenye afya ni jukumu lako wewe mwenyewe. Una wajibu wa kujifunza na kujua njia mbalimbali za kusaidia kutunza ngozi yako.Katika kufanikisha hili elimu juu ya aina ya ngozi, vyakula bora kwa ajili ya ngozi, muundo wa ngozi na jinsi ngozi inafanya kazi ni muhimu zaidi katika kukusaidia kuchagua njia sahihi na bora ya kutunza ngozi yako.