Faida na Madhara ya Uzazi wa mpango kwa kutumia njia ya kijiti, sindano na vidonge
Uzazi wa mpango una faida nyingi za kiafya na kimaisha. Licha ya kuwa ni jambo lenye faida, uzazi wa mpango una changamoto nyingi za kiafya kutokana na njia ambazo hutumika kufanikisha jambo hili.
Zipo njia nyingi na salama ambazo unaweza kuzitumia kupanga uzazi, miongoni mwa njia hizo ni matumizi ya homoni katika namna mbalimbali kama vile vijiti, vidonge na sindano.
Pamoja na kuwa na faida zake, Matumizi ya homoni kupanga uzazi ni moja ya njia za uzazi wa mpango ambayo huambatana na madhara na matokeo mengi yasiyo rafiki kwa mtumiaji.
Kwa wanawake njia hizi za kupanga uzazi kutumia homoni huleta athari nyingi za kiafya kutokana na namna zinavyofanya kazi.
Njia hizi hutumia homoni kuthibiti au kuzuia kutungwa kwa mimba kwa namna zifuatazo ambazo ni:
Katika mwili homoni hizi za Estrojeni na Projesteroni hutengenezwa na mwili na kutumiwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo katika mfumo wa uzazi.
Lakini katika muundo wa dawa homoni za Progestrin ndio ambazo hutumiwa zaidi kuliko homoni asili ya projesteroni.
Progestrin ni aina ya Projesteroni ambayo hutengenezwa kiwandani.
Kutokana na ufanisi wa kawaida wa homoni ya projesteroni asili ndani ya mwili, Progestrin ni aina ya projesteroni iliyoboreshwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kiutendaji pale itumiwapo kama tiba.
Kuna aina kadhaa ya Progestrin ambazo hutengenezwa kiwandani. Aina hizi hutegemea zaidi chanzo kilichopelekea homoni hii ya Progestrin kutengenezwa.
Baadhi ya aina za homoni hii ya Progestrin ni pamoja na:
Ili yai kurutubishwa ni lazima lipevuke, kwa kuzuia upevukaji wa yai maana yake hakuna yai linaloweza kurutubishwa na hatimaye hakuna mimba inayoweza kutungwa.
Athari za homoni ya Progestrin si katika mfumo wa uzazi pekee bali homoni hii huathiri kazi na sehemu mbalimbali za mwili.
Uwezo huu wa homoni hii kuathiri sehemu mbalimbali za mwili kunafanya matumizi ya Progestrin kama njia ya kupanga uzazi kuambatana na madhara kadhaa ya afya.
Ili kupunguza madhara ya matumizi ya Progestrin katika kupanga uzazi. Mwanamke anaweza kutumia dawa za kupanga uzazi zenye mchanganyiko wa Progestrin na estrojeni.
Estrojeni pia ni homoni ya uzazi na hufanya kazi kinyume na homoni ya Progestrin.
Kwa hivyo matumizi ya dawa mseto ya Progestrin na estrojeni husaidia kupunguza madhara yanayosababishwa na homoni hizi ikiwa zitatomika pekee.
Si kila mwanamke anaweza kupata madhara atumiapo homoni ya Progestrin pekee.
Baadhi ya wanawake matumizi ya Progestrin pekee yanaweza kuwafaa bila kuathiri afya zao kwa kiwango kikubwa.
Njia hii ya kupanga uzazi kwa kutumia homoni inaweza kutolewa kwa namna mbalimbali kama ifuatavyo:
Homoni hii ya levonogestrel hufanya kazi kwa namna zifuatazo:
Ingawa kinaweza kudumu kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Hii ndio njia pekee ya homoni ambayo hutumiwa mara moja na kudumu kwa muda mrefu wa hadi miaka 5.
Njia hii pia inahitaji upasuaji mdogo ambapo vijiti hupachikwa maeneo mbalimbali ya mwili hasa katika paja au mkoo.
Kwa kawaida kila kijiti hubeba kiwango cha Progestrin ambacho huweza kutumika mwaka 1. Kwa hivyo idadi ya vijiti mara nyingi huenda sambamba na miaka.
Kutokana na madhara mbalimbali ya homoni ya Progestrin mwilini, njia hii ya vipandikizi ndio njia inayoongoza kusababisha matatizo mbalimbali kwa watumiaji.
Hii ni miongoni mwa njia ambayo inahitaji mtumiaji kuchunguzwa kwa kina kabla ya kutumia.
Sindano inaweza kuchomwa matakoni au mkononi. Moja ya madhara makubwa ya njia hii ni kupungua kwa ujazo wa mifupa kwa mtumiaji.
Upungufu wa ujazo wa mifupa kwa mwanamke huaambatana na matatizo mbalimbali ya uzazi ikiwemo kukosa hedhi.
Matumizi yake ni kidonge 1 kila siku kwa muda uleule bila kukosea au kusahau.
Ikiwa mtumiaji atasahau kumeza dawa kwa muda wa masaa 12 basi anashauri kutojamiana kwa kuwa anaweza kupata ujauzito.
Mwanamke anaweza kupata madhara kadhaa kutokana na matumizi ya dawa hizi ikiwemo,
Si kila mwanamke atapata athari zitokanazo na matumizi ya homoni katika kupanga uzazi.
Kuna wanawake ambao njia hii huwafaa zaidi kuliko njia nyingine, vivyo hivyo kuna wanawake ambao njia hii hawashauriwi kutumia kutokana na sababu mbalimbali.
Zipo njia nyingi na salama ambazo unaweza kuzitumia kupanga uzazi, miongoni mwa njia hizo ni matumizi ya homoni katika namna mbalimbali kama vile vijiti, vidonge na sindano.
Pamoja na kuwa na faida zake, Matumizi ya homoni kupanga uzazi ni moja ya njia za uzazi wa mpango ambayo huambatana na madhara na matokeo mengi yasiyo rafiki kwa mtumiaji.
Kwa wanawake njia hizi za kupanga uzazi kutumia homoni huleta athari nyingi za kiafya kutokana na namna zinavyofanya kazi.
Njia hizi hutumia homoni kuthibiti au kuzuia kutungwa kwa mimba kwa namna zifuatazo ambazo ni:
- Kuthibiti au kuzuia upevukaji wa yai la mwanamke.
- Kuongeza ute katika mlango wa kizazi ili kuzuia manii kuingia.
- Kusababisha kusinyaa kwa mfuko wa uzazi.
Homoni za Uzazi kwa mwanamke
Homoni ambazo huathiriwa zaidi na njia za kupanga uzazi za kisasa ni homoni za Estrojeni na Projesteroni.Katika mwili homoni hizi za Estrojeni na Projesteroni hutengenezwa na mwili na kutumiwa sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo katika mfumo wa uzazi.
Lakini katika muundo wa dawa homoni za Progestrin ndio ambazo hutumiwa zaidi kuliko homoni asili ya projesteroni.
Progestrin ni aina ya Projesteroni ambayo hutengenezwa kiwandani.
Kutokana na ufanisi wa kawaida wa homoni ya projesteroni asili ndani ya mwili, Progestrin ni aina ya projesteroni iliyoboreshwa kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa kiutendaji pale itumiwapo kama tiba.
Kuna aina kadhaa ya Progestrin ambazo hutengenezwa kiwandani. Aina hizi hutegemea zaidi chanzo kilichopelekea homoni hii ya Progestrin kutengenezwa.
Baadhi ya aina za homoni hii ya Progestrin ni pamoja na:
- levonogestrel.
- Norethindrone.
- Etonogestrel.
- Nestorone.
- Cyproterone acetate.
Kazi za Progestrin katika kupanga uzazi.
Kazi kubwa ya homoni ya Progestrini ni kuzuia upevukaji wa yai na kuongeza uzito wa ute katika mlango wa kizazi.Ili yai kurutubishwa ni lazima lipevuke, kwa kuzuia upevukaji wa yai maana yake hakuna yai linaloweza kurutubishwa na hatimaye hakuna mimba inayoweza kutungwa.
Athari za homoni ya Progestrin si katika mfumo wa uzazi pekee bali homoni hii huathiri kazi na sehemu mbalimbali za mwili.
Uwezo huu wa homoni hii kuathiri sehemu mbalimbali za mwili kunafanya matumizi ya Progestrin kama njia ya kupanga uzazi kuambatana na madhara kadhaa ya afya.
Ili kupunguza madhara ya matumizi ya Progestrin katika kupanga uzazi. Mwanamke anaweza kutumia dawa za kupanga uzazi zenye mchanganyiko wa Progestrin na estrojeni.
Estrojeni pia ni homoni ya uzazi na hufanya kazi kinyume na homoni ya Progestrin.
Kwa hivyo matumizi ya dawa mseto ya Progestrin na estrojeni husaidia kupunguza madhara yanayosababishwa na homoni hizi ikiwa zitatomika pekee.
Si kila mwanamke anaweza kupata madhara atumiapo homoni ya Progestrin pekee.
Baadhi ya wanawake matumizi ya Progestrin pekee yanaweza kuwafaa bila kuathiri afya zao kwa kiwango kikubwa.
Njia hii ya kupanga uzazi kwa kutumia homoni inaweza kutolewa kwa namna mbalimbali kama ifuatavyo:
Njia za uzazi wa mpango za muda mrefu.
#1: Njia ya kitanzi ya uzazi wa mpango.
Hii ni njia ambayo inahitaji upasuaji ili kukipachika kitanzi katika mji wa uzazi wa mwanamke. Hiki ni kifaa maalumu mithiri ya kitanzi ambacho huwa na homoni ya Progestrin hususa ni levonogestrel.Homoni hii ya levonogestrel hufanya kazi kwa namna zifuatazo:
- Kusababisha uzalisha mkubwa wa ute ambao huziba mlango wa uzazi mbegu isiweze kupita.
- Kubadili muundo wa mfuko wa uzazi kwa kuufanya kuwa na mbo la kusinyaa.
- Kuzuia yai kupevuka na kutolewa kutoka katika ovari.
Ingawa kinaweza kudumu kwa zaidi ya mwaka mmoja.
#2: Njia ya uzazi wa mpango ya vipandikizi.
Njia hii inahusisha vipandikizi vya vifaa maalumu vyenye mfano wa vijiti vya kiberiti. Vijiti hivi vinakuwa na homoni ya Progestrin ambayo huzuia yai kupevuka.Hii ndio njia pekee ya homoni ambayo hutumiwa mara moja na kudumu kwa muda mrefu wa hadi miaka 5.
Njia hii pia inahitaji upasuaji mdogo ambapo vijiti hupachikwa maeneo mbalimbali ya mwili hasa katika paja au mkoo.
Kwa kawaida kila kijiti hubeba kiwango cha Progestrin ambacho huweza kutumika mwaka 1. Kwa hivyo idadi ya vijiti mara nyingi huenda sambamba na miaka.
Kutokana na madhara mbalimbali ya homoni ya Progestrin mwilini, njia hii ya vipandikizi ndio njia inayoongoza kusababisha matatizo mbalimbali kwa watumiaji.
Hii ni miongoni mwa njia ambayo inahitaji mtumiaji kuchunguzwa kwa kina kabla ya kutumia.
Njia za uzazi wa mpango za muda mfupi.
#1: Sindano za uzazi wa mpango.
Njia hii hutumia sindano na ni tiba ya homoni ya Projestrin. Mtumiaji huchomwa sindano kila baada ya miezi 3.Sindano inaweza kuchomwa matakoni au mkononi. Moja ya madhara makubwa ya njia hii ni kupungua kwa ujazo wa mifupa kwa mtumiaji.
Upungufu wa ujazo wa mifupa kwa mwanamke huaambatana na matatizo mbalimbali ya uzazi ikiwemo kukosa hedhi.
Mtumiaji wa njia hii anashauriwa kutumia vyakula vya kalisiumu na vitamini D ili kupunguza athari za njia hii.
#2: Vidonge vya uzazi wa mpango.
Vidonge vya uzazi wa mpango vinaweza kuwa vimetengenezwa na homoni ya projestrin pekee au mseto wa projestrin na estrojen.Matumizi yake ni kidonge 1 kila siku kwa muda uleule bila kukosea au kusahau.
Ikiwa mtumiaji atasahau kumeza dawa kwa muda wa masaa 12 basi anashauri kutojamiana kwa kuwa anaweza kupata ujauzito.
Mwanamke anaweza kupata madhara kadhaa kutokana na matumizi ya dawa hizi ikiwemo,
- damu kuganda,
- hedhi kuharibika na
- maradhi ya saratani.
#3: Matumizi ya plasta za uzazi wa mpango.
Hizi ni plasta maalumi ambazo huweza kupachikwa katika maeneo mbalimbali ya mwili kama vile chini ya kitovu, matakoni na mkononi.
Plasta hizi hutengenezwa kwa homoni, mara nyingi hujumuisha homoni mseto za projestrini na estrojeni kwa pamoja.
Plasta moja hubadilishwa kila baada ya wiki 3, na wiki ya 4 mwanamke hapaswi kutumia plasta hii ili kupisha mzunguko wake wa hedhi.
Ringi hili hutumiwa mara moja kwa muda kwa kila baada ya wiki 3, na hutolewa wiki ya 4 kupisha hedhi na baadae, siku 7 baada ya hedhi kuisha hupachikwa lingine.
Plasta hizi hutengenezwa kwa homoni, mara nyingi hujumuisha homoni mseto za projestrini na estrojeni kwa pamoja.
Plasta moja hubadilishwa kila baada ya wiki 3, na wiki ya 4 mwanamke hapaswi kutumia plasta hii ili kupisha mzunguko wake wa hedhi.
#4: Matumizi ya ringi maalumu ukeni.
Ringi hili ni maalumu nahupachikwa ndani ya uke. Ringi hili limeundwa na homoni mseto za projestrini na estrojeni kwa pamoja.Ringi hili hutumiwa mara moja kwa muda kwa kila baada ya wiki 3, na hutolewa wiki ya 4 kupisha hedhi na baadae, siku 7 baada ya hedhi kuisha hupachikwa lingine.
Faida za kutumia homoni kupanga uzazi.
- Husaidia kupunguza maumivu ya hedhi kwa baadhi ya wanawake.
- Kupunguza na kuondoa aina fulani za uvimbe katika mfuko wa uzazi.
- Husaidia kuzuia mimba kuharibika.
- Kwa baadhi ya wanawake husaidia kuleta msawazo wa mzunguko wa hedhi usioeleweka.
- Kuleta nafuu ya upotevu wa damu wakati wa hedhi hasa kwa wanawake wenye upungufu wa madini joto ya chuma.
Athari na madhara ya uzazi wa mpango kutumia homoni.
- Matumizi ya muda mrefu ya vidonge vya uzazi wa mpango husababisha maradhi ya saratani ya utumbo mpana, saratani ya vifuko vya mayai (ovari) na saratani ya ukuta wa uzazi.
- Matumizi ya dawa mseto za vidonge vya uzazi wa mpango huweza kusababisha maradhi ya moyo na mzunguko wa damu. Uwezekano huwa mkubwa zaidi kwa walevi na wavutaji.
- Kuongezeka kwa uzito.
- Kuathirika kwa hamu ya kujamiana, kuongezeka kupita kiasi au kupungua kupita kiasi.
- Kutapika na kichefuchefu.
- Sonona.
- Wanawake wanaotumia homoni kupanga uzazi wako katika hatari ya damu kuganda maeneo mbalimbali ya mwili. Hivyo kuwa katika hatari kubwa ya kupata kiharusi au shambulizi la moyo.
- Kutokwa na damu nyingi ya hedhi mara kwa mara.
- Matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango hasa vyenye preogestrin pekee huweza kusababisha chunusi.
- Kuvurugika kwa mzunguko wa hedhi.
Hitimisho.
Matumizi ya homoni katika kupanga uzazi ni miongoni mwa njia bora zaidi za kupanga uzazi ikiwa zitatumika kwa ufasaha.Si kila mwanamke atapata athari zitokanazo na matumizi ya homoni katika kupanga uzazi.
Kuna wanawake ambao njia hii huwafaa zaidi kuliko njia nyingine, vivyo hivyo kuna wanawake ambao njia hii hawashauriwi kutumia kutokana na sababu mbalimbali.
Vilevile zipo homoni nyingi ambazo hutumika kupanga uzazi, aina fulani ya homoni inaweza isikufae lakini nyingine ikakufaa zaidi.
Kwa hivyo elimu na ushauri wa kitaalamu bila kusahau ushirikiano wako mtumiaji na mtaalamu wa afya ndio nguzo kuu ya kufanikisha maamuzi sahihi ya njia ipi inakufaa.
Kwa hivyo elimu na ushauri wa kitaalamu bila kusahau ushirikiano wako mtumiaji na mtaalamu wa afya ndio nguzo kuu ya kufanikisha maamuzi sahihi ya njia ipi inakufaa.