Tiba ya kichefuchefu, kutapika na kiungulia kwa mjamzito
Kichefuchefu, kutapika, kupata haja kubwa ngumu na kiungulia wakati wa ujauzito ni matatizo ya kawaida ambayo hujitokeza kwa wanawake wengi.
Matatizo haya husababishwa na mabadiliko mbalimbali ya mwili kipindi cha ujauzito. Kwa sehemu kubwa matatizo haya hujitokeza hasa miezi 3 ya mwanzo.
Baadhi ya wanawake matatizo haya yanaweza kuathiri shughuli zao za kila siku kwa kiasi kikubwa.
Moja ya changamoto ya kuyakabili matatizo haya ni tahadhari juu ya matumizi ya dawa mbalimbali wakati wa ujauzito.
Dawa nyingi si salama wakati wa ujauzito, jambo hili linaongeza changamoto juu ya namna ipi ni bora ya kupambana na matatizo haya.
Katika makala hii tutaangazia njia salama ambazo unaweza kuzitumia kukabiliana na matatizo haya kichefuchefu, kutapika, kupata haja kubwa ngumu na kiungulia wakati wa ujauzito.
Mjamzito anashauriwa kutumia njia ambazo zinahusisha lishe, mazoezi na mabadiliko ya tabia fulani katika kukabiliana na matatizo haya kuliko kutumia dawa.
Pamoja na kwamba dawa nyingi si salama wakati wa ujauzito, lakini kuna wakati njia hizi za lishe, mazoezi na mabadiliko ya tabia fulani hushindwa kuleta ahueni.
Katika hali unaweza kupatiwa dawa za kisasa kwa ajili ya kukabiliana na matatizo haya. Ni muhimu kufahamu kuwa mjamzito hatakiwi kutumia dawa yeyote bila kuwasiliana na mtaalamu wa afya kwa ajili ya ushauri sahihi.
Matatizo haya husababishwa na mabadiliko mbalimbali ya mwili kipindi cha ujauzito. Kwa sehemu kubwa matatizo haya hujitokeza hasa miezi 3 ya mwanzo.
Baadhi ya wanawake matatizo haya yanaweza kuathiri shughuli zao za kila siku kwa kiasi kikubwa.
Moja ya changamoto ya kuyakabili matatizo haya ni tahadhari juu ya matumizi ya dawa mbalimbali wakati wa ujauzito.
Dawa nyingi si salama wakati wa ujauzito, jambo hili linaongeza changamoto juu ya namna ipi ni bora ya kupambana na matatizo haya.
Katika makala hii tutaangazia njia salama ambazo unaweza kuzitumia kukabiliana na matatizo haya kichefuchefu, kutapika, kupata haja kubwa ngumu na kiungulia wakati wa ujauzito.
Tiba ya kichefuchefu na kutapika kwa mjamzito
- Usikae bila kula kwa muda mrefu.
- Tumia chai ya Tangawizi mara kwa mara
- Tumia vyakula vyenye vitamini B6 kwa wingi
- Unaweza kutumia biskuti wakati wa asubuhi
- Tumia chakula kiasi, usile chakula kingi kwa wakati mmoja
- Usitumie vyakula vyenye harufu kali
- Epuka matumizi ya vipodozi vyenye harufu kali
- Usitumie sabuni au visafisha nyumba vyenye harufu kali
- Usitumie vyakula vya moto sana
Tiba ya kiungulia kwa mjamzito
- Tumia chakula chenye mafuta kiasi
- Kunywa maji ya kutosha kabla na baada ya kula
- Tumia matunda kwa wingi
- Usitumie vyakula vikali na vichachu hasa matunda machachu na kahawa
- Fanya mazoezi ya kutembea mara baada ya kula
- Usile chakula lisaa 1 hadi 2 kabla ya kulala
- Tumia maziwa au Yogurt kwa ajili ya kupunguza kiungulia
- Usitumie vyakula vyenye mafuta mengi
Tiba ya kupata haja kubwa ngumu kwa mjamzito
- Tumia vyakula vya nyuzinyuzi kama vile ndizi, njegele na viazi vitamu
- Kunywa maji ya kutosha na juisi ya matunda
- Kula kiasi lakini mara kwa mara na si kula chakula kingi kwa wakati mmoja
Hitimisho
Matatizo ya kichefuchefu, kutapika na kiungulia kwa mjamzito ni ya kawaida na mara nyingi hayahitaji dharula ya kitabibu.Mjamzito anashauriwa kutumia njia ambazo zinahusisha lishe, mazoezi na mabadiliko ya tabia fulani katika kukabiliana na matatizo haya kuliko kutumia dawa.