Faida 9 za kiafya za embe na sehemu za mti wa muembe mwilini.
Bila shaka radha nzuri na utamu wa tunda la embe ndio vitu pekee vinakuvutia kuhusu mmea huu adhimu. Lakini umeshawahi kujiuliza kuwa mmea wa muembe una faida kubwa zaidi kuliko kile tunachokipata kwenye tunda pekee?
Ukiachilia tunda la embe lenyewe, mmea wote wa muembe una faida katika miili yetu. Sehemu zote za muembe yaani majani, magome, maua na mizizi uweza kutumiwa kama sehemu ya lishe au tiba.
Faida za embe na sehemu zote za mmea wa muembe zilianza kuonekana toka enzi za kale, ambapo mmea huu ulitumika kama kama chakula vile vile kama tiba.
Lakini jamii maarufu na inayolimwa kwa wingi duniani ni ile ya Mangifera indica. Jamii hii huzalisha embe zenye muonekano, harufu na rangi tofauti.
Nchini Tanzania jamii hii ya mmea huu wa Mangifera indica huzalisha jamii ya embe ambazo kwa sehemu kubwa huwa na rangi ya kijani au nyekundu zinapokuwa mbichi.
Na hubadilika rangi na kuwa njano, njano na nyekundu au hubaki na ukijani wake pindi embe zake zinapokomaa na kuiva.
Jamii hii ya embe inayopatikana Tanzania ndio jamii inayoongoza kwa kuwa na faida mbalimbali za kiafya na za kilishe mwilini mwetu licha ya kuzalishwa chini ya kiwango.
Tafiti mbalimbali zimefanywa kuthibitisha faida za embe kutoka jamii ya Mangifera indica na kubaina faida kadhaa za kiafya.
Pamoja na kuwa na mamia ya kemikali ndani ya mmea huu, kemikali zifuatazo ndio kamikali mama katika mmea huu wa muembe;
Matumizi ya embe mara kwa mara ni kinga dhidi ya magonjwa sugu vilevile magonjwa ambayo husababishwa na kuzidi kwa sumu mwilini kama vile;
Hii inatokana na kemikali ya mangiferin ambayo imeonyesha uwezo wa kipekee wa kupambana na magonjwa mbalimbali.
Mfano Tumor nuclear factor, ambazo husababisha kufanyika kwa uvimbe mwilini.
Vilevile huongeza utengenezwaji wa kemikali za glutathione katika seli, kemikali hii husaidia kuzilinda ogani mbalimbali mwilini dhidi ya sumu.
Hivyo matumizi ya embe na sehemu za mmea wa muembe ni kinga bora dhidi ya uvimbe na matatizo ya saratani.
Vyakula vyenye nyuzinyuzi husaidia mmen’enyo wa chakula vilevile kuimarisha ufyonzwaji wa maji mwilini.
Kwa hivyo matumizi ya embe ya mara kwa mara si tu kutibu bali kuimarisha na kutoa kinga ya macho dhidi ya magonjwa.
Baadhi ya virutubisho hivyo ni;
Zifuatazo ni sehemu za mti wa muembe hutumiwa na binadamu ama kama lishe au tiba.
Unaweza kuloweka majani, maua, magome au mizizi katika maji safi kwa siku 3 hadi 5 kisha tumia kama ifuatavyo;
Nusu glasi ya maji yaani 100ml mara mbili kwa siku walau siku mbili katika kila wiki kwa matumizi ya kawaida.
Glasi 1 ya juisi ya magome pekee mara mbili kwa siku walau siku 3 katika wiki kwa ajili ya kutibu minyoo, kuharisha na kisukari.
Kwa wagonjwa ambao wanatumia dawa za kisasa, usitumie dawa hii kabla ya kuwasiliana na mfamasia au daktari.
Kwa watu wenye matatizo ya macho tumia embe kadri uwezavyo.
Ikiwa unahitaji kutumia sehemu yoyote ya muembe kwa ufanisi zaidi, sehemu hizi pia hupatikana katika vifungashio vya kisasa katika ubora na viwango vya kitaalamu.
Unaweza kupata sehemu hizi katika namna ya unga ama mafuta kutoka maduka ya dawa za kienyeji na mitishamba.
Ikiwa unatarajia kutumia muembe kama tiba ni vyema kufahamu ya kuwa kemikali ndani ya mmea na huu hasa majani na magome zinaweza kuwa hatari kwa afya yako pia endapo utatumia kupita kawaida.
Ukiachilia tunda la embe lenyewe, mmea wote wa muembe una faida katika miili yetu. Sehemu zote za muembe yaani majani, magome, maua na mizizi uweza kutumiwa kama sehemu ya lishe au tiba.
Faida za embe na sehemu zote za mmea wa muembe zilianza kuonekana toka enzi za kale, ambapo mmea huu ulitumika kama kama chakula vile vile kama tiba.
Fahamu mmea huu wa muembe.
Mmea wa muembe ni moja ya mimea inayopatikana duniani kote, na kuna jamii zisizopungua 30 mmea huu wa muembe.Lakini jamii maarufu na inayolimwa kwa wingi duniani ni ile ya Mangifera indica. Jamii hii huzalisha embe zenye muonekano, harufu na rangi tofauti.
Nchini Tanzania jamii hii ya mmea huu wa Mangifera indica huzalisha jamii ya embe ambazo kwa sehemu kubwa huwa na rangi ya kijani au nyekundu zinapokuwa mbichi.
Na hubadilika rangi na kuwa njano, njano na nyekundu au hubaki na ukijani wake pindi embe zake zinapokomaa na kuiva.
Jamii hii ya embe inayopatikana Tanzania ndio jamii inayoongoza kwa kuwa na faida mbalimbali za kiafya na za kilishe mwilini mwetu licha ya kuzalishwa chini ya kiwango.
Tafiti mbalimbali zimefanywa kuthibitisha faida za embe kutoka jamii ya Mangifera indica na kubaina faida kadhaa za kiafya.
Viambata muhimu ndani ya embe na mmea wa muembe.
Sehemu mbalimbali za muembe kiwemo tunda lake zina kiwango kikubwa cha kemikali mbalimbali ambazo zimethibitishwa kitaalamu kuwa na faida za kiafya na za kilishe.Pamoja na kuwa na mamia ya kemikali ndani ya mmea huu, kemikali zifuatazo ndio kamikali mama katika mmea huu wa muembe;
- Mangiferin: Hii ndio kemikali mama ndani ya mmea wa muembe na hupatikana zaidi katika magome ya mti wa muembe.
- Chromones; Kemikali hii hupatikana kwa wingi katika mizizi ya mti wa muembe.
- Mafuta muhimu: Mafuta haya yana kemikali za humelene, elemene, ocimene, linalool, nerol na kemikali nyinginezo.Majani na maua ya muembe ndio sehemu ambazo mafuta haya hupatikana kwa wingi .
- Kemikali za vitamini A, E na C, beta carotene, xanthophylls na tacopherols: Kemikali hizi hupatikana kwa wingi katika tunda na mbegu laini iliyo katika kokwa kokwa la embe.
- polyphenols,
- flavanoids,
- triterpenoids,
- tannis,
- isomangiferin,
- gallic acids,
- protocatechic acid,
- catechin,
- mangoleanone,
- friedelin na
- mangsterols.
Faida za embe na sehemu za mti wa muembe mwilini.
#1: Kuondoa sumu mwilini.
Tunda la embe ni moja ya tiba nzuri ya kuondoa sumu mbalimbali za mwili kutokana na uwepo wa vya viantioksideshaji vikuu vya vitamini E,C na beta carotene.Matumizi ya embe mara kwa mara ni kinga dhidi ya magonjwa sugu vilevile magonjwa ambayo husababishwa na kuzidi kwa sumu mwilini kama vile;
- Saratani mbalimbali za mwili.
- Maumivu ya mwili.
- Maradhi ya ini.
- Maradhi sugu ya figo.
- Kuleta nafuu kwawagonjwa wa kisukari aina ya 2.
- Kuongeza utendaji kazi wa homoni za insulini ambazo husaidia mmeng’enyo wa sukari mwilini.
- Vilevile hupunguza kasi ya ufyonzwaji wa sukari kutoka katika mfumo wa chakula (tumboni).
#2: Kutibu tatizo la minyoo.
Matumizi ya magome ya mti wa muembe ambayo ya kiwango kikubwa cha kemikali ya mangiferin yameonyesha uwezo wa kutibu tatizo la minyoo hususa ile inayosababishwa na minyoo jamii ya Trichinella spiralis.#3: Kinga dhidi ya uvimbena saratani.
Kemikali ndani ya magome ya mti wa muembe yamethibitika kutibu na kuzuia saratani mbalimbali ikiwemo saratani ya utumbo mpana na saratani ya damu.Hii inatokana na kemikali ya mangiferin ambayo imeonyesha uwezo wa kipekee wa kupambana na magonjwa mbalimbali.
#4: Huimarisha kingaya mwili.
Mangiferin imeonyesha uwezo mkubwa wa kuzuia utendaji kazi wa baadhi ya kemikali mbalimbali za mwili.Mfano Tumor nuclear factor, ambazo husababisha kufanyika kwa uvimbe mwilini.
Vilevile huongeza utengenezwaji wa kemikali za glutathione katika seli, kemikali hii husaidia kuzilinda ogani mbalimbali mwilini dhidi ya sumu.
Hivyo matumizi ya embe na sehemu za mmea wa muembe ni kinga bora dhidi ya uvimbe na matatizo ya saratani.
#5: Kuzuia kuharisha.
Mbegu laini iliyo ndani ya kokwa la embe husaidia kutibu tatizo la tumbo na kuharisha. Ufanisi huongezeka zaidi ikiwa litachanganywa na mafuta ya mnyonyo.#6: Kinga bora dhidi ya maradhi ya ini.
Lupenol katika mafuta ya muembe pamoja na mbegu laini ya embe, mchanganyo huu unasaidia kutoa ulinzi wa kutosha dhidi ya hatari mbalimbali zinazolikabili ini.#7: Kusaidia kupata haja kubwa kwa urahisi.
Embe ni kati ya vyakula vichache ambayo ni vyanzo bora vya nyuzinyuzi.Vyakula vyenye nyuzinyuzi husaidia mmen’enyo wa chakula vilevile kuimarisha ufyonzwaji wa maji mwilini.
#8: Kuimarisha afya ya macho.
Beta carotene ndani ya tunda la embe ambayo ndio inalipa embe rangi yake nzuri ya kuvutia ya manjano ni kemikali muhimu katika utendaji kazi wa macho.Kwa hivyo matumizi ya embe ya mara kwa mara si tu kutibu bali kuimarisha na kutoa kinga ya macho dhidi ya magonjwa.
#9: Chanzo bora cha lishe.
Ndani ya embe kuna virutubisho mbalimbali ambavyo hutumiwa na mwili kila siku katika kufanikisha shughuli mbalimbali za mwili.Baadhi ya virutubisho hivyo ni;
- Vitamins A, C, K na E.
- Madini joto ya potasiumu na magnesiumu.
- Protini.
- Mafuta.
- Wanga.
- Sukari.
Zifuatazo ni sehemu za mti wa muembe hutumiwa na binadamu ama kama lishe au tiba.
- Tunda hasa lililoiva.
- Majani machanga.
- Maua.
- Magome.
- Mizizi.
- Mbegu laini.
Kwa matumizi ya tiba.
Majani, maua, magome na mizizi vinaweza kutumiwa katika namna ya unga au juisi.Unaweza kuloweka majani, maua, magome au mizizi katika maji safi kwa siku 3 hadi 5 kisha tumia kama ifuatavyo;