Vyakula muhimu kwa mama mjamzito
Lishe bora kwa mama mjamzito ndio nguzo kuu ya ukuaji na maendeleo bora ya mama na mtoto. Miongoni mwa kundi muhimu zaidi la chakula kwa mama mjamzito ni vitamini muhimu.
Virutubisho hivi ni muhimu sana kwa wajawazito hasa katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito.
Umuhimu wa virutubisho hivi vya vitamini kwa mjamzito unatokana
na kazi muhimu za virutubisho katika ukuaji wa ujauzito.
Baadhi ya kazi muhimu za virutubisho hivi vya vitamini kwa
mama mjamzito ni pamoja na;
- Kutengenezwa damu hasa kwa mama mjamzito,
- kuimarisha afya ya ngozi kwa mama na mtoto,
- ukuaji wa ubongo wa mtoto,
- ukuaji wa mifupa na misuli ya mtoto,
- afya ya macho ya mama na mtoto,
- kuimarisha kinga na ukuaji wa seli za mwili.
Kuna aina kadhaa za virutubisho hivi vya vitamini, ambapo kwa
sehemu kubwa ni salama kwa mjamzito ingawa kuna baadhi ya vitamini vinapaswa
kudhibitiwa kiwango chake kwa kuwa vinaweza kuleta madhara makubwa kwa mjamzito
na mtoto aliyeko tumboni.
Mfano;
Vitamini A ni muhimu lakini ikiwa vitatumiwa kupita
kiwango vinaweza kusababisha matatizo ya kiafya kwa mama na mtoto.
Vyakula muhimu kwa mama mjamzito.
Sehemu hii ya Makala itaelezea baadhi ya virutubisho muhimu vya vitamini kwa mjamzito, kiwango kiwango kinachostahili, vyanzo muhimu vya aina husika ya vitamini na faida zake kwa mjamzito.
#1: Vitamini A (retinol)
Faida kuu za vitamini A ni kusaidia ukuaji bora wa seli za
mwili, macho, ngozi, damu na kuimarisha kinga ya mwili, hivyo kumkinga mjamzito
na mtoto dhidi ya maradhi.
Wastani wa kawaida wa matumizi ya vitamini A kwa mjamzito ni
kati ya 10000IU/kg hadi 20000IU/kg kwa siku.
Vyanzo vikubwa vya virutubisho hivi vya vitamini A
- Samaki,
- karoti,
- brocoli na
- nyama.
#2: Vitamini B1 (Thiamine).
Faida za vitamini B1 NI Kusaidia ukuaji wa ubongo wa mtoto,
moyo na mfumo wa fahamu.
Wakati wa ujauzito uhitaji wa vitamini hii huongezeka hadi
kufikia 1.3mg kwa siku sawa na gramu 250 za nyama ya ngombe au 200gm za vyama
ya nguruwe, pia sawa na gramu 300 za njegele.
Vyakula vinginevyo ambavyo ni chanzo kikuu cha vitamini B1 ni
- ngano na
- amila.
#3: Vitamini B2 (Riboflavin).
Faida za vitamin B2 ni kusaidia maendeleo ya ukuaji ya mtoto
tumboni. Mjamzito anapaswa kutumia si chini ya 1.6mg ya vitamini B2 kwa siku.
Chanzo kikuu cha aina hii ya vitamini ni vyakula vya
- Maini
- soya na
- uyoga.
#4: Vitamin B9 (folic acid).
Moja ya vitamini muhimu zaidi kwa mjamzito na mwanamke
anayejiandaa kupata ujauzito.
Aina hii ya vitamini ni muhimu kwa sababu husaidia
utengenezwaji wa damu ili kukidhi hitaji la ongezeko la damu kwa mjamzito.
Vilevile husaidia kuimarisha mfumo wa fahamu na ubongo.
Upungufu wa vitamini hii kwa mjamzito hupelekea mtoto kuzaliwa
na matatizo mengi ikiwemo mtindio wa ubongo.
Kwa bahati mbaya miili yetu haina uwezo wa kutengeneza aina
hii ya vitamini. Kwa hivyo mjamzito anapaswa kuipata kutoka katika vyakula na
virutubisho maalumu.
Kiwango kinachotakiwa kwa mjamzio ama mwanamke anayetarajia
ujauzito ni kati ya (300-400) microgramu. Kiwango hiki ni kikubwa kuweza
kupatikana kwa namna ya kawaida kupitia vyakula.
Kwa hivyo mjamzito anapaswa kutumia virutubisho vya ziada
vya vitamini hii kwa muda wa mwezi mmoja wa kwanza wa ujauzito mfululizo.
Baadhi ya vyakula vyenye virutubisho hivi vya vitamini B9 ni
- ndimu,
- machungwa na
- limao.
#5: Vitamini B6 (pyridoxine).
Vitamini hii husaidia ufanyaji kazi wa mwili katika seli,
ukuaji wa ubongo na mfumo wa fahamu. Kiwango cha matumizi kwa mjamzito ni 2.2mg
kwa siku.
vyanzo vikuu vya aina hii ya vitamini B6 ni
- Njegere,
- ndizi,
- kuku na
- viazi.
#6: Vitamin B12 (cobalamin).
Hii ni vitamini muhimu ambayo husaidia katika kufanikisha
utengenezwaji wa damu mwilini. Inapaswa kuwa kwa kiwango kikubwa ili
kufanikisha ongezeko la damu kwa mjamzito.
Upungufu wa vitamini hii husababisha tatizo la upungufu wa
damu (anemia) kwa mjamzito ikiwa hataongeza matumizi ya vitamini hii.
Mjamzito anapaswa kutumia vyakula vyenye vitamini hii kwa
wingi ama kutumia virutubisho maalumu ili kuhakikisha kiwango cha vitamini hii
mwilini kinakuwa katika uwiano sahihi.
Chanzo kikuu cha aina hii ya vitamini B12 ni pamoja na
- Nyama nyekundu (ng’ombe, nguruwe au mbuzi)
#7: Vitamin C (ascorbic acid).
Vitamini C ni muhimu kwa sababu husaidia kuimarisha kinga ya
mwili kwa mjamzito, husaidia kufyonzwa kwa madini joto ya chuma, kuimarisha
tishu za misuli na mifupa laini ya mwili hasa kwa mtoto anaekua.
Kiwango kinachopendekezwa kitaalamu kwa mjamzito ni 80mg kwa
siku.
Matunda hasa yenye asili ya uchachu ndio chanzo kikuu cha vitamini C. Baadhi ya matunda hayo ni
- beriberi,
- machungwa,
- limao na
- nyanya.
Vilevile baadhi ya mbogamboga kama brocoli na kabeji ni
chanzo kizuri cha vitamini C.
#8: Vitamin D (Calciferol).
Hii ni muhimu katika kuimarisha afya ya ngozi ya mjamzito,
lakini pia ukuaji wenye afya wa ngozi ya mtoto aliyeko tumboni.
Mwili huzalisha vitamini hii kupitia ngozi, uzalishwaji wa
vitamini D mwilini kupitia ngozi unategemea sana mwanga wa jua hasa ule wa jua
la saa 12 asubuhi.
Lakini mbali na mwili kuwa na uwezo wa kutengeneza vitamini
D, mahitaji ya mjamzito huwa ni makubwa kiasi kwamba utengenezwaji wa itamini D
katika ngozi pekee haukidhi mahitaji.
Mjamzito anashauriwa kutumia vyakula vyenye kiwango kikubwa
cha vitamini D kadri awezavyo.
Mafuta ya samaki ndio chakula pekee asili ambacho tunaweza
kupata vitamini D. Kwa mjamzito anashauriwa kutumia virutubisho maalumu vya
vitamini D ikiwa itahitajika.
#9: Choline.
Kirutubisho hiki si vitamini wala madini joto lakini ni muhimu
sana kwa mjamzito na mtoto aliyeko tumboni.
Kirutubisho hiki husaidia katika utengenezwaji na ukuaji wa
seli a mjamzito na mtoto, ukuaji wa ubongo, ugwemgongo na mfumo wa fahamu kwa
ujumla.
Pia husaidia utengenezwaji na ufanyaji kazi wa viamshi vya umeme
mwilini ambavyo hufanya kazi ya kusafilisha taarifa mbalimbali katika mwili.
Virutubisho hivi hupatikana zaidi katika vyakula vifuatavyo
- Spinachi,
- Maziwa,
- Soya,
- Samaki,
- Ndizi na
- Ngano.
Muhimu kuhusu vyakula vya mjamzito.
Hivi ni vyakula muhimu kundi la vitamini ambalo mjamzito
anapaswa kutumia katika kiwango elekezi ili kuimarisha afya yake lakini pia
kuimarisha afya na ukuaji bora wa mtoto aliye tumboni.
Mambo mengi yanaweza kuathiri upatikanaji na ufuatiliaji wa
mlo kamili kipindi cha ujauzito huku kubwa likiwa ni uchumu wa familia.
Katika kutambua hilo afya plus tumekukuchambulia na
kukupendekezea vyakula na nyanzo mbalimbali vya virutubisho hivi ambavyo ni
rahisi na nafuu zaidi kupatikana.
Kumbuka mtoto ni zawadi kubwa katika maisha na ndio huleta
dhana nzima ya maisha na furaha katika familia. Hakikisha unapata watoto wenye
afya na timamu kwa kuzingatia ushauri na mapendekezo ya kitaalamu.
Hakikisha unahudhuria kliniki kwa ajili ya uratibu wa
ujauzito wako lakini pia mshirikishe mtaalamu wa afya anayeratibu ujauzito wako
ikiwa kuna jambo au ushauri wowote wa kitaalamu.