Aina za maumivu ya mwili na jinsi ya kutibu.
Maumivu ya mwili ni hali ya muitikio wa mwili dhidi ya ajali au hitilafu mbalimbali za tishu katika mwili.
Muitikio huu unahusisha mlolongo tata wa mawasiliano kati ya neva za eneo lililoathirika na ubongo, ambao pia unahusisha hisia.
Ingawa ni muitikio usiopendeza mwili, maumivu ni moja ya tendo muhimu katika mwili kwa vile ndio ishara pekee inayotoa taarifa kwamba eneo fulani la mwili limeharibiwa au kupata jeraha.
Hivyo basi, maumivu hutusaidia kufahamu matatizo mbalimbali yanayokabili miili yetu ili kuyatafutia ufumbuzi kwa haraka.
Mbali na kuwa ni jambo muhimu katika kututaarifu hitilafu katika miili yetu. Maumivu ni moja ya matatizo yanayoghalimu fedha nyingi sana katika kupambana nayo bila ufanisi.
Baadhi ya sababu zinazopelekea mapambano dhidi ya kutibu maumivu kutokuwa na ufanisi ni pamoja na;
Tofauti za mapokezi haya ya uzito wa maumivu kwa mtu yanatokana na sababu zifuatazo;
Ambapo mgonjwa anashidwa kufikisha taarifa sahihi za uzito wa maumivu yake. Vilevile upande wa mtoa huduma naye anaweza kushindwa kupokea taarifa za maumivu katika uzito stahili.
Mambo haya yanapaswa kuzingatiwa na pande zote mbili, mgonjwa na mtoa huduma ili kuongeza ufanisi wa tiba.
Ni wajibu wa mtaalamu wa afya kufahamu na kumuelewesha mgonjwa ya kuwa si kila maumivu yanatokana na ajali za tishu ndani ya mwili.
Kuna maumivu ambayo asili yake haitokani na ajali za moja kwa moja za tishu ndani ya mwili, mfano maumivu ya moyo dhidi ya kuondokewa na mpendwa (kifo).
Hizi ni aina mbili za maumivu ambazo matibabu yake hayawezi kumalizwa kwa dawa ya aina moja.
Mgonjwa anapaswa kufahamu kuwa zaidi ya njia moja ya kutibu maumivu inahitajika kwa aina fulani ya maumivu mbali na kutumia dawa za kutuliza maumivu pekee.
Si vyema kutumia dawa kutokana na mazoea kwa sababu dawa hizi zinaweza kuwa hatari kwa afya.
Ii kuongeza ufanisi wa kupambana na tatizo la maumivu, kujua aina ya maumivu ni hatua moja kubwa ya kufahamu chanzo sahihi hivyo kuongeza ufanisi katika kuchagua tiba sahihi.
Aina za maumivu.
Kuna aina tofauti za maumivu ambazo hujitokeza katika miili yetu. Katika miili yetu maumivu huweza kujitokeza katika aina moja au zaidi.
Inapotokea maumivu katika sehemu fulani ya mwili yakajitokeza katika aina zaidi ya moja.
Basi hii hutajwa kama faida kwa vile husaidia kupatikana kwa dondoo na taarifa muhimu za chanzo cha maumivu hayo.
Zifuatazo ni aina mbalimbali za maumivu ya mwili ambayo unapaswa kuyafahamu ili kuongeza nafasi ya kuwa na uwezo wa kufikisha taarifa sahihi kwa mtoa huduma pindi uhitajikapo kufanya hivyo.
Hivyo katika muktadha huu kuna aina kuu 3 za maumivu ambazo ni;
Yanaweza kutokea kwa mara moja na kuisha au yakawa na muendelezo na kutokea kwa vipindi tofauti.
Mfano wa maumivu ya aina hii ni;
Aina hii ya maumivu huwa ni ya kutarajiwa na mgonjwa huweza kutumia njia kadhaa kutabiri ni wakati gani yanaweza kujitokeza.
Mfano wa maumivu ya aina hii ni;
Kitaalamu, maumivu ambayo hudumu kwa zaidi ya miezi 3 bila kuisha hutafsiriwa kama ni maumivu sugu.
Ni moja ya aina ya maumivu ambayo huwatesa watu wengi na hutumia gharama kubwa kuleta nafuu kwa mgonjwa.
Mfano wa maumivu ya aina hii ni;
Hivyo katika muktadha huu kuna aina kuu 3 za maumivu ambazo ni;
Kuna wakati aina hii ya maumivu huweza kutokea zaidi ya mara moja kwa wakati mmoja katika eneo la mwili.
Mfano maumivu ya tumbo yanaweza kutokea katika sehemu zote za tumbo kwa wakati mmoja.
Maumivu haya huwa katika namna ya mwale ambayo hutokea mara moja na kupotea.
Maumivu haya huweza kujirudia yakiwa na uelekeo wa aina moja, mfano kutoka mguuni hadi kiunoni kila mara au yanaweza kujirudia kutoka mguuni yakiwa na uelekeo tofauti.
Moja ya chanzo kikubwa cha maumivu haya ni majeraha ya mifupa na neva.
Mfano wa maumivu ya aina hii ni;
Hivyo katika muktadha huu kuna aina kuu 2 za maumivu ambazo ni;
Maumivu ya aina hii huwa ni makali sana kwa sababu sehemu za nje za mwili zimeundwa na kiwango kikubwa cha neva kama moja ya njia za ulinzi wa mwili.
Majeraha ya kujikata, kupigwa ngumi na moto ni aina ya majeraha ambayo huathiri tishu za nje za mwili.
Maumivu haya huwa si makali na ni vigumu kuyahisi hasa ikiwa jeraha ndani ya tishu husika ni dogo.
Tishu au ogani yeyote inaweza kuathiriwa lakini nyongo, utumbo, mishipa ya damu na ini ni moja tishu zinazoathiriwa zaidi.
Majeraha katika tishu au ogani za ndani za mwili ndio sababu kubwa ya maumivu aina ya rufaa. Ambapo mgonjwa anashindwa kuhisi maumivu sehemu ya nje ya mwili.
Mfano;
Hivyo katika muktadha huu kuna aina kuu 3 za maumivu ambazo ni;
Tishu zinazoathiriwa ni zile zinazofikiwa na seli za neva, seli ambazo huusika katika usafirishwaji wa taarifa za hisia na miguso katika mfumo wa fahamu wa kati, yaani ubongo na ugwe mgongo.
Mfano maumivu yatokanayo na ajali za kuvunjika mfupa.
Ambapo katika hatua za mwanzo maumivu huwa ni makali sana lakini hupungua kadri jeraha linavyopona.
Aina hii ya maumivu hutokana na hitilafu katika seli za neva, ambapo seli hizi hushindwa kusafirisha taarifa kwa ufasaha.
Kushindwa kusafirishwa kwa taarifa katika neva kunasababisha taarifa hizi kutafsiriwa kama maumivu zifikapo katika ubongo.
Hii ni aina ya maumivu ambayo dawa za kawaida za kutuliza maumivu haziwezi kusaidia.
Hitilafu katika ubongo, ugwe mgongo ama zinazozunguka seli za neva zinaweza kuwa sababu ya aina hii ya maumivu.
Watu wenye kisukari ni moja ya kundi linaloathiriwa zaidi na aina hii ya maumivu.
Maumivu yatokanayo na hitilafu katika seli za neva yanapaswa kutiliwa maanani kwa vile kushindwa kuyadhibiti kunaweza kupelekea tatizola kudumu.
Moja ya mfumo unaoathiriwa ni mfumo wa fahamu ambao ndio unahusika na utafsiri wa taarifa.
Kuathiriwa kwa mfumo huu kunaweza kusababisha maumivu sehemu mbalimbali za mwili.
Hii ni moja ya aina ya maumivu ambayo si rahisi kuitibu kutokana na namna inavyosababishwa.
Dawa pekee hazina msaada katika kupambana na aina hii ya maumivu isipokuwa ushirikiano wa mgonjwa mwenyewe.
Ni vyema kufahamu ni jambo lipi linamtatiza mgonjwa na kutafuta namna ya kumsaidia kulitatua jambo husika.
Watu wa aina hii hupata maumivu ambayo chanzo chake chaweza kuwa ni ajali, saikoojia ama hitilafu za kiutendaji katika mwili.
Mara nyingi sababu zote hizi hujitokeza kwa wakati mmoja hivyo kufanya aina hii ya maumivu kuwa ngumu zaidi kutibika.
Ili kumsaidia mtu aliye katika tatizo hili ni vyema njia zaidi ya moja ya kutibu maumivu kutumiwa.
Kufahamu aina za maumivu ni jambo muhimu kwa sababu inasaidia kung’amua chanzo cha tatizo kwa urahisi.
Vilevile kutoa nafasi sahihi juu ya aina ya maumivu uliyonayo ni njia pekee inayoweza kusaidia kuchagua njia sahihi ya kutibu tatizo kwa ufanisi.
Muitikio huu unahusisha mlolongo tata wa mawasiliano kati ya neva za eneo lililoathirika na ubongo, ambao pia unahusisha hisia.
Ingawa ni muitikio usiopendeza mwili, maumivu ni moja ya tendo muhimu katika mwili kwa vile ndio ishara pekee inayotoa taarifa kwamba eneo fulani la mwili limeharibiwa au kupata jeraha.
Hivyo basi, maumivu hutusaidia kufahamu matatizo mbalimbali yanayokabili miili yetu ili kuyatafutia ufumbuzi kwa haraka.
Mbali na kuwa ni jambo muhimu katika kututaarifu hitilafu katika miili yetu. Maumivu ni moja ya matatizo yanayoghalimu fedha nyingi sana katika kupambana nayo bila ufanisi.
Baadhi ya sababu zinazopelekea mapambano dhidi ya kutibu maumivu kutokuwa na ufanisi ni pamoja na;
- Kutokuwa na elimu ya kutosha juu ya aina ya maumivu.
- Matumizi ya dawa chini ya kiwango.
- Machaguo ya dawa yasiyo sahihi.
- Wasiwasi na mghafiliko kati ya mgonjwa na mtoa huduma.
Tofauti za mapokezi haya ya uzito wa maumivu kwa mtu yanatokana na sababu zifuatazo;
- Misukumo ya kimila, desturi na tamaduni.
- Mtazamo na hisia binafsi.
- Uzoefu wa aina ya maumivu kwa mtu.
Ambapo mgonjwa anashidwa kufikisha taarifa sahihi za uzito wa maumivu yake. Vilevile upande wa mtoa huduma naye anaweza kushindwa kupokea taarifa za maumivu katika uzito stahili.
Uelewa na Ufahamu juu ya tofauti ya maumivu ya mwili.
Katika kupunguza daraja la utofauti wa ufikishaji na upokeaji wa taarifa za maumivu yapo mambo kadhaa ya kuzingatia.Mambo haya yanapaswa kuzingatiwa na pande zote mbili, mgonjwa na mtoa huduma ili kuongeza ufanisi wa tiba.
Ni wajibu wa mtaalamu wa afya kufahamu na kumuelewesha mgonjwa ya kuwa si kila maumivu yanatokana na ajali za tishu ndani ya mwili.
Kuna maumivu ambayo asili yake haitokani na ajali za moja kwa moja za tishu ndani ya mwili, mfano maumivu ya moyo dhidi ya kuondokewa na mpendwa (kifo).
Hizi ni aina mbili za maumivu ambazo matibabu yake hayawezi kumalizwa kwa dawa ya aina moja.
Mgonjwa anapaswa kufahamu kuwa zaidi ya njia moja ya kutibu maumivu inahitajika kwa aina fulani ya maumivu mbali na kutumia dawa za kutuliza maumivu pekee.
Matumizi sahihi ya dawa kulingana na aina ya maumivu.
Mgonjwa anapaswa kufahamu ya kuwa chaguzi sahihi ya dawa kwa kiwango kinachostahili ndio njia bora ya kupambana na tatizo.Si vyema kutumia dawa kutokana na mazoea kwa sababu dawa hizi zinaweza kuwa hatari kwa afya.
Ii kuongeza ufanisi wa kupambana na tatizo la maumivu, kujua aina ya maumivu ni hatua moja kubwa ya kufahamu chanzo sahihi hivyo kuongeza ufanisi katika kuchagua tiba sahihi.
Aina za maumivu.
Kuna aina tofauti za maumivu ambazo hujitokeza katika miili yetu. Katika miili yetu maumivu huweza kujitokeza katika aina moja au zaidi.
Inapotokea maumivu katika sehemu fulani ya mwili yakajitokeza katika aina zaidi ya moja.
Basi hii hutajwa kama faida kwa vile husaidia kupatikana kwa dondoo na taarifa muhimu za chanzo cha maumivu hayo.
Zifuatazo ni aina mbalimbali za maumivu ya mwili ambayo unapaswa kuyafahamu ili kuongeza nafasi ya kuwa na uwezo wa kufikisha taarifa sahihi kwa mtoa huduma pindi uhitajikapo kufanya hivyo.
Aina ya maumivu kwa kuzingatia muda.
Mgawanyo huu wa maumivu unazingatia ni kwa muda gani tatizo la maumivu limekuwapo au linatokea.Hivyo katika muktadha huu kuna aina kuu 3 za maumivu ambazo ni;
Maumivu ya ghafla.
Hii ni aina ya maumivu ambayo hutokea kulingana na ajali ya ghafla ya mwili na hudumu kwa muda mfupi kisha kuisha.Yanaweza kutokea kwa mara moja na kuisha au yakawa na muendelezo na kutokea kwa vipindi tofauti.
Mfano wa maumivu ya aina hii ni;
- Kupigwa ngumi.
- Kujikata.
- Kuungua na maji au moto.
- Kuchomwa na kitu chenye ncha kali.
- Kubanwa na mlango n.k.
Maumivu kujirudia.
Haya ni maumivu ambayo hutokea mara kwa mara, hudumu kwa muda kadhaa kisha kuisha yenyewe baada ya hali fulani ya mwili kutengamaa.Aina hii ya maumivu huwa ni ya kutarajiwa na mgonjwa huweza kutumia njia kadhaa kutabiri ni wakati gani yanaweza kujitokeza.
Mfano wa maumivu ya aina hii ni;
- Maumivu wakati wa hedhi.
- Maumivu ya shambulizi la moyo.
- Na maumivu ya kipanda uso.
Maumivu sugu.
Haya ni maumivu ambayo hutokea na kuwepo kwa muda wote na hupotea kwa kutumia dawa pekee.Kitaalamu, maumivu ambayo hudumu kwa zaidi ya miezi 3 bila kuisha hutafsiriwa kama ni maumivu sugu.
Ni moja ya aina ya maumivu ambayo huwatesa watu wengi na hutumia gharama kubwa kuleta nafuu kwa mgonjwa.
Mfano wa maumivu ya aina hii ni;
- Maumivu ya neva kwa wenye kisukari.
- Miguu kuwaka moto.
- Maumivu kwa watu wenye saratani (kansa).
- Ajali mbaya.
- Kupotelewa na mtu wako wa karibu.
- Maumivu ya magoti na maungio ya mwili yatokanayo na athritisi.
Aina ya maumivu kwa kuzingatia ukubwa wa sehemu ya mwili iliyohusika.
Mgawanyo huu wa maumivu unazingatia ukubwa wa sehemu iliyoathiriwa na maumivuHivyo katika muktadha huu kuna aina kuu 3 za maumivu ambazo ni;
Maumivu ya eneo moja (focal pain).
Ni aina ya maumivu ambayo hutokea katika eneo moja la mwili ambayo yanaweza kuwa ya ghafla, kujirudia au ya muda mrefu.Kuna wakati aina hii ya maumivu huweza kutokea zaidi ya mara moja kwa wakati mmoja katika eneo la mwili.
Mfano maumivu ya tumbo yanaweza kutokea katika sehemu zote za tumbo kwa wakati mmoja.
Maumivu yanayosambaa (radiating pain).
Katika aina hii ya maumivu, maumivu husambaa kutoka katika chanzo na kusafiri katika maneo na tishu jirani na eneo lililoathirika.Maumivu haya huwa katika namna ya mwale ambayo hutokea mara moja na kupotea.
Maumivu haya huweza kujirudia yakiwa na uelekeo wa aina moja, mfano kutoka mguuni hadi kiunoni kila mara au yanaweza kujirudia kutoka mguuni yakiwa na uelekeo tofauti.
Moja ya chanzo kikubwa cha maumivu haya ni majeraha ya mifupa na neva.
Maumivu rufaa (reffered pain).
Haya ni maumivu ambayo hutokea sehemu tofauti na ile ambayo imepata jeraha au kuathiriwa.Mfano wa maumivu ya aina hii ni;
- Maumivu ya kifua, mabega na mikono yatokanayo na shambulizi la moyo.
- Pia maumivu ya vidole, mabega na viganja yanayotokana na matatizo katika kibofu cha mkojo.
Aina ya maumivu kwa kuzingatia tissue zilizojeruhiwa.
Mgawanyo huu wa maumivu unazingatia aina ya tishu zilizopatwa na tatizo la maumivu.Hivyo katika muktadha huu kuna aina kuu 2 za maumivu ambazo ni;
Maumivu tishu za nje ya mwili (somatic pain).
Aina hii ya maumivu huusisha tishu za nje za mwili yaani ngozi.Maumivu ya aina hii huwa ni makali sana kwa sababu sehemu za nje za mwili zimeundwa na kiwango kikubwa cha neva kama moja ya njia za ulinzi wa mwili.
Majeraha ya kujikata, kupigwa ngumi na moto ni aina ya majeraha ambayo huathiri tishu za nje za mwili.
Maumivu tishu za ndani za mwili (visceral pain).
Haya ni maumivu ambayo hutokana na majeraha ya tishu na ogani za ndani za mwili.Maumivu haya huwa si makali na ni vigumu kuyahisi hasa ikiwa jeraha ndani ya tishu husika ni dogo.
Tishu au ogani yeyote inaweza kuathiriwa lakini nyongo, utumbo, mishipa ya damu na ini ni moja tishu zinazoathiriwa zaidi.
Majeraha katika tishu au ogani za ndani za mwili ndio sababu kubwa ya maumivu aina ya rufaa. Ambapo mgonjwa anashindwa kuhisi maumivu sehemu ya nje ya mwili.
Mfano;
- Maumivu ya kifua, mabega na mikono yatokanayo na shambulizi la moyo.
- Pia maumivu ya vidole, mabega na viganja yanayotokana na matatizo katika kibofu cha mkojo.
Aina ya maumivu kwa kuzingatia chanzo au sababu.
Mgawanyo huu wa maumivu unazingatia chanzo au sababu kuu ya maumivu.Hivyo katika muktadha huu kuna aina kuu 3 za maumivu ambazo ni;
Maumivu yatokanayo na jeraha katika tishu (nociceptive pain).
Haya ni maumivu ambayo yanasababishwa na ajali za moja kwa moja katika tishu zinazofikiwa na seli za neva.Tishu zinazoathiriwa ni zile zinazofikiwa na seli za neva, seli ambazo huusika katika usafirishwaji wa taarifa za hisia na miguso katika mfumo wa fahamu wa kati, yaani ubongo na ugwe mgongo.
Mfano maumivu yatokanayo na ajali za kuvunjika mfupa.
Ambapo katika hatua za mwanzo maumivu huwa ni makali sana lakini hupungua kadri jeraha linavyopona.
Maumivu yasiyotokana na jeraha katika tishu (neuropathic pain).
Mtu huweza kupata maumivu bila kupatwa na jeraha lolote la moja kwa moja katika tishu.Aina hii ya maumivu hutokana na hitilafu katika seli za neva, ambapo seli hizi hushindwa kusafirisha taarifa kwa ufasaha.
Kushindwa kusafirishwa kwa taarifa katika neva kunasababisha taarifa hizi kutafsiriwa kama maumivu zifikapo katika ubongo.
Hii ni aina ya maumivu ambayo dawa za kawaida za kutuliza maumivu haziwezi kusaidia.
Hitilafu katika ubongo, ugwe mgongo ama zinazozunguka seli za neva zinaweza kuwa sababu ya aina hii ya maumivu.
Watu wenye kisukari ni moja ya kundi linaloathiriwa zaidi na aina hii ya maumivu.
Maumivu yatokanayo na hitilafu katika seli za neva yanapaswa kutiliwa maanani kwa vile kushindwa kuyadhibiti kunaweza kupelekea tatizola kudumu.
Maumivu yatokanayo na sababu za kisaikolojia (psychogenic pain).
Baadhi ya matatizo ya kisaikolojia kama vile msongo wa mawazo huathiri utendaji kazi wa mwili kwa kiwango kikubwa.Moja ya mfumo unaoathiriwa ni mfumo wa fahamu ambao ndio unahusika na utafsiri wa taarifa.
Kuathiriwa kwa mfumo huu kunaweza kusababisha maumivu sehemu mbalimbali za mwili.
Hii ni moja ya aina ya maumivu ambayo si rahisi kuitibu kutokana na namna inavyosababishwa.
Dawa pekee hazina msaada katika kupambana na aina hii ya maumivu isipokuwa ushirikiano wa mgonjwa mwenyewe.
Ni vyema kufahamu ni jambo lipi linamtatiza mgonjwa na kutafuta namna ya kumsaidia kulitatua jambo husika.
Maumivu yatokanayo na sababu binafsi (idiopathic pain).
Kuna wakati mtu hupata maumivu kutokana na sababu binafsi ambazo huweza kusababishwa na mtazamo, magonjwa , jeraha au saikolojia.Watu wa aina hii hupata maumivu ambayo chanzo chake chaweza kuwa ni ajali, saikoojia ama hitilafu za kiutendaji katika mwili.
Mara nyingi sababu zote hizi hujitokeza kwa wakati mmoja hivyo kufanya aina hii ya maumivu kuwa ngumu zaidi kutibika.
Ili kumsaidia mtu aliye katika tatizo hili ni vyema njia zaidi ya moja ya kutibu maumivu kutumiwa.
Hitimisho.
Hizi ni aina mbalimbali za maumivu ambazo kwa wakati fulani tunaweza kuzipata.Kufahamu aina za maumivu ni jambo muhimu kwa sababu inasaidia kung’amua chanzo cha tatizo kwa urahisi.
Vilevile kutoa nafasi sahihi juu ya aina ya maumivu uliyonayo ni njia pekee inayoweza kusaidia kuchagua njia sahihi ya kutibu tatizo kwa ufanisi.