Faida za Aloe Vera na jinsi ya kutumia
Aloe vera ama kwa lugha ya kiswahili Mshubiri ni moja ya mimea inayotambulika zaidi duniani kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na magonjwa mbalimbali hasa yanayoathiri ngozi.
Baadhi ya faida za aloe vera ni pamoja na uwezo wake wa kutibu magonjwa ya ngozi na tatizo la kupata haja kubwa ngumu.
Mmea wa aloe vera hustawi maeneo yote duniani, lakini hustawi zaidi maeneo ya joto na mvua nyingi ambapo Afrika ya mashariki na kusini mwa afrika hutajwa kama vinara wa uzalishaji wa mmea huu.
Mmea wa aloe vera hustawi maeneo yote duniani, lakini hustawi zaidi maeneo ya joto na mvua nyingi ambapo Afrika ya mashariki na kusini mwa afrika hutajwa kama vinara wa uzalishaji wa mmea huu.
Mmea huu huoteshwa kwa kupandikiza majani yaliyokomaa. Baada ya kustawi majani ya mmea huu huvunwa na utomvu wake kukamuliwa.
Aloe vera hutoa shubiri/gel za aina mbili;
- Shubiri/gel safi mithili ya maji ambao hupatikana kwa kukamua sehemu ya juu ya jani,
- Shubiri/gel ya manjano ambao ni chungu zaidi na hupatikana kwa kukamua sehemu ya shina ya jani.
Tafiti mbalimbali zinathibitisha kwamba hakuna dawa yoyote ambayo inazidi utendaji kazi wa shubiri/gel kutoka katika mmea wa Aloe vera kulingana na kwamba ndani ya shubiri ya Aloe vera kuna kemikali ambazo si rahisi kutengenezwa viwandani.
Je, kuna nini ndani ya Aloe vera gel?
Aloe vera hutoa shubiri/gel za aina mbili, shubiri/gel safi na shubiri/gel yenye rangi ya manjano.Shubiri/gel safi hutumika kwa ajili ya kutibu matatizo mbalimbali ikiwemo:
- vidonda,
- mapunye,
- vibalango,
- michubuko,
- vidonda vya moto na
- kuipa ngozi afya njema,
Kwa upande mwinginw shubiri/gel yenye rangi ya manjano hukamuliwa na kukaushwa na hutumiwa zaidi kwa kutibu tatizo la kupata haja kubwa ngumu.
Ndani ya shubiri/ aloe vera gel kuna kemikali adhimu amabazo kwa umoja wao zinafanya mmea huu kukosa mpinzani linapokuja suala la nani anafaa kutunza ngozi yako.
Ndani ya shubiri/ aloe vera gel kuna kemikali adhimu amabazo kwa umoja wao zinafanya mmea huu kukosa mpinzani linapokuja suala la nani anafaa kutunza ngozi yako.
Zifuatazo ni kemikali ambazo zipo ndani ya mmea huu wa mualovera.
- Kemikali za Anthraquinones: Ni kundi la kemikali ambalo hutumiwa zaidi katika kutibu tatizo la kupata haja kubwa ngumu au kukosa haja kubwa. Aloe vera ni moja ya mimea iliyojaliwa kuwa na kiwango kikubwa cha kemikali hizi. Baadhi ya chemikali katika kundi hili ambayo inapatikana ndani ya mualovera ni aloin na aloe-emodin. Kemikali hii hupatikana kwa wingi katika shubiri /aloe vera gel ya manjano.
- Kemikali za Resins: Kundi hili la kemikali huupatia mmea huu uwezo wa kuua na kuangamiza vimelea vya magonjwa, lakini pia huipatia ulinzi shubiri /aloe vera gel dhidi ya wadudu na vimelea hatarishi. Baadhi ya kemikali zilizopo ndani alo vera kutoka kudi hili la kemikali ni alpha-pinene, beta-pinene, limonene na tricyclic. Kemikali hizi hupatikana kwa wingi katika aina zote za shubiri /aloe vera gel.
- Kemikali za tannis: Hizi hufanya kazi kama vioksideshaji ndani ya mwili, zina uwezo wa kusaidia kupunguzwa kwa kemikali na chaji sumu mwilini. Palmitic acid, E-Phytol, Linolenic acid, Diisooctylphtalate, flavonoids, sterols, triterpenes na mucilages.
- Kemikali ya Aloectin B: Hii ndio silaha kuu inayopatikana katika mmea wa Aloe vera hasa shubiri /aloe vera gel safi, ni ambayo ndio rafiki yako mkubwa wa ngozi pengine kuliko kitu chochote umewahi tumia.
Kazi kubwa ya kemikali hii ni uwezo wa kuongeza utendaji kazi wa kinga za mwili na kupelekea vidonda na majeraha kupona kwa haraka zaidi.
Lakini pia aloectin B ina nguvu ya kuondoa mapunye, vibalango, chunusi, upele na kupambana na aina yoyote ya matatizo ya ngozi.
Faida za Aloe Vera gel
Tayari una dondoo muhimu za kuweza kutambua ni kwa namna gani Aloe vera inaweza kutumika kama mmea tiba. Zifuatazo ni baadhi ya faida za kutumia Aloe vera kama mmea tiba.#1: Kutibu vidonda vya aina mbalimbali.
Aloe vera ni pendekezo nambari moja katika kutibu matatizo ya vidonda, michubuko na ajali za moto katika ngozi na vidonda vya tumbo.Shubiri /aloe vera gel huweza kutumika kwa kupaka au kunywa. Uwezo huu ni kwasababu ya uwepo wa Aloectin B katika mmea huu.
#2: Kutibu fangasi na magonjwa mengine ya Ngozi.
Uwepo wa resins(alpha-pinene), tannis ,na Aloectin B ndani ya Aloe vera kunafanya mmea kuwa moja ya tiba za kuaminika dhidi ya maradhi mbalimbali ya ngozi.Maradhi kama
- upele,
- ngozi kutoa harufu,
- ngozi kupasuka,
- vibalango,
- miwasho
Yote haya huweza kumalizwa kabisa na mmea huu wa aloe vera.
#3: Kutibu matatizo ya Kupata haja kubwa.
Ikiwa unashida ya kukosa haja kubwa au haja kubwa ngumu kupita kawaida basi Shubiri /aloe vera gel ni chaguo sahihi na ina uwezo mkubwa wa kupambana na tatizo hili pengine kuliko dawa yoyote unayoifahamu.Pia ikiwa hupati hamu ya kula basi Aloe vera inaweza kuwa msaada mkubwa kwako. Yote haya ni kwa sababu ya uwepo wa kemikali za anthraquinones.
#4: Kuimarisha afya ya ngozi, urembo na kutibu bawasiri.
Matumizi ya kawaida ya Shubiri /aloe vera gel husaidia katika kung’aarisha na kuimarisha ngozi yako, kwa kuchanganya na mafuta kama alizeti, inaweza kukupa matokeo mazuri na kukuacha mwenye kujipenda na kutamaniwa na watu.Matumizi ya Aloe vera
Jani la Aloe vera ndio sehemu kuu inayotumiwa kama tiba, ambapo jani lake hukatwa na Shubiri /aloe vera gel inavunwa kutoka katika majani hayo.Ikiwa unahitaji Shubiri /aloe vera gel safi kwa ajili ya vidonda basi kata robo tatu ya jani kutoka juu kisha vuna shubiri.
Na ikiwa unahitaji aloe vera gel ya manjano basi kata robo ya jani la Aloe vera kutoka katika sehemu ya chini ya jani(shina).
Aloe vera gel bila kujali ni safi au ni ya manjano unaweza kutumiwa kwa kunywa ingawa shubiri ni miongoni mwa vitu vyenye radha kali ya uchungu.
Unaweza kuipata na kutumia Aloe vera katika hali tofauti ikiwemo
Aloe vera gel bila kujali ni safi au ni ya manjano unaweza kutumiwa kwa kunywa ingawa shubiri ni miongoni mwa vitu vyenye radha kali ya uchungu.
Unaweza kuipata na kutumia Aloe vera katika hali tofauti ikiwemo
- Aloe vera gel iliokaushwa.
- Aloe vera juisi.
Jinsi ya kutumia aloe vera gel.
Jinsi ya kutumia aloe vera juisi, changanya kijiko kimoja cha aloe vera gel au robo kijiko cha unga wa aloe vera katika mililita 100 za maji.Kisha tumia vijiko 3 hadi mara 4 kwa siku. Hii ni kwa wale wanaosumbuliwa na vidonda vya tumbo na kusaidia mmen’enyo wa chakula na kupata hamu ya kula.
Kwa matumizi katika ngozi, bawasiri na vidonda tumia aloe vera gel au unga wa Aloe vera gel kijiko kimoja kwa vijiko 5 vya maji safi kisha paka katika tatizo au sehemu yenye vidonda.
Kwa vidonda vikubwa na vilivyo wazi ikiwa hakuna aloe vera gel basi tumia unga wa aloe vera gel kwa kupaka bila kuchanganya na maji.
Kwa matumizi katika ngozi, bawasiri na vidonda tumia aloe vera gel au unga wa Aloe vera gel kijiko kimoja kwa vijiko 5 vya maji safi kisha paka katika tatizo au sehemu yenye vidonda.
Kwa vidonda vikubwa na vilivyo wazi ikiwa hakuna aloe vera gel basi tumia unga wa aloe vera gel kwa kupaka bila kuchanganya na maji.
Hitimisho
Aloe vera ni moja ya mimea adhimu ambayo hutumiwa zaidi kwa ajili ya kutunza na kuimarisha afya ya ngozi.
Uwezo wa aloe vera katika kutunza ngozi yako kunaufanya mmea huu kutumiwa kwa kiwango kikubwa katika bidhaa mbalimbali za urembo wa ngozi yako.
Ikiwa unaipenda ngozi yako basi hakuna chaguo lingine sahihi ambalo linaweza kuuzidi mmea huu wa aloe vera katika utunzaji wa ngozi yako.