Faida za Uzazi wa mpango na changamoto zake
Uzazi wa mpango ni hali ya kuzuia mimba kutunga kwa kuathiri mchakato wa kibaolojia unaopelekea mimba kutunga kwa kutumia njia za kisasa au za asili.
Dhana ya uzazi wa mpango ni kuzuia mimba kutunga na si kuzuia mimba kukua. Mimba inaweza kuzuiwa kutunga kwa kutumia njia mbalimbali kama vile;
Licha ya kuwa mwanamke ndio muhusika na mlengwa mkuu juu ya jambo hili, ni wajibu wa wapenzi/wanandoa wote wawili kushiriki kikamilifu ili kuepuka migongano isiyo ya lazima.
Matumizi sahihi ya njia bora na salama ya uzazi wa mpango si tu inamkinga mwanamke dhidi ya mimba zisizotarajiwa na utoaji mimba holela.
Bali, inatoa uhuru kwa wapenzi/wanandoa kuchagua muda sahihi wa kupata watoto bila kuathiri shughuli zao za uzalishaji na za kielimu.
Mbali na kutumiwa kama njia za kuzuia mimba zisizotarajiwa, baadhi ya njia za uzazi wa mpango zinasaidia kumkinga mtumiaji dhidi ya maradhi mbalimbali ya zinaa.
Mambo ya kuzingatia ni pamoja na:
Lengo kuu la kutumia njia za uzazi wa mpango ni kuzuia mimba zisizotarajiwa. Mimba zisizotarajiwa ni moja ya vikwazo vikubwa katika kufanikisha mambo mbalimbali ya kimaisha hasa kwa wanawake.
Magonjwa kama UKIMWI, gono, kaswende, pangusa, kisonono, UTI na mengineyo yanaweza kuthibitiwa kutokana na matumizi ya kondomu.
Dawa hizi hutumika pia kuleta nafuu kwa matatizo mbalimbali ya hedhi, chunusi, uvimbe katika via vya uzazi na matatizo mengine ya uzazi kwa mwanamke.
Mbali na kuwepo kwa njia mbalimbali za kupanga uzazi bado wimbi kubwa la vijana hawatumii njia hizi au wanatumia bila mafanikio.
Ziffuatazo ni changamoto mbalimbali juu ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango na jinsi ya kuzikabili.
Kwa sehemu kubwa kutojitambua huku kunasababishwa na familia na jamii kwa ujumla kwa kushindwa kutoa elimu ya kutosha juu ya afya ya uzazi hasa kutokana na sababu za kimila na desturi.
Wengi huzani matumizi ya njia za uzazi wa mpango huleta madhara makubwa na huweza kuwasababishia kupoteza uwezo wa kuzaa. Jambo hili si la kweli.
Mfano kusahau kumeza dawa kwa wakati na ni kitu gani cha kufanya badda ya hali hii kutokea.
Ni ngumu kwa mwanaume kushaurika pindi anapokuwa katika hisia na wakati mwingine mwanaume anaweza kumpiga mwanamke ikiwa mwanamke atakaidi matakwa ya mwanaume.
Mbali na kukabiliwa na hatari mbalimbali za kiafya na uhai kwa wanwake wanaotoa mimba kwa njia zisizo salama, vilevile kuna athari kubwa za kijamii, kiuchumi na kimaendeleo.
Ni jukumu la kila mzazi, mlezi na kijana kupata elimu ya afya na kuchagua njia sahihi ya uzazi wa kuepuka mimba zisizotarajiwa na kujiepusha na hatari za kiafya ili kutimiza malengo yao.
Dhana ya uzazi wa mpango ni kuzuia mimba kutunga na si kuzuia mimba kukua. Mimba inaweza kuzuiwa kutunga kwa kutumia njia mbalimbali kama vile;
- matumizi ya dawa.
- vifaa tiba maalumu.
- kemikali sumu maalumu
- kufunga kizazi
- vilevile kuna njia mbalimbali za asili ambazo hutumika
Licha ya kuwa mwanamke ndio muhusika na mlengwa mkuu juu ya jambo hili, ni wajibu wa wapenzi/wanandoa wote wawili kushiriki kikamilifu ili kuepuka migongano isiyo ya lazima.
Matumizi sahihi ya njia bora na salama ya uzazi wa mpango si tu inamkinga mwanamke dhidi ya mimba zisizotarajiwa na utoaji mimba holela.
Bali, inatoa uhuru kwa wapenzi/wanandoa kuchagua muda sahihi wa kupata watoto bila kuathiri shughuli zao za uzalishaji na za kielimu.
Mbali na kutumiwa kama njia za kuzuia mimba zisizotarajiwa, baadhi ya njia za uzazi wa mpango zinasaidia kumkinga mtumiaji dhidi ya maradhi mbalimbali ya zinaa.
Sifa za njia bora na salama ya uzazi wa mpango.
Katika kuchagua njia za uzazi wa mpango kuna mambo kadhaa ya kuzingatia ili kujihakikishia usalama na ufanisi unaokusudiwa kwa mtumiaji.Mambo ya kuzingatia ni pamoja na:
- Chagua njia ya uzazi wa mpango yenye Ufanisi wa hali ya juu.
- Zingatia Usalama wa matumizi ya njia utakayochagua.
- Chagua njia ambayo ni nafuu na haina gharama.
- Hakikisha unachagua njia ambayo ni rahisi kufikiwa na kupatikana.
- Chagua njia inayokubalika bila kuathiri imani na tamaduni.
- Chagua njia ambayo ni rahisi kutumia.
Jinsi njia za uzazi wa mpango huzuia mimba kutunga.
Njia mbalimbali za uzazi wa mpango hufanya kazi ya kuzuia kutunga kwa mimba katika misingi mikuu ifuatayo:- Kudhibiti mfumo wa homoni za uzazi hasa kwa wanawake.
- Kujiepusha na kujamiana wakati wa yai kupevuka.
- Kuzuia mawasiliano kati ya ovari na mfuko wa uzazi kwa wanawake.
- Kuzuia mawasiliano kati ya mfereji wa manii unaoonganisha korodani na uume kwa wanaume.
Faida za uzazi wa mpango.
#1: Kujikinga na mimba zisizotarajiwa:
Lengo kuu la kutumia njia za uzazi wa mpango ni kuzuia mimba zisizotarajiwa. Mimba zisizotarajiwa ni moja ya vikwazo vikubwa katika kufanikisha mambo mbalimbali ya kimaisha hasa kwa wanawake.
Mimba zisizotarajiwa humuathiri mwanamke katika nyanja mbalimbali ikiwemo:
- Kushindwa kuendelea na elimu.
- Kushindwa kujihuisha na shughuli za kiuchumi.
- Kutengwa na jamii.
- Kukosa malezi bora ya mimba.
- Kukimbiwa na mwenza.
- Kujihusisha na biashara haramu kama kuuza miili kwa lengo la kukidhi mahitaji hivyo kuhatarisha afya yake na ya mtoto.
- Mimba zisizotarijiwa hupelekea wimbi kubwa la utoaji mimba holela, utoaji mimba unaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya hata kifo.
#2: Kujikinga dhidi ya magonjwa ya zinaa (MAYAZI).
Baadhi ya njia za uzazi wa mpango kama vile matumizi ya mipira ya kondomu zina faida zaidi ya moja kwa mtumiaji.Magonjwa kama UKIMWI, gono, kaswende, pangusa, kisonono, UTI na mengineyo yanaweza kuthibitiwa kutokana na matumizi ya kondomu.
#3: Kutibu na kuleta nafuu kwa baadhi ya matatizo kwa wanawake.
Matumizi ya dawa za kuthibiti kiwango cha homoni za uzazi kwa mwanamke pia hutoa msaada zaidi ya kuzuia mimba.Dawa hizi hutumika pia kuleta nafuu kwa matatizo mbalimbali ya hedhi, chunusi, uvimbe katika via vya uzazi na matatizo mengine ya uzazi kwa mwanamke.
Changamoto zinazoathiri matumizi ya njia za uzazi wa mpango.
Vijana ndio kundi kubwa linaloathiriwa na mimba zisizotarajiwa jambao linaloathiri ndoto za vijana wengi hasa wa kike.Mbali na kuwepo kwa njia mbalimbali za kupanga uzazi bado wimbi kubwa la vijana hawatumii njia hizi au wanatumia bila mafanikio.
Ziffuatazo ni changamoto mbalimbali juu ya matumizi ya njia za uzazi wa mpango na jinsi ya kuzikabili.
#1: Vijana kushindwa kujitambua na kujielewa.
Hii inatokana na uwezo mgogo wa kijana kushindwa kufahamu madhara mbalimbali ya kiafya yanayoweza kutokea ikiwa atajihusisha na ngono.Kwa sehemu kubwa kutojitambua huku kunasababishwa na familia na jamii kwa ujumla kwa kushindwa kutoa elimu ya kutosha juu ya afya ya uzazi hasa kutokana na sababu za kimila na desturi.
#2: Majigambo na kujiona wajuzi wa mambo.
Vijana wengi wametawaliwa na dhana ya kujiona kila kitu wanajua na hawawezi kupatwa na jambo lolote hivyo kupuuza mafundisho mbalimbali ya afya ya uzazi.#3: Elimu duni juu na taarifa potofu juu ya uzazi wa mpango.
Kutokuwa na elimu na uelewa wa kutosha juu ya elimu ya afya ya uzazi inabaki kuwa ni changamoto kubwa kwa vijana wengi.Wengi huzani matumizi ya njia za uzazi wa mpango huleta madhara makubwa na huweza kuwasababishia kupoteza uwezo wa kuzaa. Jambo hili si la kweli.
#4: Tafsiri mbaya ya watu katika jamii.
Kuna nadharia ya kwamba kumpatia elimu ya uzazi kijana ni kumfundisha mambo ya kikubwa, kumruhusu na kumpa fursa ya kufanya uasherati.#5: Elimu duni ya njia sahihi za kutumia uzazi wa mpango.
Wapo watu wengi ambao hutumia njia za uzazi wa mpango bila mafanikio au hukumbwa na matatizo kadhaa ya kiafya ambayo huathiri ufanisi wa njia hizi za uzazi wa mpango.Mfano kusahau kumeza dawa kwa wakati na ni kitu gani cha kufanya badda ya hali hii kutokea.
#6: Nadharia ya kondomu kupunguza radha na utamu wa kujamiana.
Watu wengi hasa wanaume hulalamika kuwa kondomu hupunguza radha na msisimko wakati wa kujamiana jambo linalopelekea kutoitumia.#7: Makosa ya utunzaji na matumizi.
Baadhi ya njia za uzazi wa pango zinahitaji namna maaumu ya kutumia na kuhifadhi. Mfano jinsi ya kutumia kondomu kunahitaji na namna bora ya kuhifadhi vidonge vya uzazi wa mpango.#8: Aibu ya kwenda dukani au ktuo cha afya.
Wapenzi wengi hupatwa na ugumu wa kununua kondomu kutokana na mtizamo wa jamii juu ya matumizi ya kondomu.#9: Maridhiano hafifu.
Wapenzi kushindwa kuongea na kuelezana juu ya mitazamo na matakwa yao kuhusu afya ya uzazi. Kwa sehemu kubwa changamoto hii huambatana na unyanyasaji hasa kwa wanawake.Ni ngumu kwa mwanaume kushaurika pindi anapokuwa katika hisia na wakati mwingine mwanaume anaweza kumpiga mwanamke ikiwa mwanamke atakaidi matakwa ya mwanaume.
Hitimisho.
Vijana wa kike ndio kundi kubwa linaloathiriwa na mimba zisizotarajiwa hali inayopelekea wimbi kubwa la utoaji mimba usio salama.Mbali na kukabiliwa na hatari mbalimbali za kiafya na uhai kwa wanwake wanaotoa mimba kwa njia zisizo salama, vilevile kuna athari kubwa za kijamii, kiuchumi na kimaendeleo.
Ni jukumu la kila mzazi, mlezi na kijana kupata elimu ya afya na kuchagua njia sahihi ya uzazi wa kuepuka mimba zisizotarajiwa na kujiepusha na hatari za kiafya ili kutimiza malengo yao.