Siku za kupata mimba, njia za kutambua na dalili zake
Kuongezeka kwa changamoto ya mimba zisizotarajiwa kunasababishwa na mambo mengi lakini kubwa ni elimu duni ya afya ya uzazi hasa elimu ya mzunguko wa hedhi kwa kuwa siku za kupata mimba huathiriwa zaidi na mzunguko wa hedhi.
Kufahamu siku za kupata mimba katika mzunguko wako ni moja ya nyenzo kuu za kukabiliana na changamoto hii ya mimba zisizotarajiwa ambayo huambatana na matatizo kadhaa ya kimaisha.
Ili kuelewa ni wakati gani uko katika uwezekano mkubwa wa kushika mimba, elimu juu ya mzunguko wako wa hedhi ndio nguzo kuu.
Katika makala hii tutazungumzia siku za kupata mimba katika mzunguko wako wa hedhi na njia mbalimbali za kisasa na kienyeji unazoweza kuzitumia kutambua hali hii.
Kwa mwanaume aliye kamili kiafya mbegu za uzazi hutengenezwa na kupatikana muda wote wa maisha yake.
Kwa mwanamke hali ni tofauti, upatikanaji wa mbegu ya uzazi ya kike (yai) uko katika udhibiti wa tukio la kibaolojia ambalo hujulikana kama Mzunguko wa hedhi.
Tukio hili ndio huratibu na kuthibiti utengenezwaji na upevushwaji wa mbegu ya uzazi ya kike (yai).
Kwa wastani, katika kila baada ya siku 28, kuna takribani siku 3 pekee ambazo mbegu za uzazi za mwanamke huwa na uwezo wa kutunga mimba.
Ni jukumu la mwanamke na mwenza wake kuzifahamu siku hizi ikiwa wanatarajia mtoto au hawako katika mpango wa kupata mtoto.
Ni rahisi kuzifahamu siku hizi ikiwa tu mwanamke ana uwelewa wa kutosha juu ya mzunguko wake wa hedhi na mabadiliko kadhaa ya mwili katika hatua mbalimbali za mzunguko.
Bila kujali urefu wa mzunguko, siku ya kwanza ya hedhi ni siku ya kwanza ya kutokwa damu, na siku ya kupata mimba hutofautiana kulingana na urefu wa mzunguko wa hedhi.
Hatua hii kwa wastani hudumu kwa takribani siku 6 ambapo huendelea mpaka siku ya 9, siku ya 11, siku ya 16, siku ya 17 na siku ya 18 ya mzunguko kulingana na urefu wa mzunguko.
Katika siku hizi 6 uwezekano wa mwanamke kushika mimba ni mkubwa na hutajwa kama siku za kupata mimba.
Kwa mwanamke ambae ana mazoea ya kujichunguza juu ya mabadiliko mbalimbali ya mwili ni rahisi kugundua ikiwa yuko katika kipindi hiki kwa vile kipindi hiki huambatana na dalili kadhaa.
Kwa mbegu ya kiume ambayo hupelekea mtoto wa kiume huishi kwa masaa 48 pekee wakati mbegu ya kiume inayopelekea mtoto wa kike huishi masaa 72 yaani siku 3.
Katika siku 6 za yai kupevuka, mara nyingi siku ya 2 yaani siku ya 5 kwa wenye mzunguko wa siku 21, siku ya 7 kwa wenye mzunguko wa siku 26, siku ya 12 kwa wenye mzunguko wa siku 28, siku ya 13 kwa wenye mzunguko wa siku 30 na siku ya 15 kwa wenye mzunguko wa siku 32.
Kwa hivyo siku ya 3, ya 5, ya 10, ya 11na ya 12 zinatajwa kama siku ambazo mwanamke anaweza kupata mimba kwa iwapo atakutana na mwanaume katika siku hizi.
Hii inatokana na kwamba ikiwa mwanamke atajamiana, mbegu za mwanaume huweza kuishi ndani ya mfumo wa uzazi kwa masaa 72.
Kwa maana ya kwamba mbegu hizi zinaweza kuishi hadi siku ya 5, ya 7, ya 12, ya 13 na ya 15.
Ni katika siku hizi ambapo uwezekano wa yai kupevuka ni mkubwa hivyo yai huzikuta mbegu bado ziko hai na mimba huweza kutungwa.
Baadhi ya dalili za kuwa katika siku za kupata mimba ni pamoja na:
Ute huu huwa ni mzito na huwa na kiwango kikubwa cha protini za mucin ambazo huufanya kuwa mzito.
Lakini katika kipindi cha yai kupevuka ute huu huwa ni mwepesi, laini na wenye rangi nyeupe ya kung’aa.
Hii inatokana na ongezeko la kutengenezwa kwa maji hasa maeneo ya mfumo wa uzazi kunakosababishwa na ongezeko la homoni ya oestrojeni.
Mwanamke anaweza kuugundua kwa kutumia vidole au wakati mwingine huweza kujitokeza nje ya mashavu ya uke.
Wakati wa yai kupevuka mara nyingi siku moja kabla joto la mwili hupungua. Ni kawaida mwanamke kupima na kukuta jotoridi ni kati ya 36.30C hadi 36.20C.
Jotoridi huwa chini zaidi wakati wa siku ya yai kupevuka takribani 36.20C na huanza kupanda kuanzia siku ya pili ya yai kupevuka hadi kufikia 36.40C.
Baada ya siku ya pili ya yai kupevuka jotoridi la mwili hupanda hadi kufikia 36.70C na jotoridi hilo huendelea mpaka siku ya 28 ya mzunguko yaani siku ya kuanza hedhi.
Ongezeko la homoni ya progesteroni ndio husababisha ongezeko la jotoridi la mwili kwa takribani.
Hata hivyo ongezeko la joto hutokea siku ya 1 au ya 2 baada ya yai kupevuka. Kwa hivyo ongezeko la jotoridi ni ishara kwamba yai lako limepevuka siku 1 au 2 zilizopita.
Hata hivyo ongezeko la jotoridi la mwili huathiriwa na mambo mengi ikiwemo:
Kwa hivyo katika kutumia mabadiliko ya jotoridi la mwili kama ishara ya kutambua siku za kupata mimba ni vyema kuzingatia mabo yaliyotajwa hapo juu.
Njia hizo ni pamoja na:
Mimba zisizotarajiwa huweza kuwa na madhara makubwa ya kijamii, kiuchumi, kielimu, kisaikolojia na kiafya kwa ujumla.
Hakikisha unapata ujauzito wakati ambao uko tayari. Tumia elimu hii kuzuia mimba zisizotarajiwa ambazo zinaweza kukusababishia matatizo mbalimbali ya kimaisha.
Ni muhimu kutambua siku za kupata mimba katika mzunguko wako wa hedhi ili kuweza kujikinga na changamoto mbalimbali za kimaisha zinazosababishwa na mimba zisizotarajiwa.
Kufahamu siku za kupata mimba katika mzunguko wako ni moja ya nyenzo kuu za kukabiliana na changamoto hii ya mimba zisizotarajiwa ambayo huambatana na matatizo kadhaa ya kimaisha.
Ili kuelewa ni wakati gani uko katika uwezekano mkubwa wa kushika mimba, elimu juu ya mzunguko wako wa hedhi ndio nguzo kuu.
Katika makala hii tutazungumzia siku za kupata mimba katika mzunguko wako wa hedhi na njia mbalimbali za kisasa na kienyeji unazoweza kuzitumia kutambua hali hii.
Mzunguko wa hedhi na mimba
Mimba ni matokeo ya muunganiko wa mbegu ya uzazi ya kiume na mbegu ya uzazi ya kike. Kwa kawaida muunganiko huu unawezeshwa kupitia njia ya kujamiana ingawa kuna njia nyingine pia.Kwa mwanaume aliye kamili kiafya mbegu za uzazi hutengenezwa na kupatikana muda wote wa maisha yake.
Kwa mwanamke hali ni tofauti, upatikanaji wa mbegu ya uzazi ya kike (yai) uko katika udhibiti wa tukio la kibaolojia ambalo hujulikana kama Mzunguko wa hedhi.
Tukio hili ndio huratibu na kuthibiti utengenezwaji na upevushwaji wa mbegu ya uzazi ya kike (yai).
Kwa wastani, katika kila baada ya siku 28, kuna takribani siku 3 pekee ambazo mbegu za uzazi za mwanamke huwa na uwezo wa kutunga mimba.
Ni jukumu la mwanamke na mwenza wake kuzifahamu siku hizi ikiwa wanatarajia mtoto au hawako katika mpango wa kupata mtoto.
Ni rahisi kuzifahamu siku hizi ikiwa tu mwanamke ana uwelewa wa kutosha juu ya mzunguko wake wa hedhi na mabadiliko kadhaa ya mwili katika hatua mbalimbali za mzunguko.
Mzunguko wa hedhi na siku za kupata mimba.
Jinsi ya kuhesabu siku za mzunguko wa hedhi ni changamoto kwa wanawake wengi kutokana na sababu mbalimbali za kielimu, kiuchumi, kijamii na za kiafya.Bila kujali urefu wa mzunguko, siku ya kwanza ya hedhi ni siku ya kwanza ya kutokwa damu, na siku ya kupata mimba hutofautiana kulingana na urefu wa mzunguko wa hedhi.
Kwa kuzingatia urefu tofauti wa mzunguko wa hedhi, siku za kupata mimba kwa wanawake ni kama ifuatavyo;
Siku za kupata mimba kwa wenye mzunguko wa siku 21 au 26.
Kwa wanawake ambao mzunguko wao ni siku 21, Siku ya kupata mimba ni kati ya siku ya 3 ya mzunguko wao hadi siku ya 9 kutoka siku ya kwanza ya kutoka damu.
Yaani wanawake hawa huweza kushika mimba wakiwa bado hawajamaliza siku zao za kutoka damu. walio wengi huweza kushika mimba kuanzia siku ya 3 ya kutoka damu hadi siku ya 9 ya mzunguko wao.
Na kwa wanawake ambao mzunguko wao ni siku 26, Siku ya kupata mimba ni kati ya siku ya 5 ya mzunguko wao hadi siku ya 11 kutoka siku ya kwanza ya kutoka damu.
Siku za kupata mimba kwa wenye mzunguko wa siku 28.
Kwa wanawake ambao mzunguko wao ni siku 28, Siku ya kupata mimba ni kati ya siku ya 10 ya mzunguko wao hadi siku ya 16 kutoka siku ya kwanza ya kutoka damu.
Siku za kupata mimba kwa wenye mzunguko wa siku 30 au 32.
Kwa wanawake ambao mzunguko wao ni siku 30 , Siku ya kupata mimba ni kati ya siku ya 11 ya mzunguko wao hadi siku ya 17 kutoka siku ya kwanza ya kutoka damu.
Na Kwa wanawake ambao mzunguko wao ni siku 32, Siku ya kupata mimba ni kati ya siku ya 12 ya mzunguko wao hadi siku ya 18 kutoka siku ya kwanza ya kutoka damu.
Siku hizi za mzunguko wa hedhi yaani siku ya , siku ya 3 kwa wenye mzunguko wa siku 21, siku ya 5 kwa wenye mzunguko wa siku 26, siku ya 10 kwa wenye mzunguko wa siku 28, siku ya 11 kwa wenye mzunguko wa siku 30 na siku ya 12 kwa wenye mzunguko wa siku 32 ndio siku ambazo hatua ya upevukaji wa yai kwa mwanamke huanza.
Hatua hii kwa wastani hudumu kwa takribani siku 6 ambapo huendelea mpaka siku ya 9, siku ya 11, siku ya 16, siku ya 17 na siku ya 18 ya mzunguko kulingana na urefu wa mzunguko.
Katika siku hizi 6 uwezekano wa mwanamke kushika mimba ni mkubwa na hutajwa kama siku za kupata mimba.
Kwa mwanamke ambae ana mazoea ya kujichunguza juu ya mabadiliko mbalimbali ya mwili ni rahisi kugundua ikiwa yuko katika kipindi hiki kwa vile kipindi hiki huambatana na dalili kadhaa.
Kutunga kwa mimba.
Yai lilopevuka huishi takribani masaa 72 yaani siku 3, vilevile mbegu za kiume huishi takribani masaa 48 hadi 72 kulingana na aina ya mbegu ya kiume.Kwa mbegu ya kiume ambayo hupelekea mtoto wa kiume huishi kwa masaa 48 pekee wakati mbegu ya kiume inayopelekea mtoto wa kike huishi masaa 72 yaani siku 3.
Katika siku 6 za yai kupevuka, mara nyingi siku ya 2 yaani siku ya 5 kwa wenye mzunguko wa siku 21, siku ya 7 kwa wenye mzunguko wa siku 26, siku ya 12 kwa wenye mzunguko wa siku 28, siku ya 13 kwa wenye mzunguko wa siku 30 na siku ya 15 kwa wenye mzunguko wa siku 32.
Kwa hivyo siku ya 3, ya 5, ya 10, ya 11na ya 12 zinatajwa kama siku ambazo mwanamke anaweza kupata mimba kwa iwapo atakutana na mwanaume katika siku hizi.
Hii inatokana na kwamba ikiwa mwanamke atajamiana, mbegu za mwanaume huweza kuishi ndani ya mfumo wa uzazi kwa masaa 72.
Kwa maana ya kwamba mbegu hizi zinaweza kuishi hadi siku ya 5, ya 7, ya 12, ya 13 na ya 15.
Ni katika siku hizi ambapo uwezekano wa yai kupevuka ni mkubwa hivyo yai huzikuta mbegu bado ziko hai na mimba huweza kutungwa.
Dalili za siku ya kupata mimba.
Kwa sehemu kubwa dalili hizi husababishwa na mabadiliko ya homoni katika kipindi hiki cha yai kupevuka.Baadhi ya dalili za kuwa katika siku za kupata mimba ni pamoja na:
#1: Kutokwa na ute mwembamba na laini ukeni.
Kwa kawaida kutokwa na ute maeneo ya uke ni jambo la kawaida katika hatua mbalimbali za mzunguko wa hedhi.Ute huu huwa ni mzito na huwa na kiwango kikubwa cha protini za mucin ambazo huufanya kuwa mzito.
Lakini katika kipindi cha yai kupevuka ute huu huwa ni mwepesi, laini na wenye rangi nyeupe ya kung’aa.
Hii inatokana na ongezeko la kutengenezwa kwa maji hasa maeneo ya mfumo wa uzazi kunakosababishwa na ongezeko la homoni ya oestrojeni.
Mwanamke anaweza kuugundua kwa kutumia vidole au wakati mwingine huweza kujitokeza nje ya mashavu ya uke.
#2: Kupungua na kuongezeka kwa joto la mwili.
Kuanzia siku ya kwanza ya kutokwa damu ya hedhi jotoridi la mwanamke hushuka na kuwa katika wastani wa 36.40.CWakati wa yai kupevuka mara nyingi siku moja kabla joto la mwili hupungua. Ni kawaida mwanamke kupima na kukuta jotoridi ni kati ya 36.30C hadi 36.20C.
Jotoridi huwa chini zaidi wakati wa siku ya yai kupevuka takribani 36.20C na huanza kupanda kuanzia siku ya pili ya yai kupevuka hadi kufikia 36.40C.
Baada ya siku ya pili ya yai kupevuka jotoridi la mwili hupanda hadi kufikia 36.70C na jotoridi hilo huendelea mpaka siku ya 28 ya mzunguko yaani siku ya kuanza hedhi.
Ongezeko la homoni ya progesteroni ndio husababisha ongezeko la jotoridi la mwili kwa takribani.
Hata hivyo ongezeko la joto hutokea siku ya 1 au ya 2 baada ya yai kupevuka. Kwa hivyo ongezeko la jotoridi ni ishara kwamba yai lako limepevuka siku 1 au 2 zilizopita.
Hata hivyo ongezeko la jotoridi la mwili huathiriwa na mambo mengi ikiwemo:
- Homa na maradhi ya mwili.
- Ulevi.
- Msongo wa mawazo.
- Mazoezi ya mwili.
- Kuwahi au kuchelewa kulala.
- Jotoridi la mahali unapoishi.
- Matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango n.k.
Kwa hivyo katika kutumia mabadiliko ya jotoridi la mwili kama ishara ya kutambua siku za kupata mimba ni vyema kuzingatia mabo yaliyotajwa hapo juu.
Dalili nyinginezo za kuwa katika siku za kupata ujauzito ni:
- Kuongezeka kwa uwezo wa kutambua harufu.
- Matiti kujaa na chuchu kuvimba.
- Kuongezeka kwa hamu ya kujamiana.
- Maumivu ya tumbo la chini.
Njia za kisasa za kutambua siku za kupata mimba.
Mbali na njia za asili za kutambua siku za kupata mimba, vilevile zipo njia za kitaalamu ambazo unaweza kutumia ili kutambua ni siku gani sahihi kwako kupata ujauzito.Njia hizo ni pamoja na:
Uchunguzi wa kutumia kifaa mwangwi cha Ultrasonography.
Kipimo hiki huangalia mabadiliko ya ndani ya mfumo wa uzazi ambayo huambatana na kipindi cha yai kupevuka, mfano muonekano wa vifuko vya kutunzia mayai.Uchunguzi wa homoni mbalimbali katika mkojo.
Kipindi cha yai kupevuka na baada homoni mbalimbali huzalishwa kwa viwango tofauti na homoni hizi huweza kuonekana kupitia mkojo.- Homoni za luteinizing ambazo huongezeka kipindi cha yai kupevuka.
- Homoni za progesterone katika damu na pregnanediol 3‐glucuronide katika mkojo ambazo huongezeka siku moja baada ya yai kupevuka.
- Vilevile homoni za follicular stimulating ambazo huongezeka siku 1 kabla ya yai kupevuka.
Hitimisho.
Elimu juu ya mzunguko wa hedhi ni jambo muhimu zaidi katika kuzitambua siku za kupata mimba.Mimba zisizotarajiwa huweza kuwa na madhara makubwa ya kijamii, kiuchumi, kielimu, kisaikolojia na kiafya kwa ujumla.