Aina za chunusi, chanzo, sababu na tiba
Chunusi ni uvimbe unaotokea katika ngozi, uvimbe ambao unatokana na kutengenezwa kwa mafuta mengi kupita kiasi katika ngozi.
Tatizo la chunusi linaweza kuathiri sehemu yoyote ya ngozi lakini maeneo ya usoni, shingoni, mgongoni, matakoni na kifuani ndio sehemu ambazo huathiriwa zaidi.
Sehemu hizi huathiriwa zaidi na chunusi kwa sababu kuu zifuatazo;
Kazi kubwa ya vitundu hivi vilivyounganisha tezi za sebum na mashina ya vinyweleo ni kupitisha mafuta yanayozalishwa katika tezi na kuyapeleka sehemu ya nje ya ngozi.
Mafuta haya yanapofika sehemu ya nje ya ngozi huyeyuka na kusambaa katika ngozi, jambo hili linapelekea ngozi kuwa na muonekano nadhifu, mwororo na wenye kung’ara.
Ikiwa mlolongo huu wa utengenezwaji na usafirishwaji wa mafuta kutoka katika tezi za sebum kupeleka sehemu ya nje ya ngozi kupitia vitundu hivi utaathiriwa, basi tatizo la chunusi linaweza kujitokeza.
Mafuta haya hulundikana na kuchanganyikana na seli za ngozi zilizokufa kiasi cha kupelekea kutengenezwa kwa mchanganyiko mzito wa mafuta na seli zilizokufa ambao huwa na muonekano wa rangi nyeupe.
Si rahisi kwa mchanganyiko huu wa mafuta na seli zilizokufa kupita katika vitundu vya kutolea mafuta vilivyopo katikati ya tezi za sebum na mashina ya vinyweleo.
Hali hii inasababisha mchanganyiko huu kuziba vitundu hivi.
Mchanganyiko huu ndani ya ngozi unaweza kutawaliwa na bakteria, ikiwa bakteria wataingia katika mchanganyiko huu watazaliana na kuzalisha kemikali mbalimbali.
Kemikali hizi zinazozalishwa na bakteria husababisha mfumo wa kinga wa mwili kuzalisha askari kwa ajili ya kuwakabili bakteria husika.
Askari wanaozalishwa na mwili ili kupambana na bakteria hawa, husababisha kutengenezwa kwa uvimbe. Uvimbe huu ambao unasababishwa na askari wa mwili wako ndio huitwa chunusi.
Chunusi hizi hutokea ndani ya ngozi, ingawa kuna wakati inaweza kujitokeza kwa nje ya ngozi. Chunusi ya ndani inaweza kuwa na muonekano wa aina mbili, yenye ncha ya rangi nyeupe au yenye ncha ya rangi nyeusi.
Chunusi ya aina hii huwa na muonekano wa uvimbe mdogo wenye rangi nyekundu na huambatana na Maumivu makali endapo utaguswa.
Chunusi ya aina hii ni hatari kwa sababu ni rahisi kusambaza kwa bakteria hawa na kuambukiza maeneo ya jirani ikiwa chunusi hii itapasuka.
Hii ndio sababu kuu kwanini hutakiwi kupasua chunusi.
Chunusi ya aina hii huwa ni kubwa kimuonekano, yenye usaha na maumivu makali muda wote. Ikiwa chunusi ya aina hii itaisha basi huacha kovu la moja kwa moja.
Ni jukumu lako kuhakikisha unaisaidia ngozi kupambana na kiwango kikubwa cha mafuta ili kujiepusha na tatizo hili.
Katika kufanikisha jambo hili lishe bora, kujua aina ya ngozi yako na matumizi sahihi ya vipodozi ni jambo muhimu.
Tatizo la chunusi linaweza kuathiri sehemu yoyote ya ngozi lakini maeneo ya usoni, shingoni, mgongoni, matakoni na kifuani ndio sehemu ambazo huathiriwa zaidi.
Sehemu hizi huathiriwa zaidi na chunusi kwa sababu kuu zifuatazo;
- Sehemu hizi zina kiwango kikubwa cha tezi za mafuta, tezi ambazo huzalisha mafuta katika ngozi. Mfano usoni na mgongoni.
- Baadhi ya maeneo haya ni rahisi kuyagusa na mikono mara kwa mara, jambo hili husababisha uchafu, bakteria na mafuta ya ziada katika viganja kusambaa maeneo haya. Mfano usoni.
- Sababu nyingine ni kwamba baadhi ya maeneo haya huvuja jasho kwa kiasi kikubwa na kuachwa bila kusafishwa kwa muda mrefu. Hii ni sababu kuu kwa chunusi za matakoni na mapajani hasa kwa watu wanofanya mazoezi
Tezi ya sebum na mafuta katika ngozi
Chunusi huathiri zaidi vitundu vidogo vya kupitisha mafuta ambavyo huunganisha sehemu ya ndani ya ngozi (tezi ya sebum) na sehemu ya nje ya ngozi (mashina ya vinyweleo).Kazi kubwa ya vitundu hivi vilivyounganisha tezi za sebum na mashina ya vinyweleo ni kupitisha mafuta yanayozalishwa katika tezi na kuyapeleka sehemu ya nje ya ngozi.
Mafuta haya yanapofika sehemu ya nje ya ngozi huyeyuka na kusambaa katika ngozi, jambo hili linapelekea ngozi kuwa na muonekano nadhifu, mwororo na wenye kung’ara.
Ikiwa mlolongo huu wa utengenezwaji na usafirishwaji wa mafuta kutoka katika tezi za sebum kupeleka sehemu ya nje ya ngozi kupitia vitundu hivi utaathiriwa, basi tatizo la chunusi linaweza kujitokeza.
Jinsi gani chunusi hutokea?
Chunusi hutokea ikiwa ni matokeo ya kutengenezwa kwa mafuta mengi kupita kiasi katika tezi za sebum.Mafuta haya hulundikana na kuchanganyikana na seli za ngozi zilizokufa kiasi cha kupelekea kutengenezwa kwa mchanganyiko mzito wa mafuta na seli zilizokufa ambao huwa na muonekano wa rangi nyeupe.
Si rahisi kwa mchanganyiko huu wa mafuta na seli zilizokufa kupita katika vitundu vya kutolea mafuta vilivyopo katikati ya tezi za sebum na mashina ya vinyweleo.
Hali hii inasababisha mchanganyiko huu kuziba vitundu hivi.
Mchanganyiko huu ndani ya ngozi unaweza kutawaliwa na bakteria, ikiwa bakteria wataingia katika mchanganyiko huu watazaliana na kuzalisha kemikali mbalimbali.
Kemikali hizi zinazozalishwa na bakteria husababisha mfumo wa kinga wa mwili kuzalisha askari kwa ajili ya kuwakabili bakteria husika.
Askari wanaozalishwa na mwili ili kupambana na bakteria hawa, husababisha kutengenezwa kwa uvimbe. Uvimbe huu ambao unasababishwa na askari wa mwili wako ndio huitwa chunusi.
Aina za chunusi
Kuna aina kuu nne za chunusi kwa kuzingatia ni kwa kiwango gani zimeathiri ngozi, aina hizo ni;- Aina ya kwanza ni chunusi ya ndani (Comedo)
- Pili ni chunusi ya nje isiyo na usaha (Papule)
- Tatu ni chunusi ya nje iliyo na usaha (Pustule)
- Nne ni chunusi sugu ya nje yenye usaha (Cyst)
01: Chunusi ya ndani
Aina hii ya chunusi hutokea ikiwa mlundikano wa mafuta na seli zilizokufa zimeziba sehemu ya karibia na nje ya ngozi, yaani chini ya mashina ya vinyweleo.Chunusi hizi hutokea ndani ya ngozi, ingawa kuna wakati inaweza kujitokeza kwa nje ya ngozi. Chunusi ya ndani inaweza kuwa na muonekano wa aina mbili, yenye ncha ya rangi nyeupe au yenye ncha ya rangi nyeusi.
- Chunusi ya ndani yenye ncha nyeupe: hii hutokea ikiwa mlundikano huu utatokea ndani ya ngozi, yaani hakuna sehemu ya chunusi iliyojitokeza nje.
- Chunusi ya ndani yenye ncha nyeusi: Hii hutokea ikiwa sehemu ya chunusi itajitokeza kwa nje. Ikiwa sehemu ndogo ya chunusi itajitokeza, basi sehemu iliyojitokeza inapokutana na hewa ya oksijeni huungua na kutengeneza weusi.
02: Chunusi ya nje isiyo na usaha
Hii ni aina ya chunusi ambapo mlundikano wa mafuta na uchafu umeanzia ndani na kujitokeza mpaka nje ya ngozi kuzunguka mashina ya vinyweleo.Chunusi ya aina hii huwa na muonekano wa uvimbe mdogo wenye rangi nyekundu na huambatana na Maumivu makali endapo utaguswa.
03: Chunusi ya nje yenye usaha
Ikiwa chunusi ya nje isiyo na usaha itatawaliwa na bakteria itsababisha kutengenezwa kwa usaha na vilevile kuongezeka ukubwa.Chunusi ya aina hii ni hatari kwa sababu ni rahisi kusambaza kwa bakteria hawa na kuambukiza maeneo ya jirani ikiwa chunusi hii itapasuka.
Hii ndio sababu kuu kwanini hutakiwi kupasua chunusi.
04: Chunusi sugu ya nje yenye usaha
Hii ni aina ya chunusi ambayo huathiri eneo kubwa la ngozi. Aina hii inaweza kuathiri hadi matabaka mengine ya ndani ya ndozi.Chunusi ya aina hii huwa ni kubwa kimuonekano, yenye usaha na maumivu makali muda wote. Ikiwa chunusi ya aina hii itaisha basi huacha kovu la moja kwa moja.
Chunusi husababishwa na nini?
Kuna sababu kuu 5 ambazo husababisha chunusi, sababu hizo ni:- Mabadiliko ya homoni za uzazi
- Kutengenezwa kwa mafuta mengi
- Kutumia vipodozi vya kuchichubua ngozi
- Uwepo wa bakteria katika ngozi
- Mzio au aleji
- Majeraha madogo ya ngozi.
Jinsi gani ya kutibu chunusi?
Njia kuu ya kutibu chunusi ni kuisaidia ngozi kuondoa mafuta ya ziada. Unaweza kufanikisha hili kwa kufanya yafuatayo:- Kutumia dawa za kuondoa chunusi za kunywa
- Kutumia dawa za kuondoa chunusi za kupaka
- Kuzingatia lishe maalumu kwa ajili ya kupambana na chunusi
- Njia za asili za kuondoa chunusi.
Hitimisho
Chunusi ni moja ya tatizo kubwa la ngozi linalowasumbua watu wengi. Kutengenezwa kwa mafuta mengi katika ngozi ndio sababu kuu ya tatizo hili.Ni jukumu lako kuhakikisha unaisaidia ngozi kupambana na kiwango kikubwa cha mafuta ili kujiepusha na tatizo hili.
Katika kufanikisha jambo hili lishe bora, kujua aina ya ngozi yako na matumizi sahihi ya vipodozi ni jambo muhimu.