Njia za kuondoa seli za ngozi zilizokufa na faida zake katika urembo wa ngozi
Kumenya ngozi ambayo ina kiwango kikubwa cha seli zilizokufa ni moja ya mbinu bora zaidi za kuimarisha afya ya ngozi na muonekano wake.
Kisayansi, seli za ngozi yako zinakufa kila baada ya wiki 1 hadi 3, ndani ya kipindi hiki seli za mwili huzeeka na Kupoteza uwezo wa kufanya kazi.
Unahitaji kutumia mbinu za ziada za kuodoa seli hizi zilizokufa (exfoliation) ili kuikinga ngozi yako dhidi ya madhara mbalimbali yanayoweza kujitokeza, kama vile chunusi, mapunye, vibarango na ukurutu.
Pamoja na kwamba mwili wako una njia ambazo huzitumia katika kuhakikisha seli hizi zilizokufa zinaondolewa na kuacha seli mpya kwa ajili ya kuendelea na kazi mbalimbali katika ngozi yako.
Ufanisi wa mwili katika kuondoa seli hizi zilizokufa una changamoto nyingi, mojawapo ni aina ya ngozi. Ili kusaidia mchakato mzima wa kuondolewa kwa seli hizi, unashauri kutumia njia za ziada za kuziondoa seli hizi.
Ikiwa seli hizi hazitaondolewa kwa wakati hubadilika na kuwa uchafu, uchafu huu unaweza kuvutia vimelea wa aina mbalimbali jambo linaloweza kusababisha matatizo mbalimbali ya ngozi.
Katika Makala hii tutakuelezea aina za vimenya ngozi (viondoa seli zilizokufa) kulingana na aina ya ngozi yako.
Usishawishike kumenya ngozi yako mara kwa mara eti kwa sababu labda ina mafuta mengi.
Tumia scrubs hizi zote kwa kupaka usoni au katika ngozi, Usisugue, unachotakiwa kufanya ni kusambaza mchanganyiko wa scrub uliyochagua.
Kwa scrub za unga, tumia kwa kuchanganya na maji au mafuta kama vile mafuta ya mzeituni au alizeti.
Ni rahisi kupata matatizo ikiwa hufahamu kutumia mashine hizi.
Kwa sehemu kubwa njia hii hutumiwa na wataalamu wa afya katika masuala ya ngozi na hutumiwa zaidi katika kliniki za ngozi.
Unaruhusiwa kutumia ikiwa hazikuletei shida yeyote ya ngozi, lakini kama ukitumia unapata matatizo ni vizuri kuziepuka na kuchagua vimenya ngozi sahihi kwa ngozi yako.
Kuondoa seli zilizokufa ni jambo zuri katika kuimarisha urembo wa ngozi, lakini si lazima kutumia mbinu hii kwa sababu mwili wako unaweza kufanikisha kazi hii ikiwa utaupatia mahitaji muhimu.
Lishe bora na matumizi sahihi ya mafuta ya ngozi na vipodozi ni miongoni mwa mahitaji muhimu ya mwili ili kufanikisha kazi hii.
Kisayansi, seli za ngozi yako zinakufa kila baada ya wiki 1 hadi 3, ndani ya kipindi hiki seli za mwili huzeeka na Kupoteza uwezo wa kufanya kazi.
Unahitaji kutumia mbinu za ziada za kuodoa seli hizi zilizokufa (exfoliation) ili kuikinga ngozi yako dhidi ya madhara mbalimbali yanayoweza kujitokeza, kama vile chunusi, mapunye, vibarango na ukurutu.
Pamoja na kwamba mwili wako una njia ambazo huzitumia katika kuhakikisha seli hizi zilizokufa zinaondolewa na kuacha seli mpya kwa ajili ya kuendelea na kazi mbalimbali katika ngozi yako.
Ufanisi wa mwili katika kuondoa seli hizi zilizokufa una changamoto nyingi, mojawapo ni aina ya ngozi. Ili kusaidia mchakato mzima wa kuondolewa kwa seli hizi, unashauri kutumia njia za ziada za kuziondoa seli hizi.
Ikiwa seli hizi hazitaondolewa kwa wakati hubadilika na kuwa uchafu, uchafu huu unaweza kuvutia vimelea wa aina mbalimbali jambo linaloweza kusababisha matatizo mbalimbali ya ngozi.
Katika Makala hii tutakuelezea aina za vimenya ngozi (viondoa seli zilizokufa) kulingana na aina ya ngozi yako.
Jinsi ya kuondoa seli zilizokufa katika ngozi (kumenya ngozi)
Kumenya ngozi kuna faida nyingi katika kuimarisha urembo wa ngozi, lakini unapaswa kuwa na kiasi katika kutumia mbinu hii.Usishawishike kumenya ngozi yako mara kwa mara eti kwa sababu labda ina mafuta mengi.
Bila kujali aina ya ngozi unashauri kutumia mbinu hii kwa kiwango kisichozidi mara 3 kwa wiki hasa kwa watu wenye ngozi za kawaida.
Ikiwa utazidisha matumizi ya njia hii utapelekea tatizo la mshituko wa ngozi, tatizo hili hupelekea mwili kuzalisha homoni za Cortisol.
Madhara ya homoni hii ya cortisol si katika ngozi tu, bali katika sehemu nyingine za mwili wako huathiriwa pia.
Ngozi kuwa nyekundu, ngozi kuvimba, ngozi kujimenya yenyewe na kuwa na muonekano wa mithili ya vipande vya ngozi vinavyoning’inia.
Hizi zote ni ishara kwamba unatumia mbinu hii kupita kiasi na unashauriwa kusimama kutumia njia hii kwa muda mpaka ngozi yako itakapotengamaa.
Ikiwa utamenya ngozi yako kupita kiasi katika kiwango ambacho kitatengeneza vidonda na kuhisi ngozi kuwaka moto unaweza kutumia aloe vera gel ili kusaidia ngozi kutengamaa.
Unaweza kutumia mbinu hii wakati wowote ngozi yako itakapohitaji kupata huduma hii, iwe mchana au usiku.
Ngozi ya uso ndio huwa shabaha ya mbinu hii ingawa unaweza kutumia mbinu hii katika sehemu yeyote ya ngozi.
Ili kumenya ngozi ya uso iliyo na sele zilizokufa zingatia hatua hizi:
Bidhaa hizi zimegawanywa katika makundi makuu 4 ambayo ni:
Matokeo yake ni kutengenezwa kwa uchafu ambao ni mchanganyiko wa vimenya ngozi, seli zilizokufa, jasho na mafuta.
Mchanganyiko huu unaotengenezwa ni rahisi kuondolewa na maji na unaweza kutumia maji safi ya kawaida ili kuondoa mchanganyiko wa uchafu huu katika uso wako au maeneo mengine ya ngozi.
Viondoa seli zilizokufa (Vimenya ngozi) maarufu katika kundi hili ni pamoja na;
Viondoa seli zilizokufa (Vimenya ngozi) maarufu katika kundi hili ni pamoja na;
Acha walau dakika 10 hadi 20 ili kuruhusu vimeng’enya katika matunda haya kufanya kazi kwa ufasaha.
Baadhi ya scrub za asili kwa ajili ya kuondoa seli za ngozi zilizokufa ni pamoja na;
Vilevile unga wa mahindi uliopondwa vizuri ni moja ya scrub ya asili yenye ufanisi wa hali ya juu.
Ikiwa utazidisha matumizi ya njia hii utapelekea tatizo la mshituko wa ngozi, tatizo hili hupelekea mwili kuzalisha homoni za Cortisol.
Madhara ya homoni hii ya cortisol si katika ngozi tu, bali katika sehemu nyingine za mwili wako huathiriwa pia.
Ngozi kuwa nyekundu, ngozi kuvimba, ngozi kujimenya yenyewe na kuwa na muonekano wa mithili ya vipande vya ngozi vinavyoning’inia.
Hizi zote ni ishara kwamba unatumia mbinu hii kupita kiasi na unashauriwa kusimama kutumia njia hii kwa muda mpaka ngozi yako itakapotengamaa.
Ikiwa utamenya ngozi yako kupita kiasi katika kiwango ambacho kitatengeneza vidonda na kuhisi ngozi kuwaka moto unaweza kutumia aloe vera gel ili kusaidia ngozi kutengamaa.
Ni wakati gani sahihi wa kuondoa seli zilizokufa katika ngozi?
Kila mtu ana wakati wake ambao ngozi yake inahitaji huduma ya kumenywa kutokana na kuwepo kwa seli zilizokufa.Unaweza kutumia mbinu hii wakati wowote ngozi yako itakapohitaji kupata huduma hii, iwe mchana au usiku.
Ngozi ya uso ndio huwa shabaha ya mbinu hii ingawa unaweza kutumia mbinu hii katika sehemu yeyote ya ngozi.
Ili kumenya ngozi ya uso iliyo na sele zilizokufa zingatia hatua hizi:
- Osha uso wako au ngozi yako kwa maji safi na salama.
- Weka kumenya ngozi chako maeneo ya komwe, eneo la juu la taya na katika mashavu kisha anza kusugua taratibu ili kukisambaza kimenya ngozi chako uso mzima.
- Baada ya kumenya ngozi kusambaa uso mzima, acha kwa dakika kadhaa
- Na mwisho osha uso wako ili kuondoa kumenya ngozi pamoja na uchafu
- vilainisha ngozi (Softener),
- viimarisha rangi ya ngozi (Toning),
- vizuia maji kutoka katika ngozi (Moisturizer).
Aina za viondoa seli za ngozi zilizokufa (Vimenya ngozi)
Kuna aina tofauti ya bidhaa za urembo ambazo unaweza kuzitumia ili kuondoa seli za ngozi zilizokufa.Bidhaa hizi zimegawanywa katika makundi makuu 4 ambayo ni:
01: Vimenya ngozi vyenye asili ya kemikali.
Vimenya ngozi hivi vimeundwa na kemikali maalumu ambazo huyeyusha seli zilizokufa, jasho, mafuta katika ngozi na uchafu wa aina mbalimbali katika ngozi.Matokeo yake ni kutengenezwa kwa uchafu ambao ni mchanganyiko wa vimenya ngozi, seli zilizokufa, jasho na mafuta.
Mchanganyiko huu unaotengenezwa ni rahisi kuondolewa na maji na unaweza kutumia maji safi ya kawaida ili kuondoa mchanganyiko wa uchafu huu katika uso wako au maeneo mengine ya ngozi.
Viondoa seli zilizokufa (Vimenya ngozi) maarufu katika kundi hili ni pamoja na;
- Glycolic acid ambacho hutengenezwa kutoka katika sukari
- Phenol
- Lactic acid hutengenezwa kutoka katika maziwa
- Salicylic acid hutengenezwa kutoka katika mmea wa white willow
Jinsi ya kutumia
- Paka maeneo ya usoni au maeneo mengine ya ngozi.
- Usisugue aina hii ya vimenya ngozi, paka kisha acha kwa dakika chache na kitafanya kazi chenyewe bila kusugua katika ngozi
02: Vimenya ngozi vyenye asili ya Vimeng’enya
Vimeng’enya ni aina ya dutu ambazo hupatikana mwilini vilevile katika matunda mbalimbali. Iwapo dutu hizi zitawekwa katika ngozi basi zina uwezo wa kumenya seli zilizokufa.Viondoa seli zilizokufa (Vimenya ngozi) maarufu katika kundi hili ni pamoja na;
- Vimeng’enya vya papain ambavyo hupatikana kwa wingi katika Papai
- Vimeng’enya vya bromelain ambavyo hupatikana zaidi katika Nanasi.
- Vilevile maboga yana vimen’genya ambavyo unaweza kutumia kuondoa seli zilizokufa katika ngozi
Acha walau dakika 10 hadi 20 ili kuruhusu vimeng’enya katika matunda haya kufanya kazi kwa ufasaha.
03: Vimenya ngozi aina ya scrubs
Unaweza kutumia scrub maalumu kwa ajili ya kuondoa seli za ngozi zilizokufa. Zipo scrubs za aina tofauti kulingana na mahitaji ambazo unaweza kuzitumia kuondoa seli zilizokufa katika ngozi.Baadhi ya scrub za asili kwa ajili ya kuondoa seli za ngozi zilizokufa ni pamoja na;
- Unga laini wa maganda ya karanga yaliyopondwa: Scrub hii si nzuri sana kutokana na asili ya ugumu maganda ya karanga, ni rahisi kwa scrub hii kukusababishia majeraha katika ngozi.
- Udongo laini: Unaweza kutumia udongo laini ambao ni maalumu kwa ajili ya kuondoa seli zilizokufa katika ngozi. Udongo huu unapatikana maduka ya urembo, na nchini Tanzania udongo huu unapatikana mikoa ya kanda ya kati.
- Unga laini mithili ya poda unaotokana na mahindi au ngano.
- Unga laini wa mchele
- Kemikali za polyurethane au silicone: Polyurethane na silicone, ni aina ya scrubs ambazo ni laini na salama zaidi dhidi ya majeraha ya ngozi.
Vilevile unga wa mahindi uliopondwa vizuri ni moja ya scrub ya asili yenye ufanisi wa hali ya juu.
Tumia scrubs hizi zote kwa kupaka usoni au katika ngozi, Usisugue, unachotakiwa kufanya ni kusambaza mchanganyiko wa scrub uliyochagua.
Kwa scrub za unga, tumia kwa kuchanganya na maji au mafuta kama vile mafuta ya mzeituni au alizeti.
04: Vimenya ngozi vya mitambo
Zipo mitambo/mashine ambazo unaweza kutzitumia ili kuondoa seli zilizokufa katika ngozi. Si rahisi kuzitumia machine hizi kwa sababu zina hitaji uwelewa wa kiwango cha juu.Ni rahisi kupata matatizo ikiwa hufahamu kutumia mashine hizi.
Kwa sehemu kubwa njia hii hutumiwa na wataalamu wa afya katika masuala ya ngozi na hutumiwa zaidi katika kliniki za ngozi.
05: Vimenya ngozi mchanganyiko
Kuna wakati unaweza kukutana na bidhaa ya kukusaidia kuondoa seli zilizokufa katika ngozi ambayo ina mchanganyiko wa vimenya ngozi zaidi ya kimoja.Unaruhusiwa kutumia ikiwa hazikuletei shida yeyote ya ngozi, lakini kama ukitumia unapata matatizo ni vizuri kuziepuka na kuchagua vimenya ngozi sahihi kwa ngozi yako.
Hitimisho
Urembo wa ngozi ni muhimu kwa ajili ya kuimarisha muonekano wako. Kuna mambo mengi ambayo unapaswa kufanya ili kuboresha muonekano wa ngozi yako.Kuondoa seli zilizokufa ni jambo zuri katika kuimarisha urembo wa ngozi, lakini si lazima kutumia mbinu hii kwa sababu mwili wako unaweza kufanikisha kazi hii ikiwa utaupatia mahitaji muhimu.
Lishe bora na matumizi sahihi ya mafuta ya ngozi na vipodozi ni miongoni mwa mahitaji muhimu ya mwili ili kufanikisha kazi hii.