Faida za vitamini E mwilini, madhara na vyakula vyenye vitamini E
Kama vitamini A, B, C, D, E na K ni wanafunzi katika darasa, basi Vitamini E ndio mwanafunzi ambaye siku zote ataondoka na alama A+ katika mitihani ya kuimarisha afya ya moyo, kuondoa sumu mwilini na kuimarisha kinga ya mwili.
Unapozungumzia sumu za mwili, kwa sehemu kubwa husababishwa na chaji huru mwilini. Kuwepo kwa chaji huru mwilini hukusababishia matatizo mbalimbali ya kiafya ikiwemo;
Vitamini E imegawanyika katika makundi makubwa 2 ambayo ni tocopherols na tocotrienols. Katika kila kundi kuna wanachama wanne ambao ni alpha, beta, gamma, na delta.
Makundi yote ni muhimu, lakini kundi la tocopherols ndio kundi ambalo lina ufanisi wa hali ya juu wa kupambana na sumu mwilini.
Hata hivyo hutakiwi kuwa na wasiwasi juu ya kundi lipi unalipata wapi, kwa sababu vyakula vingi vya asili, vitamini E katika vyakula hivi hupatikana katika muundo wa alpha tocopherol. Muundo ambao ni bora zaidi.
Jedwali linaloonesha viwango vya vitamini E kwa kila siku katika makundi mbalimbali ya watu
Makundi haya ni kama yafuatayo:
Kwa watu ambao tatizo ni kubwa wanaweza kutumia vidonge maalumu vyenye virutubisho vya vitamini E.
Katika kufanikisha hili unahitaji kiondoa sumu cha mwili chenye ufanisi na gharama nafuu. Vitamini E ni chaguo nambali 1 katika kufanikisha hili.
Unahitaji kiasi kisichopungua miligramu 8 hadi 12 kila siku ili kuusaidia mwili kupambana na sumu hizi, ingawa unaweza kutumia kiasi cha vitamini E utakacho kwa sababu dozi kubwa ya vitamini E haina madhara yeyote katika mwili.
Ili kuongeza ufanisi, changanya Vitamin E, Vitamin A na Vitamin C kwa pamoja, hapo utakuwa umetengeneza askari imara katika mwili wako ambaye hawezi kushindwa na adui wa aina yeyote.
Unapozungumzia sumu za mwili, kwa sehemu kubwa husababishwa na chaji huru mwilini. Kuwepo kwa chaji huru mwilini hukusababishia matatizo mbalimbali ya kiafya ikiwemo;
- Saratani
- Kukuzeesha mapema
- Matatizo ya uti
- Kuharibika kwa kiwambo cha seli za mwili
- Kuvuruga ph ya mwili
- Kudhoofisha kinga yako ya mwili
Faida za vitamini E mwilini
Unahitaji vitamini E mwilini kwa sababu zifuatazo- Kuondoa sumu za mwili (chaji huru). Ni lazima kuondoa sumu hizi mwilini kwa sababu uwepo wako unafanya uharibifu mkubwa katika seli za mwili.
- Kutibu na kukukinga na maradhi ya moyo: Vitamini E inazuia kutengenezwa kwa mafuta kutoka kwenye rehemu, zuio la utengenezwaji wa mafuta kutoka katika rehemu linapunguza uwepo wa vipande vya mafuta katika mishipa ya damu ambavyo vinaweza kuziba mishipa ya damu na kusababisha shambulizi la moyo au kiharusi.
- Kutibu na kukukinga na maradhi ya saratani: Chaji huru mwilini ni moja ya sababu kuu za saratani, uwezo wa vitamini E kupambana na sumu hizi unafanya virutubisho hivi kuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa wa saratani hasa saratani ya mlango wa kizazi na saratani ya matiti.
- Kuimarisha kumbukumbu hasa kwa wazee: Unapozeeka mwili unapunguza ufanisi, vivyo hivyo kiwango cha chaji huru huongezeka na kuangamiza seli za mwili. Seli za ubongo ni miongoni mwa seli ambazo huathiriwa zaidi na kupelekea matatizo kadhaa ikiwemo tatizo la kupoteza kumbukumbu.
- Kutibu matatizo ya ugumba kwa wanaume: Moja ya seli zinazoathiriwa na chaji huru mwilini ni mbegu za kiume. Kwa baadhi ya wanaume tatizo la ugumba linaweza kutatuliwa kwa matumizi ya vitamini E mara kwa mara. Tumia 200IU kila siku kwa mwezi mmoja.
Faida nyinginezo za vitamini Eni pamoja na;
- Maumivu ya matiti na uvimbe
- Husaidia watu wenye kisukari
- Kutibu ugonjwa wa DVT
- Kutibu ugonjwa wa kiharusi
- Kuimarisha afya ya macho
Vyakula vyenye vitamini E kwa wingi
Miili yetu haiwezi kutengeneza Vitamini E, tunahitaji kuvipata vyakula hivi kutoka katika vyakula.Vitamini E imegawanyika katika makundi makubwa 2 ambayo ni tocopherols na tocotrienols. Katika kila kundi kuna wanachama wanne ambao ni alpha, beta, gamma, na delta.
Makundi yote ni muhimu, lakini kundi la tocopherols ndio kundi ambalo lina ufanisi wa hali ya juu wa kupambana na sumu mwilini.
Hata hivyo hutakiwi kuwa na wasiwasi juu ya kundi lipi unalipata wapi, kwa sababu vyakula vingi vya asili, vitamini E katika vyakula hivi hupatikana katika muundo wa alpha tocopherol. Muundo ambao ni bora zaidi.
Jedwali linaloonesha viwango vya vitamini E kwa kila siku katika makundi mbalimbali ya watu
|
Kiwango kinachotakiwa cha vitamini E mwili kwa
makundi ya watu |
|
|
Miaka |
Dozi ya vitamini eE katika miligramu |
|
0-1 |
3-4 |
|
1-10 |
6-7 |
|
Wanaume 11+ |
10 |
|
Wanawake 11+ |
8 |
|
Wajawazito |
10 |
|
Wanaonyonyesha |
12 |
Vyakula vyenye vitamini E kwa wingi;
- Mafuta ya mlozi
- Siagi ya karanga na karanga
- Parachichi
- Mhazeli (hazenult)
- Viazi vitamu
- Mafuta ya ngano
- Mafuta ya alizeti ma alizeti
- Maembe
Dalili za Upungufu wa vitamini E mwilini
Hakuna madhara ya moja kwa moja ya upungufu wa vitamini E. Ikiwa utakosa kiwango kinachotakiwa na mwili kwa muda mrefu unaweza kupata matatizo mbalimbali kama vile:- Kupoteza kumbukumbu
- Maumivu ya uti wa mgongo
- Kuharibika kwa macho
- Maumivu ya neva
- Maumivu ya misuli
Watu walio katika hatari ya kupata upungufu wa vitamini E
Kuna baadhi ya makundi ya watu yako katika hatari kubwa ya kupatwa na tatizo la upungufu wa vitamini E.Makundi haya ni kama yafuatayo:
- Watu wenye uvimbe katika kizazi: Kundi hili huwa na hitilafu za ufyonzwaji wa vitamini E kutoka katika mfumo wa chakula kuingia katika seli. Ikiwa una tatizo hili wasiliana na daktari au mfamasia kwa ushauri zaidi.
- Una ugonjwa wa Crohn: Watu hawa hawana uwezo wa kufyonza vitamini E hasa kutoka maeneo ya utumbo .
- Watu wenye maradhi ya ini: Ikiwa una matatizo ya ini uwezo wako wa kuchakata vitamini E ni mdogo, wasiliana na mtaalamu wa afya kwa ushauri.
- Unatumia dawa za kupunguza mafuta mwilini: Mfano cholestyramine na colestipol. Dawa hizi huzuia ufyonzwaji wa vitamini muhimu mwilini ikiwemo vitamini E.
Kwa watu ambao tatizo ni kubwa wanaweza kutumia vidonge maalumu vyenye virutubisho vya vitamini E.
Hitimisho
Mwili wako unatengeneza sumu kila sekunde ikiwa ni sehemu ya utendaji kazi wake. Ni jukumu lako kuhakikisha unausaidia mwili kupunguza sumu hizi ili kuimarisha utendaji kazi wake.Katika kufanikisha hili unahitaji kiondoa sumu cha mwili chenye ufanisi na gharama nafuu. Vitamini E ni chaguo nambali 1 katika kufanikisha hili.