Chanzo cha kupata tezi dume na madhara yake
Uzee ni dawa, huu ni msemo unaoupa uzee heshima na matamanio ya karibu kila kijana kufikia katika hatua hii.
Licha ya heshima ya hii, uzee una changamoto nyingi mno za kiafya ambazo nyingi si rahisi kuzithibiti kwa kuwa ni za kibaolojia na ni za lazima kutokea.
Ukuaji wa tezi hii huwa ni wa kawaida wakati wa kuzaliwa na kasi ya ukuaji huongezeeka wakati wa balehe.
Moja ya changamoto kubwa kwa wazee na wanaume kwa ujumla ni tatizo la uvimbe wa tezi dume.
Tazizo hili la tezi dume si la lazima sana kwa mzee kuwa nalo, lakini kadri unavokuwa ndivyo uwezekana wa kupata tatizo hili huwa mkubwa.
Tazizo hili la tezi dume si la lazima sana kwa mzee kuwa nalo, lakini kadri unavokuwa ndivyo uwezekana wa kupata tatizo hili huwa mkubwa.
Sababu kuu ni kwamba tezi dume haishi kukua. Ukuaji huu wa tezi dume ndio unaweza kuwa tatizo kwako ikiwa kuna mambo mengine ya ziada yatachagiza.
Takwimu zinaonyesha kadri umri unavyoongezeka ndivyo wezekano wa kupata tatizo la tezi dume unakuwa mkubwa.
Takwimu zinaonyesha kadri umri unavyoongezeka ndivyo wezekano wa kupata tatizo la tezi dume unakuwa mkubwa.
Asilimia 60 ya wazee wenye kati ya umri wa miaka 50-60 wanatatizo hili. Na zaidi ya asilimia 80 ya wazee kati ya miaka 80 na kuendelea wanatatizo hili la tezi dume.
Tatizo hili la tezi dume huweza kumpata mwanaume yeyote katika umri wowote lakini wanaume walio katika balehe na wazee ndio wako katika hatari zaidi.
Tatizo hili la tezi dume huweza kumpata mwanaume yeyote katika umri wowote lakini wanaume walio katika balehe na wazee ndio wako katika hatari zaidi.
Ugonjwa wa tezi dume ni kitu gani?
Ugonjwa wa tezi dume ni matokeo ya seli zinazounda tezi hii ya kiume kukua na kuongezeka idadi bila uratibu maalumu wa mwili.Ukuaji huu unasababisha kuvimba kwa tezi hii na kuminya ama kugandamiza mlija unaopitisha manii na mkojo(urethra).
Kuminyika au kugandamizwa kwa mlija wa manii ndio husababisha kuibuka kwa matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi na mifumo iliyo jirani na mfumo wa uzazi.
Kuminyika au kugandamizwa kwa mlija wa manii ndio husababisha kuibuka kwa matatizo mbalimbali katika mfumo wa uzazi na mifumo iliyo jirani na mfumo wa uzazi.
Moja ya mfumo ambao huweza kuathiriwa zaidi na ugonjwa wa tezi dume ni mfumo wa mkojo.
Tezi dume inapatikana katikati ya puru na uume, mbele ya puru chini ya kibofu. Ni makutano ya mlija wa mkojo na mlija wa manii. Milija yote miwili inaingia hapa na unatoka kama mlija mmoja kuelekea katika uume.
Je, Tezi dume ni ugonjwa?
Hapana, tezi dume si ugonjwa. Tezi dume ni ogani ya mwili ambayo ambayo inapatikana kwa mwanaume.Tezi dume inapatikana katikati ya puru na uume, mbele ya puru chini ya kibofu. Ni makutano ya mlija wa mkojo na mlija wa manii. Milija yote miwili inaingia hapa na unatoka kama mlija mmoja kuelekea katika uume.
Sayansi ya tezi dume.
Tezi dume hufanya kazi kuu mbili kwa mwanaume ambazo ni:- Kuzalisha shahawa ambazo husaidia kuzipatia mbegu za kiume chakula na ulinzi dhidi ya hali ya kitindikali katika uke(ute huu una asili ya magadi).
- Na kazi ya pili ni kuthibiti utoaji mkojo na utoaji mbegu za kiume, katika tezi hii kuna misuli ambayo hudhibiti kufunguka na kufunga kwa milango ya mkojo na mbegu za kiume kadri inavyopaswa.
Vilevile wakati wa kutoa manii misuli hii hufunga mlango wa kibofu ili manii yasiingie kibofuni.
Ukuaji wa tezi hii huwa ni wa kawaida wakati wa kuzaliwa na kasi ya ukuaji huongezeeka wakati wa balehe.
Ongezeko hili linatokana na kuongezeka kwa uzalishwaji wa homoni za kiume ambazo ndio hufanya kazi kubwa ya ukuaji wa tezi hii.
Ukuaji huongezeka zaidi baada ya miaka 40 na kuendelea kwa sababu uthibiti wa mwili katika uzalishwaji wa homoni ya DHT huwa dhaifu.
Ukuaji huongezeka zaidi baada ya miaka 40 na kuendelea kwa sababu uthibiti wa mwili katika uzalishwaji wa homoni ya DHT huwa dhaifu.
Jambo hili hupelekea kiwango kikubwa cha DHT katika mwili, DHT ni homoni ama kichocheo ambacho ndio huusika zaidi na ukuaji wa tezi hii.
Tezi dume husababishwa na nini?
Mpaka sasa, ulinmwengu wa sayansi unaamini chanzo cha ugonjwa wa tezi dume ni uthibiti mbovu wa uzalishwaji wa homoni ya dihydrotestosterone (DHT).Homoni hii ya DHT inatokana na homoni ya uzazi iitwayo testosterone ambayo huzalishwa katika korodani.
Baada ya kuzalishwa, homoni hii hubadilishwa kwenda katika homoni ya DHT, homoni ya DHT inapofika katika tezi dume inajishikiza katika vipokezi maalumu vilivyo katika tezi dume.
Baada ya kuzalishwa, homoni hii hubadilishwa kwenda katika homoni ya DHT, homoni ya DHT inapofika katika tezi dume inajishikiza katika vipokezi maalumu vilivyo katika tezi dume.
Baada ya kujishikiza vipokezi hivi vinapeleka taarifa katika kiini cha seli za tezi dume na ukuaji unaanza mara moja.
Ikiwa ukuaji huu hautadhibitiwa basi tezi dume hukua kupita kawaida na kuvimba. Uvimbe unaotokana na ukuaji huu ndio huitwa ugonjwa wa tezi dume.
Hii si saratani bali ni ongezeko la seli ambazo ni hai na zinaweza dhibitiwa, wakati mwingine zinaweza kubadilika na kuwa seli za saratani.
Licha ya kwamba homoni ya testosterone hupungua kadri unavyozeeka lakini uwezekano wa kupata tatizo la tezi dume unaongezeka.

Hii inaashiria si DHT pekee ndio chanzo bali kuna mambo mengine ambayo yanahusika katika kutokea kwa ugonjwa wa tezi dume.
Mambo hayo yanadhaniwa kuchangia ugonjwa wa tezi dume ni pamoja na :
Mambo hayo yanadhaniwa kuchangia ugonjwa wa tezi dume ni pamoja na :
- Matatizo ya kisukali
- Kiwango kikubwa cha vichocheo vya norepinephrine, angiotensin II na insulin
- Maambukizi ya njia ya mkojo
- Kuvimba kwa tezi dume
- Kupungua kwa kipenyo cha mrija wa mkojo
- Kovu kwenye shingo ya kibofu ambalo husababishwa na matokeo ya upasuaji
- Mawe kwenye kibofu au kwenye figo
- Matatizo na mishipa inayodhibiti kibofu cha mkojo
- Saratani ya tezi dume au kibofu
Madhara ya uvimbe wa tezi dume
Katika hatua za awali tezi dume si tatizo hatarishi la afya. Kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo tatizo huwa kubwa na kuwa hatari kwa afya ikiwa haritaanza kudhibitiwa.Yafuatayo ni madhara ya ugonjwa wa tezi dume.
#1: Kusababisha uvimbe katika tezi:
Ongezeko la chembe hai za uhai(seli) katika tezi dume kunasababisa tezi hii kuwa kubwa na kutuna/kuvimba.
Kuvimba huku kunasababisha milija ya mkojo na ule wa manii kuminyika na kupungua kipenyo.
Kupungua kwa kipenyo cha milija hii muhimu kunaathiri utoaji wa mkojo na utoaji wa manii pia.
#2: Kusababisha maambukizi katika mfumo wa mkojo
Kutokana na kupungua au kuziba kwa milija ya mkojo, kunakuwa na ugumu wa kutoka kwa mkojo kwa njia ya kawaida.
Hii inapelekea misuli iliyopo katika kibofu kuongeza hali ya kusinyaa na kutanuka ikiwa ni jitihada mbadala za mwili za kutoa mkojo.
Jambo hili linapelekea kuta za kibofu kutanuka na kuongezeka ukubwa. Kuongezeka ukubwa kwa kuta za kibofu na kuongezeka kutanuka na kusinyaa kwa misuli inayounda kuta hizo kunaweza sababisha mkojo kurudi katika figo.
Hali hii ni hatari zaidi kwa vile unaweza kupata maradhi ya figo kama vile UTI, mawe katika figo na figo kushindwa kufanya kazi.
#3: Kukosa hamu ya kujamiana
Hii ni kwa sababu ya kuminyika kwa mishipa ya damu iliyoko katika tezi dume na maeneo ya jirani.
#4: Madhara mengine ya tezi dume
- kupungukiwa nguvu za kiume na
- kushindwa kusimamisha uume.
- maambukizi ya mfumo wa mkojo
- mawe katika kibofu cha mkojo
- kutokwa na damu katika njia ya mkojo
- kukosa uwezo wa kukojoa ghafla
Hitimisho
Ni vigumu kufahamu ikiwa una tatizo la tezi dume. Mara nyingi uchunguzi wa mara kwa mara ni muhimu zaidi ili kufuatilia ukubwa wa tezi yako.
Si lazima kila mgonjwa wa tezi dume kupatiwa matibabu, na kama ikitakiwa hivyo basi mabadiliko ya mtindo wa maisha, dawa, na upasuaji ni baadhi ya njia za kutibu tezi dume.