Faida za Saw palmetto kwa wanaume na jinsi ya kutumia
Faida za Saw palmetto (Serenoa repens ) mwilini ni za kipekee kutokana na aina ya matatizo ambayo mmea huu unaweza kuyatibu.
Moja ya matatizo yanayoweza kutibiwa na mmea huu wa Saw palmetto ni maradhi uvimbe wa tezi dume.
Uwezo huu wa saw palmetto kutibu uvimbe katika tezi dume kunaufanya mmea huu kuwa ni mmea wa lazima kwa wanaume wanaojali afya zao.
Uwezo wa saw palmetto kudhibiti utengenezwaji wa homoni za DHT mwilini ni mkubwa kulinganisha na uwezo wa dawa za kisasa zitumiwazo kutibu tatizo za finesteride hasa unapotumiwa na mmea wa nettle root.
Lakini pia kemikali za phytosterols ndani ya saw palmetto husaidia kupunguza kiwango cha rehemu mwilini na uvimbe maeneo mbalimbali ya mwili.
Saw palmetto ni msaada mkubwa kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume hasa linalosababishwa na upungufu wa testosterone.
Ufanisi wa saw palmetto kutibu nguvu za kiume huongezeka zaidi ikiwa itatumika sambamba na mbegu za maboga.
Vilevile kemikali hizi za phytosterols huongeza uwezo wa seli za ulinzi za mwili kuangamiza na kuua seli zinazokua bila uthibiti na mpangilio.
Moja ya sababu zinazopelekea nywele kupotea kwa kasi ni uwepo wa homoni ya DHT mwilini.
Kwa hivyo udhibiti wa homoni hii ni msaada mkubwa wa kuzuia nywele kupotea hivyo kucheleweshwa kwa tatizo la upara.
Unaweza kutumia unga huu kwenye chai au kinywaji chochote kama sehemu ya chakula cha kila siku.
Pia unaweza kutumia mililita 150 ( robo tatu ya glasi) kila siku za juisi ya saw palmetto iliyotengenezwa kutokana na kulowekwa kwa mbegu halisi za palmetto kwa muda wa siku 7.
Pia unaweza kutumia 100mg za unga wa saw palmeto kwa siku walau siku 3 katika wiki.
Mtu yeyote anaweza na anashauriwa kutumia mmea huu kwa ajili ya kunufaika na faida zake.
Moja ya matatizo yanayoweza kutibiwa na mmea huu wa Saw palmetto ni maradhi uvimbe wa tezi dume.
Uwezo huu wa saw palmetto kutibu uvimbe katika tezi dume kunaufanya mmea huu kuwa ni mmea wa lazima kwa wanaume wanaojali afya zao.
Kwa wanaume wanaweza kuuita mmea huu “dhahabu ya kijani”kwa kuwa mbali na kutibu tezi dume lakini pia;
Uthibitisho wa kisayansi juu ya uwezo wa mmea huu unaufanya kuwa chaguo namba moja kwa matibabu ya tezi dume maeneo mbali ya dunia.
Italia, Ujerumani, Ufaransa na Marekani, Saw palmetto ndio chaguo namba moja kwa matibabu ya tezi dume kutokana na kuwa na faida za ziada mbali na kutibu tezi dume.
Baadhi ya kemikali muhimu ndani ya mafuta muhimu ya saw palmetto ni caprylic, capric, lauric, myristic, palmitic, stearic, oleic, linoleic na linolenic.
Na moja ya stroidi muhimu zaidi ndani ya saw palmetto ni Beta sitsterol, nyinginezo ni lupeol, stigmastrerol ba lupenone.
Mbali na viambata tiba hivi vilevile katika saw palmetto kuna flavanoidi na wanga.
Kiwango cha kemikali ndani ya saw palmeto hutofautiana kulingana na jamii ya mmea na maeneo ambao unapatikana.
Jamii za mmea wa palmetto kutoka Amerika ndio unatajwa kuwa na kiwango kikubwa cha kemikali hizi.
- Huimarisha mfumo wa uzazi wa mwanaume.
- Kupunguza kasi ya kutengenezwa kwa upara.
- Kutibu maradhi ya uvimbe katika mfumo wa uzazi.
- Kutibu maradhi mbalimbali ya mfumo wa mkojo.
Uthibitisho wa kisayansi juu ya uwezo wa mmea huu unaufanya kuwa chaguo namba moja kwa matibabu ya tezi dume maeneo mbali ya dunia.
Italia, Ujerumani, Ufaransa na Marekani, Saw palmetto ndio chaguo namba moja kwa matibabu ya tezi dume kutokana na kuwa na faida za ziada mbali na kutibu tezi dume.
Je, kuna nini ndani ya Saw pameto?
Viambata tiba vikuu ndani saw palmetto ni kundi la mafuta (fatty acids) na kundi la kemikali za steroidi (phytosterols).Baadhi ya kemikali muhimu ndani ya mafuta muhimu ya saw palmetto ni caprylic, capric, lauric, myristic, palmitic, stearic, oleic, linoleic na linolenic.
Na moja ya stroidi muhimu zaidi ndani ya saw palmetto ni Beta sitsterol, nyinginezo ni lupeol, stigmastrerol ba lupenone.
Mbali na viambata tiba hivi vilevile katika saw palmetto kuna flavanoidi na wanga.
Kiwango cha kemikali ndani ya saw palmeto hutofautiana kulingana na jamii ya mmea na maeneo ambao unapatikana.
Jamii za mmea wa palmetto kutoka Amerika ndio unatajwa kuwa na kiwango kikubwa cha kemikali hizi.
Faida za saw palmetto mwilini.
Kitaalamu mmea huu umethibitishwa kutibu magonjwa kadhaa huku ukionyesha ufanisi wa hali ya juu kwa matatizo yafuatayo.#1: Kutibu tatizo la uvimbe katika tezi dume.
Kemikali za mafuta ndani ya saw palmetto zimeonyesha uwezo mkubwa wa kuzuia na kudhibiti utengenezwaji wa testosterone kwa wingi mwilini.Vilevile kuzuia na kudhibiti utengenezwaji wa homoni ya DHT kutoka homoni ya testosterone.
Kwa kufanya hivi kemikali ya DHT katika mwili hupungua katika kiwango kinachohimilika na mwili.
Uwezo wa saw palmetto kudhibiti utengenezwaji wa homoni za DHT mwilini ni mkubwa kulinganisha na uwezo wa dawa za kisasa zitumiwazo kutibu tatizo za finesteride hasa unapotumiwa na mmea wa nettle root.
Lakini pia kemikali za phytosterols ndani ya saw palmetto husaidia kupunguza kiwango cha rehemu mwilini na uvimbe maeneo mbalimbali ya mwili.
#2: Kuimarisha mfumo wa uzazi kwa mwanaume.
Kutokana na kuzuiwa kwa testosterone kubadilishwa kuwa DHT, saw palmetto husaidia kuimarisha afya ya mfumo wa uzazi wa mwanaume.Saw palmetto ni msaada mkubwa kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume hasa linalosababishwa na upungufu wa testosterone.
Ufanisi wa saw palmetto kutibu nguvu za kiume huongezeka zaidi ikiwa itatumika sambamba na mbegu za maboga.
#3: Kuondoa sumu mwilini.
Kemikali za phytosterols ndani ya saw palmetto ni kiantioksideshaji kizuri cha mwili ambacho husaidia kupunguza sumu za mwili hasa maeneo ya mfumo wa uzazi.Vilevile kemikali hizi za phytosterols huongeza uwezo wa seli za ulinzi za mwili kuangamiza na kuua seli zinazokua bila uthibiti na mpangilio.
#4: Kupunguza kasi ya kutengenezwa kwa upara.
Kutokana na uwezo wake wa kudhibiti utengenezwaji wa homoni ya DHT, saw palmetto husaidia kupungua kwa kasi ya kupotea kwa nywele hasa za kichwani.Moja ya sababu zinazopelekea nywele kupotea kwa kasi ni uwepo wa homoni ya DHT mwilini.
Kwa hivyo udhibiti wa homoni hii ni msaada mkubwa wa kuzuia nywele kupotea hivyo kucheleweshwa kwa tatizo la upara.
Jinsi ya kutumia saw palmetto kama tiba
Mbegu za mmea wa saw pametto ndio hasa zitumiwazo kama tiba. Mbegu hizi zinaweza kupatikana katika namna tofauti ikiwemo;- Mbegu halisi iliyokaushwa.
- Unga wa mbegu iliyopondwa.
- Katika namna ya juisi ya mbegu.
- Katika namna ya vidonge.
Kwa matumizi ya tezi dume na uvimbe
Tumia kati ya 200mg hadi 400mg za unga wa saw palmetto kila siku kwa wiki 2 mfululizo kisha 100mg kwa kila siku.Unaweza kutumia unga huu kwenye chai au kinywaji chochote kama sehemu ya chakula cha kila siku.
Pia unaweza kutumia mililita 150 ( robo tatu ya glasi) kila siku za juisi ya saw palmetto iliyotengenezwa kutokana na kulowekwa kwa mbegu halisi za palmetto kwa muda wa siku 7.
Kwa matatizo ya nguvu za kiume na kuzuia upara
Tumia mililita 100 (nusu glasi) ya juisi ya saw palmetto iliyotengenezwa kwa mbegu za palmetto zilizopondwa na kulowekwa walau kwa siku 5, mara mbili kwa siku walau siku 3 za wiki.Pia unaweza kutumia 100mg za unga wa saw palmeto kwa siku walau siku 3 katika wiki.
Tahadhali ya matumizi ya saw palmetto.
Mmea huu wa saw palmetto hautpaswi kutumiwa kwa makundi yafuatayo ya watu.
- Wanawake wajawazito.
- Watoto.
- Watu wanaotumia dawa za kusaidia damu kusafiri kwa urahisi kama vile Aspirin, Clopidogrel na Warfarin.
- Watu wanaotumia dawa za uzazi wa mpango na zile zinazoathiri mfumo wa homoni.
- Vilevile watu wanaotumia finesteride kwa ajili ya tezi dume wanapaswa kuwasiliana na wataalamu wa afya kabla ya kuanza kutumia saw palmetto.
Hitimisho
Saw palmetto, ambayo kwa wanaume wanaweza kuiita dhahau ya kijani ni moja ya mimea ya lazima kwa wanaume kutokana na faida zake hasa katika kuimarisha afya ya tezi dume.
Mtu yeyote anaweza na anashauriwa kutumia mmea huu kwa ajili ya kunufaika na faida zake.
Unaweza kutumia mmea huu kama sehemu ya kinga dhidi ya matatizo yaliyotajwa ambayo mmea huu unaweza kuyatibu.
Ikiwa tayari ni muathirika wa moja ya matatizo yaliyotajwa hapo juu unashauriwa kuwasiliana na mtaalamu wa dawa (Mfamasia) au daktari ili kupata ushauri sahihi wa namna gani ya kutumia saw palmetto.
Ikiwa tayari ni muathirika wa moja ya matatizo yaliyotajwa hapo juu unashauriwa kuwasiliana na mtaalamu wa dawa (Mfamasia) au daktari ili kupata ushauri sahihi wa namna gani ya kutumia saw palmetto.