Dalili za ugonjwa wa PID, chanzo na Tiba
PID (Pelvic inflammatory Disease) ni maambukizi katika mfumo wa uzazi wa mwanamke ambayo hushambulia sehemu mbalimbali za mfumo wa uzazi ikiwemo tumbo, mirija ya uzazi na ovari.
Kwa sehemu kubwa ugonjwa huu husababishwa na bakteria wa aina kuu mbili ambao ni chlamydia na gonorrhea. Kujamiana ndio njia kuu ambayo husambaza ugonjwa huu kwa urahisi.
Mara nyingi dalili za pid hujionyesha wakati tatizo limeshakuwa kubwa kiasi ambacho mwanamke anakuwa amepoteza uwezo wa kushika mimba.
Kitendo cha mirija hii kuharibiwa ni cha muda mrefu na bahati mbaya ni kuwa wakati mirija hii inaharibiwa hakuna dalili zozote ambazo mwanamke anaweza kuziona.
Mimba inaweza kujishikiza sehemu yeyote ya mfumo wa uzazi au jirani na mfumo wa uzazi badala ya kujishikiza katika sehemu ya juu ya mfuko wa uzazi.
Mimba kutunga nje ya uzazi ni hatari kwa sababu mara nyingi husababisha kifo kwa mama na mtoto. Njia pekee ya kumsaidia mama huyu ni kuitoa mimba kupitia upasuaji.
Njia pekee ya kumsaidia mwanamke mwenye shida hii ni upasuaji na kumtolea kizazi chote.
Vilevile hakikisha unawasiliana na mtaalamu wa afya ikiwa umegundulika na ugonjwa wowote wa zinaa ili kupata matibabu sahihi wewe na mwenza wako.
Kubwa kabisa ni kuweka mazoea ya kufanya uchunguzi na vipimo vya PID mara kwa mara walau mara 2 kwa mwaka.
Kwa baadhi ya wanawake bado tatizo hili linaweza lisionyeshe dalili zozote kubwa hata kama limeshafikia hatua ya kuharibu ogani za mfumo wa uzazi.
Dalili za ugonjwa wa PID sugu kwa wanawake
Tatizo hili la PID linapaswa kutiliwa shaka muda wowote mwanamke anapolalamika na kusumbuliwa na dalili zifuatazo.- Maumivu kali chini ya kitovu.
- Maumivu ya nyonga
- Uvimbe na maumivu maeneo ya shingo ya uzazi hasa linapoguswa eneo hili.
- Homa kali.
- Maumivu wakati wa kukojoa.
- Kutokwa na ute au majimaji ukeni ulioambatana na harufu.
- Maumivu wakati wa kujamiana.
- Hedhi isiyo na mpangilio.
- Maumivu sehemu ya juu ya tumbo upande wa kulia. Maumivu haya husababishwa na uvimbe katika mfumo wa uzazi.
- Baadhi ya watu huweza kupata kichefuchefu na kutapika
Jinsi ya kupima na kutambua ugonjwa wa PID.
Hakuna kipimo cha moja kwa moja cha PID. PID inaweza ktambuliwa kwa kutumia mkusanyiko wa vipimo na uchunguzi wa macho.Baadhi ya njia zinazotumika ni;
Kutumia kifaa cha speculum.
Kifaa hiki huingizwa ukeni na kutanua uke kiasi cha kuwezesha mtaalamu wa afya kuona shingo ya uzazi.Mtaalamu wa afya atachunguza muonekano wa shingo ya uzazi kwa kutazama uwepo wa uvimbe, michubuko, vidonda na uwepo wa usaha.
Ikiwa vitu hivi vitaonekana basi ni kiashiraia mojawapo cha uwepo wa PID.
Kupima sampuli ya damu maabara.
Mtaalamu wa afya anaweza kuchukua damu kutoka katika shingo ya uzazi na kuifanyia uchunguzi maabara ili kubaini uwepo wa bakteria wa chlamydia au gonorrhea.Kutumia kipimo cha mionzi, sauti, sumaku na kipimo cha kamera.
Mtaalamu wa afya anaweza kutumia vifaa vya X-ray, CT scan, Utrasound au MRI.Vifaa hivi hutumika Kuchunguza sehemu za ndani za mfumo wa uzazi hasa ikiwa tatizo limeshapelekea kutengenezwa usaha.
Madhara ya ugonjwa wa PID kwa wanawake.
Ugonjwa wa PID unaweza kusababisha athari za muda mfupi na athari za muda mrefu.Athari hizi zinaweza kutibiwa na kupona lakini nyingine huacha kilema cha maisha.
Baadhi ya athari za PID ni kama ifuatavyo;
#1: Kutengenezwa kwa usaha sehemu za mfumo wa uzazi.
Moja ya madhara ya PID sugu ni kutengenezwa kwa usaha katika maeneo mbalimbali ya mfumo wa uzazi.Usaha unaweza kutengenezwa katika ukuta wa uzazi, mirija ya falopia au ovari (kiwanda cha mayai).
#2: Maradhi ya katika ogani za jirani na mfumo wa uzazi.
Hii hutokea ikiwa vijipu vya usaha uliotengenezwa vinapasuka na usaha unamwagikia ogani nyingine za maeneo ya karibu na mfumo wa uzazi.Ndani ya usaha kuna bakteria ambao kusambaa kwao kunaongeza tatizo.
Ikiwa maeneo yanayozunguka ini ndio yataahtiriwa basi husababisha ugonjwa ujulikanao kama Fitz-Hugh-Curtis syndrome.
#3: Maradhi katika Ini.
Usaha huu unaweza kuwa mwingi kiasi cha kufika maeneo ya ini. Ikiwa utafika maeneo haya, bakteria hawa wanaweza kuathiri maeneo yanyozunguka ini au ini lenyewe.Ikiwa maeneo yanayozunguka ini ndio yataahtiriwa basi husababisha ugonjwa ujulikanao kama Fitz-Hugh-Curtis syndrome.
#4: Mwanamke kupoteza uwezo wa kuzaa.
PID sugu huweza kusababisha mwanamke kuwa mgumba na kupoteza uwezo wa kupata mtoto.Hii inatokana na kuharibika au kuziba kwa mirija ya falopia ambayo hupitisha yai ambalo liko tayari kurutubishwa.
Kitendo cha mirija hii kuharibiwa ni cha muda mrefu na bahati mbaya ni kuwa wakati mirija hii inaharibiwa hakuna dalili zozote ambazo mwanamke anaweza kuziona.
#5: Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi.
Hii inatikana na kuziba au kuharibika kwa milija ya falopia kiasi cha kushindwa kusafirisha yai kutoka katika ovari mpakatika kifuko cha uzazi.Mimba inaweza kujishikiza sehemu yeyote ya mfumo wa uzazi au jirani na mfumo wa uzazi badala ya kujishikiza katika sehemu ya juu ya mfuko wa uzazi.
Mimba kutunga nje ya uzazi ni hatari kwa sababu mara nyingi husababisha kifo kwa mama na mtoto. Njia pekee ya kumsaidia mama huyu ni kuitoa mimba kupitia upasuaji.
#6: Maumivu makali maeneo ya mfumo wa uzazi na jirani.
Maumivu haya husababishwa na uvimbe na makovu katika mfumo wa uzazi. Maumivu haya huwa ni makali kiasi kwamba hakuna dawa ya maumivu inaweza kusaidia.Njia pekee ya kumsaidia mwanamke mwenye shida hii ni upasuaji na kumtolea kizazi chote.
#7: Madhara mengineyo ya ugonjwa wa PID
- Matatizo ya mzunguko wa hedhi
- Saratani ya shingo ya kizazi
Tiba ya Ugonjwa wa PID.
Njia pekee ya kutibu PID ni kupima uwepo wa bakteria wa gonorrhea na chlamydia.Tiba za kisasa
Ikiwa bakteria hawa wataonekana basi wanatakiwa kuwaangamiza haraka iwezekanavyo kwa kutumia dawa kutoka kundi la Antibiotiki.
Kutokana na uwezo wa bakteria hawa kutengeneza usugu wa dawa hizi, inashauriwa mgonjwa kutumia dawa mseto.
Matumizi ya antibiotiki mbili kwa wakati mmoja ni njia bora zaidi za kupambana na bakteria hawa kuliko matumizi ya dawa aina moja.
Baadhi ya dawa zinazotumika kutibu bakteria hawa ni dawa mseto za Ceftriaxone 250mg (sindano) na Azithromycin 1g (vidonge).
Kutokana na uwezo wa bakteria hawa kutengeneza usugu wa dawa hizi, inashauriwa mgonjwa kutumia dawa mseto.
Matumizi ya antibiotiki mbili kwa wakati mmoja ni njia bora zaidi za kupambana na bakteria hawa kuliko matumizi ya dawa aina moja.
Baadhi ya dawa zinazotumika kutibu bakteria hawa ni dawa mseto za Ceftriaxone 250mg (sindano) na Azithromycin 1g (vidonge).
Tiba asili ya PID
Baadhi ya mitishamba ambayo hutumiwa ni
- Mwarobaini.
Matumizi ya mwarobaini kutibu PID yanahitaji maandalizi ya kitaalamu ili kupata dozi inayostahili ya 5mg hadi 10mg kila siku kwa siku 14.
Jinsi ya kuzuia na kujikinga na ugonjwa wa PID.
Zipo njia mbalimbali ambazo unaweza kuzitumia kujikinga na maradhi ya PID lakini kubwa ni kujiepusha na magonjwa ya zinaa kwa kuachana na ngono zembe. Njia nyinginezo ni kama;- Kuwa mwaminifu kwa mpenzi wako.
- Hakikisha unatibu magonjwa yoyote ya zinaa ikiwa utayapata.
- Epukana na ngono.
- Tumia kinga wakati wa kujamiana mfano kondomu.
- Tumia vidonge vya uzazi wa mpango kadri inavyotakiwa.
- Kuwa msafi wakati wote hasa kipindi cha hedhi.
- Epuka kuosha ama kupaka manukato ukeni ikiwa huna uhakika na usalama wake.
Hitimisho
Wasiliana na mtaalamu wa afya uonapo dalili zozote zisizo za kawaida katika maeneo ya mfumo wa uzazi mfano vipele ukeni, maumivu makali ya tumbo, matatizo ya hedhi, kutokwa damu na uchafu ukeni.
Vilevile hakikisha unawasiliana na mtaalamu wa afya ikiwa umegundulika na ugonjwa wowote wa zinaa ili kupata matibabu sahihi wewe na mwenza wako.
Kubwa kabisa ni kuweka mazoea ya kufanya uchunguzi na vipimo vya PID mara kwa mara walau mara 2 kwa mwaka.