Dalili za tezi dume, jinsi ya kupima na Tiba.
Ttatizo la uvimbe wa tezi dume ni miongoni mwa matatizo ya kawaida sana kwa wanaume hasa umri unavyozidi kuwa mkubwa. Uvimbe wa tezi dume unaweza kusababisha matatizo mbalimbali mwilini ikiwemo maradhi ya figo na kushindwa kutoa mkojo.
Ili kutambua uvimbe huu unaweza kutumia njia ya kawaida ya kidole au njia za kitaalamu zaidi.
Ikiwa tatizo tayari limesha kuwa kubwa zipo dalili kadhaa ambazo zinaweza kuashiria uwepo wa tatizo hili la uvimbe katika tezi dume.
Ikiwa tatizo tayari limesha kuwa kubwa zipo dalili kadhaa ambazo zinaweza kuashiria uwepo wa tatizo hili la uvimbe katika tezi dume.
Dalili za uvimbe wa tezi dume
- Hamu ya kutaka kukojoa mara kwa mara
- Kupata shida ya kutoa mkojo.
- Hali ya Kuhisi ya kwamba mkojo bado haujaisha katika kibofu.
- Kutumia nguvu nyingi kupita kawaida wakati wa kutoa mkojo.
- Kupungua kwa kasi ya utokaji wa mkojo.
- Kupoteza hamu ya kujamiana na kupungua uwezo wa kusimamisha uume kwa muda mrefu.
- Wakati mwingine mtu anaweza kuhisi maumivu wakati wa kukojoa.
Jinsi ya kutambua tatizo la uvimbe katika tezi dume.
Katika kugundua uwepo wa uvimbe katika tezi dume kuna mambo muhimu ya kuzingatia ili kuongeza ufasaha katika uchunguzi wa tatizo.Mambo hayo ni kama ifuatavyo.
- Ni lini mgonjwa ameanza kuona dalili.
- Hali ya ujumla ya afya ya mgonjwa ikiwemo historia ya kujamiana.
- Athari za tatizo kwa mgonjwa na jinsi zinavyoathiri maisha yake ya kila siku.
- Kuna dawa zozote mgonjwa anatumia au anazotumia.
Jinsi ya kupima uvimbe katika tezi dume
1: Njia ya kawaida ya kutumia kidole.
Hii ni njia ambayo inahusisha makadilio ya ukubwa wa tezi. Njia hii ni vizuri kufanywa na mtaalamu wa masuala ya mfumo wa mkojo ili kupata majibu yenye usahihi.Kutumia njia hii mtaalamu wa afya/daktari atatumia kidole kirefu cha kati na ataingiza katika njia ya haja kubwa.
Kidole kikiwa ndani atapapasa kwa kubonyeza taratibu upande wa mbele, yaani uume uliko. Ikiwa atafanikiwa kuigusa tezi hii basi anaweza tambua ikiwa imevimba au la kwa kukadiria ukubwa wa tezi dume.
2: Njia ya kupima na kuchunguza mkojo.
Mkojo wa mgonjwa unapimwa kwa ajili ya kuchunguza vitu vifuatavyo- Uwepo wa damu, vimelea, sukari nap rotini katika mkojo. Kipimo hiki husaidia kutambua iwapo kuna tatizo lingine linalosababisha dalili anazolalamika mgonjwa.
- Uwepo wa dutu za Creatinine, nitrogen na chumvi au madini joto mengineyo katika mkojo. Hii husaidia kutambua ikiwa tatizo linasababishwana matatizo sugu ya figo.
3: Njia ya kupima kutumia kifaa mwangwi.
Kifaa cha mwangwi ambacho hujulikana kama ultrasound hutumika katika kuchunguza sehemu za ndani za tezi dume na maeneo yanayozunguka. Kipimo hiki ni bora zaidi na kina asilimia kubwa za usahihi.Jinsi ya kutibu tatizo la uvimbe katika tezi dume.
Katika kutibu tatizo la uvimbe katika tezi dume mgonjwa ana machaguo mawili ya matibabu,- moja ni kutumia dawa maisha yake yote,
- na pili ni tiba ya mara moja ambayo ni kufanyiwa upasuaji.
#1: Matibabu ya kutumia dawa.
Kutibu uvimbe wa tezi dume si rahisi hata kidogo kwa vile hakuna njia rahisi ya kugundua tatizo hilo na liko katika hatua ipi. Kigezo kikubwa cha kuanza matibabu ya uvimbe wa tezi dume ni ushirikiano wa mgonjwa kwa mtaalamu wa afya.Mgonjwa anapaswa kuwa muwazi na mwenye ushikiano ili kubaini ni kwa kiwango gani tatizo ni kubwa na ni aina gani ya matibabu mgonjwa anapaswa kupatiwa.
#2: Uangalizi na ufuatiliaji wa mgonjwa.
Ikiwa mgonjwa amebainika kuwa na uvimbe katika tezi dume bila dalili zozote ambazo zinaweza kuathiri majukumu yake ya kila siku, basi mgonjwa wa aina hii hahitaji kutumia dawa za aina yeyote.Hii ni kwa sababu dawa zinazotumiwa kutibu tatizo hili zinaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya kuliko faida ambayo mgonjwa ataipata.
Kwa wagonjwa wa aina hii muongozo wa matibabu ya uvimbe wa tezi dume unapendekeza mgonjwa kuwekwa katika uangalizi na ufuatiliwaji wa karibu.
Ungalizi huu utahusisha ufuatiliaji wa karibu wa maendeleo ya mgonjwa, mabadiliko ya kiafya na pia mapendekezo ya matibabu sahihi muda wowote ikiwa kutakuwa na ulazima wa matibabu hayo kwa mgonjwa katika kipindi husika.
Kwa wagonjwa wa aina hii muongozo wa matibabu ya uvimbe wa tezi dume unapendekeza mgonjwa kuwekwa katika uangalizi na ufuatiliwaji wa karibu.
Ungalizi huu utahusisha ufuatiliaji wa karibu wa maendeleo ya mgonjwa, mabadiliko ya kiafya na pia mapendekezo ya matibabu sahihi muda wowote ikiwa kutakuwa na ulazima wa matibabu hayo kwa mgonjwa katika kipindi husika.
#3: Dawa ya uvimbe katika tezi dume.
Mgonjwa atatakiwa kutumia dawa ikiwa tu tatizo limekuwa kubwa kiasi cha kuathiri shughuli zake za kila siku.Kuhusu aina gani ya dawa mgonjwa anapaswa kutumia inategemea pia na hatua ambayo tatizo limefikia.
Mpaka sasa kuna makundi mawili tu ya dawa ambazo zinatumiwa kuleta nafuu ya tatizo la uvimbe katika tezi dume.
Mpaka sasa kuna makundi mawili tu ya dawa ambazo zinatumiwa kuleta nafuu ya tatizo la uvimbe katika tezi dume.
- Kundi la kwanza ni dawa zinazozuia uzalishwaji wa homoni mbalimbali za mwili hasa testestorone na DHT,
- Kundi la pili ni dawa zinazosaidia kusinyaa kwa misuli iliyoko katika tezi dume, kibofu na maeneo jirani ya tezi dume.
Dutasteride na finasteride ni mfano wa dawa ambazo husaidia kupunguza kasi ya utengenezwaji wa homoni za DHT.
Moja ya athari za kutumia dawa hii ni kupungua kwa hamu ya kujamiana na kupungua kwa nguvu za kiume(uwezo wa kusimamisha uume kwa muda mrefu).
Wakati tamsulocin, doxazosin, terazosin na alfuzosin ni mfano wa dawa ambazo husaidia kusinyaa kwa misuli iliyoko katika tezi dume, kibofu na maeneo jirani ya tezi dume.
Wakati tamsulocin, doxazosin, terazosin na alfuzosin ni mfano wa dawa ambazo husaidia kusinyaa kwa misuli iliyoko katika tezi dume, kibofu na maeneo jirani ya tezi dume.
Dawa hizi hutumiwa na watu wenye tatizo la uvimbe katika tezi dume hasa tatizo likiwa kubwa na tayari limesambaa hadi kwenye mfumo wa mkojo.
Kwa wagonjwa ambao wako katika hatua mbaya za tatizo, yaani hatua ambayo uvimbe ni mkubwa zaidi na misuli ya kibofu pia imeongezeka ukubwa.
Kwa wagonjwa ambao wako katika hatua mbaya za tatizo, yaani hatua ambayo uvimbe ni mkubwa zaidi na misuli ya kibofu pia imeongezeka ukubwa.
Katika hatua hii mgonjwa hushauriwa kutumia tiba mseto, yaana kutumia mchanganyiko wa dawa mbili kwa wakati mmoja.
Baadhi ya dawa mesto ambazo hutumiwa zaidi Tanzania ni Tamsulocin na Finesteride, nyinginezo ni doxazosin na Finesteride, pamoja na terazosin na Finesteride.
Baadhi ya dawa mesto ambazo hutumiwa zaidi Tanzania ni Tamsulocin na Finesteride, nyinginezo ni doxazosin na Finesteride, pamoja na terazosin na Finesteride.
#4: Dawa asili ya uvimbe katika tezi dume
Kama yalivyo magonjwa mengine, uvimbe katika tezi dume pia inaweza kupatiwa nafuu kupitia mimea tiba mbalimbali.Mimea tiba ya
- saw palmetto(mbegu),
- mbegu za maboga,
- African plum tree(magome),
- South African star grass(mzizi),
- Pine(mzizi),
- Stinging nettle(mizizi),
- Spruce(mzizi).
Mimea hii imethibitishwa kitaalamu kuwa na uwezo mkubwa wa kuleta nafuu au kutibu tatizo hili la uvimbe katika tezi dume. Unaweza kutumia mmea mmoja au ukachanganya zaidi ya mmoja kwa matokeo mazuri zaidi.
Hitimisho
Uvimbe katika tezi dume ni tatizo la kawaida sana kwa wanaume hasa wale wenye umri mkubwa.
Mbali na wanaume wenye umri mkubwa vijana ambao wako katika balehe pia huweza kupatwa na tatizo hili.
Ni vyema kufanya uchunguzi wa mara kwa mara wa tezi dume ili kubaini ikiwa kuna tatizo lolote la uvimbe katika hatua za awali.
kuchelewa kutambua tatizo la uvimbe katika tezi dume kunaweza kusababisha madhara mengine ya kiafya kama vile kuharibika kwa figo.