Dawa za asili za kutibu fangasi za ukeni

Baada ya kutazama dawa za kisasa za kutibu fangasi za ukeni, katika makala hii tutaangazia dawa za asili/kienyeji za kutibu tatizo la fangasi za ukeni.

Kuna mitishamba, vyakula, madini joto na njia kadhaa za asili ambazo unaweza kuzitumia kutibu tatizo la fangasi sugu ukeni.

Kama ilivyo kwa njia za kisasa za kutibu fangasi, njia za asili pia zinaweza kutumika kwa namna 3, yaani kupaka, kupachika na kumeza/kunywa.

Dawa hizi za asili hufanya kazi katika misingi mikuu ifuatayo:

  • Kutibu matatizo au sababu zilizopelekea fangasi za ukeni kutokea
  • Kudhibitiukuaji wa moja kwa moja wa fangasi wa Candida albicans
  • Kusaidia kuweka hali ya uke katika msawazo wa chaji
  • Kusaidia au kupunguza miwasho, michubuko na uvimbe katika uke
  • Kuimarisha kinga ya mwili
  • Kudhibiti uzalishwaji wa ute ukeni

Dawa za asili za fangasi za ukeni

Faida kubwa ya kutumia njia za asili za kutibu fangasi ukeni ni uwezekano mdogo wa fangasi hawa kutengenezwa usugu wa dawa hizi.

Ili kuongeza ufanisi wa dawa hizi unashauriwa kutumia zaidi ya njia moja ya asili katika kupambana na tatizo la fangasi sugu.

Zifuatazo ni dawa asili za kutibu fangasi sugu za ukeni:

01: Matumizi ya Boric acid

Boric acid ni kemikali ya asili ambayo hupatikana katika mazingira yetu. Kemikali hii imeundwa na elementi za Boron, Hydrojeni na Oksijeni.

Kemikali hii ina nguvu na uwezo wa kuangamiza vimelea wa aina mbalimbali ikiwemo fangasi, bakteria na virusi.

Jinsi ya kutumia boric acid kutibu fangasi za ukeni

Kemikali huu hutumiwa kwa kupachika ukeni, inapatikana katika muundo wa vidonge na unga. 

Tumia kidonge cha boric acid kwa kupachika ukeni na kukiacha kwa muda usiopungua masaa 8 hasa nyakati za usiku.

Kemikali hii hupatikana katika maduka ya dawa ya dawa katika muundo wa vidonge au unga. 

Unaweza kununua unga na kutengenezwa kidonge, lakini hakikisha unapata maelekezo muhimu juu ya namna gani unaweza kutengenezwa kidonge kutokana na unga wa boric acid.

Boric acid inasaidia kuondoa muwasho, michubuko na kuwaka mlinganyo mzuri wa hali ya uke.

02: Kitunguu saumu

Kitunguu saumu ni miongoni mwa mimea ambayo ina uwezo wa kipekee wa kuangamiza vimelea mbalimbali wa magonjwa kwa ufanisi mkubwa.

Tafiti mbalimbali zimethibitishwa uwezo wa Kitunguu saumu katika kutibu fangasi hususa ni fangasi sugu.

Jinsi ya kutumia Kitunguu saumu kutibu fangasi sugu za ukeni

Kitunguu saumu hutumika kutibu fangasi za ukeni kwa kupachika punje zake ukeni.

Unachotakiwa kufanya ni kumenya punje ya Kitunguu kisha ipachike ukeni, hakikisha unaisukumia ndani kadri uwezavyo.

Acha kwa muda usiopungua masaa 8 kabla ya kutoa, wakati wa usiku ni bora zaidi.

Ili kurahisisha matumizi ya Kitunguu saumu unaweza kupaka mafuta ya mimea kama vile nazi au alizeti, katika punje ya Kitunguu ili kurahisisha uingiaji wake katika uke.

Kitunguu saumu ni tiba bora hasa kwa fangasi sugu za ukeni na inafanya kazi kwa kuua vimelea hawa wa fangasi.

03: Mimea ya Goldenseal, Goldthread, na Oregon Grape Root

Mimea hii yote ina kemikali za berberine na palmatine, kemikali hizi zina uwezo wa kuangamiza fangasi na vimelea mbalimbali wa magonjwa.

Goldenseal unatajwa kuwa na ufanisi zaidi na unaweza kutumiwa peke yake.

Jinsi ya kutumia Goldenseal

Unaweza kuandaa mzizi wa mmea huu na kuuloweka kwenye maji ya moto kwa muda wa dakika 10 hadi 20.

Kisha tumia maji yenye mchanganyiko huu kwa kuoshea uke mara 1 kwa siku 3 hadi 5.

Mmea huu pia unapatikana katika muundo wa vidonge au unga. Tumia kidonge kwa kupachika ukeni.

Vilevile unaweza kununua unga wa Goldenseal kisha ukatengeneza kidonge chake mwenyewe.

 Hakikisha unapata ushauri na maelekezo muhimu ya kutengenezwa kidonge hiki kutoka kwa mfamasia.

Mbali na kutumia katika muundo wa vidonge, mimea hii pia inaweza kutumiwa kwa kunywa.

Muhimu

Mimea hii haipaswi kutumiwa na wajawazito kwa sababu inaweza kusababisha mimba kuharibika.

Jambo lingine la muhimu kufahamu ni kwamba utumiapo mimea hii kwa nia ya kupachika, inasababisha uke kutoa ute wa manjano. 

Ute huu ni salama na unatokana na kemikali za berberine ndani ya mimea hii.

04: Mafuta ya mti wa chai (Tea tree)

Mafuta kutoka katika mmea huu ni moja ya dawa muhimu za kutibu fangasi ukeni.

Matumizi ya vidonge vya kupachika vinavyotengenezwa na mafuta haya kwa siku 5 yameonyesha uwezo mkubwa wa kuangamiza jamii mbalimbali ya fangasi zinazoathiri uke.

Unaweza kupata mafuta haya katika maduka mengi ya dawa za kisasa au dawa za asili.

05: Matumizi ya maziwa mgando (Yoghurt) yenye bakteria wa Lactobacillus

Bakteria wa Lactobacillus husaidia kuleta mlinganyo wa vimelea wa faida mwilini wakiwemo vimelea wa candida albicans ambao hupatikana kwa wingi katika uke.

Matumizi ya vyakula vyenye bakteria hawa husaidia kuongeza bakteria hawa mwilini na kusaidia kuleta mlinganyo wa vimelea wa fangasi katika uke.

Wanawake wenye tatizo la fangasi ukeni wanashauriwa kutumia yoghurt kwa kiasi kikubwa.

06: Matumizi ya mmea wa Orbukoi (Terminalia mollis)

Orbukoi ni jina la kimasai, mmea huu unapatikana maeneo mengi ya Tanzania na ni miongoni mwa tiba bora za fangasi aina zote.

Tumia mmea huu kwa kutengenezwa kuloweka mizizi, magome na majani laini katika maji ya moto kwa dakika zisizopungua 15.

Chuja na subiri mchanganyiko uwe wa vuguvugu kisha tumia kwa kuosha uke wako, mara moja kwa siku kwa muda siku 5 hadi 14.

Mbali na kutibu fangasi mmea huu ni miongoni mwa mimea michache yenye uwezo wa kuangamiza virusu vya UKIMWI.

07: Matumizi ya mmea wa Mkulo (Ocotea usambarensis)

Mmea huu pia hujulikana kwa jina la Mseri (kichaga) na muheti (kihehe). Mafuta ya mmea huu yanaweza kutumika kutibu fangasi za ukeni katika muundo wa vidonge vya kupachika.

Vilevile unaweza kuchanganya mafuta haya na mafuta ya alizeti, mzeituni au nazi na kutumia kwa kupaka ukeni.

Mimea mingine ya kutibu fangasi ukeni ni pamoja na:

  • Mkunazi (Bafalo thorn), hujulikana pia kama Olelailai kwa kimaasai: Juisi ya magome, mizizi na majani hutumika kuoshea uke.
  • Licorice: Vidonge vinavyotokana na unga wa mizizi ya mmea huu hupachikwa ukeni au juisi ya mizizi ya mmea huu unaweza kutumia kuoshea uke.
  • Calendula, mizizi ya mmea wa Comfrey, Lavender, mizizi ya mmea wa Marshmallow: mimea hii ndio inatajwa kuwa na Ufanisi wa hali ya juu katika kutibu magonjwa ya ngozi ikiwemo Fangasi.

Wasiliana na Mfanasia au mtaalamu wa mitishamba ili kupata ushauri sahihi wa namna na kiwango sahihi cha kutumia mimea hii.

Hitimisho

Hizi ni baadhi ya njia za asili za kutibu fangasi za ukeni, kwa sehemu kubwa njia hutumika kwa njia ya kupachika ukeni, ingawa baadhi zinaweza kutumika kwa njia ya kuoshea uke.

Hata hivyo, kutibu fangasi za ukeni kwa kutumia dawa hizi kwa njia ya kuosha uke si salama kutokana na sababu kwamba dawa hizi zinaua kiasi kikubwa cha vimelea wa faida mwilini, lakini pia maangalizi ya dawa hizi yanaweza yasiwe salama kiasi cha kupeklekea maambukizi zaidi.

Iwapo unafikiria kutumia njia hizi za asili ili kutibu fangasi za ukeni hakikisha unapata ushauri sahihi kutoka kwa mfamasia au daktari.

Next Post Previous Post
No Comment
Andika Swali au Maoni
comment url