Faida za mwarobaini katika kutibu na kupambana na magonjwa

Faida za mwarobaini katika kutibu na kupambana na magonjwa mbalimbali zinathibitishwa na tafiti mbalimbali duniani. 

Umaarufu wa mmea huu ni uwezo wake wa kutibu magonjwa ya ngozi na nywele.

Vilevile mmea tiba huu hutumika kutibu magonjwa ya pumu, vibarango, mashambulizi ya chawa kichwani ,mapunye, kisukari, dawa ya kuua wadudu na dawa ya kupanga uzazi.

Historia ya mmea wa mwarobaini.

Historia ya maandishi inaonyesha mmea huu umeanza kutumiwa kama tiba maeneo ya bara la Asia, hasa nchi za India na Iran. Baadae umaarufu wa mmea huu ulisambaa duniani kote.

Mmea huu unastawishwa kwa kupandikiza mbegu zake. Majani pamoja na magome huvunwa katika kipindi chote cha mwaka.

Sehemu zote za mmea huu hutumika kama tiba, kuanzia majani, mizizi, magome, matawi laini pamoja na mbegu zake.

Faida za mwarobaini kutibu zinatokana na nini?

Ndani ya mmea huu kuna kemikali za kipekee ambazo zinafanya mmea huu kukosa mpinzani linapokuja suala la ni mmea gani una uwezo wa kutibu magonjwa zaidi ya 10 kwa uhakika. 

Baadhi ya kemikali hizo ni kama zifuatazo;

  • Kemikali za Liminoids: Kama ni siraha basi hili ni bomu la nyuklia ndani ya mwarobaini. Tafiti mbalimbali zimethibitisha uwezo wa kemikali hizi za Liminoids katika kupambana na magonjwa. Kemikali hii ina uwezo wa kuua na kuangamiza bakteria, fangasi, plasmodiamu (vimelea vya malaria), virusi na kuangamiza seli za saratani.
  • Kemikali ya Meliacins: Utafiti wa kisayansi umeonyesha kemikali hii kuwa na uwezo mkubwa wa kupambana na seli za saratani kwa kuzuia ukuaji wa seli usio na udhibiti.
  • Kemikali za Triterpenoid bitters: Kundi hili la kemikali linajumuisha maelfu ya kemikali ambayo kwa umoja wao au muunganiko wao umeonyesha mafanikioa makubwa ya kupambana na vimelea. Baadhi ya magonjwa yanayotibiwa na kemikali hizi ni pamoja na uvimbe, magonjwa ya bakteria, magonjwa ya fangasi na vilevile kuimalisha kinga ya mwili.
  • Kemikali nyinginezo: Kemikali nyinginezo ambazo hupatikana ndani ya mmea wa mwarobaini ni pamoja na Tannis ambazo husaidia kupunguzwa kwa kemikali na chaji sumu mwilini.

Pia kuna kemikali za sterols ambazo husaidia kupunguza kiwango cha rehemu hatari mwilini na kutibu maradhi ya saratani ya mfumo wa chakula. 

Vilevile kemikali za sterols husaidia kupunguza matatizo ya mfumo wa mzunguko wa damu.

Flavanoids pia hupatikana kwa wingi katika mwarobaini. Kemikali hizi zimeonyesha uwezo mkubwa wa kutoa kinga dhidi ya magonjwa ya mzunguko wa damu na mfumo wa fahamu kama vile kusahau.

Faida za mwarobaini katika mwili mwili.

Mwarobaini ni moja kati ya mimea adimu ambayo huweza kutibu maradhi zaidi ya 10 kwa ufanisi wa hali ya juu. 

Yapo magonjwa mengi ambayo huweza kutibiwa kwa kutumia mwarobaini, yafuatayo ni baadhi ya mgonjwa hayo;

01: Husaidia kutibu magonjwa ya ngozi.

Uwepo wa kemikali kadhaa ndani ya mwarobaini hasa Liminoids kunaupa mmea huu uwezo wa kipekee wa kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi.

Magonjwa kama mba za kichwani, mapunye, vibarango, fangasi, chawa kichwani na malengelenge. Magonjwa yote haya yanaweza kutibiwa na kuisha kabisa kwa kutumia mwarobaini.

02: Husaidia kutibu magonjwa ya vidonda vya tumbo.

Ikiwa tatizo la vidonda vya tumbo limesababishwa na bakteria, matumizi ya mwarobaini kwa kunywa ni moja ya tiba bora zaidi na za uhakika. Hii ni kwa sababu ya uwepo wa Liminoids.

03: Husaidia kutibu maradhi ya minyoo.

Uwezo wa Liminoids kuangamiza wadudu kunafanya mwarobaini kuwa chaguo namba moja la tiba ya minyoo mwilini. Mwarobaini ni bora zaidi hasa kwa minyoo ya tumbo.

04: Hutumika kutibu malaria.

Ukiwa ni ugonjwa unaongoza kwa vifo Afrika kwa Watoto chini ya umri wa miaka 5. Ni neema iliyoje kutambua kuwa mwarobaini pekee unaweza kuwa msaada mkubwa kwako na kwa mwanao.

Tumia kwa kunywa juisi ya mwarobaini na hautatumia tena dawa za kisasa za malaria.

05: Husaidia kutibu magonjwa mbalimbali ya bakteria na fangasi.

Kwa kutumia mwarobaini unaweza kutibu magonjwa kama UTI, PID, typhoid, majipu, maradhi ya koo, chunusi, gono na mengine mengi.

06: Husaidia kutibu tatizo la kisukali aina ya pili.

Kemikali ndani ya mwarobaini hasa katika mafuta ya mwarobaini husaidia kupunguza kiwango cha sukari mwilini. 

Kwa kufanya hivi mwarobaini hupunguza mzigo kwa seli ambazo haziitikii vyema homoni ya insulin.

07: Hutumika kama kinga ya wadudu mbalimbali.

Liminoids ndani ya mwarobaini husaidia kuwafukuza wadudu mbalimbali akiwemo mbu. Kwa kupaka, mwarobaini hutoa kinga bora dhidi ya wadudu wengi hasa mbu.

08: Husaidia kutibu maradhi ya meno na kinywa.

Matawi laini ya mwarobaini hutumiwa kama tiba ya magonjwa ya kinywa kama vile harufu mbaya mdomoni. Vilevile unaweza kutumia mwarobaini kungarisha meno.

09: Hutumiwa kama tiba ya macho.

Juisi ya majani ya mwarobaini hutumiwa kutibu magonjwa ya macho kamavile majeraha ya macho, macho kutoa machozi, maradhi ya bakteria machoni na macho yenye uono hafifu.

 Ni sehemu ipi ya mmea wa mwarobaini hutumika kama tiba?

Unaweza kunufaika na sehemu zote za mmea wa mwarobaini kama tiba. Maua, matunda, mbegu, majani, magome na matawi laini vyote vina faida za kitabibu mwilini.

Sehemu hizi za mwarobaini huweza kuandaliwa katika namna mbalimbali kama vile;

  • Juisi
  • Unga
  • Mafuta kutoka katika mbegu.
  • Losheni.

Jinsi ya kuandaa mwarobaini kama tiba.

Matumizi kwa ajili ya vidonda ya tumbo, minyoo na malaria.

Maandalizi: Tumia majani kuandaa juisi. Loweka majani katika maji au pombe kali mfano gongo kwa muda wa siku 2 hadi 3. Ili kuruhusu kiwango cha kutosha cha kemikali kuvunwa katika majani.

Tumia kwa kunywa kwa ajili ya malaria, vidonda vya tumbo, minyoo na kisukari. 

Vilevile juisi hii unaweza kupaka kwa magonjwa ya ngozi. Pia juisi hii unaweza kuitumia kwa matatizo ya macho kwa kuweka tone 1 au mawili kila siku.

Matumizi kwa ajili ya magonjwa ya ngozi.

Mbali na juisi ya majani ya mwarobaini, mafuta ya mwarobaini hutumika zaidi katika kutibu magonjwa ya Ngozi. Tumia kwa kupaka eneo la ngozi lililoathirika.

Mafuta haya pia husaidia kutibu maradhi ya nywele, paka nywele zako Pamoja na shina la nywele kadri inavyohitajika.

Namna za kutengeneza jusi za mwarobaini.

Tengeneza juisi ya majani ya mwarobaini kwa kuyaloweka katika maji au pombe kwa muda wa siku 2 hadi 3 kabla ya kutumia.

Pia unaweza kutengeneza juisi ya mwarobaini kwa kuchemsha magome ya mwarobaini na maji kwa takribani dakika 10. 

Juisi ya magome ina faida kama ilivyo ya majani lakini juisi ya magome imeonyesha ziada ya kutibu bawasili.

Tahadhari

Matumizi ya mafuta ni hatari kwa vile yana uwezo mkubwa kuunguza na kuharibu mwili. Tumia kwa wastani na maelekezo maalumu kwa ajili ya usalama wako.

Vilevile mwarobaini hautakiwi kutumiwa kwa mama mjamzito. Tafiti zinzonyesha kwa mama mjamzito mwarobaini unaweza kuharibu ukuaji wa mtoto.

Hitimisho

Haya ni baadhi ya magonjwa yanayoweza kutibiwa na mmea wa mwarobaini kwa ufanisi wa hali ya juu.

Yapo magonjwa mengi ambayo yanaweza kutibiwa na mmea huu wa kipekee. Jambo muhimu la kuzingatia ni namna bora ya kuuandaa mmea huu ili kunufaika na faida zake.

Ikiwa unatamani kutumia mmea huu tafadhari wasiliana na mtaalamu wa dawa na tiba (mfamasia) kwa ajili ya ushauri sahihi namna bora ya kutumia mmea huu.

Next Post Previous Post
No Comment
Andika Swali au Maoni
comment url