Kipanda uso husababishwa na nini? aina zake, madhara na tiba
Kipanda usoni aina ya maumivu ya kichwa ambayo hutokea upande mmoja wa kichwa. Maumivu haya ni makali na huwa ni ya kujirudia.
Kipanda usoni hutokea katika nyakati na kwa namna tofauti, na huweza kudumu kwa kati ya dakika 20 hadi lisaa 1.
Tatizo hili linaweza kumpata mtu wa rika yeyote, mtoto au mkubwa. Tafiti zinaonyesha 60% mpaka 70% ya waathiriwa wa tatizo hili ni wanawake.
Kwa watu wengi tatizo la kipanda usoni linaweza kupelekea mtu kushindwa kufanya shughuli zake za kila siku.
Kipanda uso uso husababishwa na nini?
Zipo sababu kadhaa zinazoweza kusababisha tatizo la kipandauso, baadhi ya sababu ambazo zinaweza kupelekea aina hii ya maumivu ya kichwa ni pamoja na
- Mabadiliko ya ratiba na namna ya ulalaji.
- Matumizi ya vyakula vilivyo na kemikali za tyramine, monosodium glutamate, nitrates, chocolate na matunda jamii ya machungwa na limao.
- Mabadiliko ya homoni na vichocheo vya mwili ambavyo husababishwa na matumizi ya dawa zinazoathiri mfumo wa homoni kama vile zile za uzazi wa mpango.
- Kutokuwapo kwa ulinganifu wa vichocheo vya mwili, mfano kupungua kwa vichocheo vya serotonin katika ubongo.
- Kukaribia au kuwa katika kipindi cha hedhi kwa wanawake, hii ni moja ya sababu kubwa ya kipanda uso kwa wanawake wengi.
- Mabadiliko ya kiutendaji ya mfumo wa fahamu.
- Shinikizo la damu.
Aina za kipandauso.
Shambulizi la kipanda uso linaweza kuja katika namna kuu mbili,- Kipandauso kilichoandamana na mauzauza na
- Kipanda uso kisichoambatana na mauzauza
Kwa kipanda uso kinachoambatana na mauzauza mgonjwa hupata maono yasiyo ya kweli, kushindwa kuongea, lakini pia uwezo wa kuchanganua harufu na na kusikia hubadilika.
Dalili za kipanda uso
- Kupata haja kubwa ngumu.
- Shingo na mgongo kukaza mara kwa mara bila sababu ya msingi.
- Kiu na haja ndogo huongezeka kuliko kawaida.
- Kupata miayo mfululizo.
- Maumivu makali ya upande mmoja wa kichwa, mara nyingi sehemu ya mbele ya kichwa.
- Kichefuchefu na kutapika
- Kupoteza hamu ya chakula
- Kupoteza hamu ya kujamiana
- Kutokwa na jasho na kutetemeka mwili
- Kupauka kwa ngozi ya mwili
- Kuwa na uwezo mkubwa wa kuhisi mwanga
Vihatarishi vya kipanda uso
Mambo hatarishi yanayoweza kukuweka katika mazingira ya kupata shambulizi la kipanda uso kwa urahisi zaidi.
- Shinikizo kubwa la damu.
- Uvutaji wa sigara.
- Matumizi ya dawa za kupanga uzazi.
- Namna kinatokea
- Nyakati
- Nistoria katika familia
- Ukubwa wa maumivu kutoka kwa mgonjwa
Taarifa hizi muhimu hutumika kusaidia kubaini uwepo wa tatizo kwa mgonjwa.
Ikiwa mgonjwa anapata maumivu makali yanayoambatana na mauzauza kupita kawaida kipimo cha MRI kinaweza kutumika ili kubaini ikiwa kuna tatizo jingine ambalo huchagiza maumivu ya kipanda uso isivyo kawaida.
Dawa ya Kipanda uso
Ili kutibu kipanda uso taarifa muhimu kama vile eneo la kichwa ambalo hupata maumivu, aina ya maumivu, ni mara ngapi maumivu hutokea, matokeo ya tiba iliyopita ikiwa mgonjwa alipata dawa, uwepo wa maradhi mengineyo na uwepo wa mauzauza.Dawa ya kipanda uso cha kawaida
Ikiwa kipandauso hutokea mara chache mfano mara 1 hadi 2 katika mwezi basi mgonjwa anashauriwa kutumia dawa pale tu tatizo linapotokea.
Mfano wa dawa ambazo hutumika ni pamoja;
- Dawa za kutuliza maumivu(ibuprofen, naproxen),
- Dawa maalumu za kutuliza maumivu(sumatriptan),
- Kundi la dawa zijulikanazo kama alkaloids(ergotamine).
Na vilevile mgonjwa anaweza pewa dawa za kuzuia kutapika na kichefuchefu ikiwa kuna ulazima.
Matumizi ya hewa ya oksijeni ni moja ya tiba bora zaidi ya kipandauso.
Matumizi ya hewa ya oksijeni ni moja ya tiba bora zaidi ya kipandauso.
Mgonjwa anapaswa kutulia sehemu yenye hewa safi na isiyo na mwanga mkali huku akiwa amefunga macho, pia tumia kitambaa chenye ubaridi kupitisha eneo lote la kichwa linalouma.
Dawa ya kipanda uso sugu
Kwa mgonjwa ambaye kipanda uso hutokea kati ya mara 2 hadi 3 kwa wiki, hii hutafsiriwa kama ni tatizo sugu na mgonjwa anashauriwa kutumia dawa muda wote kama sehemu ya kinga kuzuia mashambulizi ya kipanda uso.Dawa ambazo hutumika zaidi ni ;
- B-blockers(dawa za kupunguza shinikizo la damu mfano propranolol)
- Calcium channel blockers (dawa za kupunguza shinikizo la damu mfano verapamil)
Makundi haya ya dawa hutumika zaidi kama kinga ya kipanda uso, ambapo utashauriwa kutumia kadri mtaalamu wa dawa atakavyoona inafaa.
Moja ya changamoto za kutibu kipandauso ni mgonjwa kutopata nafuu hata kama ametumia dawa.
Moja ya changamoto za kutibu kipandauso ni mgonjwa kutopata nafuu hata kama ametumia dawa.
Hii inatokana na sababu kwamba watu wengi walio na tatizo la kipanda uso hushambuliwa na aina zaidi ya moja ya maumivu ya kichwa.
Jambo hili linafanya matumizi pekee ya dawa za kutibu kipandauso yasilete matokeo chanya kwa vile kila aina ya maumivu ya kichwa hutibiwa tofauti.
Hitimisho
Kwa wagonjwa wengi maumivu ya kichwa ya kipanda uso ni ya kawaida na yanaisha pale mgonjwa anapotumia dawa za maumivu.Kwa watu ambao husumbuliwa na tatizo sugu la kipanda uso ambalo huambatana na mauzauza, matatizo ya kusikia na kunusa, tatizo hili linaweza kusababisha madhara ya moja kwa moja katika mfumo wa fahamu na neva kwa ujumla.
Ikiwa upo kwenye kundi la watu wanaosumbuliwa na tatizo sugu la kipanda uso, hakikisha unaonana na wataamu wa maumivu ya kichwa.