Matatizo 6 ya kaida ya mzunguko wa hedhi na sababu zake
Mzunguko wa hedhi ni tukio la kibaolojia ambalo hutokea kwa mwanamke yeyeto aliyekamili kiafya.
Kwa wastani mwanamke huanza kupata hedhi akiwa na kati ya umri wa miaka 12 hadi 15, lakini pia hedhi huweza kujitokeza mapema zaidi ya miaka 8 au ikachelewa zaidi hadi miaka 16.
Kuwahi au kuchelewa kwa hedhi haina maana kuwa mwanamke ana tatizo.
Kundi kubwa la wanawake hupata hedhi kila baada ya siku 28 au 32, mzunguko wa hedhi ulio katika wastani wa siku hizi hutajwa kama ni mzunguko salama na wa kawaida.
Kundi kubwa la wanawake hupata hedhi kila baada ya siku 28 au 32, mzunguko wa hedhi ulio katika wastani wa siku hizi hutajwa kama ni mzunguko salama na wa kawaida.
Mzunguko wa hedhi unaweza kuwa mfupi hadi kufikia siku 21 au kuwa mrefu hadi siku 35.
Kupata mzunguko wa hedhi mfupi chini ya siku 28 au mrefu zaidi ya siku 32, kwa baadhi ya wanawake yaweza kuwa ni jambo la kawaida na salama lakini kwa wengine huweza kuwa ni ishara kwamba kuna jambo haliko sawa kuhusu mfumo wake wa uzazi.
Je, mzunguko wako ni wa siku 28 na haujawahi ona tofauti yoyote ya kuchelewa au kuwahi?
Je, mzunguko wako ni wa siku 28 na haujawahi ona tofauti yoyote ya kuchelewa au kuwahi?
Basi ni moja ya wanawake wachache kwa kuwa mamilioni ya wanawake katika nyakati tofauti wamewahi kuona tofauti ya mzunguko wao kwa maana ya kwamba mzunguko wao wa hedhi hubadilika bila mpangilio maalumu.
Mzunguko wa hedhi usio na mpangilio si tu unakupa shida ya kutambua kwa ufasaha ni wakati gani sahihi wa kupata ujauzito lakini pia ni ishara kuwa mfumo wako wa uzazi unahitaji marekebisho.
Mzunguko wa hedhi usio na mpangilio si tu unakupa shida ya kutambua kwa ufasaha ni wakati gani sahihi wa kupata ujauzito lakini pia ni ishara kuwa mfumo wako wa uzazi unahitaji marekebisho.
Sababu za matatizo ya mzunguko wa hedhi
Mzunguko wa hedhi ambao hauko katika mpangilio maalumu yaweza sababishwa na mambo mbalimbali kama vile- Kutokuwa na uwezo wa kupevusha yai,
- Uwezo wa mwanamke kupevusha yai ni mdogo na hutokea mara chache,
- Msongo wa mawazo,
- Sonona,
- Kubadili namna ya kuishi ikiwamo mazingira,
- Kujihusisha na mazoezi,
- Lishe
- Magonjwa
Matatizo mbalimbali ya mzunguko wa hedhi
Vifuatavyo ni viashiria kwamba mzunguko wako wa hedhi hauko sawa na sababu zake za kwanini tatizo hilo linatokea.
Hii ni kwa wanawake ambao hawatumii njia yoyote ya uzazi wa mpango ambao unahusisha matumizi ya dawa za homoni.
01: Kuwa na mzunguko mfupi wa chini ya siku 25
Ikiwa mzunguko wako ni chini ya siku 21, inamaanisha yai lako hupevuka haraka zaidi.Hali hii inaweza kusababishwa na mambo yafuatayo;
- kuanza kupungua kwa hifadhi ya mayai katika ovari,
- ongezeko la kupita kawaida la homoni ya follicle stimulating homoni ambayo huusika na kupevusha yai
- matatizo katika tezi ya pituitary ambayo husaidia kuzalisha homoni ya progesterone homoni, homoni hii huchelewesha upevushwaji wa yai.
Kwa mwanamke ambaye mzunguko wake ulikuwa katika mpangilio maalumu yaani siku 28 au 32 na baadae ukabadilika na kuanza kutokea katika muda wa chini ya siku 21 ni moja ya ishara kubwa kuwa kiwango cha mayai kiweshuka na kuelekea mwisho.
Hali hii hutokea zaidi kwa wanawake ambao wana umri wa zaidi ya miaka 35.
Kwa wanawake ambao wako chini ya umri wa miaka 30 na hupata shida hii ya mzunguko mfupi yawezekana kiwango cha Progesterone na Luteinizing Hormone kiko chini.
Kwa wanawake ambao wako chini ya umri wa miaka 30 na hupata shida hii ya mzunguko mfupi yawezekana kiwango cha Progesterone na Luteinizing Hormone kiko chini.
Hivyo matumizi ya dawa au vyakula vyenye uwezo wa kuongeza homoni ya progesterone inaweza saidia kumaliza tatizo.
02: Kupata hedhi mara chache au kukosa hedhi kwa muda mrefu
Mzunguko wa hedhi ulio zaidi ya siku 32 yaani 35 na zaidi ni ishara kwamba uwezo wa mayai ya mwanamke kupevuka ni mdogo.Hali hii inaweza kusababishwa na mambo yafuatayo;
- kufanya mazoezi mazito kupita kawaida
- kufanya kazi ngumu zaidi
- mabadiliko ya uzito wa mwili
- magonjwa katika mifuko ya ovari, magonjwa haya husababisha mabadiliko ya uwiano wa homoni za uzazi
Kwa mwanamke mwenye maradhi katika ovari huambatana na viashiria vingine kama vile;
- kuota nywele kupita kawaida
- kuongezeka uzito
- chunusi
- maradhi katika mfuko wa uzazi
- kushindwa kwa ovari kusaidia upevushwaji wa mayai
- matatizo katika tezi ya thyroid
- kiwango kikubwa cha homoni ya prolactin.
03: Kutokwa damu siku za katikati za mzunguko wako wa hedhi
Kutoka damu katikati ya siku za kawaida za mzunguko wako wa hedhi ni ishara kwamba mfuko wa uzazi una matatizo au kutokuwapo kwa uwiano wa homoni za mfumo wa uzazi.Yapo mambo mengi ambayo huweza sababisha matatizo katika mfuko wa uzazi, baadhi ya mambo hayo ni pamoja na;
- Michubuko au vidonda katika mlango wa uzazi ambayo mara nyingi husababishwa na maambukizi ya magonjwa kama fangasi au kufanya ngono na mwanaume au midoli yenye uume mrefu kupita kawaida.
- Uvimbe katika mlango wa uzazi au katika mfuko wa uzazi ambao husababishwa na magonjwa ya zinaa, au mradhi mengine.
04: Kutokwa na damu nyingi ya hedhi kupita kawaida
Hedhi inayoambatana na damu nyingi kupita kawaida husababishwa na maradhi kama vile;- uvimbe katika mfuko wa uzazi
- kutokuwa na mpangilio maalumu wa hedhi
- maradhi katika ovari
- kuwa na uzito mkubwa kupita kawaida
- kuharibika kwa mimba
Damu nyingi kupita kawaida ni hatari kwa vile inaweza pelekea tatizo la upungufu wa damu(seli nyekundu za damu).
Mara nyingi kutokana na kupoteza sehemu muhimu ya damu(seli nyekundu) wanawake wanaopata hedhi yenye damu nyingi hupatwana kizunguzungu na uchovu wa mara kwa mara.
Fika kituo cha afya kwa ajili ya vipimo na uchunguzi zaidi.
05: Kupata damu nyepesi wakati wa hedhi
Ikiwa damu yako ni vyepesi sana, yawezekana isiwe tatizo, kama ni mwenye bahati!, lakini inaweza kuwa ni ishara ya kwamba mfuko wako wa uzazi hauandaliwi vyema kuweza kumudu ukuaji wa mtoto pindi yai limefanikiwa kurutubishwa.Kwa sehemu kubwa hali hii husababishwa na kuacha matumizi ya dawa za uzazi wa mpango, lakini pia hutokea ikiwa ndio mwanamke anaanza kupata hedhi(balehe).
06: Maumivu makali kipindi cha hedhi
Zaidi ya asilimia 50 ya wanawake hupata maumivu wakati wa hedhi, maumivu hayo yametafsiriwa katika namna kuu mbili;Maumivu ya awali au ya msingi ya hedhi
Maumivu haya hutokea kwa kila mwanamke ambayo sababu yake kubwa ni kutengenezwa kwa kemikali zijulikanazo kama prostaglandims.
Kemikali hizi husaidia kurekebisha joto la mwili hasa wakati wa hedhi, lakini kubwa ni kusaidia kutanuka na kusinyaa kwa ukuta wa uzazi. Kutanuka na kusinyaa ndio kunasaidia ukuta kuharibiwa na kutolewa nje kama damu.
Maumivu haya huwa ni makali zaidi kwa mwanamke ambaye anaanza kupata hedhi na ambaye bado hajazaa, kuzaa kunaweza saidia kupunguza ukali wa maumivu haya.
Maumivu ya upili au yasiyoya msingi
Aina hii ya maumivu ya hedhi husababishwa na magonjwa ama uzalishwaji wa prostaglandins.
Maumivu haya huwa ni makali kupita kawaida ambapo mwanmke huweza hata kuzimia. Maradhi ambayo hupelekea tatizo hili ni pamoja na Uvimbe, saratani, PID au maradhi katika mlango au mfuko wa uzazi.
Kutengenezwa kwa prostaglandins husababisha maumivu, kichefuchefu, kutapika na homa kali, kwa hivyo matumizi ya dawa za kutuliza maumivu kama ibuprofen zinaweza kukusaidia kupunguza maumivu.
Kutengenezwa kwa prostaglandins husababisha maumivu, kichefuchefu, kutapika na homa kali, kwa hivyo matumizi ya dawa za kutuliza maumivu kama ibuprofen zinaweza kukusaidia kupunguza maumivu.
Hitimisho
Mzunguko wa hedhi ni tukio muhimu la kibaolojia kwa wanawake, kwa sababu ndio tukio ambalo husaidia kutengenezwa kwa yai.
Uwezo wa kupata mimba kwa mwanamke unategemea na ufanisi wa tukio hili. Hitilafu yeyote katika tukio hili la mzunguko wa hedhi inaweza kupelekea moja au zaidi ya matatizo yaliyoainishwa katika makala hii.
Ni vizuri kwa mwanamke kufika kituo cha afya ikiwa anapata tatizo lolote katika mzunguko wake wa hedhi ili kuweza kubaini ikiwa kuna hitilafu yeyote.
Hakik