Sababu za matatizo ya mzunguko wa hedhi.
Matatizo ya mzunguko wa hedhi ni ya kawaida kwa wanawake na husababishwa na mambo mbalimbali ambayo ni ya kawaida kabisa katika jamii. Sababu hizi zinaweza kuwa za muda mfupi au za muda mrefu.
Wakati mwingine baadhi ya sababu hizi huweza kuleta madhara au mabadiliko ya muda mrefu au ya moja kwa moja ikiwa zitatokea mfululizo na kwa muda mrefu bila kuthibitiwa.
Baadhi ya sababu zinazopelekea matatizo ya mzunguko wa hedhi huweza kuthibitiwa kiurahisi, huku nyingine zikihitaji dharula ya kitabibu.
Kulingana na utofauti wa sababu hizi, vilevile wanawake hupata matatizo ya hedhi kwa namna tofauti.
Pombe huhuongeza uzalishwaji wa homoni ya prolactin ambayo inazuia upevushwaji wa yai hivyo husababisha mwanamke kukosa hedhi.
Sigara hupunguza kiwango cha homoni ya oestrogen hivyo kuchelewesha upevushwaji wa yai.

Baadhi ya matatizo hayo ni kutokwa damu nyingi kupita kiasi, kutokwa damu katikati ya mwezi, kukosa hedhi na maumivu makali wakati wa hedhi.
Matukio haya yanaweza kuwa ni ya furaha au huzuni. Mfano;
Kushindwa kuzalishwa kwa GnRH pia kunasimamisha utengenezwaji wa homoni za LH na FSH. Homoni za LH na FSH ndio husaidia kupevuka kwa yai la mwanamke.
Kwa hivyo kuzuiwa kwa homoni hizi maana yake yai halipevuki au linapevuka isivyokawaida.
Sababu za matatizo ya mzunguko wa hedhi kwa wanawake.
Zifuatazo ni sababu kuu ambazo husababisha matatizo ya mzunguko wa hedhi kwa wanawake na ni kwa namna gani;01: Msongo wa mawazo
Msongo wa mawzo hutafsiriwa kama tukio au mlolongo wa matukio katika mwili au fikra ambayo hubadili utendaji kazi wa mwili kifiziolojia na kikemikali.Matukio haya yanaweza kuwa ni ya furaha au huzuni. Mfano;
- Matukio yanayohusu kufanya mitihani au kupokea matokeo ya mitihani.
- Kuwa safarini au mbali na nyumbani.
- Kuvunjika kwa mahusiano muhimu.
- Ajali mbaya au matukio ya ukatili.
- Kupata aina Fulani ya maradhi au kuugua kwa muda mrefu.
Jinsi Msongo wa mawazo unasababisha matatizo ya hedhi.
Msongo wa mawazo husababisha sehemu katika ubongo iitwayo hypothalamus kuacha kuzalisha kemikali ya GnRH. Kemikali hii ya GnRH ndio ambayo hupelekea kuzalishwa kwa homoni mbili ambazo ni LH na FSH.Kushindwa kuzalishwa kwa GnRH pia kunasimamisha utengenezwaji wa homoni za LH na FSH. Homoni za LH na FSH ndio husaidia kupevuka kwa yai la mwanamke.
Kwa hivyo kuzuiwa kwa homoni hizi maana yake yai halipevuki au linapevuka isivyokawaida.
Mara nyingi stress husababisha hedhi isiyo na mpangilio, kukosa hedhi kwa muda mrefu hadi miezi 6 na kutokwa damu nyingi hata katikati ya mwezi.
Vilevile msongo wa mawazo husababisha kuzalishwa kwa homoni za adrenalini ambazo hupelekea mabadiliko mbalimbali ya mwili kama vile;
Kuongezeka uhitaji chakula mwili wakati huohuo hamu ya chakula hupungua. Jambo hili husababisha mwili kutumia hifadhi ya chakula cha mafuta na protini.
Kutumika kwa hifadhi hii ya chakula ndio hupelekea mwili kukonda, kupungua uzito ambayo ni sababu mojawapo ya matatizo ya hedhi na kuvuruga mlinganyo wa homoni mwilini.

02: Uzito mdogo wa mwili.
Mtu hutajwa kuwa na uzito mdogo ikiwa kiwango cha mafuta mwilini ni chini ya asilimia 22 ya jumla ya uzito wake wa mwili.Wanawake huhitaji walau asilimia 17 ya uzito wa mwili wao uwe umeundwa na mafuta ili apate hedhi.
Kwa wastani mwanamke anahitaji asilimia 22 ya mwili wake uwe umeundwa na mafuta ili apate hedhi salama inayoeleweka na yenye mpangilio maalumu.
Ikitokea kiwango cha mafuta kwa mwanamke ni chini ya asilimia 20 ya uzito wa mwili wake basi moja ya matatizo atakayopata ni kukosa kabisa hedhi kwa muda fulani.
Moja ya kundi linaloathiriwa na tatizo hili ni wanamichezo wa kike, wanamitindo, wanawake wenye uzito mdogo na wanawake wanofanya mazoezi kupunguza uzito na unene.
Vilevile baadhi ya magonjwa yanweza kusababisha kupungua uzito kwa kiwango kikubwa ni saratani, kuharisha na tatizo la kutokula (anorexia nervosa na bulimia nervosa).
Nifanyeje kujua kiwango cha mafuta mwilini mwangu?
Kiwango cha mafuta hupatikana kutumia kikokotoo cha body mass index (BMI).

Kwa kutumia kikokotoo hiki unaweza kujua kiwango cha mafuta mwilini ikiwa unafahamu uzito wako na urefu wako.
Jinsi ya kukokotoa BMI, unachukua uzito wako katika kizio cha kilogramu unagawanya na kepeo cha pili cha urefu wako katika kizio cha mita. Yaani;
Majibu ya BMI na ufafabuzi wake:
Utendaji hafifu wa hypothalamus unaathiri utengenezwaji wa homoni ya Oesrogen. Kutokuzalishwa kwa homoni hii kunazuia upevushwaji wa yai na kupelekea mwanamke kukosa hedhi.
Vilevile wanawake wenye uzito mdogo hukabiliwa na tatizo la ujazo duni wa mifupa kwa sababu ni homoni hii ya Oesrogen ndio ambayo husaidia kuimarisha ujazo wa mifupa.
Jambo la msingi ni kuhakikisha hauzidishi kiwango hiki cha mafuta mwilini lakini si kuacha kula kabisa. Kwani kufanya hivyo kunapelekea upungufu wa mafuta mwilini.
Vilevile kuna kundi la wanawake ambalo huangaika kupanga lishe ikiwa ni sehemu ya matibabu ya aina fulani ya maradhi kama kisukari na maradhi ya moyo.
Wengine ni wanawake ambao hushindwa kutumia aina Fulani ya vyakula kwa sababu ya mzio au aleji. Wanawake hawa wanashauriwa kutafuta vyakula mbadala ili kuepukana na tatizo la kukosa baadhi ya virutubisho muhimu.
Kupungua kwa mafuta mwilini husababisha matatizo yafuatayo, Kupungua uzito, Kupungua kwa homoni ya leptin inayozalishwa na tishu za mafuta. Homoni hii ya leptini husaidia utendaji kazi wa hypothalamus.
Kwa wanawake ambao wana upungufu wa virutubisho vya Calcium husumbuliwa na tatizo la ujazo duni wa mifupa na uzito mdogo.
Kitambi hupunguza kemikali ya SHBG mwilini. Kupungua kwa kemikali hii kunaongeza kiwango cha homoni ya oestrogens kwenye damu.
Kuwepo kwa oestrogens kwa wingi kwenye damu kunasababisha mwanamke kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi.
Pia Kuwepo kwa oestrogens kwa wingi kunasababisha ukuaji usio wa kawaida wa ukuta wa uzazi, chunusi, uvimbe na uwezekano wa kupata saratani ya matiti.
Jinsi ya kukokotoa BMI, unachukua uzito wako katika kizio cha kilogramu unagawanya na kepeo cha pili cha urefu wako katika kizio cha mita. Yaani;
BMI = UZITO KATIKA KILOGRAMU / (UREFU KATIKA MITA)2
Majibu ya BMI na ufafabuzi wake:
- Chini ya 20 hutafsiriwa kama una uzito mdogo.
- 20–25 hutafsiriwa kama uzito wako uko sawa.
- 26–30 hutafsiriwa kama una uzito mkubwa kuliko kawaida.
- Zaidi ya 30 hutafsiriwa kama una fetma (kitambi)
Jinsi uzito mdogo unasababisha matatizo ya hedhi
Uzito mdogo unasababisha utendaji hafifu wa hypothalamus, sehemu katika ubongo inayoamuru kuzalishwa kwa homoni mbalimbali za mwili.Utendaji hafifu wa hypothalamus unaathiri utengenezwaji wa homoni ya Oesrogen. Kutokuzalishwa kwa homoni hii kunazuia upevushwaji wa yai na kupelekea mwanamke kukosa hedhi.
Vilevile wanawake wenye uzito mdogo hukabiliwa na tatizo la ujazo duni wa mifupa kwa sababu ni homoni hii ya Oesrogen ndio ambayo husaidia kuimarisha ujazo wa mifupa.
03: Ukosefu/upungufu wa aina fulani ya lishe kwa muda mrefu.
Baadhi ya wanawake huamini kuwa ili kulinda umbo la mwili na kuzuia uzito ni vyema kuepuka vyakula vya mafuta kiasi cha kuacha kabisa kutumia vyakula hivi. Si sahihi na ni makosa makubwa.Jambo la msingi ni kuhakikisha hauzidishi kiwango hiki cha mafuta mwilini lakini si kuacha kula kabisa. Kwani kufanya hivyo kunapelekea upungufu wa mafuta mwilini.
Vilevile kuna kundi la wanawake ambalo huangaika kupanga lishe ikiwa ni sehemu ya matibabu ya aina fulani ya maradhi kama kisukari na maradhi ya moyo.
Wengine ni wanawake ambao hushindwa kutumia aina Fulani ya vyakula kwa sababu ya mzio au aleji. Wanawake hawa wanashauriwa kutafuta vyakula mbadala ili kuepukana na tatizo la kukosa baadhi ya virutubisho muhimu.
Kupungua kwa mafuta mwilini husababisha matatizo yafuatayo, Kupungua uzito, Kupungua kwa homoni ya leptin inayozalishwa na tishu za mafuta. Homoni hii ya leptini husaidia utendaji kazi wa hypothalamus.
Kwa wanawake ambao wana upungufu wa virutubisho vya Calcium husumbuliwa na tatizo la ujazo duni wa mifupa na uzito mdogo.
04: Tatizo la kitambi
Kitambi hutafsiriwa kama hali ya kuwa na kiwango cha mafuta mwilini kinachozidi asilimia 30 ya jumla ya uzito wako. Kiwango hiki hutafutwa kutumia kikokotoo cha BMI.Kitambi hupunguza kemikali ya SHBG mwilini. Kupungua kwa kemikali hii kunaongeza kiwango cha homoni ya oestrogens kwenye damu.
Kuwepo kwa oestrogens kwa wingi kwenye damu kunasababisha mwanamke kutokwa damu nyingi wakati wa hedhi.
Pia Kuwepo kwa oestrogens kwa wingi kunasababisha ukuaji usio wa kawaida wa ukuta wa uzazi, chunusi, uvimbe na uwezekano wa kupata saratani ya matiti.
05: Mazoezi makali ya mwili
Mazoezi ya kawaida na wastani ni muhimu kwa afya ya mwili kwa vile yana faida nyingi kiafya.Mazoezi yana msaada mkubwa katika kupambana na maradhi yakiwemo matatizo ya kukosa hedhi, hedhi isiyo na mpangilio na maumivu ya hedhi.
Kutembea, kuogelea, kuendesha baiskeli, kukimbia na yoga ni mazoezi yenye msaada mkubwa kwa afya.
Lakini mazoezi kupita kawaida ni hatari kwa afya ya uzazi kwa vile mitikisiko ya mwili kupita kawaida inaweza kusababisha kuhama kwa milija ya falopia.
Lakini kubwa ni kupungua kwa kiwango kikubwa utengenezwaji wa GnRH kutoka katika hypothalamus.

Kupungua kwa kemikali hii kunapelekea kuzuiwa kwa uzalishwaji wa homoni za LH na FSH. Jambo linalopelekea mwanamke kukosa hedhi au kupoteza uwezo wa kuzaa kabisa.
Baadhi ya dawa hizo ni kama ifuatavyo;
Dawa hizi huweza kukusababishia matatizo kama kutokwa damu katikati ya mwezi au kukosa hedhi kwa muda kadhaa.
06: Matumizi ya dawa
Kuna dawa za aina nyingi ambazo huathiri mzunguko wa hedhi. Kuna ambazo hupunguza kiwango cha damu, ambazo huongeza na ambazo huzuia hedi isitokee.Baadhi ya dawa hizo ni kama ifuatavyo;
Vidonge vya uzazi wa mpango.
Kuna dawa za aina nyingi katika kundi hili, baadhi ya dawa hizo ni levonogestrel maarufu kama P2 ambazo hutumika kuzuia urutubishwaji wa yai.Dawa hizi huweza kukusababishia matatizo kama kutokwa damu katikati ya mwezi au kukosa hedhi kwa muda kadhaa.
Dawa za kutibu uvimbe katika kuta za uzazi.
Mfano wa dawa hizo ni kundi la GnRH agonists. Dawa hizi huzuia upevushwaji wa yai hivyo hakuna hedhi vilevile hupunguza ujazo wa mifupa ya mwanamke.Dawa za mzio/aleji na uvimbe.
Mfano wa dawa hizo ni prednisolone, hydrocortisone, betamethasone and dexamethasone (Decadron). Dawa hizi hupunguza ujazo wa mifupa kwa kiwango kikubwa hasa zikitumika mfululizo kwa muda wa miezi 2.07: Matumizi ya pombe, sigara, madawa ya kulevya na kahawa
Vyote hivi vinasababisha matatizo katika mzunguko wa hedhi.
Pombe huhuongeza uzalishwaji wa homoni ya prolactin ambayo inazuia upevushwaji wa yai hivyo husababisha mwanamke kukosa hedhi.
Sigara hupunguza kiwango cha homoni ya oestrogen hivyo kuchelewesha upevushwaji wa yai.
Sigara husababisha hedhi isiyo na mpangilio na wakati mwingine mwanamke kupoteza uwezo wa kuzaa.
Hitimisho
Hizi ni baadhi ya sababu kuu zinazosababisha matatizo mbalimbali yanayohusu mzunguko wa hedhi.Baadhi ya wanawake huweza kuwa na zaidi ya sababu moja, jambo linaloongeza uwezekano wa kupata matatizo mbalimbali ya hedhi.
Sababu hizi si tu zinasababisha matatizo katika mzunguko wa hedhi bali husababisha matatizo mengineyo katika mfumo wa uzazi. Mfano saratani, uvimbe, maambukizi katika mfumo wa uzazi na ugumba.
Sababu hizi si tu zinasababisha matatizo katika mzunguko wa hedhi bali husababisha matatizo mengineyo katika mfumo wa uzazi. Mfano saratani, uvimbe, maambukizi katika mfumo wa uzazi na ugumba.
Ikiwa una matatizo yoyote ya mzunguko wa hedhi, jaribu kujitafakari kwa kulinganisha sababu zilizotajwa katika makala hii na ni kwa namna gani zinakuathiri.