UKIMWI ni nini? ifahamu historia ya UKIMWI Tanzania?
UKIMWI ni kifupi cha neno Upungufu wa Kinga MWIlini. Ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na virusi aina ya HIV.
Ni miongoni mwa majanga ya ulimwengu ambayo yamesababisha vifo vingi zaidi vya watu huku Afrika ikiwa ndio eneo lililoathiwa zaidi na janga hili.
Kwa mujibu wa takwimu za umoja wa mataifa, mpaka sasa, UKIMWI umeshasababisha zaidi ya vifo milioni 40 duniani kote, huku vifo zaidi ya million 27 ni kutoka Afrika pekee.

Aina za virusi vya UKIMWI (HIV)
Kwa kuzingatia tabia za kijenetiki na uwezo wa kusababisha ugonjwa wa UKIMWI, virusi hivi vya ukimwi (HIV) vimegawanywa katika aina kuu mbili;- Virusi vya UKIMWI aina ya kwanza (HIV-1), virusi hivi ndio hutajwa kama virusi hatari zaidi kwa sababu vina kasi kubwa ya maambukizi na hushambulia CD4 kwa kasi kubwa. HIV-1 huathiri zaidi watu wa maeneo ya kusini mwa afrika (Jangwa la Sahara).
- Virusi vya UKIMWI aina ya pili (HIV-2), aina hii ya virusi hutajwa kuwa na uwezo mdogo wa kuathiri CD4, vilevile vina kasi ndogo ya maambukizi ukilinganisha na HIV-1. HIV-2 huathiri zaidi watu wa maeneo ya magharibu mwa afrika.
HIV-1 na HIV-2 pia zimegawanyika katika makundi mengine madogo, lakini katika makala hii hatutajadili mgawanyiko huu.
Asili na chanzo cha virusi hivi vya UKIMWI (HIV) inadhaniwa kwamba vilitoka katika wanyama aina ya Sokwe.
Nadharia hii inatokana na sababu kwamba sokwe na jamii nyingine ya nyani ni wanyama ambao hushambuliwa zaidi na virusi wajulikanao kama Simian Immunodeficiency virus (Siv).
Virusi hawa hufanana kwa kiasi kikubwa na virusi wa Human Immunodeficiency virus (HIV), kuanzia tabia na jinsi wanavyosambaa.
Inasemekana virusi hawa wa Simian Immunodeficiency virus (Siv) waliingia ndani ya mwili wa binadamu na kupitia mabadiliko kadhaa.
Kuna aina kuu mbili za virusi wa Simian Immunodeficiency virus (Siv), SIVcpz na SIVsm.
Virusi wa SIVcpz hushambulia zaidi jamii ya sokwe kutoka maeneo ya Afrika ya kati.
Wakati SIVsm hushambulia zaidi jamii ya sokwe kutoka Afrika ya magharibi.
Athari na mabadiliko ya virusi wa Simian Immunodeficiency virus (Siv) wanapoingia katika mwili wa binadamu yanategemea na aina yake.
Ambapo, virusi vya UKIMWI aina ya kwanza (HIV-1) vinadhaniwa kuwa asili yake ni mabadiliko ya Simian Immunodeficiency virus (SIVcpz) kutoka jamii ya sokwe wanaopatikana maeneo ya Afrika ya kati.
Wakati, virusi vya UKIMWI aina ya pili (HIV-2) vinadhaniwa kuwa asili yake ni mabadiliko ya Simian Immunodeficiency virus (SIVsm) kutoka jamii ya sokwe wanaopatikana maeneo ya Afrika ya magharibi, hasa maeneo ya nchi ya Cameroon.
Inadhaniwa kwamba kati ya mwaka 1920 hadi 1940, ndio kipindi ambacho virusi hawa walianza kusambaa miongoni mwa binadamu.
Mwaka 1981, wagonjwa wa kwanza waliripotiwa kuwa na ugonjwa wa ajabu nchini marekani, miaka 2 baadae, UKIMWI uliweza kutambulika kama Ugonjwa unaosababishwa na HIV.
Nchini Tanzania mgonjwa wa kwanza wa UKIMWI aliripotiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1984 katika mkoa wa Kagera.
Sababu kubwa ni kwamba katika ukanda huu ndipo kunapatikana virusi aina ya upili (HIV-1) ambavyo ndio vinatajwa kuwa hatari na uwezo mkubwa wa kusababisha UKIMWI.
Hata hivyo sababu hii haihalalishi ugonjwa huu katika maeneo haya, Una nafasi ya pekee katika kukomesha tatizo hili.
Zingatia kanuni bora za kujikinga na virusi vya UKIMWI, kama vile kutumia kondomu, kujiepusha na shughuli hatarishi kama vile michoro ya mwilini (tatoo), kuwa mwaminifu na kuendelea kukumbushana juu ya hatari za ugonjwa huu dhidi ya ndugu na jamaa.
Asili ya UKIMWI na virusi vya UKIMWI (HIV)
HIV ni aina ya virusi kutoka jamii ya virusi ijulikanayo kama Retroviridae.Asili na chanzo cha virusi hivi vya UKIMWI (HIV) inadhaniwa kwamba vilitoka katika wanyama aina ya Sokwe.
Nadharia hii inatokana na sababu kwamba sokwe na jamii nyingine ya nyani ni wanyama ambao hushambuliwa zaidi na virusi wajulikanao kama Simian Immunodeficiency virus (Siv).
Virusi hawa hufanana kwa kiasi kikubwa na virusi wa Human Immunodeficiency virus (HIV), kuanzia tabia na jinsi wanavyosambaa.
Inasemekana virusi hawa wa Simian Immunodeficiency virus (Siv) waliingia ndani ya mwili wa binadamu na kupitia mabadiliko kadhaa.
Kuna aina kuu mbili za virusi wa Simian Immunodeficiency virus (Siv), SIVcpz na SIVsm.
Virusi wa SIVcpz hushambulia zaidi jamii ya sokwe kutoka maeneo ya Afrika ya kati.
Wakati SIVsm hushambulia zaidi jamii ya sokwe kutoka Afrika ya magharibi.
Athari na mabadiliko ya virusi wa Simian Immunodeficiency virus (Siv) wanapoingia katika mwili wa binadamu yanategemea na aina yake.
Ambapo, virusi vya UKIMWI aina ya kwanza (HIV-1) vinadhaniwa kuwa asili yake ni mabadiliko ya Simian Immunodeficiency virus (SIVcpz) kutoka jamii ya sokwe wanaopatikana maeneo ya Afrika ya kati.
Wakati, virusi vya UKIMWI aina ya pili (HIV-2) vinadhaniwa kuwa asili yake ni mabadiliko ya Simian Immunodeficiency virus (SIVsm) kutoka jamii ya sokwe wanaopatikana maeneo ya Afrika ya magharibi, hasa maeneo ya nchi ya Cameroon.
Inadhaniwa kwamba kati ya mwaka 1920 hadi 1940, ndio kipindi ambacho virusi hawa walianza kusambaa miongoni mwa binadamu.
Mwaka 1981, wagonjwa wa kwanza waliripotiwa kuwa na ugonjwa wa ajabu nchini marekani, miaka 2 baadae, UKIMWI uliweza kutambulika kama Ugonjwa unaosababishwa na HIV.
Nchini Tanzania mgonjwa wa kwanza wa UKIMWI aliripotiwa kwa mara ya kwanza mwaka 1984 katika mkoa wa Kagera.
Hitimisho
Nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara ndio ambazo zimeathiriwa zaidi na janga hili la UKIMWI.Sababu kubwa ni kwamba katika ukanda huu ndipo kunapatikana virusi aina ya upili (HIV-1) ambavyo ndio vinatajwa kuwa hatari na uwezo mkubwa wa kusababisha UKIMWI.