Dawa za asili za kutibu chunusi sugu
Kudhibiti kiwango cha mafuta kinachozalishwa katika ngozi, kuua bakteria wa P.acne na kudhibiti uondolewaji wa seli za ngozi zilizokufa ndio shabaha kuu za kupambana na chunusi.
Ili kufanikisha hili unaweza kutumia njia za kisasa za kutibu chunusi au njia za asili za kutibu chunusi.
Katika makala hii tutaangazia njia za asili za kutibu chunusi na jinsi ya kutumia njia hizi.
Njia za asili za kupambana na chunusi ni mjumuisho unaozingatia mambo kadhaa kama vile;
Zifuatazo ni njia mbalimbali za asili unaweza kuzitumia kutibu chunusi.
Ni miongoni mwa mitishamba muhimu zaidi katika kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi ikiwemo michubuko, vidonda, mapunye na mba.
Mafuta haya huchanganywa katika bidhaa mbalimbali za kutibu magonjwa ya ngozi, lakini pia unaweza kuipata katika uasili wake.
Tafiti mbalimbali zinaonyesha mafuta ya mti wa chai yana uwezo sawa na dawa ya kisasa ya kutibu chunusi ya Benzoyl peroxide.
Mafuta ya mti wa chai yanayotumika kutibu chunusi ni yenye nguvu ya 5%, ambayo hutumika kwa kupaka.
Vilevile mmea huu una uwezo wa kuangamiza bakteria wanaosababisha chunusi na majipu.
Mmea huu unaweza kutumika kwa kupaka au kunywa.
Kwa matumizi ya kupaka
Kwa matumizi ya kupaka tengeneza losheni, ambapo unatakiwa kuchukua unga wa maua ya mmea huu kisha chemsha unga wa maua ya mmea huu, nta (wax) na maji kidogo, halafu koroga taratibu mpaka maji yatakapokauka.
Vilevile unaweza kutengenezwa ointment kwa kuchukua majani makavu ya mmea huu kisha chemsha katika mafuta (petroleum jelly) kwa dakika 15, toa mchanganyiko wako jikoni kisha chuja ili kupata ointment.
Tumia ointment au losheni kwa kupaka maeneo yaliyoathirika mara 2 hadi 3 kwa siku.
Kwa matumizi ya kunywa
Chukua maua ya mmea huu, kisha weka katika maji ya moto na uache kwa dakika 15 huku ukikoroga.
Ili kufanikisha hili unaweza kutumia njia za kisasa za kutibu chunusi au njia za asili za kutibu chunusi.
Katika makala hii tutaangazia njia za asili za kutibu chunusi na jinsi ya kutumia njia hizi.
Dawa za asili za kutibu chunusi sugu
Unapochagua njia za asili kupambana na chunusi, tambua ya kwamba hakuna dawa ya aina moja ya asili ya kutibu chunusi.Njia za asili za kupambana na chunusi ni mjumuisho unaozingatia mambo kadhaa kama vile;
- Lishe bora
- Ufuatiliaji wa mwenendo wa mifumo inayoathiriwa na vichocheo vya homoni za uzazi, mfano mzunguko wa hedhi
- Mitindo ya maisha
- Mitishamba na
- Msongo wa mawazo
Zifuatazo ni njia mbalimbali za asili unaweza kuzitumia kutibu chunusi.
01: Mafuta ya mti wa chai (Tea tree oil)
Mafuta haya huvunwa kutoka katika mmea wa melaleuca wenye asili yake nchini Australia. Viambata ndani ya mafuta haya vina uwezo wa kuangamiza bakteria, fangasi na virusi.Ni miongoni mwa mitishamba muhimu zaidi katika kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi ikiwemo michubuko, vidonda, mapunye na mba.
Mafuta haya huchanganywa katika bidhaa mbalimbali za kutibu magonjwa ya ngozi, lakini pia unaweza kuipata katika uasili wake.
Tafiti mbalimbali zinaonyesha mafuta ya mti wa chai yana uwezo sawa na dawa ya kisasa ya kutibu chunusi ya Benzoyl peroxide.
Mafuta ya mti wa chai yanayotumika kutibu chunusi ni yenye nguvu ya 5%, ambayo hutumika kwa kupaka.
02: Mmea tiba wa Calendula
Ni moja ya mimea iliyofanyiwa utafiti wa kina. Uwezo wake wa kipekee wa kuzuia na kupunguza uvimbe kunaufanya mmea huu kuwa moja ya mimea muhimu katika kutibu magonjwa ya ngozi ikiwemo chunusi.Vilevile mmea huu una uwezo wa kuangamiza bakteria wanaosababisha chunusi na majipu.
Mmea huu unaweza kutumika kwa kupaka au kunywa.
Kwa matumizi ya kupaka
Kwa matumizi ya kupaka tengeneza losheni, ambapo unatakiwa kuchukua unga wa maua ya mmea huu kisha chemsha unga wa maua ya mmea huu, nta (wax) na maji kidogo, halafu koroga taratibu mpaka maji yatakapokauka.
Vilevile unaweza kutengenezwa ointment kwa kuchukua majani makavu ya mmea huu kisha chemsha katika mafuta (petroleum jelly) kwa dakika 15, toa mchanganyiko wako jikoni kisha chuja ili kupata ointment.
Tumia ointment au losheni kwa kupaka maeneo yaliyoathirika mara 2 hadi 3 kwa siku.
Kwa matumizi ya kunywa
Chukua maua ya mmea huu, kisha weka katika maji ya moto na uache kwa dakika 15 huku ukikoroga.
Chuja mchanganyiko wako tayari kwa matumizi ya kunywa, vilevile unaweza kuchanganya na asali au sukari ili kupata radha nzuri.
Kwa matumizi ya kunywa tumia mililita 150 mara 2 hadi 3 kwa siku.
Unaweza kutumia kwa kupaka au kunywa.
Kwa kupaka, changanya unga wa karafuu na Kitunguu saumu kilichopondwa kisha paka maeneo yaliyoathirika.
Kwa matumizi ya kunywa, changanya karafuu na Kitunguu saumu katika maji ya vuguvugu kisha chuja ili kupata juisi safi. Tumia mililita 100 ya mchanganyiko huu mara 3 kwa siku.
Vilevile unaweza kutumia mafuta ya mimea hii kwa kupaka, changanya tone 1 la mafuta ya karafuu na Kitunguu saumu kisha paka sehemu iliyoathiriwa na chunusi.
Kama hutaki kutumia dawa hizo basi limao ni mbadala dhabiti wa dawa hizo.
Tumia juisi ya tunda hili kupaka eneo lililoathirka mara 2 hadi 3 kwa siku.
Udongo laini ni moja ya vitu vinavyoweza kukusaidia kufyonza mafuta ya ziada katika ngozi yako. Tengeneza mask kavu ya udongo kisha paka maeneo yaliyoathiriwa na chunusi.
Ili kuongeza ufanisi unaweza kuchanganya mask ya udongo na unga wa mmea tiba wowote kati ya hizi zilizotajwa katika makala hii.
Matumizi ya mafuta ya mmea huu kwa kupaka ni msaada mkubwa kwa magonjwa mbalimbali ya ngozi ikiwemo chunusi.
Mbali na mafuta yake kutumika kwa kupaka, majani ya mmea huu pia yanaweza kutumika kwa ajili ya kuoga au kujifukiza.
Mbali na kusaidia kutibu chunusi, Chaste Berry ni mmea muhimu kwa wanawake hasa wanaosumbuliwa na matatizo ya hedhi kwa sababu za homoni.
Mmea huu una uwezo wa kupunguza uvimbe vilevile kuangamiza bakteria wa chunusi.
Mizizi ya mmea huu ina kemikali ya Glycyrrhizin ambayo hufanya kazi sawa na dawa za kisasa za kuondoa uvimbe za kundi la corticosteroids.
Mizizi ndio sehemu ambyo hutumika zaidi, unaweza kutengenezwa losheni, cream au ointment kutokana na unga wa mizizi ya mmea huu.
Mmea huu hutumiwa zaidi kwa kunywa ambapo mizizi ya mmea huu huchemshwa katika maji kwa muda usiopungua dakika 20.
Vilevile unaweza kutumia mmea huu kwa kuoga au kupaka katika ngozi.
Mimea tiba mengineyo ya kutibu chunusi ni pamoja na;
Mimea tiba katika makala hii inaweza kuandaliwa kwa namna tofauti. Ikiwa unatamani kuanza kutumia mimea tiba hii hakikisha unapata maelezo sahihi ya namna gani ya kuandaa mimea tiba hii.
Bila kujali aina ya njia unayotumia, mimea tiba yote hii inaweza kuchanganywa na asali kwa sababu kuu 2,
Kwa matumizi ya kunywa tumia mililita 150 mara 2 hadi 3 kwa siku.
03: Mimea tiba ya Kitunguu saumu na karafuu
Unaweza kutumia mmojawapo kati ya mimea hii ingawa mchanganyiko wa mimea hii unashauriwa zaidi. Mimea yote hii ina uwezo wa kuangamiza bakteria wanaosababisha chubusi.Unaweza kutumia kwa kupaka au kunywa.
Kwa kupaka, changanya unga wa karafuu na Kitunguu saumu kilichopondwa kisha paka maeneo yaliyoathirika.
Kwa matumizi ya kunywa, changanya karafuu na Kitunguu saumu katika maji ya vuguvugu kisha chuja ili kupata juisi safi. Tumia mililita 100 ya mchanganyiko huu mara 3 kwa siku.
Vilevile unaweza kutumia mafuta ya mimea hii kwa kupaka, changanya tone 1 la mafuta ya karafuu na Kitunguu saumu kisha paka sehemu iliyoathiriwa na chunusi.
04: Matumizi ya limao
Limao ni tunda lenye vitamini nyingi mojawapo ni vitamini A. Dawa zote kubwa za kisasa za kutibu chunusi zimeundwa na vitamini A.Kama hutaki kutumia dawa hizo basi limao ni mbadala dhabiti wa dawa hizo.
Tumia juisi ya tunda hili kupaka eneo lililoathirka mara 2 hadi 3 kwa siku.
05: Matumizi ya udongo laini (clay)
Mafuta ni moja ya sababu kubwa za chunusi, kudhibiti kiwango cha mafuta katika ngozi ndio shabaha kuu ya kutibu chunusi.Udongo laini ni moja ya vitu vinavyoweza kukusaidia kufyonza mafuta ya ziada katika ngozi yako. Tengeneza mask kavu ya udongo kisha paka maeneo yaliyoathiriwa na chunusi.
Ili kuongeza ufanisi unaweza kuchanganya mask ya udongo na unga wa mmea tiba wowote kati ya hizi zilizotajwa katika makala hii.
06: Mmea tiba wa Chamomile
Mmea huu una kemikali za Apigenin ambazo hudhaniwa kuwa na uwezo mkubwa wa kupunguza uvimbe.Matumizi ya mafuta ya mmea huu kwa kupaka ni msaada mkubwa kwa magonjwa mbalimbali ya ngozi ikiwemo chunusi.
Mbali na mafuta yake kutumika kwa kupaka, majani ya mmea huu pia yanaweza kutumika kwa ajili ya kuoga au kujifukiza.
07: Mmea tiba wa Chaste Berry
Ni miongoni mwa mimea michache ambayo hudhibiti utengenezwaji wa homoni za uzazi.Mbali na kusaidia kutibu chunusi, Chaste Berry ni mmea muhimu kwa wanawake hasa wanaosumbuliwa na matatizo ya hedhi kwa sababu za homoni.
08: Mmea tiba wa Chinese Skullcap
Huu ni miongoni mwa mmea ambao hutumiwa zaidi kwenye bidhaa za vipodozi vya kutibu magonjwa mbalimbali ya ngozi.Mmea huu una uwezo wa kupunguza uvimbe vilevile kuangamiza bakteria wa chunusi.
09: Mmea tiba wa Licorice
Mmea mwingine ambao hudhibiti kutengenezwa kwa homoni za uzazi ni Licorice.Mizizi ya mmea huu ina kemikali ya Glycyrrhizin ambayo hufanya kazi sawa na dawa za kisasa za kuondoa uvimbe za kundi la corticosteroids.
Mizizi ndio sehemu ambyo hutumika zaidi, unaweza kutengenezwa losheni, cream au ointment kutokana na unga wa mizizi ya mmea huu.
10: Mmea tiba wa Echinacea
Moja ya tiba zenye ufanisi wa hali ya juu ya kutibu magonjwa ya ngozi ni mmea huu wa Echinacea.Mmea huu hutumiwa zaidi kwa kunywa ambapo mizizi ya mmea huu huchemshwa katika maji kwa muda usiopungua dakika 20.
Vilevile unaweza kutumia mmea huu kwa kuoga au kupaka katika ngozi.
Mimea tiba mengineyo ya kutibu chunusi ni pamoja na;
- Slippery elm (Ulmus rubra)
- Asali
- Myrrh (Commiphora molmol)
- Dandelion (Taraxacum officinale)
- Comfrey (Symphytum officinale)
- Oregon Grape Root
- Witch Hazel
- Lavender (Lavandula officinalis)
- Ashwagandha (Withania somnifera)
Muhimu!
Mimea tiba katika makala hii inaweza kuandaliwa kwa namna tofauti. Ikiwa unatamani kuanza kutumia mimea tiba hii hakikisha unapata maelezo sahihi ya namna gani ya kuandaa mimea tiba hii.
Bila kujali aina ya njia unayotumia, mimea tiba yote hii inaweza kuchanganywa na asali kwa sababu kuu 2,
- kwanza ni kuimarisha utendaji kazi tiba husika,
- lakini pia asali husaidia kuhifadhi dawa zako ulizotengeneza zisiharibiwe na wadudu hasa zile ambazo umetumia maji kuziandaa.
Lishe muhimu kwa watu wenye chunusi
Kuzingatia lishe sahihi ni moja ya njia bora za kupambana na chunusi. Baadhi ya vyakula muhimu na vya lazima kwa wagonjwa wa chunusi ni pamoja na;
Kuna mitishamba na vyakula vya aina nyingi tofauti ambavyo havijaorodheshwa katika makala hii lakini vina msaada mkubwa katika kutibu chunusi.
Kutibu chunusi kuna changamoto nyingi, hasa unapotumia dawa za asili. Njia asili za kutibu chunusi mara nyingi huanza kuonyesha matokeo chanya kati ya wiki 3 hadi 5 baada ya kuanza kuzitumia.
Hakuna matokeo ya siku moja, weka nia na kuwa na muendelezo mzuri wa matumizi ya njia hizi zitakusaidia.
- Tumia vyakula vyenye au virutubisho vya Vitamini A
- Vyakula au virutubisho vya Vitamini C kwa wingi
- Vyakula vyenye madini joto ya Zinc
- Tumia vyakula vyenye vitamini B6 kwa wingi hasa wanawake
Hitimisho
Hizi ni baadhi ya dawa asili za kutibu chunusi. Orodha hii imezingatia utafiti wa kina wa hivi karibuni, hata hivyo orodha hii si chaguo la mwisho.Kuna mitishamba na vyakula vya aina nyingi tofauti ambavyo havijaorodheshwa katika makala hii lakini vina msaada mkubwa katika kutibu chunusi.