Dawa za kisasa za kutibu chunusi sugu
Ili kuleta ufanisi katika kutibu na kupambana na tatizo la chunusi, matibabu ya tatizo hili yanapaswa kulenga shabaha kuu 4 ambazo ni;
Ufanisi wa kutibu chunusi unaongezeka zaidi ikiwa utatumia njia mseto, yaana utachagua zaidi ya njia moja ya matibabu.
Katika makala hii tutakuelezea njia za kisasa za kutumia ili kutibu na kupambana na tatizo hili la chunusi.
Unashauriwa kutumia dawa za kisasa za kupaka ikiwa chunusi zako ni za kawaida. Dawa za kumeza zinapaswa kutolewa kwa kibali maalumu cha daktari.
Usitumie dawa za kumeza na baadhi ya dawa za kupaka za kutibu chunusi bila kibali cha daktari au mfamasia kwa sababu iwapo dawa hizi zitatumika kinyume na taratibu zinaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya.
Baadhi ya dawa kutoka katika kundi hili ni Tetracycline, Clindamycin, Erythromycin na Triclosan.
Dawa hizi hutibu chunusi kwa kuangamiza bakteria wa P.acne, bakteria huyu ndio husababisha tatizo la chunusi.
Madhara ya dawa hizi za kupaka za kuua bakteria
Benzoyl Peroxide hutibu chunusi kwa kuzuia bakteria wa P.acne kuzaliana kwa wingi. Msombo huu unafanya kazi ya kusaidia kutengenezwa kwa hewa ya oksijeni katika ngozi.
Bakteria wa P.acne hawezi kuishi katika sehemu yenye kiasi kikubwa cha hewa ya Oksijeni.
Madhara ya kutumia Benzoyl Peroxide
Dawa hii inafanya kazi kwa kusaidia kuyeyusha mchanganyiko wa jasho, mafuta na seli zilizokufa katika ngozi.
Kwa kufanya hivi kemikali hii inazuia mchanganyiko huu kuziba matunda ya vinyweleo vilevile inazuia kugandamana kwa mchanganyiko huu katika ngozi.
Madhara ya dawa hii ni pamoja na;
Kemikali hii hufanya kazi ya kudhibiti na kuondoa seli zilizokufa katika ngozi.
Udhibiti wa seli zilizokufa katika ngozi ni muhimu kwa sababu seli hizi zinapochanganyikana na mafuta katika ngozi husababisha ngozi kutawaliwa na bakteria wa P.acne.
Dawa hizi hufanya kazi kwa kusaidia mchakato mzima wa kutengenezwa kwa seli za ngozi.
Zinathibiti kiwango cha seli zinazokufa na kuratibu mchakato wa kawaida wa mwili wa kuziondoa seli hizi zilizokufa katika ngozi.
Madhara ya dawa hizi za Retinoids
Kemikali hii inafanya kazi kwa kuangamiza bakteria katika ngozi. Ni dawa pekee ambayo inaweza kutumika mseto na dawa nyingine yeyote ya kupaka bila matatizo.
Madhara ya dawa hii
Kuna madhara kadhaa ya kutumia dawa hizi hasa ikiwa utatumia bila kufuata ushauri wa kitaalamu, baadhi ya madhara ya kutumia dawa hizi ni;
Kuna madhara mbalimbali ya kutumia dawa hizi za uzazi wa mpango, kubwa ni kuongezeka kwa uwezekano wa kupata saratani katika mfumo wa uzazi, hasa wananwake.
Dawa hii inafanya kazi kwa Kudhibiti mlinganyo wa homoni za uzazi, Kudhibiti kutengenezwa kwa mafuta mengi katika ngozi na kuangamiza bakteria.
Pamoja na ufanisi mkubwa wa dawa hii katika kutibu chunusi, Isotretinoin si dawa salama kwa kila mtu hasa wajawazito.
Ina madhara kadhaa katika mwili wako ikiwemo
Usishike ujauzito ikiwa bado unatumia dawa hii.
Hakuna dawa yoyote kati ya dawa hizi ambayo inaweza kutibu na kuondoa chunusi milele.
Tiba zote hizi ni za muda tu, tatizo linaisha unapozitumia ukiacha kutumia baada ya muda linarudi.
Njia pekee za kutibu chunusi ni kujitathmini mitindo yako ya maisha na kuifanyia kazi ile ambayo inaweza kukababisha wewe kupata chunusi.
- Kudhibiti mlinganyo wa homoni za uzazi
- Kudhibiti kutengenezwa kwa mafuta mengi katika ngozi
- Kuchagua vipodozi sahihi kulingana na aina ya ngozi yako
- Kuimarisha usafi binafsi wa ngozi
Ufanisi wa kutibu chunusi unaongezeka zaidi ikiwa utatumia njia mseto, yaana utachagua zaidi ya njia moja ya matibabu.
Katika makala hii tutakuelezea njia za kisasa za kutumia ili kutibu na kupambana na tatizo hili la chunusi.
Dawa za kisasa za kutibu chunusi
Dawa hizi zinaweza kutumika kwa kupaka au kwa kunywa, inategemea na aina ya chunusi na kiwango ambacho ngozi imeathiriwa.Unashauriwa kutumia dawa za kisasa za kupaka ikiwa chunusi zako ni za kawaida. Dawa za kumeza zinapaswa kutolewa kwa kibali maalumu cha daktari.
Usitumie dawa za kumeza na baadhi ya dawa za kupaka za kutibu chunusi bila kibali cha daktari au mfamasia kwa sababu iwapo dawa hizi zitatumika kinyume na taratibu zinaweza kusababisha madhara makubwa ya kiafya.
Dawa za kupaka za kutibu chunusi
01: Dawa za kupaka za kuua bakteria.
Kundi hili la dawa za kupaka hutumiwa kutibu chunusi za kawaida.Baadhi ya dawa kutoka katika kundi hili ni Tetracycline, Clindamycin, Erythromycin na Triclosan.
Dawa hizi hutibu chunusi kwa kuangamiza bakteria wa P.acne, bakteria huyu ndio husababisha tatizo la chunusi.
Madhara ya dawa hizi za kupaka za kuua bakteria
- Ngozi kuungua
- Michubuko katika ngozi
- Clindamycin husababisha kuharisha damu na maumivu ya tumbo
- Dawa hizi ni rahisi kutengenezwa usugu.
02: Dawa ya kupaka ya Benzoyl Peroxide
Benzoyl Peroxide ni moja ya dawa zinazotumika zaidi kutibu chunusi za kupaka. Umaarufu wa dawa hii unatokana na ufanisi wake katika kutibu chunusi.Benzoyl Peroxide hutibu chunusi kwa kuzuia bakteria wa P.acne kuzaliana kwa wingi. Msombo huu unafanya kazi ya kusaidia kutengenezwa kwa hewa ya oksijeni katika ngozi.
Bakteria wa P.acne hawezi kuishi katika sehemu yenye kiasi kikubwa cha hewa ya Oksijeni.
Madhara ya kutumia Benzoyl Peroxide
- Inasababisha ngozi kuwa kavu
- Inamenya ngozi
- Inaweza kusababisha michubuko na ngozi kuungua
- Husababisha mzio kwa baadhi ya watu
03: Dawa ya kupaka ya Salicylic Acid
Salicylic Acid ni dawa nyingine ya kupaka ambayo inaweza kupatikana peke yake au ikiwa imechanganywa na vipodozi vingine.Dawa hii inafanya kazi kwa kusaidia kuyeyusha mchanganyiko wa jasho, mafuta na seli zilizokufa katika ngozi.
Kwa kufanya hivi kemikali hii inazuia mchanganyiko huu kuziba matunda ya vinyweleo vilevile inazuia kugandamana kwa mchanganyiko huu katika ngozi.
Madhara ya dawa hii ni pamoja na;
- kumenya ngozi,
- kusababisha ngozi kuwa kavu na
- michubuko katika ngozi
04: Dawa ya kupaka ya Alpha-hydroxy Acids
Alpha-hydroxy Acids ni tindikali inayopatikana katika matunda mbalimbali ikiwemo machungwa, limao na miwa.Kemikali hii hufanya kazi ya kudhibiti na kuondoa seli zilizokufa katika ngozi.
Udhibiti wa seli zilizokufa katika ngozi ni muhimu kwa sababu seli hizi zinapochanganyikana na mafuta katika ngozi husababisha ngozi kutawaliwa na bakteria wa P.acne.
05: Dawa za kupaka za vitamini A (Retinoids)
Retinoids ni dawa za kupaka zinazotengenezwa kwa vitamini A. Mfano wa dawa hizi ni Tretinoin na Differin.Dawa hizi hufanya kazi kwa kusaidia mchakato mzima wa kutengenezwa kwa seli za ngozi.
Zinathibiti kiwango cha seli zinazokufa na kuratibu mchakato wa kawaida wa mwili wa kuziondoa seli hizi zilizokufa katika ngozi.
Madhara ya dawa hizi za Retinoids
- Kumenya ngozi
- Kuchubua ngozi
- Kuifanya ngozi kuwa nyepesi na rahisi kuharibika.
06: Dawa ya kupaka ya Azelaic acid
Ni miongoni mwa dawa salama zaidi za kupaka. Kemikali hii pia inapatikana katika vyakula mbalimbali hasa ngano.Kemikali hii inafanya kazi kwa kuangamiza bakteria katika ngozi. Ni dawa pekee ambayo inaweza kutumika mseto na dawa nyingine yeyote ya kupaka bila matatizo.
Madhara ya dawa hii
- Azelaic acid inazuia kutengenezwa kwa melanini, melanini ndio inaipa ngozi yako rangi nyeusi au kahawia.
- Inamenya ngozi
- Inasababisha michubuko ya ngozi
Dawa za kisasa za kunywa za kutibu chunusi
Ikiwa tatizo lako la chunusi ni kubwa kiasi ambacho dawa za kupaka pekee hazikusaidi, basi unaweza kutumia dawa mbalimbali za vidonge.01: Antibiotiki za kutibu chunusi
Dawa hizi zinafanya kazi ya kuua na kuangamiza bakteri wa P.acne. Baadhi ya dawa zinazotumika kutibu chunusi ni Tetracycline, Clarithromycin, Clindamycin, Doxycycline na Erythromycin.Kuna madhara kadhaa ya kutumia dawa hizi hasa ikiwa utatumia bila kufuata ushauri wa kitaalamu, baadhi ya madhara ya kutumia dawa hizi ni;
- Inaongeza uwezekano wa kupata fangasi za ukeni kwa wanawake
- Kutapika
- Zinapunguza ufanisi wa dawa za kupanga uzazi, ikiwa unatumia dawa kupanga uzazi
- Ni rahisi mwili kutengenezwa usugu wa dawa
02: Dawa za kupanga uzazi
Dawa za kupanga uzazi zinaweza kusaidia kutibu chunusi kwa sababu zinathibiti kiwngo cha homoni za androjeni. Homoni za androjeni ni miongoni mwa visababishi vikubwa vya chunusi.Kuna madhara mbalimbali ya kutumia dawa hizi za uzazi wa mpango, kubwa ni kuongezeka kwa uwezekano wa kupata saratani katika mfumo wa uzazi, hasa wananwake.
03: Isotretinoin
Ni dawa ambayo ina kiwango kikubwa cha vitamini A. Isotretinoin ni dawa ambayo inatajwa kuwa na ufanisi wa hali ya juu kuliko dawa yoyote ya kisasa ya kutibu chunusi.Dawa hii inafanya kazi kwa Kudhibiti mlinganyo wa homoni za uzazi, Kudhibiti kutengenezwa kwa mafuta mengi katika ngozi na kuangamiza bakteria.
Pamoja na ufanisi mkubwa wa dawa hii katika kutibu chunusi, Isotretinoin si dawa salama kwa kila mtu hasa wajawazito.
Ina madhara kadhaa katika mwili wako ikiwemo
- Husababisha uke kuwa mkavu
- Matatizo mengine ya ngozi
- Kutokwa damu puani
- Upungufu wa damu
- Mapunye na ngozi kuwa kavu
- Ikiwa itatumiwa na mjamzito kuna uwezekano wa 90% mtoto akazaliwa na mapungufu ya kiafya.
Usishike ujauzito ikiwa bado unatumia dawa hii.
Hitimisho
Hizi ni baadhi ya dawa za kisasa za kutibu chunusi. Dawa nyinginezo za kutibu chunusi ni pamoja na Dapsone, vitamini B3, Spironolactone, corticosteroids na Sulfur.Hakuna dawa yoyote kati ya dawa hizi ambayo inaweza kutibu na kuondoa chunusi milele.