Dalili za UKIMWI, Tiba na aina ya vipimo vya UKIMWI
UKIMWI, Upungufu wa Kinga MWIlini, ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na virusi aina ya HIV. Ni miongoni mwa magonjwa makubwa ya kihistoria ulimwenguni kutokana na kusababisha idadi kubwa ya vifo tangu kugunduliwa kwa ugonjwa huu.
Kuna uzushi na nadharia mbalimbali kuhusu asili ya ugonjwa huu wa UKIMWI. Katika makala hii tumekuandalia dondoo muhimu kuhusu ugonjwa huu, dondoo zitakazojibu maswali yako yote kuhusu ugonjwa huu wa UKIMWI.
Virusi hawa hushambulia seli mbalimbali za mwili ikiwemo seli nyeupe za damu zijulikanazo kama CD4.
CD4 ni seli za mwili zinazohusika na kuupatia mwili ulinzi dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Kushambuliwa kwa seli hizi kunadhoofisha ulinzi wa mwili dhidi ya magonjwa na kupelekea ulinzi au mwili kupungua au kudhoofu.
Kupungua kwa ulinzi au kinga ya mwili ndio hupelekea tatizo la Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI).
Njia kuu ambayo virusi hawa husambaa ni kupitia ngono zembe (kujamiana bila kutumia kinga).
Hatari ya kupata virusi vya UKIMWI huongezeka zaidi kwa watu ambao hujihusisha na mapenzi ya jinsia moja(mashoga), vilevile wanawake ambao huingiliwa kinyume na maumbile(Anal sex).
Njia nyinginezo ambazo zinaweza kusababisha virusi hawa kusambaa au kuambukizwa ni;
Ikiwa utazingatia miongozo bora ya jinsi ya kuishi na virusi hawa wa HIV, basi virusi hawa hawataweza kufanya uharibifu kwa kiasi cha kusababisha UKIMWI
Muda wa ambao dalili za UKIMWI zinaweza kuanza kuonekana ni kati ya miaka 2 hadi 25, au zaidi. Itategemea ni kwa namna gani umewapa nafasi virusi hawa wa HIV kufanya uharibifu mwilini mwako.
Tunapozungumzia kuwapa nafasi virusi hawa ni kutozingatia kanuni na miongozo bora ya kuishi na virusi wa HIV, ikiwa ni pamoja na kuchelewa kufahamu kama tayari unaishi na virusi hawa.
Kwa sasa dawa zinazopatikana ni dawa za kufubaza makalI ya virusi vya UKIMWI, Anti-Retroviral Drugs (ARV). Dawa hizi zinapunguza kasi ya virusi wa HIV kuangamiza seli za CD4.
Utafiti unaonyesha jinsi utakavyowahi kuanza kutumia dawa za ARV ndivyo utavyoishi muda mrefu bila kupata UKIMWI, pengine ukaufikia hata umri wa kawaida wa kuishi.
Hatua hizo ni kama Ifuatavyo:
Baadhi ya watu huweza kuonyesha dalili zifuatazo;
Kuna uzushi na nadharia mbalimbali kuhusu asili ya ugonjwa huu wa UKIMWI. Katika makala hii tumekuandalia dondoo muhimu kuhusu ugonjwa huu, dondoo zitakazojibu maswali yako yote kuhusu ugonjwa huu wa UKIMWI.
UKIMWI husababishwa na nini?
UKIMWI unasababishwa na virusi aina ya HIV.Virusi hawa hushambulia seli mbalimbali za mwili ikiwemo seli nyeupe za damu zijulikanazo kama CD4.
CD4 ni seli za mwili zinazohusika na kuupatia mwili ulinzi dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Kushambuliwa kwa seli hizi kunadhoofisha ulinzi wa mwili dhidi ya magonjwa na kupelekea ulinzi au mwili kupungua au kudhoofu.
Kupungua kwa ulinzi au kinga ya mwili ndio hupelekea tatizo la Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI).
Jinsi gani virusi vya UKIMWI husambaa?
Virusi vya UKIMWI(HIV) vinasambaa kwa njia yeyote itakayopelekea majimaji au damu ya mtu mwenye virusi vya HIV itagusana na damu au majimaji ya mtu asiye na virusi hawa.Njia kuu ambayo virusi hawa husambaa ni kupitia ngono zembe (kujamiana bila kutumia kinga).
Hatari ya kupata virusi vya UKIMWI huongezeka zaidi kwa watu ambao hujihusisha na mapenzi ya jinsia moja(mashoga), vilevile wanawake ambao huingiliwa kinyume na maumbile(Anal sex).
Njia nyinginezo ambazo zinaweza kusababisha virusi hawa kusambaa au kuambukizwa ni;
- Kuwekewa damu yenye virusi, hata hivyo sababu hii kwa sasa ni nadra sana kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia ya uchunguzi wa damu katika maabara za damu.
- Kuchangia vitu vyenye ncha kali, Mfano sindano na wembe.
- Kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto hasa wakati wa kujifungua, njia hii pia ni nadra sana kwa sasa hivi ikiwa mama mjamzito atawahi kuhudhuria kliniki.
- Wakati wa kunyonyesha, ikiwa mama anayenyonyesha atakuwa ni muathirika basi uwezekano wa kumuambukiza mtoto wake ni mkubwa.
Je ni kweli unaweza kuwa na HIV na usipate UKIMWI?
Ndio, unaweza kuwa na HIV na usipate UKIMWI kwa sababu HIV ni virusi, na UKIMWI ni matokeo ya uharibifu unaoweza kufanywa na virusi vya UKIMWI.Ikiwa utazingatia miongozo bora ya jinsi ya kuishi na virusi hawa wa HIV, basi virusi hawa hawataweza kufanya uharibifu kwa kiasi cha kusababisha UKIMWI
Dalili za UKIMWI huonekana baada ya muda gani?
Dalili kuu huanza kujitokeza pale kiwango kikubwa cha seli za CD4 kimeathiriwa.Muda wa ambao dalili za UKIMWI zinaweza kuanza kuonekana ni kati ya miaka 2 hadi 25, au zaidi. Itategemea ni kwa namna gani umewapa nafasi virusi hawa wa HIV kufanya uharibifu mwilini mwako.
Tunapozungumzia kuwapa nafasi virusi hawa ni kutozingatia kanuni na miongozo bora ya kuishi na virusi wa HIV, ikiwa ni pamoja na kuchelewa kufahamu kama tayari unaishi na virusi hawa.
Je, UKIMWI una dawa?
Mpaka sasa hakuna dawa wala chanjo ya kutibu na kuzuia virusi wa HIV na UKIMWI.Kwa sasa dawa zinazopatikana ni dawa za kufubaza makalI ya virusi vya UKIMWI, Anti-Retroviral Drugs (ARV). Dawa hizi zinapunguza kasi ya virusi wa HIV kuangamiza seli za CD4.
Ni wakati gani sahihi wa kuanza kutumia dawa za UKIMWI(ARV)?
Wakati wowote utakapogundulika na virusi wa HIV unashauriwa kuanza kutumia ARV mara moja.Utafiti unaonyesha jinsi utakavyowahi kuanza kutumia dawa za ARV ndivyo utavyoishi muda mrefu bila kupata UKIMWI, pengine ukaufikia hata umri wa kawaida wa kuishi.
Dalili za awali za UKIMWI
Ili mtu kupata UKIMWI, kuna hatua kuu 3 ambazo anapitia, katika kila hatua kuna dalili ambazo hujitokeza.Hatua hizo ni kama Ifuatavyo:
Hatua ya kwanza (Kipindi cha maambukizi ya HIV)
Hatua hii ni ya mwanzo na hutokea katika kipindi cha wiki 2 hadi 4 baada ya maambukizi. Katika hatua hii virusi wa HIV huzaliana na kushambulia CD4 kwa kasi kubwa.Baadhi ya watu huweza kuonyesha dalili zifuatazo;
- Mapunye katika ngozi
- Mafua
- Homa
- Kutokwa jasho wakati wa usiku
- Vidonda mdomoni
- Kupungua uzito ghafla
- Kuharisha
- Vidonda na michubuko mdomoni
- Homa za vipindi
- Kuvimba kwa tonsili
- Uchovu na mwili kuishiwa nguvu
- Maumivu ya kichwa na mwili.
Hatua ya pili (kipindi kisicho na dalili)
Katika hatua hii kasi ya kuzaliana ya virusi wa HIV hupungua kwa kiasi kikubwa.Hatua hii hina dalili zozote, na kama mgonjwa hatotumia dawa (ARV) inaweza kudumu kwa miaka isiyozidi 10.
Ikiwa mgonjwa ataanza kutumia ARV basi anaweza kuishi miaka mingi zaidi bila kupata UKIMWI.
Vilevile kwa mgonjwa anayetumia ARV katika hatua hii uwezekano wa kuambukiza wengine huwa ni mdogo hadi asilimia 0% ikiwa atatumia dawa hizi kwa ufasaha.
Hatua hii hutokea ikiwa CD4 za mgonjwa ni chini ya seli 200 za CD4 katika mirolita 1 ya damu.
Katika hatua hii mgonjwa anakuwa na kiasi kikubwa cha virusi katika damu na anaweza kuambukiza wengine kiurahisi zaidi.
Dalili za mgonjwa wa Ukimwi katika hatua hii ni pamoja na;
Kipimo hiki kwa sasa kinapatikana katika maduka mengi ya dawa kwa gharama nafuu, katika na vituo vya afya, huduma ya vipimo vya HIV ni bure.
Zingatia kanuni bora za kujikinga na virusi vya UKIMWI, kama vile kutumia kondomu, kujiepusha na shughuli hatarishi kama vile michoro ya mwilini (tatoo), kuwa mwaminifu na kuendelea kukumbushana juu ya hatari za ugonjwa huu dhidi ya ndugu na jamaa.
Ukiwa utagundulika na virusi vya UKIMWI, anza kutumia ARV haraka iwezekanavyo, kwa sababu kuwahi kuanza kutumia ARV kunaweza kukufanya kuishi miaka mingi zaidi lakini pia itapunguza kazi ya wewe kuwaambukiza wengine.
Ikiwa mgonjwa ataanza kutumia ARV basi anaweza kuishi miaka mingi zaidi bila kupata UKIMWI.
Vilevile kwa mgonjwa anayetumia ARV katika hatua hii uwezekano wa kuambukiza wengine huwa ni mdogo hadi asilimia 0% ikiwa atatumia dawa hizi kwa ufasaha.
Hatua ya tatu (kipindi cha UKIMWI)
Hii ni hatua ya mwisho ambapo virusi vya HIV vimeshafanya uharibifu kiasi cha kusababisha UKIMWI. Katika hatua hii mwili wako hauwezi tena kupambana na magonjwa hata yale ya kawaida.Hatua hii hutokea ikiwa CD4 za mgonjwa ni chini ya seli 200 za CD4 katika mirolita 1 ya damu.
Katika hatua hii mgonjwa anakuwa na kiasi kikubwa cha virusi katika damu na anaweza kuambukiza wengine kiurahisi zaidi.
Dalili za mgonjwa wa Ukimwi katika hatua hii ni pamoja na;
- Kuharisha damu na maji
- Kikohozi kikavu
- Kifua kikuu
- Kutokwa jasho muda mwingi
- Vidonda mdomoni na kooni
- Kukonda kupita kawaida
- Fangasi mdomoni
- Kupoteza hamu ya kula
- Ugonjwa wa kaposis sarcoma
- Maradhi ya saratani
- Mkanda wa jeshi
- Kuvimba kwa tonsili
Aina ya vipimo vya UKIMWI.
Virusi vya UKIMWI vinaweza kuonekana ndani ya siku 11 baada ya mtu kuambukizwa kwa kutumia kipimo cha kutambua protini za vinasaba vya HIV, Nucleic acid test (NAT).Kipimo hiki kwa sasa kinapatikana katika maduka mengi ya dawa kwa gharama nafuu, katika na vituo vya afya, huduma ya vipimo vya HIV ni bure.
Hitimisho
Usichukulie poa, UKIMWI upo na watu wengi wanaishi na ugonjwa huu. Hakikisha unapima afya yako wakati wowote unapodhani umejiweka katika mazingira hatarishi ya kupata ugonjwa huu.Zingatia kanuni bora za kujikinga na virusi vya UKIMWI, kama vile kutumia kondomu, kujiepusha na shughuli hatarishi kama vile michoro ya mwilini (tatoo), kuwa mwaminifu na kuendelea kukumbushana juu ya hatari za ugonjwa huu dhidi ya ndugu na jamaa.