Faida za mahindi katika kutibu macho na figo.

Bila shaka mahindi ni chakula kinachotumiwa zaidi barani Afrika kuliko chakula kingine chochote.

Matumizi ya mahindi kama chakula kikuu Afrika kumepelekea watu kudhani mahindi hutumika kama chakula kwa ajili ya kutupatia nishati pekee.

Je, Unafahamu ya kwamba faida za mahindi ni zaidi ya kutupatia nishati.

Kitaalamu mmea huu unajulikana kwa jina la Zea mays. Mmea huu unapatikana karibu kila pande ya dunia huku Tanzania ikiwa ni moja ya wazalishaji wakubwa wa mmea huu.

Nchini Tanzania mmea huu huzalishwa zaidi mikoa ya kusini mwa Tanzania huku Rukwa na Ruvuma zikiwa ni vinara wa uzalishaji.

Tafiti mbalimbali zimethibitisha uwezo wa mahindi katika kutibu maradhi ya mfumo wa mkojo, michubuko, majipu na ugonjwa wa manjano.

Hii inatokana na uwepo wa kemikali kadhaa ndani ya mahindi ambazo zina uwezo wa kupambana na magonjwa haya.

Kemikali zilizopo ndani ya mahindi na faida zake mwilini.

Mahindi mabichi, punje na nyuzinyuzi zake ndio sehemu ambazo kemikali tiba hupatikana kwa wingi zaidi kuliko sehemu nyingine ya mmea huu. 

Kemikali hizi ndio ambazo ndio zinaupa muhindi uwezo wake wa kutibu na kuzuia magonjwa mbalimbali.

Baadhi ya kemikali hizo ni pamoja na: 
  • Kemikali za Flavonoids, ambazo huongeza kinga, kuua bakteria na kusaidia mzunguko wa damu.
  • Carotenoids:  Kemikali za Carotenoids ambazo hupatikana kwa wingi katika nyuzinyuzi za muhindi, kemikali hizi huimarisha uwezo wa kuona na afya ya macho. Kemikali za carotenoids zinazopatikana kwa wingi katika mahindi ni lutein na zeaxanthin.
  • Anthocyanins: Vilevile mahindi hasa yale ya rangi ya zambarau yana kemikali ya Anthocyanins ambayo ni kioksideshaji kikubwa mwilini. Hivyo husaidia kuondoa sumu za mwili.
  • Ferulic acid: Mahindi pia yana Ferulic acid kiantioksideshaji kwa kiwango kikubwa kuliko nafaka yoyote. Kemikali hii husaidia kuondoa chaji huru ambazo ni sumu za mwilini.
Mbali na kemikali tiba hizi, mahindi pia ni chanzo kikubwa cha wanga. Kemikali hizi za wanga ndizo ambazo huupatia mwili nguvu.

Pia ndani ya mahindi kuna vitamin E, vitamin B, protini, mafuta na madini joto mbalimbali kama vile copper, manganese, zinc na Phosphorus.

Faida za mahindi mwilini.

01: Kutibu magonjwa ya macho

Ili macho yafanye kazi vizuri yanahitaji kemikali za carotenoids. Mahindi moja ya mimea adimu yenye kiwango kikubwa cha kemikali hii ya carotenoids ni moja ya tiba bora na msaada mkubwa katika kutibu tatizo macho.

02: Kupunguza uvimbe kwa wajawazito

Kwa wanawake wajawazito ambao huvimba kutokana na maji kuwa mengi mwilini. Matumizi ya juisi ya mahindi ni msaada mkubwa kwao.

03: Kupunguza sumu mwilini

Viantioksideshaji vya Anthocyanins na Ferulic acid ndani ya muhindi vinatosha kukupa ulinzi thabiti dhidi ya chaji huru mwilini. 

Matumizi ya juisi au supu ya mahindi mara kwa mara yanaimarisha kinga ya mwili wako dhidi ya sumu hizi.

04: Kutibu michubuko, majipu na uvimbe

Matumizi ya kupaka ya mchanganyo mzito wa nyuzi nyuzi za mahindi na mahindi yaliyopondwa ni msaada mkubwa kwa matatizo mbalimbali ya ngozi.

05: Kutibu maradhi ya figo

Mahindi husaidia kukojoa mara kwa mara, hii ni faida kwa watu wanaosumbuliwa na maradhi ya uvimbe katika figo na tezi dume.

Matumizi ya juisi ya mahindi ni msaada mkubwa kwa watu hawa, si tu kuwasaidia kupata haja ndogo. Vilevile kupunguza maumivu yatokanayo na kulazimisha mkojo kutoka.

06: Kutibu ugonjwa wa manjano

Ugonjwa wa manjano husababishwa na matatizo mbalimbali hasa uvimbe katika ini na figo. 

Kwa vile mahindi husaidia kutibu maradhi ya figo vilevile wagonjwa wa manjano wanaweza kunufaika kwa kutumia mahindi.

Ni sehemu ipi ya mmea wa mahindi hutumika kama tiba?

Sehemu kuu zinazotumika kama tiba ni punje za mahindi, nyuzinyuzi za mahindi na maganda ya mahindi. 

Matumizi ya mahindi mabichi ndio ambayo yana faida za kiafya zilizoainishwa hapo juu.

Sehemu hizi huweza kutumika kuandaliwa na kutumika katika namna tofauti kama vile.
  • Juisi.
  • Unga.
  • Mafuta.
  • Katika namna ya mkorogo mzito.

Jinsi ya kuandaa na kutumia mahindi kama tiba.

Kwa matumizi ya kutibu maradhi ya mfumo wa mkojo.

Maandalizi:

Vuna nyuzinyuzi za mahindi, unaweza kuzikausha au kuzitumia zikiwa mbichi. Kisha tengeneza juisi ya nyuzinyuzi hizo kwa kuiloweka katika maji au pombe kwa muda wa siku 2 hadi 3.

Matumizi:

Kwa maradhi ya tezi dume, uvimbe katika figo, mawe katika figo na mwili kuvimba kwa kujaa maji hasa wajawazito tumia glasi 4 hadi 6 kwa kunywa mara 2 hadi 3 kwa siku.

Kutibu macho, manjano na kuondoa sumu tumia robo tatu ya glasi ya juisi ya nyuzinyuzi za mahindi mara 2 hadi 3 kwa siku.

Kwa matumizi ya matatizo ya ngozi.

Maandalizi:

Ponda au saga punje za mahindi mabichi Pamoja na nyuzinyuzi za mahindi ili kutengeneza mkorogo mzito, kisha paka sehemu ilioathirika mara 3 kila siku.

Hitimisho

Mahindi ni moja ya vyakula vinavyotumiwa zaidi afrika, mbali na kutupatia nishati ya mwili, mahindi yanaweza kutumiwa kama tiba au kinga ya magonjwa mbalimbali kama yalivyoainishwa katika makala hii.  

Muhimu kufahamu kwamba mahindi ya njano pekee ndio yenye faida nyingi za kutibu na kupambana na magonjwa kuliko aina nyingine za mahindi.
Next Post Previous Post
No Comment
Andika Swali au Maoni
comment url