Vipimo muhimu kwa mama mjamzito
Unapopata mimba kuna mabadiliko mengi ya lazima ambayo hutokea katika mwili wako. Kuongezeka uzito, kuongezeka sukari ya mwili, mabadiliko katika mzunguko wa damu na mabadiliko ya kinga ya mwili.
Ili kuhakikisha mabadiliko haya hayaleti athari zozote kwa mama mjamzito, ni lazima mjamzito kufanyiwa vipimo muhimu vya afya kipindi chote cha ujauzito wake ili kufahamu ikiwa hali ya afya mjamzito inaweza kuathiriwa na mabadiliko haya.
Kuna vipimo kadhaa ambavyo ni vya lazima kwa mjamzito, vipimo hivi hufanywa ili kuchunguza baadhi ya matatizo ya kiafya ambayo huathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya lazima ambayo hutokea kwa mjamzito.
Katika makala hii tutaangazia vipimo muhimu ambavyo mjamzito anapaswa kufanyiwa kuanzia siku ya kwanza kuhudhuria kliniki hadi kufikia kipindi cha kujifungua.
Kwa kawaida BMI ya mwanamke inapaswa kuwa kati ya 18.5 hadi 24.5, baada ya ujauzito ongezeko la kawaida la uzito kwa mjamzito ni kilogramu 5 hadi 11, kulingana na aina ya ujauzito.
Wanawake ambao wana kitambi au uzito mdogo wako katika hatari ya kupata matatizo katika kipindi cha ujauzito.
Uzito mkubwa unaweza kusababisha madhara yafuatayo kwa mama na mtoto;
Shikizo la damu kwa wajawazito halipaswi kuzidi 120/80mmHg.
Ni muhimu kufahamu ikiwa mjamzito ana tatizo la shinikizo la damu, kwa sababu shinikizo la damu linaweza kusababisha matatizo mbalimbali kwa mjamzito ikiwemo;
Baadhi ya matatizo yanayotakiwa kuchunguzwa ni pamoja na;
Hii itasaidia kutambua ikiwa kuna tatizo, vilevile itatoa nafasi ya matibabu bora ikiwa tatizo la upungufu wa damu litaonekana.
Katika uchunguzi wa damu, mambo muhimu yanayotakiwa kuangaliwa ni
Unapokuwa na ujauzito antibodi zako zinaweza kuutafsiri ujauzito wako kama kitu kigeni na zinaweza kuanza mchakato wa kukiua na kukiondoa mwilini mwako.
Hali hii inatokea ikiwa kundi la damu la mtoto aliyeko tumboni lina protini za rhesus ambazo ni tofauti na protini za rhesus zilizopo katika damu ya mama.
Ikiwa damu ya mama ina protini za rhesus, basi hakuna hatari yeyote bila kujali ikiwa damu ya mtoto ina protini hizo ama haina.
Kama mwanamke hana protini hizi za rhesu zinaweza kutengenezwa wakati mwanamke ni mjamzito.
Ikitokea protini za rhesus katika damu ya mama zitachelewa kutengenezwa hadi wiki ya 28 ya ujauzito basi mama atachomwa sindano maalumu itakayo zuia vita ya protini za rhesus wakati wa kujifungua hasa ikiwa damu ya mtoto itakuwa na protini hizi.
Ni muhimu sana kufanya kipimo hiki kwa sababu tofauti ya protini za rhesus kati ya mama na mtoto zinaweza kusababisha vita inayopelekea damu kuganda na hatimaye kusababisha kifo cha mama na mtoto.
Ni vizuri mjamzito kuchunguzwa hali yake ya sukari mwilini ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.
Ikiwa atabainika na ugonjwa huu, mjamzito atapatiwa matibabu na kupona kabisa hivyo kuepusha matatizo ya kiafya ambayo mtoto anaweza kuyapata ikiwa mjamzito atakuwa na ugonjwa huu.
Baadhi ya athari za kaswende ni pamoja na;
Ikiwa mjamzito ana tatizo hili, hatua muhimu zinapaswa kuchukuliwa haraka iwezekanavyo ikiwa ni pamoja na kunza kwa tiba itakayopunguza uwezekano wa mama kumuambukiza mtoto tumboni.
Mjamzito anashauriwa kuanza kutumia dawa za kufubaza makala ya VVU haraka iwezekanavyo ili kupunguza uwezekano wa kumuambukiza mtoto aliye tumboni.
Ugonjwa wa PID, gono na chlamidia ni miongoni mwa magonjwa yanayotakiwa kuchunguzwa kwa mjamzito kutokana na madhara yanayoweza kusababisha kwa mama na mtoto.
Ikiwa kipimo kitaonyesha bado haujapatiwa chanjo ya ugonjwa huu basi atatakiwa kupata chanjo hii mara baada ya kujifungua.
Hata hivyo ni vizuri kufanya vipimo vya rubella miezi 2 kabla ya ujauzito ili uweze kupata chanjo hii mapema kabla ya ujauzito, kwa sababu huweza kupewa chanjo hii wakati wa ujauzito.
Vilevile kipimo hiki husaidia kujua ikiwa mimba imejishikiza sehemu sahihi au la.
Ni vizuri mwanamke kuhudhuria kliniki haraka iwezekanavyo pale anapogundua kuwa ni mjamzito.
Kwa kufanya hivyo itasaidia kufahamu ikiwa mjamzito ana matatizo yeyote ya kiafya ambayo yanaweza kuathiri ukuaji wa mimba.
Ili kuhakikisha mabadiliko haya hayaleti athari zozote kwa mama mjamzito, ni lazima mjamzito kufanyiwa vipimo muhimu vya afya kipindi chote cha ujauzito wake ili kufahamu ikiwa hali ya afya mjamzito inaweza kuathiriwa na mabadiliko haya.
Kuna vipimo kadhaa ambavyo ni vya lazima kwa mjamzito, vipimo hivi hufanywa ili kuchunguza baadhi ya matatizo ya kiafya ambayo huathiriwa kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya lazima ambayo hutokea kwa mjamzito.
Katika makala hii tutaangazia vipimo muhimu ambavyo mjamzito anapaswa kufanyiwa kuanzia siku ya kwanza kuhudhuria kliniki hadi kufikia kipindi cha kujifungua.
Vipimo muhimu kwa mama mjamzito
Uzito na kimo
Uzito na urefu zinapaswa kuchunguzwa kwa katika ziara ya kwanza ya mama mjamzito, ili kufahamu Body Mass Index.Kwa kawaida BMI ya mwanamke inapaswa kuwa kati ya 18.5 hadi 24.5, baada ya ujauzito ongezeko la kawaida la uzito kwa mjamzito ni kilogramu 5 hadi 11, kulingana na aina ya ujauzito.
Wanawake ambao wana kitambi au uzito mdogo wako katika hatari ya kupata matatizo katika kipindi cha ujauzito.
Uzito mkubwa unaweza kusababisha madhara yafuatayo kwa mama na mtoto;
- Kuharibika kwa mimba
- kuzaa mtoto aliyekufa na kuharibika
- Ugonjwa wa kisukari
- Shinikizo la damu
- Kifafa cha mimba
- Matatizo ya moyo
- Kukosa usingizi usingizi
- Matatizo ya ukuaji kwa mtoto
- Pumu ya utotoni
- Unene wa kupindukia kwa mtoto
Shinikizo la damu
Tathmini ya awali ya shinikizo la damu ni muhimu kwa wajawazito, inasaidia kutambua mjamzito ana tatizo hili.Shikizo la damu kwa wajawazito halipaswi kuzidi 120/80mmHg.
Ni muhimu kufahamu ikiwa mjamzito ana tatizo la shinikizo la damu, kwa sababu shinikizo la damu linaweza kusababisha matatizo mbalimbali kwa mjamzito ikiwemo;
- Kifafa cha mimba
- Mimba kuharibika
- Kuharibika kwa placenta
- Mtoto kushindwa kukua
- Kuzaa mtoto njiti
- Mtoto kuzaliwa na uzito mdogo
Uchunguzi wa via vya uzazi
Ni muhimu kufanya uchunguzi wa nje na ndani wa via vya uzazi ikiwa kuna ulazima. Uchunguzi huu unasaidia kutambua ikiwa mwanamke ana matatizo yoyote ya kutambua au kuzaliwa katika mfumo wake wa uzazi.Baadhi ya matatizo yanayotakiwa kuchunguzwa ni pamoja na;
- Saratani katika shingo ya kizazi
- Uvimbe katika maeneo ya mfumo wa uzazi
- Maambukizi ya PID
Kipimo cha kutambua kiwango cha damu
Ni lazima mwanamke achunguzwe kiasi cha damu katika mwili wake katika hatua mbalimbali za ukuaji na utunzaji wa ujauzito wake.Hii itasaidia kutambua ikiwa kuna tatizo, vilevile itatoa nafasi ya matibabu bora ikiwa tatizo la upungufu wa damu litaonekana.
Katika uchunguzi wa damu, mambo muhimu yanayotakiwa kuangaliwa ni
- Kiwango cha Hemoglobini: Dutu hizi husaidia kusafiri kwa hewa ya oksijeni katika maeneo mbalimbali ya mwili ikiwemo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Tatizo hili kwa sehemu kubwa husababishwa na upungufu wa virutubisho muhimu vya madini chuma, vitamini B12 na vitamini B9 (folic acid).
- Kiwango cha seli nyeupe za damu: Seli hizi husaidia damu kuganda ikiwa umepata jeraha. Ni tatizo la kawaida kwa mjamzito ambao husumbuliwa na shinikizo la damu.
- Upungufu wa seli nyeupe unapelekea mwanamke kukosa sifa ya kupata sindano ya kusaidia kutuliza maumivu inayochomwa katika uti wa mgongo.
- Kupungua kwa seli nyeupe za damu kunaweza kusababisha kupotea kwa damu nyingi kuliko kawaida wakati wa kujifungua.
- Upungufu wa dutu za hemoglobini katika damu husababisha kifafa cha mimba.
Uchunguzi wa kundi la damu na antibodi zake
Antibodi ni aina ya protini zinazotengenezwa na mfumo wa kinga wa mwili wako. Kazi ya antibody ni kupambana na vitu vigeni vinavyoingia mwilini mwako.Unapokuwa na ujauzito antibodi zako zinaweza kuutafsiri ujauzito wako kama kitu kigeni na zinaweza kuanza mchakato wa kukiua na kukiondoa mwilini mwako.
Hali hii inatokea ikiwa kundi la damu la mtoto aliyeko tumboni lina protini za rhesus ambazo ni tofauti na protini za rhesus zilizopo katika damu ya mama.
Ikiwa damu ya mama ina protini za rhesus, basi hakuna hatari yeyote bila kujali ikiwa damu ya mtoto ina protini hizo ama haina.
Kama mwanamke hana protini hizi za rhesu zinaweza kutengenezwa wakati mwanamke ni mjamzito.
Ikitokea protini za rhesus katika damu ya mama zitachelewa kutengenezwa hadi wiki ya 28 ya ujauzito basi mama atachomwa sindano maalumu itakayo zuia vita ya protini za rhesus wakati wa kujifungua hasa ikiwa damu ya mtoto itakuwa na protini hizi.
Ni muhimu sana kufanya kipimo hiki kwa sababu tofauti ya protini za rhesus kati ya mama na mtoto zinaweza kusababisha vita inayopelekea damu kuganda na hatimaye kusababisha kifo cha mama na mtoto.
Kipimo cha kutambua sukari ya mwili
Ni muhimu kwa mama mjamzito kuchunguzwa ikiwa ana tatizo la kisukari kwa sababu kipindi cha ujauzito ufanisi wa homoni ya insulin hupungua kwa kiasi kikubwa hasa baada ya placenta kutengenezwa.Ni vizuri mjamzito kuchunguzwa hali yake ya sukari mwilini ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.
- Kisukari kinapaswa kudhibitiwa mapema kwa sababu zifuatazo;
- Kujifungua mtoto mwenye uzito mkubwa
- Uwezekano mkubwa wa kujifungua kwa upasuaji
- Kifafa cha mimba
- Shinikizo la damu
- Mimba kuharibika
Kipimo cha kaswende
Kutokana na athari za ugonjwa huu kwa mtoto, kila mjamzito ni lazima kufanya kipimo hiki mapema iwezekanavyo.Ikiwa atabainika na ugonjwa huu, mjamzito atapatiwa matibabu na kupona kabisa hivyo kuepusha matatizo ya kiafya ambayo mtoto anaweza kuyapata ikiwa mjamzito atakuwa na ugonjwa huu.
Baadhi ya athari za kaswende ni pamoja na;
- Mimba kuharibika
- Mtoto kufa
- Matatizo ya upofu na kiziwi kwa mtoto
Kipimo cha homa ya ini inayosababishwa na virusi vya Hepatitis B
Kipimo hiki ni muhimu kwa wajawazito katika kutambua ikiwa mjamzito ana tatizo hili au hana.Ikiwa mjamzito ana tatizo hili, hatua muhimu zinapaswa kuchukuliwa haraka iwezekanavyo ikiwa ni pamoja na kunza kwa tiba itakayopunguza uwezekano wa mama kumuambukiza mtoto tumboni.
Kipimo cha UKIMWI
Mjamzito anapaswa kupima ugonjwa wa UKIMWI mapema zaidi ili kufahamu ikiwa ana maambukizi ya ugonjwa huu.Mjamzito anashauriwa kuanza kutumia dawa za kufubaza makala ya VVU haraka iwezekanavyo ili kupunguza uwezekano wa kumuambukiza mtoto aliye tumboni.
Vipimo vya magonjwa mbalimbali ya bakteria
Mjamzito anatakiwa kufanya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali yanayoambukizwa na bakteria ambayo yanaweza kuathiri ukuaji wa mimba na afya ya mtoto tumboni.Ugonjwa wa PID, gono na chlamidia ni miongoni mwa magonjwa yanayotakiwa kuchunguzwa kwa mjamzito kutokana na madhara yanayoweza kusababisha kwa mama na mtoto.
Kipimo cha Rubella
Kipimo cha ugonjwa rubella kitasaidia kufahamu ikiwa mjamzito ameshapatiwa chanjo au bado.Ikiwa kipimo kitaonyesha bado haujapatiwa chanjo ya ugonjwa huu basi atatakiwa kupata chanjo hii mara baada ya kujifungua.
Hata hivyo ni vizuri kufanya vipimo vya rubella miezi 2 kabla ya ujauzito ili uweze kupata chanjo hii mapema kabla ya ujauzito, kwa sababu huweza kupewa chanjo hii wakati wa ujauzito.
Vipimo vya kutumia mwangwi wa sauti (ultrasound scan)
Kipimo hiki ni muhimu katika hatua mbalimbali za ukuaji wa mtoto tumboni kwa sababu husaidia kukadiria umri wa ujauzito, lakini pia husaidia kutambua ikiwa ujauzito ni wa mtoto mmoja au mapacha.Vilevile kipimo hiki husaidia kujua ikiwa mimba imejishikiza sehemu sahihi au la.
Vipimo vinginevyo
Vipimo vinginevyo ambavyo sio vya lazima lakini baadhi ya wajawazito wanaweza kulazimika kuvifanya kulingana na mapendekezo ya mtaalamu wa afya anayeratibu kliniki yake ni pamoja na;- Ugonjwa wa mkanda wa jeshi (herpes simplex)
- Fangasi ukeni
- Mapungufu ya utendaji kazi wa tezi ya thyroid
Hitimisho
Baada ya mwanamke kupata ujauzito, mambo mengi hubadilika. Mabadiliko ya kimwili na kibaolojia yanayotokea baada ya mwanamke kushika ujauzito yanahitaji uangalizi wa karibu sana.Ni vizuri mwanamke kuhudhuria kliniki haraka iwezekanavyo pale anapogundua kuwa ni mjamzito.
Kwa kufanya hivyo itasaidia kufahamu ikiwa mjamzito ana matatizo yeyote ya kiafya ambayo yanaweza kuathiri ukuaji wa mimba.